RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Wapiganaji wa al-Shabaab nchini Somalia wameikamata bandari ndogo katika jimbo lenye madaraka ya ndani la Puntland, ishara ya karibuni ya kundi hilo la itikadi kali kuimakrisha harakati zake katika nchi hiyo ya upembe wa Afrika.
Gavana wa eneo la Mudug la jimbo la Puntland Hassan Mohamed amesema wanamgambo wa al-Shabaab wakiwa na maboti kadhaa waliukamta mji wa Garad hapo jana.
Msururu wa mashambulizi mwaka jana ya Jeshi la Umoja wa Afrika - AMISOM na jeshi la Somalia ilisaidia kuwatimua wanamgambo hao wa al-Shabaab kutoka maeneo muhimu waliyokuwa wameyateka katika eneo la kusini mwa Somalia.
Wakati huo, maafisa walisema wapiganaji hao walihamia upande wa kaskazini na kuingia jimbo la Puntland, eneo ambalo haliko chini ya operesheni ya AMISOM.
Lakini katika wiki za karibuni wanamgambo hao pia wameiteka upya miji kadhaa midogo na kufanya mashambulizi makali katika eneo la kusini mwa nchi.