ALUTA-CONTINUA ACADEMY. (A.C.A)

Kwa kuongezea anzisha na paper( series) labda kila jumamosi.
Utavuna madogo sana .
Nakumbuka enzi zetu tulikuwa tunapiga Paper za pure Tandika kwa muhunzi na Mwenge mapambano.
Kuna madogo am sure washamaliza topic naw wanakuja likizo kupiga paper za kutosha .
 
Hatua nzuri.

Ushauri wangu, jaribu kufanya utafiti kuhusu walimu maarufu wa hesabu za Advance waliopo mjini(Mchikichini, Mwenge, Temeke) akina Mwalami, Muhunzi n.k halafu utengeneze programu ambayo ni tofauti na wao ili uvutie wanafunzi.

Asilimia kubwa watu wanaelekeza wadogo/watoto wao waende Mchikichini kwa Mwalami, Temeke kwa Muhunzi au Mwenge maana -ao ndio waliozoeleka sana.

Jitahidi usambaze vipeperushi mapema mashuleni kabla shule hazijagungwa ili wanafunzi wawe washapata taarifa yako.

Tengeneza vipeperushi vya kutosha, tafuta mtu avisambaze shule kubwa za mjini(Azania, Tambaza, Jangwani, Benja, Kibasila, Loyola, Pugu, Minaki) . Vipeperushi vikiwafikia hao na wao watawapasha marafiki zao wengine wa mikoani wanaotarajia kuja kusoma tuit huku mjini.

Hakikisha kazi unaipiga kwa umahiri wa hali ya juu kulingana na uwezo wako, hakuna litakaloshindikana.

Mwanzo ni mgumu, usife moyo, ukipata hata wanafunzi watano piga pindi....
Nashukuru sana mkuu MWIFA

Kuhusu hao walimu wengine nalifanyia kazi nakuahidi kwa hilo

Upande wa vipeperushi kusambaza shule zingine bado sina connection (si unajua mjini bila connection mambo hayaendi)

Ila matangazo nafanya sana na ntafanya sana

Ila sitaanza na wanafunzi wa tano kwasababu watu wengi imewafikia na washaanza kuwasiliana na mim, sio chini ya 20
IMG_20190525_092346.jpg
 
Ndugu A-LUTA CONTINUA ACADEMY

Hongera kwa ulipofikia hadi sasa.

Mytake
- Ili ujumbe huu kwenye (posti ya kwanza) uwafikie Walengwa / wanafunzi / walezi wengi zaidi, Fanya yafuatayo

1. Fungua Instagram account
2. Weka post moja, kisha
3. Ifanyie promo kwa kulipia

Sababu walegwa wa rika hilo (Wanafunzi ) asilimia 95 wana insta / facebook account, hivyo watapata ujumbe kwa haraka sana, ila jiandae uwe na eneo la kutosha sambamba na walimu mahili.

==========
Update
- Anzia hapa hapa JF ku_promote hii thread yako, na hakika matokeo utayaona, wasiliana na JamiiForums au Maxence Melo wakupe utaratibu.

Kila lakheri
Ntalifanyia kazi mkuu, acha kwanza nianze na huu Uzi
 
Kwa kuongezea anzisha na paper( series) labda kila jumamosi.
Utavuna madogo sana .
Nakumbuka enzi zetu tulikuwa tunapiga Paper za pure Tandika kwa muhunzi na Mwenge mapambano.
Kuna madogo am sure washamaliza topic naw wanakuja likizo kupiga paper za kutosha .
Sawa mkuu huo ushauri ntazidi kuetekeleza
Miezi mitatu nyuma hadi sasa nshatoa sana series za maths paper I
Ukiangalia vizuri apo kwenye zingatia, yeah kuna kipengele cha series paper II, najua pure mathematics bila kufanya mitihani bado haujafanya kitu
IMG_20190525_093226.jpg
 
