Ama jengo livunjwe ama Mitambo ihamishiwe mbali

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,890
Habari ambazo ninazipata hapa zinasema kwmaba ile mitambo ya kuzalisha umeme ya MW 100 juzi bada ya kufungwa na kuwashwa pale Ubungo imepelekea jengo la Tanesco kutaka kuja chini .Wataalam wameamua kuzima machine na hizo na sasa wanashauri kuihamishia mitambo hiyo mbali na pale .Wana hofia gharama ni kubwa sana ama wavunje jengo la Tanesco ambalo wanasema itakuwa gharama kubwa .

Kwa kuwa hizi ni tetesi tu basi naamini wako watu hapa wanazijua hizi habari kwa undani tafadhali waje watupe yaliyo jiri hapo Ubungo na mitambo hiyo kutaka kula jumba la tanesco .
 
mtu ananua mtambo wa umeme kama ananunua machungwa unategemea nini?
labda walifikiri huo mtambo watauweka hewani.
 
Ni Tetesi Kwa Hio Ni Bora Kuipeleka Kunakohusika

Mtu wa Pwani I just used the neno tetesi niko kazini na kwa kawaida JF wako kazini pia so iachwe hapa naomba sana .Wewe pita uende kwenye mada zingine .Nyie ndiyo hao hao tunasema mnatuvuruga .
 
Hata na mimi nimeshaipata hii issue. Inafaa iwe ni breaking news na wenye habari zaidi watuletee.
  1. EIA nafikiri ilifanyika je riport yao ilipitishwaje na ni nani walioifanya?
  2. Habari nilizonazo mimi ni kuwa Mitambo mipya ya Tegeta ya Tanesco ilishapigiwa kelele kuwa inatetemesha ardhi, sasa ilikuwaje hii ya Ubungo ikafungwa tena katikati ya Mji bila kuangalia hili?
  3. Kama ni kuhamisha majengo itabidi isiwe la Tanesco peke yake, ila na wale wote waiojenga nyumba zao karibu na hii mitambo itabidi nao wahamishwe, including ofisi za TBS, idara ya Maji na Chuo chake n.k, n.k.
Hii habari inatakiwa ifike magazetini na kujadiliwa katika kikao cha bunge kinachoendlea, maan nchi sio ajabu ikaingia tena gizani.
 
Hata na mimi nimeshaipata hii issue. Inafaa iwe ni breaking news na wenye habari zaidi watuletee.
  1. EIA nafikiri ilifanyika je riport yao ilipitishwaje na ni nani walioifanya?
  2. Habari nilizonazo mimi ni kuwa Mitambo mipya ya Tegeta ya Tanesco ilishapigiwa kelele kuwa inatetemesha ardhi, sasa ilikuwaje hii ya Ubungo ikafungwa tena katikati ya Mji bila kuangalia hili?
  3. Kama ni kuhamisha majengo itabidi isiwe la Tanesco peke yake, ila na wale wote waiojenga nyumba zao karibu na hii mitambo itabidi nao wahamishwe, including ofisi za TBS, idara ya Maji na Chuo chake n.k, n.k.
Hii habari inatakiwa ifike magazetini na kujadiliwa katika kikao cha bunge kinachoendlea, maan nchi sio ajabu ikaingia tena gizani.Kubwa Jinga fika Ubungo utapata habari zote .Sasa wanataka ku cover up lakini sisi tumesha inyaka nakuimwaga hapa .Watu wa magazeti wafike huko wapata ukweli maana machine zime zimwa kwa kasheshe lake
 
Kubwa Jinga fika Ubungo utapata habari zote .Sasa wanataka ku cover up lakini sisi tumesha inyaka nakuimwaga hapa .Watu wa magazeti wafike huko wapata ukweli maana machine zime zimwa kwa kasheshe lake

Mkuu Lunyungu,
Bahati mbaya niko mbali sana na Ubungo kwa leo hii. Lakini kiukweli ni kuwa hii site ya ubungo haifai kutumika kwa ajili ya kuzalishia umeme. Kwanza ni pa-dogo mno na ni hatari kwa raia.

Lakini waTZ tumezoea sana kuburuzwa na wageni maana wataalamu wetu wengi nao hawajayaona haya madudu zaidi ya kuyasoma tu kwenye vitabu. Ukichanganya na uvivu wa kufikiria au ukosefu wa muda kwa sababu ya kufukuzia shilingi, basi matokeo yake ndio haya, tunarundika kila kitu hata pasipofaa.

Ni vema wana JF walio karibu na Ubungo na waandishi wa habari wakafika hapo Tanesco Ubungo na kuhoji waliopo ili angalau waanzishe/kukomaza mjadala maana umeme ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa.
 
Kuna ushauri mizuri sana ya kitaalamu katika bandiko la Jengo lililobomoka hapo Bongo ambayo inaweza kutumika katika kutafuta suluhisho la kadhia hii...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom