Aluta kontinyua: Watani wa jadi 3 sisi 0


M

mzee wa wau

Member
Joined
Oct 4, 2010
Messages
21
Likes
2
Points
0
M

mzee wa wau

Member
Joined Oct 4, 2010
21 2 0

Hii nimeikuta kwenye blog moja maarufu hapa nchini.Wadau kama hamjaiona itupieni macho.

Mkuu wa kaya napenda kuleta malalamiko rasmi kwa serikali yetu na kuwataarifu watanzania wenzangu jinsi wakenya wanavyopata kazi kinyemela hapa nchini na kuwafukuza watanzania ili hatua zipasazo zichukuliwe haraka maake vinginevyo watanzania wote wataishia kuwa wamachinga tu ! Huu ni uchunguzi wangu tangu soko huria lianze julai mosi mwaka huu

This will show how Kenyans are hypocritic and a nuisance to Tanzanian's development!

Ikumbukwe kwamba lengo la soko huru lilikuwa ni kufungua milango ya uwekezaji na ufanyaji kazi kwenye eneo letu la Afrika Mashariki kwa kuondoa vikwazo visivyo vya lazima na mpaka sasa makubaliano ni kwamba wananchama wa nchi 5 za Afrika Mashariki wanaweza kufanya kazi kwenye nchi yoyote ila kwa hapa kwetu wageni lazima waombe vibali vya kufanyia kazi wanapopata kazi hapa kwa muda wa miaka 5 ijayo ambapo vitaondolewa kabisa.

Hivyo Mkenya, Mganda,Mrundi,au Mrwanda akija hapa akipata kazi kihalali ataomba kibali uhamiaji . Ikumbukwe kuwa wenzetu Wakenya walianza ubepari zamani hivyo si ajabu ni nchi ya 2 kufanya biashara kwa wingi na Tanzania baada ya Uingereza hivyo pia tunategemea wakenya wengi wawepo kufanya kazi Tanzania lakini kwa kushindanishwa na wazalendo .

Cha ajabu mzee ni kwamba hawa wenzetu badala ya kutumia ushindanishi unaotakiwa sokoni kwa kuangalia vigezo na uwezo wa mtu wao wameanza kutumia propaganda,mizengwe na mbinu nyingine chafu za kuwaondoa watanzania kwenye nafasi zao na kuwapa wakenya.

Utakuta mtu anapewa kazi kwenye kampuni ya kikenya then anapigwa zengwe kuwa utendaji wake ni mbovu na kesho yake analetwa mkenya hata kama mtanzania ni mzuri kwa vigezo vyote au pia kuna kazi zinahitaji training kwao hawatakupa hiyo training kwa makusudi ili ionekane huwezi kazi wamlete mkenya!

Mbinu nyingine wanayotumia wanakupeleka training kwao Nairobi labda mwezi mzima na huku nyuma wanamleta mkenya anafanya kazi zako kisha wewe ukimaliza training unaambiwa hukufikia vigezo wanavyotaka hivyo ujiuzuru au wakufukuze kazi au watakutafutia kisa chochote tu hata cha maisha yako binafsi yasiyohusiana na kazi yako halafu unatishiwa kuwa watakufukuza au ujiuzuru nwenyewe! Kisha wanaenda uhamiaji kumwombea kibali mkenya wao wakitoa sababu kuwa mtanzania waliyemweka ameshindwa kufikia vigezo wanavyotaka

Wadau hizi ni baadhi ya mbinu tu wanazotumia hawa wenzetu kunyakua kazi wa watanzania kwa nguvu ! Kuna mifano mingi na watu wengi wameathirika na hizi mbinu chafu za wakenya hivyo naona muda muafaka umefika wa mamlaka husika kufanyia kazi hili jambo!

Tunaelewa kuwa Kenya maisha ni magumu sana ndo maana wanakimbilia huku kutafuata kazi wakati hakuna watanzania waliofanikiwa kupata kazi Kenya kwa kuomba tu kwenye makampuni ya Kikenya ukiacha wanaopelekwa na makampuni nya kimataifa yaliyopo Tanzania . Hii ni kwasababu Wakenya wana dharau sana (Kenyans are very arrogant) kwa mataifa mengine ya Afrika Mashariki na wanajiona wao wanajua kila kitu. Hii imesababisha hata wao kwa wao wabaguane kimakabila hivyo kampuni ya Mkikuyu huwezi kumkuta Mjaluo au Mkamba ! hiki ndo chanzo cha wao kuuana mwaka juzi baada ya uchaguzi wao maake kule kwao wanaishi kwa mbinu za msituni (survival of the fittest) .

Hata hapa kwetu wafanyakazi wengi walio chini ya mabosi wakenya wanadharauliwa na kunyanyaswa kisa ni watanzania hata kama wana uwezo kuwazidi hao wakenya !

