Altare ya Wawekezaji - Tanzania isitoe Sadaka!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,461
39,928
Kwa miaka 15 sasa Taifa letu limeendelea kuhangaika na jambo moja muhimu, uwekezaji. Eneo la kwanza ambalo lilitusumbua mwanzoni mwa utawala wa Rais Mkapa katika uwekezaji ni dhana mpya kabisa ya Ubinafsishaji ambao kimsemo ulikuwa unaenda kinyume na Utaifishaji.

Wakati dhana ya Utaifishaji (nationalisation) kimsingi ilikuwa ni kuweka njia kuu za uchumi mikononi mwa Taifa, dhana hii mpya ya ubinafsishaji ingawa kwa lugha ya kimombo iliitwa "privatization" lakini kwa kiswahili neno hilo maana yake haijapatikana sawasawa. Inaonekana neno Utaifishaji linatafsirika kama kufanya kitu mali ya mtu binafsi hivyo "binafsisha" na siyo kufanya njia za uchumi kutokuwa mikononi mwa serikali. Lengo la mabadiliko ya sera hiyo ilikuwa ni kuweka njia hizi mikononi mwa sekta binafsi na siyo mikono binafsi ya viongozi, rafiki zao au ndugu zao.

Tumehangaika na hili kiasi kikubwa na kilele chake kilikuja pale ambapo waliamua kui"binafsisha" Benki ya Taifa ya Biashara ambapo ililazimu malumbano na mgongano wa kifikra wa wazi utokee. Sababu kubwa ya kuingia sera ya Ubinafsishaji kama ilivyoelezewa katika Sera za CCM ya Miaka ya 1990 ilikuwa ni kubinafsisha mashirika ambayo yana hasara na ambayo serikali haiwezi kuyabeba tena. Tatizo la NBC ni kuwa halikuwa shirika la hasara!

Hata hivyo uwekezaji ukaingia matatani zaidi hasa baada ya kufungulia "ubinafsishaji" kwenye sekta ya madini na hivyo kufanya mojawapo ya vyanzo vya mapato ya kitaifa kuwa mikononi mwa watu binafsi. Matokeo yake leo hii ukiondoa machimbo ambayo tayari yameanza kazi, kuna leseni zaidi ya 30 ambazo zimetumika kuruhusu uchunguzi wa madini mbalimbali nchini. Hadi hivi sasa karibu asilimia 100 ya uchunguzi wote umerudi na majibu chanya! Ukiondoa utata wa mafuta, leseni nyingine zote zinaonesha matokeo mazuri.

Tatizo linalotukabili ni kuwa hadi hivi sasa bado hatujaweza kutengeneza mazingira, sheria, na taratibu za kuhakikisha kuwa Taifa linanufaika na wananchi wananufaika na madini yao. Malalamiko yanayotokana na masuala ya mikataba ya madini ambayo yamelalamikwa kwa kirefu mwaka huu ni ushahidi tosha kuwa aidha sisi hatuna watu makini au sisi watu wa bei ya chini mno.

Kuendelea kufanya maamuzi ya kisiasa, kuunda kamati, kujadili Bungeni n.k hakujaweza kubadilisha bahati yetu kwenye madini na ninaamini sababu moja kubwa ni kuwa bado hatujawa majasiri kufanya maamuzi madhubuti na ya makusudi.

Hofu moja ambayo watawala wetu wanayo ni kuwa kwa kufanya maamuzi mazito, ya lazima na ya msingi watawaogopesha "wawekezaji" na hivyo watakimbia kwenda sehemu nyingine (kana kwamba na madini nayo yatakimbia). Ni kutoka na hofu hiyo isiyo na msingi Tanzania tunaambiwa inaongoza kwa "mazingira mazuri ya uwekezaji" a.k.a mazingira ya uchumaji wa mali ya Taifa kwenda makampuni ya kimataifa.

