Alumni- are you going to fit in or are you going to to change the situation? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alumni- are you going to fit in or are you going to to change the situation?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by m_kishuri, Mar 26, 2011.

 1. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  WADAU, katika pilikapilika za maisha, nimemefanyikiwa kupita kwenye University ya MACMASTER (ON-Canada). Kwenye Library yao ya Health Science nimekutana na kibao chenye ujumbe ufuatao:
  THE CLASS OF MEDICINE 1999 HAS PLEDGED THEIR SUPPORT TO THE HEALTH SCIENCES LIBRARY OF MACMASTER UNIVERSITY.

  "MAY THIS GIFT FURTHER THE EDUCATION OF STUDENTS AT MACMASTER FOR YEARS TO COME AND INSPIRE THEM TO SUPPORT THEIR UNIVERSITY."


  Ujumbe huu umenifanya nijiulize maswali kadhaa kuhusu mchango wa wanajamii wenzangu kwenye shule na vyuo tulivyopitia katika maisha yetu, haswa vyuo kama Mlimani, Sokoine, Mzumbe, n.k. Na hii haswa inatokana na sababu kwamba inapotokea mtu akakisema vibaya chuo fulani, mfano Mlimani au Sokoine, basi malumbano yanakuwa makali. Lakini swali ni je, unatoa mchango gani kuboresha hali ya wadogo zako uliowaacha pale. Kwa msisitizo zaidi, kama alivyosema Mr. Jay Naidoo, the former minister in Mandela first Gov. katika hutuba zake kwamba, Are you going to fit in or change the situation?
  Watanzania wengi, ikiwemo humu jamvini ni wepesi kulalamika kuhusu kuanguka kwa hali ya elimu nchini, lakini nadhani ni wachache sana ambao wanafanya mambo kwa vitendo ili kurekeisha hali hiyo. Mchango wako (kwa kiasi uwezacho kwenye shule yako ya zamani) unaweza ukawa chachu kubwa ya maendeleo ya elimu nchini.
  Ntakubaliana na wengi kuhusu suala la rushwa na matatizo mengineyo ya uzembe, lakini TECHNOLOGY imeturahisishia mambo kuliko hapo awali. Hivi je, MAALUMNI watano wa darasa la 1995 kutoka Faculty ya engineering pale mlimani hawawezi kujitolea kununua vitabu kadhaa, au kulipia online journals na publications ili ziweze kuwasaidia wenzao katika research zao? Au hata kubadilisha zile printer na computer wanazotumia wadogo zako kwenye ile faculty yako ya zamani, je hili haliwezekani?
  Kwa wale ambao tayari wanafanya haya, natoa hongera na shukrani za dhati. Lakini kwa wale ambao tunakalia kulalamika tu kuhusu kushuka kwa ELIMU Tanzania, si vibaya kama tukiamua ku-change the situation badala ya kufit in.
  http://hotbuzznews.net/role-of-alumni-in-higher-education/
   
 2. Smarter

  Smarter JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2011
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 455
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  it is a challenge to us all, we can start with secondary schools.....primary as well
   
 3. D

  Dkipisi Member

  #3
  Mar 26, 2011
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ahsante kwa ujumbe mwanana. Hakuna ubishi kwamba kwa hilo tuko-nyuma (karne ya 16 pengine). Nimeona pale UDSM walianza akina Mchechu (Business school) kisha majuzi Mzee Warioba ameongoza jahazi la chuo kizima. BWM alitoa changamoto nafikiri miaka miwili ilopita kwenye chuo chake cha Makerere ambako nao wako mbele kiasi.

  Ninachohisi ni kwamba pale tunapokuwa vyuoni inakuwa kana kwamba ni mpito tu (transition). Hatutulii maanani 'sustainability' ya taaluma zetu kwa siku za usoni. Hata vyuo vyenyewe havina mwamko wa kumfanya mtu 'aringie' uwepo wake na atakapoondoka. Hivi ukiangalia chuo chako leo utataka mwanao aende? Hilo ndo la kujiuliza na kuamua. Naafiki ushauri wako kwamba maneno yaishe, vitendo vianze kwa udogo huo huo tuwezavyo kila mmoja wetu na kwa umoja wetu. Ahsant
   
 4. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145

  Swadakta Smater, huko ndipo kunapohitaji mkazo mkubwa kwani huko ndipo MABONZO yanapoanzia.

   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,199
  Trophy Points: 280
  Hili bonge la thread, nilishawahi kuuliza swali hili kitambo.

  Lakini kama nilivyo suspect, wadau kuwapata hapa kazi.
   
 6. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Asante kwa hizo habari za kutia moyo ijapokuwa juhudi za wakina Warioba zinakuja miaka dahari baada ya kuondoka pale Mlimani. Kuhusu suala la kujivunia chuo au elimu uliyopata kwangu mimi silitilii maana sana kwani siamini kwamba miaka 3 au 4 uliyokuwepo pale chuoni haikuwa ya mafanyikio wala ya kujivunia. Na hii haswa inatokana na ukweli wa kwamba kati ya Watanzania milioni 42, ni chini ya asilia 5 tu ndio wenyewe University Degree (SINA UHAKIKA).

  Hivyo basi, popote ulipoipata hiyo degree yako ( Mlimani, Sokoine, Muhimbili, Mzumbe, Ardhi, au Huria) bado upo mbali sana kulinganisha na Watanzania wengine, na hivyo kukupa haki ya kuwa PROUD na Elimu yako na Chuo chako bila kuangalia mtazamo wa watu wengine kuhusu Chuo chako.
   
 7. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145

  Nakubaliana na wewe Mkuu KIRANGA. The so called Thinkers ukiwakea mada kuhusu mke wa jirani ananitamani, au mama mkwe ananitega, hapo utachoka mwenyewe na comment utakazozipata, lakini kwenye mambo ya elimu hakuna anayetaka kujadili au kufuatilia. Ni juzi tu tumejionea matokeo ya AIBU YA O-LEVEL, na kila mtu alikuwa na lakusema. Lakini je, as thinkers tunafanya nini kuwakwamua wadogo wetu badala ya kulaumu? Au ni halo tunangoja mpaka wafadhili waje kutufanyia?

   
Loading...