Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,391
- 39,484
Kwa miaka 15 sasa Taifa letu limeendelea kuhangaika na jambo moja muhimu, uwekezaji. Eneo la kwanza ambalo lilitusumbua mwanzoni mwa utawala wa Rais Mkapa katika uwekezaji ni dhana mpya kabisa ya Ubinafsishaji ambao kimsemo ulikuwa unaenda kinyume na Utaifishaji.
Wakati dhana ya Utaifishaji (nationalisation) kimsingi ilikuwa ni kuweka njia kuu za uchumi mikononi mwa Taifa, dhana hii mpya ya ubinafsishaji ingawa kwa lugha ya kimombo iliitwa "privatization" lakini kwa kiswahili neno hilo maana yake haijapatikana sawasawa. Inaonekana neno Utaifishaji linatafsirika kama kufanya kitu mali ya mtu binafsi hivyo "binafsisha" na siyo kufanya njia za uchumi kutokuwa mikononi mwa serikali. Lengo la mabadiliko ya sera hiyo ilikuwa ni kuweka njia hizi mikononi mwa sekta binafsi na siyo mikono binafsi ya viongozi, rafiki zao au ndugu zao.
Tumehangaika na hili kiasi kikubwa na kilele chake kilikuja pale ambapo waliamua kui"binafsisha" Benki ya Taifa ya Biashara ambapo ililazimu malumbano na mgongano wa kifikra wa wazi utokee. Sababu kubwa ya kuingia sera ya Ubinafsishaji kama ilivyoelezewa katika Sera za CCM ya Miaka ya 1990 ilikuwa ni kubinafsisha mashirika ambayo yana hasara na ambayo serikali haiwezi kuyabeba tena. Tatizo la NBC ni kuwa halikuwa shirika la hasara!
Hata hivyo uwekezaji ukaingia matatani zaidi hasa baada ya kufungulia "ubinafsishaji" kwenye sekta ya madini na hivyo kufanya mojawapo ya vyanzo vya mapato ya kitaifa kuwa mikononi mwa watu binafsi. Matokeo yake leo hii ukiondoa machimbo ambayo tayari yameanza kazi, kuna leseni zaidi ya 30 ambazo zimetumika kuruhusu uchunguzi wa madini mbalimbali nchini. Hadi hivi sasa karibu asilimia 100 ya uchunguzi wote umerudi na majibu chanya! Ukiondoa utata wa mafuta, leseni nyingine zote zinaonesha matokeo mazuri.
Tatizo linalotukabili ni kuwa hadi hivi sasa bado hatujaweza kutengeneza mazingira, sheria, na taratibu za kuhakikisha kuwa Taifa linanufaika na wananchi wananufaika na madini yao. Malalamiko yanayotokana na masuala ya mikataba ya madini ambayo yamelalamikwa kwa kirefu mwaka huu ni ushahidi tosha kuwa aidha sisi hatuna watu makini au sisi watu wa bei ya chini mno.
Kuendelea kufanya maamuzi ya kisiasa, kuunda kamati, kujadili Bungeni n.k hakujaweza kubadilisha bahati yetu kwenye madini na ninaamini sababu moja kubwa ni kuwa bado hatujawa majasiri kufanya maamuzi madhubuti na ya makusudi.
Hofu moja ambayo watawala wetu wanayo ni kuwa kwa kufanya maamuzi mazito, ya lazima na ya msingi watawaogopesha "wawekezaji" na hivyo watakimbia kwenda sehemu nyingine (kana kwamba na madini nayo yatakimbia). Ni kutoka na hofu hiyo isiyo na msingi Tanzania tunaambiwa inaongoza kwa "mazingira mazuri ya uwekezaji" a.k.a mazingira ya uchumaji wa mali ya Taifa kwenda makampuni ya kimataifa.
Ni kwa sababu hiyo naamini kabisa kuwa Kamati hii ya Madini endapo itakuja na mapendekezo yoyote ambayo hayatakuwa madhubuti, magumu, na ya msingi basi tutaendelea kulalamikia uwekezaji katika sekta ya madini kwa muda mrefu ujao. Binafsi, naamini kuwa baadhi ya mapendekezo ambayo yatainua mioyo ya Watanzania yanaweza kufanana na haya:
a. Kusitisha mara moja Uchimbaji wa madini katika migodi mikubwa hadi pale Madiliko ya Sheria ya Madini ya 1998 yapatishwe na mikataba yote ijadiliwe upya; asiyetaka afunge mgodi na kuondoka. Period.
b. Kutengeneza sheria ya mapato na kitengo/vitengo vya mapato ya madini katika TRA ili kuhakikisha kuwa yeyote anayezalisha analipa kodi ya mapato siyo lazima asubiri faida. Utaratibu huu ni wa ajabu kwa sababu mfanyabiashara mdogo anayeanza kabiashara kake analipa kodi zinavyotakiwa bila ya kujali gharama za mtaji wake au uwekezaji wake na hawezi kusubiri hadi apate faida ndiyo aanze kulipa. Vinginevyo sheria ya msamaha wa kodi iweze kutumika kwa "wamachinga" na wawekezaji wadogodogo.
c. Matukio ya Ujambazi kwenye migodi yawe somo na kuhakikisha kuwa vikosi vya Polisi vyenye uwezo wa kijeshi vinakuwa karibu na migodi yote mikubwa na vyenye uwezo wa kufika eneo la migodi ndani ya dakika 10 ya tukio lolote. Hivyo, usalama wa migodi na maeneo yanayozingira ni muhimu kabisa.
d. Katika mabadiliko ya sheria ya madini jambo kubwa ambalo linahitajika ni kupunguza madaraka ya Waziri mwenye dhamana ya madini na kuhakikisha baadhi ya maamuzi muhimu yafanywe na Kamisheni ya Madini badala ya mtu mmoja. Na hata yale maamuzi ya Waziri yawe na uwezo wa kutengeliwa na Kamisheni pale inapobidi.
Mabadiliko mengine ni kutunga sheria inayolazimisha full disclosure ya wawekezaji wote na hasa Financial Statements zao. Na jingine ni kuhakikisha kuwa hakuna kampuni itakayopewa tenda za nishati au madini ambayo haina financial statement za sekta hiyo, haijawahi kufanya mradi mkubwa, na ambayo inamilikiwa na mtu mmoja!
e. Kuwahakikishia na kuwajulisha wale wote ambao wana leseni za utafiti kuwa uchimbaji wowote ule utaongozwa na sheria mpya ya Fedha (siyo ile ya 1973) na pia sheria mpya ya madini as ammended.
f. Kwa upande wa madini ya Tanzanite, serikali itengeneze mfumo ambapo madini yote yanayochimbwa yanaweza kuwa traced back kwenye mgodi gani na machimbo gani. Katika kufanya hivyo, jinsi madini hayo yanasafirishwa na kuuzwa nje lazima ijulikane ili kukomesha uuzwaji wa madini haya kiholela! Naamini hata haya ya Tanzanite tunaweza kusitisha kwa muda ili kuyapa thamani zaidi; mbona wenye mafuta huwa wanaongeza mapipa au kupunguza. Kama sisi ndiyo wenye madini hayo pekee, tunaweza kusitisha kwa muda ili kumanipulate bei (its part of the game!). We didn't invent the game, and we didn't make the rules, we are just players (M. M. Original).
Hayo ndiyo mawazo yangu, na ninaomba mawazo yenu mkijaribu kujibu swali ni mapendekezo gani kutoka kamati hii mpya ya madini yatawapa moyo kuwa hatimaye serikali inataka kuokoa sekta hii na kuwanufaisha wananchi wengi?