Ni kwa sababu hiyo naamini kabisa kuwa Kamati hii ya Madini endapo itakuja na mapendekezo yoyote ambayo hayatakuwa madhubuti, magumu, na ya msingi basi tutaendelea kulalamikia uwekezaji katika sekta ya madini kwa muda mrefu ujao. Binafsi, naamini kuwa baadhi ya mapendekezo ambayo yatainua mioyo ya Watanzania yanaweza kufanana na haya:

a. Kusitisha mara moja Uchimbaji wa madini katika migodi mikubwa hadi pale Madiliko ya Sheria ya Madini ya 1998 yapatishwe na mikataba yote ijadiliwe upya; asiyetaka afunge mgodi na kuondoka. Period.

b. Kutengeneza sheria ya mapato na kitengo/vitengo vya mapato ya madini katika TRA ili kuhakikisha kuwa yeyote anayezalisha analipa kodi ya mapato siyo lazima asubiri faida. Utaratibu huu ni wa ajabu kwa sababu mfanyabiashara mdogo anayeanza kabiashara kake analipa kodi zinavyotakiwa bila ya kujali gharama za mtaji wake au uwekezaji wake na hawezi kusubiri hadi apate faida ndiyo aanze kulipa. Vinginevyo sheria ya msamaha wa kodi iweze kutumika kwa "wamachinga" na wawekezaji wadogodogo.

c. Matukio ya Ujambazi kwenye migodi yawe somo na kuhakikisha kuwa vikosi vya Polisi vyenye uwezo wa kijeshi vinakuwa karibu na migodi yote mikubwa na vyenye uwezo wa kufika eneo la migodi ndani ya dakika 10 ya tukio lolote. Hivyo, usalama wa migodi na maeneo yanayozingira ni muhimu kabisa.

d. Katika mabadiliko ya sheria ya madini jambo kubwa ambalo linahitajika ni kupunguza madaraka ya Waziri mwenye dhamana ya madini na kuhakikisha baadhi ya maamuzi muhimu yafanywe na Kamisheni ya Madini badala ya mtu mmoja. Na hata yale maamuzi ya Waziri yawe na uwezo wa kutengeliwa na Kamisheni pale inapobidi.

Mabadiliko mengine ni kutunga sheria inayolazimisha full disclosure ya wawekezaji wote na hasa Financial Statements zao. Na jingine ni kuhakikisha kuwa hakuna kampuni itakayopewa tenda za nishati au madini ambayo haina financial statement za sekta hiyo, haijawahi kufanya mradi mkubwa, na ambayo inamilikiwa na mtu mmoja!

e. Kuwahakikishia na kuwajulisha wale wote ambao wana leseni za utafiti kuwa uchimbaji wowote ule utaongozwa na sheria mpya ya Fedha (siyo ile ya 1973) na pia sheria mpya ya madini as ammended.

f. Kwa upande wa madini ya Tanzanite, serikali itengeneze mfumo ambapo madini yote yanayochimbwa yanaweza kuwa traced back kwenye mgodi gani na machimbo gani. Katika kufanya hivyo, jinsi madini hayo yanasafirishwa na kuuzwa nje lazima ijulikane ili kukomesha uuzwaji wa madini haya kiholela! Naamini hata haya ya Tanzanite tunaweza kusitisha kwa muda ili kuyapa thamani zaidi; mbona wenye mafuta huwa wanaongeza mapipa au kupunguza. Kama sisi ndiyo wenye madini hayo pekee, tunaweza kusitisha kwa muda ili kumanipulate bei (its part of the game!). We didn't invent the game, and we didn't make the rules, we are just players (M. M. Original).



Hayo ndiyo mawazo yangu, na ninaomba mawazo yenu mkijaribu kujibu swali ni mapendekezo gani kutoka kamati hii mpya ya madini yatawapa moyo kuwa hatimaye serikali inataka kuokoa sekta hii na kuwanufaisha wananchi wengi?
 
G. Kwa sababu kiasi cha madini kinachopatikana Tanzania ni kikubwa basi serikali ijenge Kituo cha kusafishia madini yote Tanzanite, Gold, diamond badala ya kupeleka nje na Kuwepo na soko hapa nchini.