WATANZANIA TUFANYEJE
Ningependa kuwashauri wadau wanapokutana na hali hii wasikae kimya na kusubiri mungu awasaidie . wajue kwamba huu ni mpango maalum ambao wenzetu wamekuja hapa kupokonya ajira za watanzania hivyo tuchukue hatua madhubuti ambazo ni pamoja nazifuatazo:
-hakikisha kila unapofanya kitu kizuri ofisini kwako bosi wako anajua .Hii itakusaidia sana wakati wa kureview performance yako kazini . wenzetu wanaijua sana kuitumia mbinu hii inayoitwa corporate politics! Akifanya jambo dogo tu lazima amwambie bosi wake hivyo kujilinda pakitokea tatizo baadaye.

Watanzania tusikae kimya kusubiri bosi wako aone mwenyewe kuwa wewe unafanya kazi vizuri sana ! mfuate bosi mweleze mafanikio yako kazini na sio kujificha bosi akipita koridoni oooh utakula wa chuya !

Pili tuhakikishe tunazijua sheria za kazi vizuri na sio kutishiwa tishiwa tu na hawa wakenya wakati nchi ni yetu bwana ! tujenge utamaduni wa kusoma haki zenu ndani ya sheria ya kazi ili likitokea jambo tuweze kujitetea ipasavyo. Japokuwa sheria zenyewe zina mapungufu kwa mfano mwajiri anapewa uhuru wa kuchagua akurudishe kazini au akuachishe kazi na kukulipa mshahara wa miezi 12 tu ! sheria ibadilishwe hii !

Tatu tujifunze bargaining skills wakati wa kuomba kazi maake utakuta wengi wetu mishahara ni midogo sana kwani wakati wa kuomba kazi tunamwachia mwajiri ajipangie mshahara wa kukulipa matokeo yake hata ukimpeleka mahakamani atakulipa vijisenti vya miezi 12 na kukufukuza kazi huku nafasi yako akipewa Mkenya na kulipwa kama expatriate.

Nne tungependa vyombo vinavyohusika na kutoa vibali vya kazi kwa wageni (hasa wizara ya mambo ya ndani, wizara ya kazi na professional bodies ) vijiridhishe kweli hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kufanya kazi ambayo kibali kinaombwa. Hivi kweli jamani hatuna wahasibu wa kutosha mpaka Mkenya aje awe management account (mhasibu wa ndani) au financial controller (mhasibu mkuu ) hapa Tanzania wakati NBAA wanatoa CPA mara 2 kwa mwaka ! hawa vijana wanaomaliza hizi qualification watafanya kazi gani sasa ? Tuachane na njaa za muda na utamaduni wa kuabudu wageni ! Tuamini wazalendo na kuwajengea uwezo wa kufanya kazi .

Tano watanzania tubadilike tujenge attitude ya kujituma kazini maake soko la kibepari ndo linavyotaka ! ukiwa mvivu kazini wakenya watazidi kuja na kuchukua nafasi zetu nasisi tutaishia kulalamika tu ! hivi sasa mabenki makubwa 3 madirector wao ni Wakenya ! mshahara wa director mmoja tu unatosha kuwalipa watanzania zaidi ya 20 wa ngazi za chini na hapo bado hujazungumzia wenzao waliowaleta toka Kenya na vitu wanavyonunua kwa makampuni yaliyo Nairobi hata kama kuna makampuni ya Tanzania yanazalisha kitu hicho hicho maake bosi ndo mwamuzi !

Naomba kuwakilisha
Mdau aliyetendwa na wakenya !!
 
Sijali

Sijali

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2010
Messages
2,106
Likes
492
Points
180
Sijali

Sijali

JF-Expert Member
Joined Sep 30, 2010
2,106 492 180
Wjinga ndi waliwaooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo!
 
3D.

3D.

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2010
Messages
1,022
Likes
9
Points
0
3D.

3D.

JF-Expert Member
Joined Sep 7, 2010
1,022 9 0
Mdau umeongea mambo ya maana sana hapa.
 
Bongolander

Bongolander

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2007
Messages
4,882
Likes
61
Points
135
Bongolander

Bongolander

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2007
4,882 61 135
Mdau umeongea mambo ya maana sana hapa.
Unachosema ni kweli. Mdogo wangu anafanya kazi na kampuni ya wakenya kila mara analalamika kuwa huwa anatukananwa na kukaripia kama mtoto kila mara. Lakini amini kuwa hata ukisema hakuna litakalotokea, sababu kuwa wanaonyanyaswa si viongozi wetu ni sisi hohehahe so no one will care.
 

Forum statistics

Threads 1,236,193
Members 475,029
Posts 29,249,316