Ama kweli nabii hakubaliki nyumbani. Je, Magufuli ni nabii? Tanzania wanambeza, Afrika wanamlilia! Tanzania yapigiwa mfano Magufuli awe Rais wa Afrika

Heshima yako mkuu Pascal.

Kwenye magonjwa ya kuambukiza kama ilivyo Covid 19 kuna concept iitwayo “Reversibility” yaani kama kisababishi(causative factor) ikiondolewa, athari zake pia zinapotea.

Sababu hapa ni hako ‘ka corona na athari ni kifo. Hivyo sidhani ni sahihi sana kukihafifisha hiki kirusi kwa misingi ya kuwa ‘kamesindikiza tu’.

Kama hizo underlying issues zilikuwepo na bado mhanga alikuwa anadunda, alafu akaingia korona na kuziamsha hizo nyingine mpaka mgonjwa kupoteza uhai basi huyu corona ndio wakala wa mwisho wa Ziraili ambaye tunatakiwa kushughulika naye.

Kumbuka kwamba hizo underlying issues(hbp, diabetes, HIV, heart diseases etc) tayari zina utaratibu wake wa kitabibu wa kupambana nazo.
Mkuu Nowonmai, asante sana kwa post hii na amimi usiamini, imenifundisha kitu kuhusu concept ya “Reversibility” yaani kama kisababishi(causative factor) na underlying issues (hbp, diabetes, HIV, heart diseases etc).

Kabla ya kuisoma hiyo concept yako, mimi nilihesabu kuwa hao wote wenye underlying issues, walikuwa ni marehemu watarajiwa, wanaosubiri tuu kufa, ila hawakujua watakufa lini, hivyo Corona imewawahisha tuu, lakini hata bila Corona ilikuwa wafe tuu!, lakini ni kupitia kwako ndio nimejifunza kuwa pamoja na kuwa na underlying issues za hbp, diabetes, HIV, heart diseases etc, sio death threatening diseases, hivyo bila Corona, wangeishi muda mrefu hivyo Corona ndio the causative agent wa premature deaths zao.
Thanks.
P
 
Wanabodi, hili ni bandiko la swali kuhusu rais Magufuli kama jee ni Nabii?. Naomba mimi nisijibu,
msikilize Mhe. Dr. Mwigulu Nchemba wewe mwenyewe umsikie amesema nini kumhusu Rais Magufuli



P
 
Wanabodi,
wakati kuna baadhi ya sisi Watanzania tunambeza rais Magufuli na serikali yake kwa baadhi ya hatua anazochukua kutatua changamoto mbalimbali zinazotukabili na kulikabili taifa letu, za kisiasa, kiuchumi na kijamii, ikiwemo changamoto hii mpya ya ugonjwa wa Corona, kuna baadhi yetu sisi Watanzania, tunambeza!. Wakati sisi tuna beza, kuna baadhi ya wenzetu wa bara la Africa wao wanamlilia rais Magufuli wakitamani rais Magufuli ndio awe rais wao kwa hatua ambazo rais Magufuli amezitumia kwa Tanzania kupambana na janga la ugonjwa wa Corona, zilizopelekea nchi ya Tanzania kuwa ni nchi ya kupigiwa mfano, huku wengine wakienda mbali zaidi kwa kutamani juhudi za kupambana na Corona kwa bara lote zima la Africa ziunganishe kujenga nguvu ya pamoja kupambana na janga la Corona na kutamani rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli ndie ateuliwe kwa kauli moja kuwa Kamanda Mkuu wa Bara la Africa katika kuongoza Mapambano dhidi ya janga la ugonjwa wa Corona kwa bara lote zima la Africa!. Wakati sisi huku tunabeza, hatuoni, hatutambui, hatuthamini thamani ya Magufuli tuliye nae, wenzetu wasie nae, wanamtamani, wanamthamini, wana muhitaji, sasa nauliza, huyu Magufuli ni mtu tuu wa kawaida au ni Nabii wa kweli wa Mungu aliyeletwa kwa Tanzania kwa ajili ya kutuokoa na kutukomboa?.
Rais Magufuli ni chaguo la Mungu!
Magufuli the real African Lion
Baeleseni Baitu Baelewe!.
P
 
Wanabodi,

Kila nipatapo nafasi, huwa naandika makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", makala hizi huwa zinachapishwa na magazeti mbalimbali, hivyo Wahariri kuweni free kuitumia makala yangu yoyote, na be free kui edit kwa kiwango chochote utakacho ona inafaa, maana hata mimi sitaki tena kuandika makala yoyote ya kuliponza gazeti lolote au Wahariri wake waitwe Dodoma au popote kuhojiwa na taasisi yoyote ikiwemo Kamati ya Bunge kwasababu za makala za Paskali Mayalla zenye kuhoji mambo magumu.

Makala zangu zote huandikwa kwa mtindo wa swali au maswali, kisha naweka hoja zangu, na kumalizia kwa lile lile swali, ili msomaji awe huru kusoma, kuelewa na kupata majibu mwenyewe, hivyo sitegemei tena kuitwa popote kuhojiwa na yeyote kuhusu maswali yangu ninayo hoji, ila ikitokea mtu yoyote una majibu yoyote, kuhusu swali langu lolote, ni ruksa kutoa majibu, (mfano lile swali nililouliza Je Bunge Linajipendekeza Kwa Serikali?, jibu lake lilikuwa rahisi tuu, "Bunge Halijipendekezi kwa Serikali).

Ile ule mtindo wangu wa kuuliza maswali magumu kwa viongozi, kwenye press conferences zao, au kwenye vipindi vyangu, bado unaendelea, natoa wito kwa viongozi wetu, msiogope maswali magumu ya waandishi wahojaji, na hata ikitokea ukaulizwa maswali magumu, na ukitokea huna jibu, uko free kutokujibu, uko free kunyamaza, au hata kumjibu mwandishi kitu kingine chochote tofauti na swali uliloulizwa.
( mfano, Swali: " Mkuu kiongozi, vipi kuhusu hili la...
Jibu: "Mayalla kwa kikwetu maana yake ni njaa)
Ni ni jibu tosha na sitauliza zaidi.

(By the way: siku ya Jumamosi ya kesho kutwa asubuhi kwenye kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari cha Star TV, nitakuwa live na Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndungulie kwa Dar es Salaam, Dodoma atakuwepo Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas, na Mwanza nguli Dotto Emanuel Bulendu kuizungungumzia Corona, huko ni maswali magumu, hakuna maswali rahisi)

Kwavile Corona ndio habari ya mjini duniani kote kwa sasa, mada yangu ya leo ya "Kwa Maslahi ya Taifa" pia itajikita mumo humo kwa kwa swali hili..."Kwa nini Nabii huwa hakubaliki nyumbani?!. Jee Rais Magufulini ni Nabii wa Mungu au ni mtu tuu wa kawaida?".

Nabii ni Nani?
. Nabii ni binaadamu au mtu yoyote anayeletwa duniani na Mungu kwa ajili ya kutimiza majukumu fulani. Nabii ni mtu mwenye maono fulani, kwa kesema maneno ya unabii yanayokuja kutokea au kutimia. Maona hayo huonyeshwa na Mungu kwa ajili ya kufanya kazi fulani ya Mungu, mfano wa Manabii ni kama Adam na Eva/Hawa, Ibrahimu, Mussa, etc. Tuna viongozi wengi wa dunia walioteuliwa na Mungu kama manabii akiwemo Mwalimu Nyerere.
Hata humu jf, tunao manabii kibao
TZ Tulipo Sipo!. Nabii Hakubaliki Nyumbani, JF Tuna Manabii wa Kweli, Tuwatumie Walisaidie Taifa!. - JamiiForums
(P'se Tofautisha Nabii na Mtume wa Mwenyeezi Mungu. Sijasema Magufuli ni Mtume, nimeuliza Magufuli ni Nabii?).

Maswali hayo yanafuatia, wakati kuna baadhi ya sisi Watanzania tunambeza rais Magufuli na serikali yake kwa baadhi ya hatua anazochukua kutatua changamoto mbalimbali zinazotukabili na kulikabili taifa letu, za kisiasa, kiuchumi na kijamii, ikiwemo changamoto hii mpya ya ugonjwa wa Corona, kuna baadhi yetu sisi Watanzania, tunambeza!. Wakati sisi tuna beza, kuna baadhi ya wenzetu wa bara la Africa wao wanamlilia rais Magufuli wakitamani rais Magufuli ndio awe rais wao kwa hatua ambazo rais Magufuli amezitumia kwa Tanzania kupambana na janga la ugonjwa wa Corona, zilizopelekea nchi ya Tanzania kuwa ni nchi ya kupigiwa mfano, huku wengine wakienda mbali zaidi kwa kutamani juhudi za kupambana na Corona kwa bara lote zima la Africa ziunganishe kujenga nguvu ya pamoja kupambana na janga la Corona na kutamani rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli ndie ateuliwe kwa kauli moja kuwa Kamanda Mkuu wa Bara la Africa katika kuongoza Mapambano dhidi ya janga la ugonjwa wa Corona kwa bara lote zima la Africa!. Wakati sisi huku tunabeza, hatuoni, hatutambui, hatuthamini thamani ya Magufuli tuliye nae, wenzetu wasie nae, wanamtamani, wanamthamini, wana muhitaji, sasa nauliza, huyu Magufuli ni mtu tuu wa kawaida au ni Nabii wa kweli wa Mungu aliyeletwa kwa Tanzania kwa ajili ya kutuokoa na kutukomboa?.

Tukiangalia kilichotokea China, kinachotokea Marekani, Utaly na nchi za ulaya, halafu tukiangalia jinsi nchi za Africa wakiwemo nchi majirani zetu wanavyo panic na kufanya lockdown, huku Rais Magufuli akiwaongoza Watanzania kwa kuwasisitiza tuzingatie ushauri wa kitaalamu wa jinsi ya kujikinga kwa kuzingatia usafi, kupunguza mikusanyiko, kuweka social distancing lakini oia kuwaambia Watanzania, Tusitishane, na Tusitishwe, kwa kinachotokea nchi nyingine, sisi tuendelee kuchapa kazi kama kawaida na Tumtegemee Mungu,

Msimamo huu wa rais Magufuli na Tanzania tunavyo deal na Corona, unaonekana kama tunacheza au tunatania kwa jambo serious kama hili.

Baada ya rais Magufuli kulihutubia taifa kuhusu Corona na kusisitiza tusitishwe, kesho yake akaonekana aki relax kwenye majabali ya Ikulu ya Chamwino, Ma critics wa Magufuli wakamuona kama mtu ambaye sio serious na hajui atendalo, walitaka atishike, agope, ababaike na kuwatisha Watanzania, hao critics kazi yao ni kubeza na kuponda kila kitu, as if waliombea hali kama ya China, Italy na Marekani ndio itokee Tanzania ili Magufuli ambuke kwa kutochukua hatua kali za tahadhari, kama majirani zetu.

Leo baada ya usingizi kukata, usiku mkubwa, katika pita pita yangu na mitandaoni nikakutana na hii kitu

The Good, the Bad and the Worse in Africa’s Anti Corona Crusades; Lesson from Tanzania - JamiiForums

Kumbe huku sisi Tanzania, tunamponda rais Magufuli anavyo deal na Corona, kumbe kuna wenzetu wanamtaka Rais Magufuli ndio awe rais wa Africa kwa kuongoza mapambano ya Corona the African Way, na Kuichulia nchi ya Tanzania iwe ndio nchi ya mfano wa mapambano haya kwa nchi nyingine kuiga hiki rais Magufuli alichokifanya, na jinsi Tanzania inavyo pambana na janga la Corona.

Hongera Sana rais wetu Magufuli, na serikali yako kwa hatua mnazochukua dhidi ya janga hili la ugonjwa wa Corona, ama kweli inawezekana kabisa wewe ukawa ni Nabii wa kweli kwa taifa letu Tanzania ambaye tumepewa na Mungu mwenyewe, kwa sababu Mungu aliyajua yote haya kuwa yatatokea kabla, hata hayajatokea na akatupatia mtu sahihi wa kutuvusha kwenye majaribu haya.

Ama kweli Nabii huwa hakubaliki nyumbani, kuna akina sisi Matomaso wa Tanzania, na humu JF tuna Matomaso wengi, ambao tulimbeza sana Magufuli, tangu ile 2014 wakati unabii wa Magufuli ulipowekwa humu
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli - JamiiForums

Lakini as times goes by baadhi ya maneno ya unabii ule yanakwenda yakifutika ila kuna mengine yanatimia moja baada ya jingine.

Hivyo inawezekana kabisa huyu Rais Magufuli ni mpango wa kweli wa Mungu kwa Tanzania?, Huyu ni mtu tuu au ni Nabii?. Mungu akisema YES, who would dare kusema No?!.

Kwenye hili vita ya Corona, Watanzania, tuweke tofauti zetu pembeni, tujiunge na rais wetu Dr. John Pombe Joseph Magufuli na serikali yake katika Mapambano dhidi ya janga hili la ugonjwa wa Corona, Together we can.

Mungu Mbariki Magufuli
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Africa
Nawatakia Alhamisi Kuu Njema.
Paskali
Update
Wanabodi, hili ni bandiko la swali kuhusu rais Magufuli kama jee ni Nabii?. Naomba mimi nisijibu,
msikilize Mhe. Dr. Mwigulu Nchemba wewe mwenyewe umsikie amesema nini kumhusu Rais Magufuli



P

Rejea za Paskali on Unabii.
  1. TZ Tulipo Sipo!. Nabii Hakubaliki Nyumbani, JF Tuna Manabii wa Kweli, Tuwatumie Walisaidie Taifa!. - JamiiForums
  2. Unaitwa nabii, nawe unachekelea? hatari sasa! - JamiiForums
  3. Mkuu Mzee Mwanakijiji, Rais Magufuli Sio Alfa na Omega. Rais Sio Mungu! Na Kwenye Utawala ni Katiba! - JamiiForums
  4. https://www.jamiiforums.com/threads...asiabudiwe-asiogopwe-bali-aheshimiwe.1023305/
  5. Angalizo kwa Wana JF: Tuwaepuke "Prophets Of The Doom", kauli zao huumba! - JamiiForums
  6. Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo! Adai yeye ni zaidi ya Rais... - JamiiForums
  7. "Nabii Kamuambukiza Mke wangu STD" - JamiiForums
  8. Mauaji ya Kisiasa, hali ngumu ya Uchumi na Utabiri wa TB Joshua juu ya hatima ya Tanzania - JamiiForums
  9. Pongezi Jeshi la Polisi. Japo Nabii hakubaliki nyumbani, Jeshi sasa ni Sikivu, Most friendly na very hospitable - JamiiForums
  10. Nabii Huwa Hakubaliki Nyumbani!, JK Ameanza Kukubalika?!. Watch ITV Leo Saa 3:45 Usiku Huu! - JamiiForums
  11. Nyakua Nyakitita: Mhadhiri DIT anayeokota makopo barabarani - JamiiForums
  12. Nabii Flora wa Mbezi Beach - JamiiForums
  13. TCRA: Vipindi vya Mahubiri Kwenye TV Pia Viangaziwe/Vithibitiwe!. Mungu Yupo Ila pia Shetani Yupo! - JamiiForums
  14. Angalizo: Kuna Wengi Wanamwabudu Shetani Wakidhani ni Mungu!. Jee Wewe Unajijua?, Jitambue!. - JamiiForums
  15. Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo? - JamiiForums
Rejea za Mandiko ya The Same Author Kuhusu Janga la Corona
  1. Mtu kama huyu ni binadamu au shetani? Anaombeaje Corona ifike Tanzania. Kuiombea nchi yako majanga, sio zaidi ya uendawazimu? Huu sio ushetani? - JamiiForums
  2. Corona: Japo ni janga, pia ni fursa. Tanzania bado hakuna maambukizi, tupunguze panic, tuongeze Elimu. WB kumwaga mihela, tuchangamkie fursa - JamiiForums
  3. Corona inatufundisha Tanzania tuna tatizo kuchanganya siasa na professionalism. Hongera Prof. Janabi kwa elimu uliyotoa, so far you are the best! - JamiiForums
  4. RC Makonda, Dar ni jiji la wote, vyama vyote. Mbowe sio mwanasiasa uchwara aliyefilisika, Zitto sio mshirikina. Tunakupenda, heshimu wote uheshimiwe - JamiiForums
  5. Je, ni kweli kuna Waziri anaugua Corona inafanywa Siri? Tunaficha nini? Hala hala kisa cha mficha maradhi! Truth & Transparency the only way out! - JamiiForums
  6. Star TV: Msemaji Mkuu wa Serekali, Dr. Hassan Abbas, azungumzia wajibu wa vyombo vya habari kuripoti janga la Corona - JamiiForums
  7. Ama kweli nabii hakubaliki nyumbani!. Je Magufuli ni nabii? Tanzania wanambeza, Afrika wanamlilia! Tanzania yapigiwa mfano Magufuli awe Rais wa Afrika - JamiiForums
  8. Vita Janga la Corona: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas, Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndungulile, kesho watakuwa live JLNH-Star TV - JamiiForums
  9. Star TV: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas na Naibu Wazuri wa Afya Dr. Faustine Ndungulile, Wanazungumzia Corona - JamiiForums
  10. Mungu ni Omnipresent. Kufuatia Local Transmission ya Corona. Je, Sasa Tushinikize Watu Wasalie Majumbani Mwao, ila Sadaka Ndio Itumwe Kwa M-Pesa? - JamiiForums
  11. Nabii Malisa: Mungu ameniambia Corona ni April tu, May hakuna Corona na hakuna atakayekufa!. - JamiiForums
  12. Kwa Kasi Sasa, Jee Tuendelee Ushujaa wa Ka-Corona, Tusitishane, Tuchape Kazi Tukiteketea, Au Sasa Tubadili Msimamo Tusitisishe Mikusanyiko Tuokoke? - JamiiForums
  13. TBC - Mjadala wa Role of The Media kwenye mapambano ya Corona, Je, Media Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo? - JamiiForums
  14. Live on Star TV: Corona Kushika Kasi Ndio Habari Kubwa Tanzania, Jee Media ya Tanzania, Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo? - JamiiForums
  15. Corona: Tusinyoosheane vidole. Kama unaweza kusaidia, please do. Usisubiri uombwe - jitokeze saidia, vinginevyo nyamaza! - JamiiForums

