Ally Keissy: Ataka wilaya,halmashauri na majimbo kupunguzwa

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725
Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy amesema moja kati ya mambo yanayoifanya Serikali ya Tanzania kuwa na matumizi makubwa ya fedha ni kuanzishwa kisiasa wilaya, halmashauri na majimbo.

“Serikali inakusanya pesa lakini matumizi yake yamekuwa makubwa kutokana na mgawanyo wa kata, tarafa, majimbo, wilaya na halmashauri nyingi ambazo zimeanzishwa kisiasa,” alisema Kessy jana Jumatano Juni 19, 2019 katika mjadala wa bajeti ya Serikali ya mwaka 2019/2020 ya Sh33.1 trilioni.

“Mfano ndugu Malocha (Ignas-mbunge wa Kwela) ana kata 30 na anahudumia jimbo lake na wengine wana kata sita, kwa nini majimbo yanakuwa hivi? Kuna halmashauri zimeanzishwa kisiasa hazina uwezo wa kukusanya mapato mpaka madiwani hawapati fedha,” amesema Keissy.

Alisema, “Serikali naiomba kaeni mpitie upya kupunguza baadhi ya majimbo, kata, tarafa, mikoa na halmashauri. Matumzi yamekuwa zaidi hata mimi nipo tayari jimbo langu kupunguzwa.”

Alisema hata wabunge wamekuwa wakilipwa posho zisizo na maana na kupendekeza wawe wanalipwa posho za kuhudhuria vikao vya chombo hicho cha kutunga sheria ili fedha nyingine zitumike katika maeneo mengine, kama kuchimba visima.
 
Mh. Kessy umeongea jambo la maana sana. Kwa kuongezea hata Wilaya zenye majimbo mawili mfano wilaya ya Mbozi au Nkasi zinatakiwa kubaki na jimbo moja. Kiufupi wilaya zote zinzatakiwa kubaki na jimbo moja kama ilivyokuwa awali.
 
Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy amesema moja kati ya mambo yanayoifanya Serikali ya Tanzania kuwa na matumizi makubwa ya fedha ni kuanzishwa kisiasa wilaya, halmashauri na majimbo.

“Serikali inakusanya pesa lakini matumizi yake yamekuwa makubwa kutokana na mgawanyo wa kata, tarafa, majimbo, wilaya na halmashauri nyingi ambazo zimeanzishwa kisiasa,” alisema Kessy jana Jumatano Juni 19, 2019 katika mjadala wa bajeti ya Serikali ya mwaka 2019/2020 ya Sh33.1 trilioni.

“Mfano ndugu Malocha (Ignas-mbunge wa Kwela) ana kata 30 na anahudumia jimbo lake na wengine wana kata sita, kwa nini majimbo yanakuwa hivi? Kuna halmashauri zimeanzishwa kisiasa hazina uwezo wa kukusanya mapato mpaka madiwani hawapati fedha,” amesema Keissy.

Alisema, “Serikali naiomba kaeni mpitie upya kupunguza baadhi ya majimbo, kata, tarafa, mikoa na halmashauri. Matumzi yamekuwa zaidi hata mimi nipo tayari jimbo langu kupunguzwa.”

Alisema hata wabunge wamekuwa wakilipwa posho zisizo na maana na kupendekeza wawe wanalipwa posho za kuhudhuria vikao vya chombo hicho cha kutunga sheria ili fedha nyingine zitumike katika maeneo mengine, kama kuchimba visima.
Kwa mfano majimbo matatu ya Kigoma yaani Mjini, kusini na kaskazini ni sawa na jimbo moja tu la Mchungaji Msigwa pale Iringa ukitokea Nduli hadi Mwangata!
 
Unamuotaga mbowe wkt umelala,Ova
Mwenzio kesha chukua ati 👇 👇 👇
images (4).jpg
 
Mikoa minane inatosha kabisa,wilaya nazo zisizidi 40 tutakuwa tumepunguza mizigo kwa mlipa kodi,na serikali mawaziri 8 naibu wao 2 wanatosha.
Makamu wa Raisi awe pia waziri mkuu.Kama kweli tunataka kujitegemea .
Mambo ya ruzuku za vyama vya kisiasa zivutwe.
Lakini ipitie bungeni iwe sheria hakuna kuongeza au kupunguza wizara au mikoa,au wilaya na majimbo ya uchaguzi.Lakini bunge hili halina uwezo au nia ya kufanya mageuzi makubwa labda bunge jipya la katiba.
 
Back
Top Bottom