Ama hakika TAKUKURU mmenishangaza kweli kweli na huu unafiki wenu usiovumilika kwa watu makini nchini

Mzukulu

JF-Expert Member
Feb 14, 2020
1,411
2,000
Kuna Taarifa nimezisoma katika Gazeti la Habari Leo Ukurasa wa Tatu na Gazeti la Majira Ukurasa wa Nne zikisema kuwa TAKUKURU sasa ndiyo wamegundua na wanaanza Kulivalia Njuga Suala zima la Rushwa za Ngono Mashuleni na hasa hasa Vyuo Vikuu. Kwa Lugha nyepesi tu yaani hapa TAKUKURU wanataka Kutuambia kuwa hili Jambo halijawahi kuwafikia Masikioni mwao hapo kabla?

Labda na mimi pia niwaombe tu hawa TAKUKURU kabla ya Kulivalia hili Njuga nao watuhakikishie je, na Kwao Ofisini Rushwa hii ya Ngono haipo?

Hivi inaingia Akilini kweli kama Mimi Mzukulu nimeanza Kusikia Shutuma hizi za Rushwa ya Ngono miaka hiyo ya 90 huko na wao wanajua Leo hii?
 

kunze

JF-Expert Member
Nov 22, 2016
379
500
Heri nusu Shari kuliko lawama,kama wamemua kuchukua hatua sasa,bado unalalamika na kama wakikaa kimya,unalalama...wapeni nafasi ili kuona TIJA yao,usiwe mwepesi wa kulaumu,ova
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
4,299
2,000
Rushwa ya ngono inagusa makundi mengi sana kwenye jamii. Na huu ndiyo ukweli. Tukiamua kupambana basi tusichague baadhi tu ya maeneo. Tuguse sehemu zote.
 

Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
7,416
2,000
Takukuru kama taasisi ndio inazinduka sasa, watendaji wake nina uhakika walilifahamu, kulishuhudia na pengine kushiriki rushwa ya ngono, popote walipopitia masomoni au katika ajira.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom