Ama kweli cha mtu Mavi, Ona jinsi Trump alivyomfokea na kumdhalilisha Netanyahu!

Ama kweli cha mtu Mavi, Ona jinsi Trump alivyomfokea na kumdhalilisha Netanyahu!

Niaje waungwa

Kitendo hili kimenikumbusha msemo wa mtegemea cha ndugu hufa masikini 🤣🤣🤣

Netanyahu si anajifanyaga ana file la Trump! Aliweke sasa hadharani tuone 🤣🤣🤣

Trump kamwaga mboga na yeye amwage ugali tuone.

Laiti Israel isingekuwa inategemea msaada wa silaha, jeshi na ulinzi kutoka Marekani, haya matusi yote na dharau visingemkuta Netanyahu.

Ona jinsi walivyoiingiza Marekani kwenye hasara kubwa ya vita.

1. Kambi zimeunguwa

2. Meli za kijeshi zimechomwa Moto

3. Ndege zilizokuwa zinasemekana hazionekana kwenye radar zimetunguliwa kama embe

4. Wanajeshi wameuwawa

5. Majeneral wakubwa wamejiuzulu

6. Hormuz imewashinda kuifungua

7. Iran imewashinda kukidhibiti

Halaf mtu kama Netanyahu anaambiwa aache kuendelea na vita Lebanon ili Iran isije tena kuanzisha mashambulizi kama ilivyopanga kufanya. Eti Neta anajifanya kumpuuza Trump. Kisha vita ikianza tena, gharama za vita abebe Trump na nchi yake, hiyo inaingia akili kweli? Unafikiri Trump mjinga kulazimisha mapatano ili vita iishe?

Sera ya Trump ya Make America Great Again imekufa kibudu, kutokana na hasara kubwa iliyoingia Marekani kwenye vita hiyo. Hivyo Netanyahu awe makini, na ajue vita hiyo inateketeza mamilioni ya kodi za Marekani bila sababu ya msingi.

Uzuri Trump ni kama hayati Magufuli. Akiwa na hasira huwa hachagui la kuongea, lolote linalokuja mdomoni ndo hilo Hilo, as long as ujumbe husika umefika.
 

Attachments

  • FB_IMG_1780384634247.jpg
    FB_IMG_1780384634247.jpg
    135.4 KB · Views: 8
Back
Top Bottom