Ama kwa hakika "Mtu Mlafi" hana kaburi

Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,772
8,958
MLAFI HANA KABURI (Greedy has no tomb)

Yaani hata sielewi nianzie wapi na nimalizie wapi maana muongo huu wa 2020 umekuja na mengi mazito yasotabirika utadhani mwali kashika mimba ya kwanza. Aso na macho haambiwi tazama maana matukio ya mwaka huu sii ya kuhadithiwa - Tulikuwepo na bado tupo..

Ni mwaka ambao tuliuanza kwa mbwembwe nyingi na majigambo ya kusherehekea shangwe za Decade, huku mdudu Korona akibisha hodi kuingia nchi za Asia na Ulaya ya Magharibi. Hammad fumba fumbua, mgeni huyooo kaingia mpaka chumbani leo Dunia nzima tunaweweseka kushikana ugoni Korona imetoka wapi?. Viongozi wa kila nchi wanapimwa Sifa zao kwa maamuzi wanayochukua dhidi ya gonjwa hili.

Leo hii tunautazama Uongozi bora kama sii Swala laa makuzi ya Uchumi na Maendeleo bali Maslahi ya watu, Kiongozi unawajali kiasi gani Wananchi wako. Umewafanyia nini kutatua matatizo yao, kufuta madhila na kero zao, sii kukalia kiti.kikubwancha IKULU. Hii inatuashiria Maendeleo ni UHAI na Mustakabali wa WATU sio NCHI, VITU wala MALI. UHAI wa watu umegeuza kabisa SIASA za nchi na maajabu zaidi ni kwamba kila Nchi na kila Kiongozi amepata majibu tofauti hata kama maamuzi yake yalishabihiana na nchi jirani.

Waswahili wanasema Tumlaani Sheitani, na kama Shetani akitusahaulisha, basi baada ya kutanabahi tusikae pamoja na wadhaalimu maana Ugonjwa kama huu umekuja wakati muafaka kabisa kwetu kutukbusha ya kwamba hakuna mbora zaidi yake Mola taala. Ni kama vile Mwenyezi Mungu ametupima IMANI zetu juu yake wakati Shetani ametawala mfumo mzima wa njia za maisha yetu.

UCHUMI umesimama, Dunia imeganda, walafi wa Mali ya Utajiri wamekuwa wadogo kama mchwa kwenye kifuu cha nazi. Maskini nao wanatembea kifua mbele kwaajivuno kwani maradhi kama haya ndio maisha yao toka nitoke - haiwapagawi. Ama kweli, Korona Shikamoo leo binadamu tupo sawa haina Tajiri wala Maskini sote tumerudi kwenye miti Shamba, maabara kubwa ya Mwenye kuumba. Limao lina hadhi Chroloquine.

Kisha, mbali na Korona, hivi nani alojua mwaka huu siri kubwa ya Ubaguzi wa rangi duniani kwa watu Weusi utajitokeza wanjawanja na kulaaniwa Dunia nzima? BLACK LIVES MATTER ilikuwa simulizi ya hadithi kwa wengi wakimtazama yule mcheza mpira wa Marekani akipiga goti wakati wimbo wa Taifa lao ukipigwa. Alionekana mhuni na kichaa fulani, wengine tukidhani Udhalimu wa askari Polisi upo Tanzania na Afrika kwa sababu wanakitumikia Chama tawala. Kumbe huko Ughaibuni ni Mfumo ulotakaswa kwa jasho na damu za watu. Lahaula Walakuwata!

Leo 2020, siri zinavuja kama mshumaa wa moto. Ubaguzi sii wa MTU bali Umetaribiwa Kimfumo. Na laukama Marekani ngome ya Walafi, isingekuwa na rais huyu pengine haya yote ya Uvunguni yasingetoka nje. Mwenyezi Mungu mkubwa na mjuzi wa yote kawaumbua. Wamarekani na sifa zote za Kidunia, leo wanaumbuka kama wanga Uchi wa.mnyama wametua juu ya paa mchama kweupe.

Nikirudi Tanzania yangu, mwaka huu nawakuta WALAFI walokuwa na mpango wa Kijasusi kumuondoa rais Magufuli kwa njama za kisiasa. Kama sii Magufuli nani alijuwa kama Uongozi wa CCM miaka ya nyuma ulikuwa na kulipana Fadhila? Wao wakisema kupeana vijiti kumbe ndani yake kulikuwa na siri kubwa wakiita Utaratibu. Ama kweli Zimwi likujualo halikuli likakwisha. Baba lao kaweka nadhiri - Adui wa Maskini ni adui wake.