MAPINDI YANAANZA TAR. 3/6/2019 KWA KIDATO CHA TANO WANAOINGIA KIDATO CHA SITA, WITO KWA WANAFUNZI WOTE WAHUSIKA KARIBUNI SANA. PIA IWAFIKIE MZAZI/MLEZI WENYE VIJANA WENYE UHITAJI HUO. SHARING IS CARING. welcome

IMG_20190525_093226.jpg
 
Two days to go,
Mathematical freedom, no more stress. Am going to convince the world that mathematics was born Africa, developed america and finalized Europe

My advice. "Forget about six packs English figure, your kids deserve parents who will help them to solve integration and complex numbers"
IMG_20190531_212651.jpg
 
Kwa wanafunzi wa A-level tu ( kidato cha 5 & 6 )
Katika somo la ADVANCED MATHEMATICS
(PCM, PGM, EGM)

MAHALI
Centre ipo buguruni rozana mtaa wa bahatisha, usawa wa dereva tax kama unaelekea bondeni mtaa wa pili mkono wa kulia

Kwa wazazi/walezi mliokua na vijana wenu wanaohusika na ADVANCED MATHEMATICS, Niwakaribishe kwa kuwahakakishia maendeleo kwa kijana wako

Wanafunzi wanaochukua ADVANCED MATHEMATICS katika michepuo yao, MNEGRO THE GREAT kwa uhakika wa ufaulu wako

BEI NI NAFUU SANA KULINGANA NA HALI ZA UCHUMI NA PIA BEI NI KULINGANA NA TOPIC HUSIKA,


"UPDATES" ZOTE ZITAKAZO HUSIANA NA A.C.A ZITAPATIKANA HAPA

SAMBAZA KWA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI
MATHEMATICS SIO TENA UGONJWA WA TAIFA

Nakaribisha ushauri, mawazo au aina yoyote ya mawazo katika kujenga

View attachment 1105540
blessed mkuu,,,hakika elimu ndiyo maarifa
 
Leo tena, siku nyingine tena. A-LUTA CONTINUA ACADEMY chini ya MNEGRO nipo katika kushirikishana mawili matatu
KWANZA kabisa niwashukuru wale wote niliofanya nao kazi katika likizo hii iliyopita na wale wazazi walioniletea vijana wao, niseme tu ASANTENI KWA KUJA
PILI, niwaambieni tu harakati zinazidi kuendelea yaani kuisha kwa program ndio kuanza kwa program nyingine
TATU, natoa wito kwa ndugu jamaa na marafiki na walezi wote wenye vijana ambao kwa namna mmoja au nyingine wana uhitaji wa mathematics. Mimi ndio suluhisho
Ambapo kwa kipindi cha likizo japo nafundisha kwa pesa lakini wengi walitokea kunishukuru kana kwamba nafundisha bure na wengine wakiniahidi kwenda kufanya mapinduzi
 
Kuna mambo mengi nayaweka sawa na projects nyingi naziandaa lakini changamoto hazijawai kuisha
Mbele yenu naombeni msaada wa mawasiliano ya shule zifuatazo, JITEGEMEE, ROYAL, SHABAN ROBERT, AIR WING, GREEN ACRE, ISLAMIC, ST. ANTONY, ST. MARY, MBEZI HIGH SCHOOL, MAKONGO, MAMA SALMA
Shule nyingi za serikali tayari nina access nazo. Wakuu hapo naombeni msaada pm itakua vizuri zaidi

Mara moja moja nikiingia humu jf huwa naona mijadala mingi ya msingi kujenga na kimaendeleo bila kusahau ujinga na upumbavu hivyo vyote katika kufanikisha maisha yanaenda
Lakini huyu member anaeenda kwa jina Kiranga , huwa ananipa maswali mengi na majibu tofauti tofauti juu ya uwepo wa Mungu.
Nikitulia nilikua naomba mjadala kuhusu uwepo wa Mungu mimi nikitumia elimu dunia hasa hasa mathematics na concept za science lakini tu awe kiwango kizuri cha elimu akiwa na uelewa wa pure mathematics
Ntamthibitishia uwepo wa mungu kwa mathematics sanjari na science kwa ujumla
 
Back
Top Bottom