Wandugu, hapa nafanya tuu follow up ya Corona nikipitia kujikumbusha niliwahi kuandika nini au kusema nini kuhusu Corona na hiki kinacho endelea sasa. Corona is real tusifanye masihara, tujilinde kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

Kila Jumamosi asubuhi kuanzia saa 1:30 hadi saa 3:00 asubuhi , Star TV, huwa ninakuwa live kwenye kipindi cha TV cha Jicho Letu Ndani ya Habari ambacho huwa kinatangwa live na Star TV kila siku za Jumamosi asubuhi, kwa Jumamosi ya kesho, mgeni wetu ni Waziri wa Habari, Dr. Harrison Mwakyembe tukijadili kuhusu athari za Corona kwenye sekta ya Habari, nini kifanyike.

Ukipata nafasi karibu utufuatilie.

P
 
Jamaa anazidi kubamba, sasa sio Waafrika tuu, hadi Wazungu, Australia wanatamani Magufuli ndie awe rais wao.
IMG-20200516-WA0003.jpg
IMG-20200516-WA0002.jpg
IMG-20200516-WA0006.jpg
IMG-20200516-WA0059.jpg
IMG-20200516-WA0000.jpg
IMG-20200516-WA0005.jpg

P
 
Habari kama hizi zinaumiza sana Wapinzani (Chadema).Wanachopenda kusikia ni Rais magufuli kawa kituko huko duniani au kafeli jambo fulani.
 
View attachment 1452993
Approval chart ya Rais Magufuli inazidi kupanda, hapa ni Sweden wanamtamani awe rais wao@.
P

Naelewa kwamba nyuzi zinaanzishwa na kuletwa huku jukwaani kwa makusudi fulani.

Ninawaelewa wa ‘swede’ kama watu wenye ustaarabu wa hali juu uliojengwa juu ya utamaduni
imara wa miaka mingi.

Sidhani kama wana sababu yoyote ya kuhitaji kuongozwa na mtu yoyote nje ya utamaduni wao.

Hiyo si kusema kwamba baadhi yao hawawezi ku approve yanayofanywa na raisi wetu.
Wanadamu tupo wengi na akili zetu ni tofauti sana kati ya mtu mmoja na mwingine.

Balozi wetu huko anaweza kuleta hizo habari kama package ya PW ya kusifia. Hiyo ni sehemu ya kazi yake. Haina query.

Lakini kuichukua kama ilivyo na kujaribu kutumezesha kwa nguvu, hapana.

Mkuu P, that would be taking praise and worship to new dimensions.

Tuweni serious kidogo.
 
Naona umeamua kuonyesha rangi halisi.Wabongo saa nyingine huwa hamjielewi.Anasifika kwa lipi.Kusimamia miradi ya mikopo.Be serious.
 
Jana wakati Rais Magufuli akikabidhi kiti cha Uenyekiti wa SADC kwa Msumbiji, Rais Magufuli na Tanzania ilipongezwa na SADC kwa jinsi Rais Magufuli alivyoshughulikia vita vya Corona.

P
 
Back
Top Bottom