Angalia basi, kabla ya Uchaguzi wa Mwaka 2015, yalizuka makundi ndani ya Chama, ndani ya Serikali hadi Usalama wa Taifa ndio nasema mimi hii baada ya kubainika kwamba Kikwete hakutaka katu kumpisha Lowassa kutokana na mipango ya Uhaini iloandaliwa mapema dhidi yake. Narudia kusema Ulafi hauna kaburi, vua gamba vaa gwanda ilikuwa chanzo cha mageuzi ya mwelekeo wa Chama cha Walafimlakini ndaninya msafara wa Mamba, Kenge nao wamo wakitafuta hifadhi chini ya Lowassa wakiamini safari ya wengi, maji hayapo Mbali.

Anyway, tuachane ya nyuma. Wanasema yalopita sii ndwele, Mwaka huu jicho la 20/20 limewaibua viongozi wakipanga njama za kumuondoa Magufuli ilihali ni kundi lile lile lilopangua ngome ya Lowassa 2015. Binadamu? Kwa nini haturidhiki. Yaani sitosahau jeshi la Membe dhidi ya Lowassa kabla ya Uchaguzi. Ya Leo hii ati nasikia kuna vita ya kiti cha Ikulu baina ya Membe vs Magufuli..

Yaani najaribu kuchanganua siri nyuma ya matarajio ya Membe hata siioni. Lakini haishangazi tena kujua wale wale wamemgeuka mteule wao kwa sababu Magufuli amewageuka, amekana kulipa Fadhila. Nakumbuka ile hotuba ya rais akisema Uchaguzi wa 2015 hakuchangiwa na MTU...ile Haikuwa bure, bila Shaka alikuwa akichomekea majibu kiulaini.

Ujio Mwezi wa 10 hii sii kama vita ya Membe vs Lowassa.. bali ni Membe vs Magufuli. Hivi kweli Mfupa ulomshinda Lowassa, Membe atauweza au ndio akili ya kuambiwa changanya na zako. Inajulikana wazi wakati kundi lile likiendelea kutafuta Wajumbe ndani na nje ya CCM Mpya, Msukuma wa Chato chale zilimcheza mapema akamrudisha Lowassa chamani, mara pap mzee wa nyeti ndani ya CCM Mpya. Ujio wa Lowassa kurudi CCM ni kama vile dole gumba kubinya kwenye kidonda! Iliwashtua wengi wa Upande ule, wengine wakajishusha kuwa wadogo wakaomba radhi mapema wakijua - YAJAYO YANAFURAHISHA..

Huoni jinsi CCM wanavyomuogopa Lissu na Mbowe hata baada ya kuwavunja miguu?
 
Daah yaani Chama kinamuogopa MTU? Ifike wakati vijana achaneni na MTU tazama Taasisi. Chadema ni Taasisi, ACT ni Taasisi hata wakiondoka Mbowe, Lissu, Zitto bado Vyama hivyo vitashindana. Hizi imani za Lissu kuogopwa ilihali hawa wote wamevikuta vyama na hakuna anayeweza shindana na Magufuli leo hii. Huo Ubunge pekee tia maji, leo unazungumzia Chama?!!
 
Kiongozi ni muhimu sana mkuu, leo hii mtu akimpiga magu nondo akatoweka utaona jinsi ccm itakavyobadilika na jinsi unafiki utakavyopungua. Lissu anajulikana ni mwiba mkali wa kufichua mambo ya ccm na jiwe kiasia ambacho jiwe alijua huyu akiwepo ni shida. Mtu ni muhimu sana haina mjadala.
 
Kwakuwa Magufuli anaweza kutumia madaraka yake kunajisi uchaguzi, ndio maana umeingia upofu na kuamini unachoaminishwa. Unaamini fika hakuna anayeweza kushindana na Magufuli, kwakuwa madictator wote hujenga hofu ya kimfumo, na taasisi zote hutii kilichopangwa, hali hii ndio imepelekea ww kuandika hii makala yako ya ngano za kiswahili.
 
Kiongozi ni muhimu sana mkuu, leo hii mtu akimpiga magu nondo akatoweka utaona jinsi ccm itakavyobadilika na jinsi unafiki utakavyopungua. Lissu anajulikana ni mwiba mkali wa kufichua mambo ya ccm na jiwe kiasia ambacho jiwe alijua huyu akiwepo ni shida. Mtu ni muhimu sana haina mjadala.

Hivi Hawa Fisimaji wa CCM wanaelewa Magufuli anaposema CCM YA MAGUFULI au Serikali ya Magufuli? Huwezi kutengenisha MTU na TAASISI please....tusidanganyane bhana.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom