Aloyce Nyanda awashangaa Watanzania wanaotumia muda mwingi kumjadili Ole sabaya badala ya shughuli za maendeleo

Hivi kuna mtu ameacha shughuli zake kwa sababu ya kumjadili Sabaya? Huyo naye amepoteza muda kwa kuzungumzia kitu ambacho hakipo. Sababu yake kubwa ya kutoa kauli hii ni kuumizwa na yaliyomtokea mfadhili wa arusi yake na shughuli za maziko ya baba yake.
 
Sisi tunamshangaa zaidi yeye Nyanda, kwa nini aliruhusu arusi yake kufadhiliwa na jambazi Sabaya.
 
Kwani yeye ndiye anayewapa chakula na kuwanunulia bando hao anaaowaita 'watanzania wa mitandaoni'?

Mahaba yake kwa sabaya yasitake kuwapangia watu nini cha kujadili.

Sabaya kawaumiza wengi lazima watu wamjadili na uovu wake uliopitiliza.
Anatafuta Kiki huyo kwani yeye ndio anaehudumia familia zetu ? Au Kuna msaada tumemwomba ?
 
Hivi haya mashamba tunayolima na ng'ombe hawa tunaofuga kipindi hiki anatulimia/ fugia huyo nyanda? Na amejuaje kwamba muda wote hatufanyi kazi Kama hatupo nae. Huyo nae atakuwa utopolo
 
Mtangazaji nguli na mwendeshaji wa kipindi cha The Big Agenda kinachorushwa na Star tv Aloyce Nyanda aka Mtozi ameonesha kushangazwa na watanzania wa mitandaoni wanaotumia muda mwingi kumjadili Lengai Ole sabayz badala ya kujikita kwenye shughuli za maendeleo.

Source: Star tv
Je na yeye haoni kwamba anapoteza muda kuwafuatilia wanaomjadili sabaya?

Actually he’s losing more
 
Mtangazaji nguli na mwendeshaji wa kipindi cha The Big Agenda kinachorushwa na Star tv Aloyce Nyanda aka Mtozi ameonesha kushangazwa na watanzania wa mitandaoni wanaotumia muda mwingi kumjadili Lengai Ole sabayz badala ya kujikita kwenye shughuli za maendeleo.

Source: Star tv
Alikuwa anakwamisha shughuli za maendeleo ya watu ndiyo maana anajadiliwa
 
Huyu ni mnufaika wa pesa za Lengai Ole Sabaya,lazima amutetee rafiki yake! Kipindi kafiwa na Baba yake Mzazi,Sabaya alisimamia mazishi mwanzo mwisho!
Kwani angekaa kimya angedaiwa na sabaya hizo gharama za mazishi ya baba yake!?
 
Kama kasema hivyo, basi hajui habari ni nini na shughuli za maendeleo ni nini.

Jana katika kijiwe wengine tumetumia muda mwingi kujadili legacy ya Colin Powell badala ya hizo “shughuli za maendeleo”. Je, siku ilipotangazwa jiwe kafariki hali ilikuwaje?
Angekuwa anajua maana ya habari asingekuwa bado yupo hapo alipo maana hamna kazi pale
 
Mtangazaji nguli na mwendeshaji wa kipindi cha The Big Agenda kinachorushwa na Star tv Aloyce Nyanda aka Mtozi ameonesha kushangazwa na watanzania wa mitandaoni wanaotumia muda mwingi kumjadili Lengai Ole sabayz badala ya kujikita kwenye shughuli za maendeleo.

Source: Star tv
Hawa watangazaji wengine ni vilaza zaidi ya wale POLISI wa Div. 0 ya kidato cha nne, yani na utangazaji wake wooote Bw. Aloyce Nyanda anashindwa kuilewa dhana ya nzima ya maendeleo.

Anashindwa kuelewa kumjadili Sabaya ni sehemu ya maendeleo?

Kimsingi kiongozi anapokwenda kinyume na maadaili ya uongozi maana yake anarudisha nyuma au anakwamisha mikakati ya usimamizi wa maendeleo

Vilevile kiongozi huyo anapowajibishwa maana yake ni kuongeza tija na ari ya maendeleo yaliyo kwamishwa na kionhozi huyo

Hivyo kumjadili Sabaya ni kuongeza chachu ya maendeleo miongoni mwa wananchi kwa kurejea maadili mabovu ya uongozi wake na kuamsha hisia za maadili ya uongozi mpya/uliopo/ujao miongoni mwa wanajamii

Hili linatakiwa liende sambamba na kumsimanga kwa kiwango kikubwa ili uongozi mpya/ulipo/ujao ujue kuwa cheo ni dhamana ya maendeleo na sio nafasi ya ubabe na kukifanya wewe ni Mungu mtu

Mi nashauri jeshi la magereza lisiishie kumpiga kipara cha kichwani tu coz jamaa anatakiwa apigwe kipara cha M*t*koni Shubaamit zake Mxieusssszzzz!!!
 
Back
Top Bottom