H. Kuzuia Mara moja upelekaji wa udongo kwa makontena nje ya nchi, ikilazimika hivyo basi lazima ipitie Dsm port maana ndio kuna scanner kubwa za kukagua container. Pia watu wa TBS na Idara ya madini Mlimani washirikishwe kukagua hiyo soil sample
 
Hivi hili la udongo mwenzenu bado sijalielewa, inakuwaje in lay man terms? Yaani wameuchimba udongo na wanajua una madini, au wamechimba udongo toka eneo lenye madini na wataenda kuangalia mbele ya safari?
 
Hivi hili la udongo mwenzenu bado sijalielewa, inakuwaje in lay man terms? Yaani wameuchimba udongo na wanajua una madini, au wamechimba udongo toka eneo lenye madini na wataenda kuangalia mbele ya safari?

Mkjj, wanachimba udongo sehemu zenye madini, wanajua zina madini, na tunajua zina madini. Udongo waliouchimba wanatoa kiwango kadhaa cha madini kwa kisingizio kuwa hicho ndiyo kinaweza kuchambuliwa kwa teknolojia ya uchambuaji madini tuliyo nayo nchini. Masaliyo yote yanawekwa kwenye makontena na kusafirishwa nje ya nchi kwa madai kuwa huko kunateknolijia za kisasa zaidi za kuchambua masalio ya madini kwenye udongo huo.

Sasa, hatuwezi kukataa ya kuwa ni kweli teknolojia wanayo na ile ya kwetu ni duni... lakini sasa, katika maisha ya Mtanzania lini tutaweza kumudu mazingira yetu wenyewe, katika ukusanyaji wa kodi na katika uchimbaji madini.. iwapo masalio ya madini katika huo udongo ni ya kuleta utata, maana hatuwezi jua kiwango kinacho chujwa nchini kuwa ni kidogo kuliko kile kinachochujwa nje au laa.


Kingine, nchi yetu kwa jinsi ilivyo barikiwa na madini na mikataba ya muda mrefu inayowekwa hivi sasa...baada ya muda si tutajikuta karibu nchi nzima imebakia kuwa HANDAKI...

Naungana na Bowbow hapo juu kuwa vituo vya kisasa vya kusafisha madini na ufuaji vijengwe hapa nchini. Hawa wawekezaji kama wanataka faida basi wachambue na kufua madini yao hapa hapa ili kodi na faida itokanayo na madini ijulikane vizuri.

SteveD.
 
Steve, kama hivyo ndivyo ilivyo; pendekezo la Bowbow, ni la makini sana. Ina maana mchanga ukishatoka sisi hatujui kiasi cha madini kinachopatikana au vipi? Na nchi gani nyingine duniani inayosafirisha mchanga wa madini kwenda nje?
 
Hivi hili la udongo mwenzenu bado sijalielewa, inakuwaje in lay man terms? Yaani wameuchimba udongo na wanajua una madini, au wamechimba udongo toka eneo lenye madini na wataenda kuangalia mbele ya safari?

Wanajua madini yamo, lakini wanadai hakuna vifaa na utaalam wa kuchambua udongo pembeni, na madini safi pembeni. Teknologia yake ni rahisi, na walishaambiwa wajenge uwezo huo hapa hapa nyumbani; lakini wanakaidi kwa vile wanazibiwa njia zao za wizi huu mkubwa.

Mkjj, hiyo (a)hapo juu usiitegemee kwa mikataba hii iliyokwishaanza kufanya kazi. Njia pekee ya kuwarudisha huko ni kumpata Chavez wa Tz, ambaye hatunaye. Usitegemee kabisa hilo kufanyika katika serikali hii iliyopo, au ya CCM yoyote!

Hata hivyo, bado siamini kamwe kuwa uundwaji wa kamati hii unalo lengo tunalolitegemea wengi. Wajumbe wanaweza wakafanya kazi nzuri katika kamati hiyo, lakini sina imani kuwa mengi yatatekelezwa, na ninaamini kuwa wananchi hatutayajua mapendekezo ambayo yanakinzana na maslahi ya wakubwa na wahanga wa sekta hii.

Kaytika mapendekezo:Ninapendekeza mikataba yote iwe wazi, na bunge liwe na nafasi ya kuijadili bila ya pingamizi.
 
