Almanusura nijiumize na losheni ilopigwa marufuku!!

Baba Mtu

JF-Expert Member
Aug 28, 2008
870
168
Wana-jf juzi nilinunua losheni iitwayo CLAIRMEN FOR MEN. Kabla sijanza kuitumia nilisoma ingredients zake na jinsi ya kuitumia, nikakuta kuwa sitakiwi nikae juani pindi nitakapopakaa hiyo losheni. Nilistuka kidogo na kujiuliza itakuwaje ikiwa ntalazimika kutembea juani. Niliamua kutembelea website ya TFDA (mamlaka ya chakula na dawa tanzania) na kuperuzi, nikaona kuwa CHLOROQUINONE NA JAMII ZAKE ZOTE ZIMEPIGWA MARUFUKU; na hiyo losheni ya claire for men ina hydroquinone ndani. Kana kwamba hiyo haitoshi nikaperuzi katika google na kuona madhara ya hydroquinone, nikachoka na kuchoka. Nitaendelea kupakaa mafuta ya nazi kama yale alokuwa akipaka bibi na babu enzi zile kwani haya mafuta ya kisasa ni hatari kwa afya yangu.
Nawaasa wana-jf na jamii kwa jumla tuwe tunasoma maelezo yaliyo katika bidhaa tuzinunuazo kabla ya kuanza kuzitumia, ukiona kuna kitu huelewi uliza kwa daktari aliye karibu nawe.
Nilichokiona katika mitandao ni hiki hapa katika links hizi:

1. TANZANIA FOOD AND DRUGS AUTHORITY

2. UK Skin Lightening - Hydroquinone Skin Bleaching

3. Banned Skin Bleaching / Skin Whitening products

4. Hydroquinone Side Effects Revealed. Discover the Truth.

5. The Truth About Hydroquinone by MedicineNet.com

6. hydroquinone topical medical facts from Drugs.com
 
Ungekuwa mweupe yakhee...kama Mkongo...asante for info
 
Sasa siku zote unapaka mafuta ya nazi, ikawaje ukataka kuanza kutumia lotion??????
 
ebwana bora iligutuka au walitaka kukugeuza albino nn?

Sasa siku zote unapaka mafuta ya nazi, ikawaje ukataka kuanza kutumia lotion??????



Hamna!! Ni mtoto nilham, mtoto wa kimanga amenipa sharti la mie kuwa mweupe ili aweze kunikubali kwani yee hataki mume mweusi!!! Mzee ndo nkaona nianze kujicream ili nami ning'ae.

Lakini kwa sharti la kutombea juani pindi npakapo hiyo loshen, basi mie naachia ngazi kwa mtoto nilham, najiweka pembeni kama 20%
 
Kazi ipo, hawa kina Nilham watatufanya tufanye mambo hata ambayo hatukuwahi ota eeh. Sasa vipi kama angetaka mweusi na mm mweupe?? Kunae lotion za reverse(white to black),
 
Hamna!! Ni mtoto nilham, mtoto wa kimanga amenipa sharti la mie kuwa mweupe ili aweze kunikubali kwani yee hataki mume mweusi!!! Mzee ndo nkaona nianze kujicream ili nami ning'ae. Lakini kwa sharti la kutombea juani pindi npakapo hiyo loshen, basi mie naachia ngazi kwa mtoto nilham, najiweka pembeni kama 20%

kila unachoambiwa kufanya lazima ufanye?
 
Jaribu samli nilham ni vema kumtia mkononi ikidunda muombe alegeze vigezo
 
Back
Top Bottom