Aluta Continua - Wananchi wafanya kweli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aluta Continua - Wananchi wafanya kweli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Idimi, Oct 13, 2007.

 1. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2007
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Kutoka gazeti la Nipashe

  Serikali ya kijiji Nyankumbu yavuliwa uongozi

  2007-10-13 08:37:59
  Na Renatus Masuguliko, PST Geita

  Uongozi wa Serikali ya Kijiji cha Nyankumbu, Wilaya ya Geita akiwemo Mwenyekiti wake, John Lunyaba, wamevuliwa uongozi baada ya kukataliwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji.

  Viongozi hao walikataliwa mbele ya uongozi wa wilaya kwa tuhuma za kushindwa kuwajibika na ubadhirifu wa zaidi ya Shilingi milioni moja.

  Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kalangalala, Bw. Hamadai Husein, alisema hatua hiyo ni halali kwa vile taratibu zote za kisheria zilizingatiwa na kuwa Mkutano Mkuu wa kijiji ambao uliwashirikisha zaidi ya wanakijiji 500, una mamlaka ya kutoa uamuzi kama huo.

  Uamuzi wa kuivunja serikali ya kijiji, ulifikiwa baada ya kubainika kuwa, wajumbe wa serikali ya kijiji ambao ndio wenye mamlaka kisheria kusimamia utekelezaji wa kila siku na uendeshaji iikiwemo kusimamia na kulinda mali ya kijiji wamekuwa wanashirikiana naye na kumlinda badala ya kumwajibisha.

  Aliongeza kuwa hatua hiyo ilifikiwa mbele ya Bw. Jackson Sombe, mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bw. George Marco alisema ameridhia utaratibu uliotumika wa kuwang�oa madarakani viongozi hao.

  Awali, katika mkutano huo uliokuwa umeitishwa rasmi kujadili matatizo ya muda mrefu kuhusu uongozi wa kijiji hicho, kumekuwepo na malalamiko dhidi ya serikli ya kijiji hicho kutowajibika.

  Pia uongozi huo umedaiwa kushirikiana na Mwenyekiti wa kijiji na baadhi ya wajumbe kufuja fedha za kijiji.

  Kwa mujibu wa taarifa ya Mkaguzi wa Halmashauri ya wilaya iliyothibitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya, Bw. Dani Mollel, ilibainika kuwa, Mweyekiti wa kijiji anatuhumiwa kutafuna zaidi ya Shilingi milioni moja.

  Fedha hizo ni pamoja na zilizotokana na malipo ya boma la kijiji, viingilio, na mradi wa uchomaji tofali.
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Oct 13, 2007
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Haya sasa mbona hizi ni TUHUMA na zimehalalishwa bila ushahidi, tena basi na hukumu imeshatolewa na viongozi wanaodai ushahidi ktk maswala ya Taifa.
  Ni wakati gani haswa maamuzi ya wananchi huwekwa mbele ya uteuzi wa viongozi?
   
 3. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2007
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Heshima Kwako Mkuu;

  Ni zilikuwa tuhuma, zikapelekwa kwenye mamlaka husika (mkutano mkuu wa kijiji) na idadi ya wajumbe umeiona, nadhani watugtumiwa wakapewa muda wajitetee, kama katiba inavyotaka, wakasema hawawataki viongozi waliochaguliwa,,, Halmashauri ya Wilaya ikaweka baraka zake, In fact mimi nimeona hawa jamaa ni matured sana kuliko hao akina... This is good governance scenerio.... Kurusha mawe kwa namna yoyote ni uhuni tu!


  Maoni yako nayaheshimu mkuu, maana mimi na wewe ni sawa sawa na kichuguu na mlima kilimanjaro,,, uko juu mzee.. lakini niruhusu sehemu chache chache niwe tofauti nawe.
   
 4. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Duh Tanzania Tanzania................inaliwa na wenye meno makali, kweli wanaipenda kwa moyo kutokana na kuneemeka bila jasho, kutegemea jasho la wengine. Sasa wavuja jasho wameshituka na wao wanataka malipo yao halali. Kazi ipo!
   
 5. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2007
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Baada ya kutimuliwa kazi ni wakati wa kuwafungulia mashitaka ya wizi na ubadhirifu. Ili waonje tamu ya chungu
   
 6. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2007
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Heshima mbele mkuu Kilitime.
  Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100 kuwa hawa Watanzania wenzetu wametumia katiba na taratibu halali kuwavua uongozi watuhumiwa. Kweli wao ni mature, kwa maana ya kwamba jinsi walivyowaweka madarakani viongozi wao ndivyo hivyo walivyowatoa. Nasema ni watuhumiwa kwa sababu hakuna mahakama iliyokaa kuwahukumu viongozi wao. Wangengoja mahakama huenda kesi hii ingechukua hata miaka kuhukumiwa, kwa mazingira ya vyombo vyetu vya kutoa haki. Kama demokrasia hii itaendelea hadi ngazi za wilaya na mikoa nina uhakika tutafika mbali, kwani sisi ndio tunaowaajiri, kwa hiyo tuna mamlaka ya kuwaondoa katika ajira viongozi wasiowajibika.

  Madilu, ni kweli kuwa sasa iwe ni wakati mwafaka kwa hawa watuhumiwa kupelekwa kunako mahakama ili wasafishwe ama wapatilizwe.
   
Loading...