M.Mwanakijiji

Kipengele (b) Kinachotakiwa hapa ni serikali kupitia wizara zake (fedha ikiwalisha TRA pamoja na Madini kuwa na kitengo maalum on weekly and monthly basis kuchukua taarifa ikiwa ni pamoja na surprise visits kwenye migodi hiyo kukagua na na kuhakiki taarifa hizo, Pia kuwe na kitengo cha inteligencia kwenye migodi hiyo.

Jinsi ya kufanya naaamini serikali wajanajua. Mfano inaweka sheria lazima mgodi uwe na servialance kamera both ndani ya jengo na nje ili kurahisisha ulinzi at the same time serikali inaweka watu wake kwenye hizo post na inaweza kukataa kutoa permits kwa watu ambao watataka kuchukua hizo nafasi na vitu vingine(hii ni njee ya mada)

Serikali ianzishe utaratibu wa kulebal madini yake kuonyesha hii ni product ya Tanzania ili nchi kama kenya inayoongoza kwa kuuza tanzanite wakati haina hayo madini itakoma. Kama ikitokea kampuni yeyote inauza nje bila label yake inajulikana ni smuglling na wachimbaji wote wanawajibishwa kisheria kutoka na kuinyima serikali mapato
 
Bowbow, hiyo ya mwisho ni muhimu sana, na siyo kwenye madini tu bali hata kwenye mazao mengine. Kati ya vitu vinavyoyanyima mazao yetu soko ni kushindwa kutrack yanatoka wapi. Hadi pale mtu aliyeko Detroit atakapoweza kununua embe toka Tanzania na likiwa na sumu wanaweza kurudi nyuma (back tracking) hadi kwenye shamba na mwembe lililotoka, ndipo tutaweza kufaidika na kilimo chetu. Haya ya kwenda kununua mahindi tandale halafu hujui yametoka wapi kwenye biashara ya kimataifa hayana nafasi tena.

Vivyo hivyo kwenye madini.
 
Mwanakijiji,
Nimeona nitumie mapendekezo yako kupanua zaidi mapendekezo yangu na hoja moja au mbili!

“a. Kusitisha mara moja Uchimbaji wa madini katika migodi mikubwa hadi pale Madiliko ya Sheria ya Madini ya 1998 yapatishwe na mikataba yote ijadiliwe upya; asiyetaka afunge mgodi na kuondoka. Period.”

Mimi naamini wapo ambao watasema hatuna nguvu kisheria([sic]) na mie huyohuyo najiuliza Uzalendo ndio nini…brightly, majibu ninayopata yameinua moyo wangu na kama mtanzania hiyo (a) hapo juu ndio nguvu yenyewe ya Uzalendo, bila kuonekana pinduani, kura ya maoni kitaifa ifanyike uamuzi wa watu ndio itakuwa sheria yenyewe. Hii iangaliwe kwa makini nasisitiza…Kura ya maoni ya kitaifa- uamuzi ndio nguvu na sheria yenyewe.

Hoja…
Lakini kusitisha mara moja si ndio kutakachotukosea hata hiyo kidogo inayokusanywa kama kodi?


“d. Katika mabadiliko ya sheria ya madini jambo kubwa ambalo linahitajika ni kupunguza madaraka ya Waziri mwenye dhamana ya madini na kuhakikisha baadhi ya maamuzi muhimu yafanywe na Kamisheni ya Madini badala ya mtu mmoja. Na hata yale maamuzi ya Waziri yawe na uwezo wa kutengeliwa na Kamisheni pale inapobidi.”

Hoja…
Sio ujinga kuuliza. Hivi hiyo dhamana si inaweza ikaulizwa bungeni literally! Hizo kamati za bunge zinafanya nini? Yaani wapi check-n-balance? Nafikiri hata zitto aliona hivi au ndio kamati za bunge na bunge hazina nguvu?



“Mabadiliko mengine ni kutunga sheria inayolazimisha full disclosure ya wawekezaji wote na hasa Financial Statements zao. Na jingine ni kuhakikisha kuwa hakuna kampuni itakayopewa tenda za nishati au madini ambayo haina financial statement za sekta hiyo, haijawahi kufanya mradi mkubwa, na ambayo inamilikiwa na mtu mmoja!”

Ni utamaduni wetu, siasa na jinsi tunavyoendesha biashara ndio umetufanya tudumae.! Mimi napendekeza tuangalie (*)International Accounting Standards Committee(IASC) and the Harmonization Of International Acounting and Reporting Standadrds hapa mtaona ni jinsi gani tumedumaa na kusababisha mashimo kwenye Financial Statements Disclosures ambazo kwa namna moja au nyingine imekuwa advantage ya wawekezaji.

“f. Kwa upande wa madini ya Tanzanite, serikali itengeneze mfumo ambapo madini yote yanayochimbwa yanaweza kuwa traced back kwenye mgodi gani na machimbo gani. Katika kufanya hivyo, jinsi madini hayo yanasafirishwa na kuuzwa nje lazima ijulikane ili kukomesha uuzwaji wa madini haya kiholela! Naamini hata haya ya Tanzanite tunaweza kusitisha kwa muda ili kuyapa thamani zaidi; mbona wenye mafuta huwa wanaongeza mapipa au kupunguza. Kama sisi ndiyo wenye madini hayo pekee, tunaweza kusitisha kwa muda ili kumanipulate bei (its part of the game!). We didn't invent the game, and we didn't make the rules, we are just players.”

Hii nakupa big up…na vilivile itolewe changamoto kwa maprograma wa kitanzania kuwa na state of the art database management system ambayo itaweza kusaidia katika hii ‘traced back’! COSTECH maybe?

"Ni mapendekezo gani kutoka kamati hii mpya ya madini yatawapa moyo kuwa hatimaye serikali inataka kuokoa sekta hii na kuwanufaisha wananchi wengi?"

Kwa kweli mapendekezo kutoka kwenye kamati yawe ya Uzalendo!. I think this could be a catalyst to (*)uncertainty avoidance culture among many Tanzanians. It will flag a true new beginning for the future of our children’s social-political and economic stability not just in Tanzania but also used as a model to true economic independence of Africa. The use of natural resources to alleviate poverty is not a new trend, but does it redistribute wealth? only if used in conjunction with redistributing wealth does it stand as an alleviator but-The trend now is to use natural resources (read minerals) to build infrastructure (and other Ufisadi use) without redistributing wealth. Among other fear of repercussion of World War III is Natural Resources and its allocation.Beware!
All and all -Tanzanite ndio tuanze nayo! We have more than, more of a bargaining power over this. Kamati lazima iiangalie hii kwa makini na upewe kipaumbele.


Nyongeza...Je uzalendo utaendana na MALENGO MUHIMU NA MISINGI YA MWELEKEO WA SHUGHULI ZA SERIKALI? ([sic]).


(*)source:Internationa Financial reporting and Analysis(Haskin’s,Ferris,Selling)
 
Wazee mimi naomba huu ukurasa mwatumie hao wa husika wa kupitia mikataba. Mwana kijiji mtumie Zitto hapa naon kuna point nzuri sana alizotoa Bowbow kwenye poest # 2

--------------------------------------------------------------------------------

G. Kwa sababu kiasi cha madini kinachopatikana Tanzania ni kikubwa basi serikali ijenge Kituo cha kusafishia madini yote Tanzanite, Gold, diamond badala ya kupeleka nje na Kuwepo na soko hapa nchini.

H. Kuzuia Mara moja upelekaji wa udongo kwa makontena nje ya nchi, ikilazimika hivyo basi lazima ipitie Dsm port maana ndio kuna scanner kubwa za kukagua container. Pia watu wa TBS na Idara ya madini Mlimani washirikishwe kukagua hiyo


Kama serikali inavyojenga Export processing zones nadhani hili lakujenga kiwanda cha kusafishia ni muhimu sana hata kama litagharimu pesa. mapendekezo hayo hapo juu nimeyapenda sana.


Mwana kijiji kwenye interview zako hebu uliza kuhusu huu utaratibu wa kusafirisha udongo wetu ni kwanini, ni wa nini, unaenda wapi na kwa faida ya nina.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom