Ally Bananga: Mwizi karudisha vitu vyetu halafu analazimisha tumsifu

ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
1,722
2,000
KAULI YA BANANGA INATISHA; "MWIZI KARUDISHA VITU VYETU ALAFU ANALAZIMISHA TUMSIFU"

Na, Robert Heriel

Moja ya watu waliotisha siku ya jana kwenye mkutano wa Kampeni wa CHADEMA huko Tabata Segerea ni pamoja Ally Bananga. Sikuwahi kumjua huyu Bananga, siku ya jana ndio nimemuona na kumsikia. Hakika huyu ni mtu muhimu sana kwa CHADEMA kwa wakati huu. CHADEMA mchukueni huyu mtu, angalau apewe Dakika kumi au kumi na tano kabla ya saa kumi na moja.

Kauli zote za Bananga ni muhimu, Kauli zote za Bananga zinashtua ubongo uliolala. Kauli zote za Bananga zinahamasisha, zinachangamsha, zinatia uchungu, na pia zinamfanya msikilizaji achukue hatua.

Bananga kila alichoongea kiliingia katika akili ya aliyekisikia. Ni watu wachache kama Bananga wenye uwezo wa kuwasilisha hoja kwa namna yake.

Kwa Mujibu wa Bananga, ameomba Muongozo kwa Mgombea wake wa Urais, kisha na wasikilizaji waliokuwa wakimsikia kuwa; Mwizi karudisha vitu alivyotuibia, alafu analazimisha tumsifu, hiyo imekaaje.

Bananga anajaribu kuzishtua akili za wasikilizaji kuwa, Mambo mengi ambayo CCM wameyasema wameyafanya yalikuwepo, ametoa mfano wa ndege, treni na reli,

Bananga anasema, mambo hayo yalikuwepo lakini yaliuawa na haohao CCM, kisha leo wanarudisha vitu vilivyokuwepo wanajisifu. Hiyo imekaaje.

Kuhusu Ndege sikuwepo, lakini Treni ya kaskazini nilikuwepo kipindi ikiwa inafanya kazi zake. Baadaye Treni ile iendayo Moshi ilikufa chini ya utawala uliowekwa na CCM. Sasa kitendo cha Serikali ya awamu hii chini ya CCM kusema imeleta maendeleo katika ufufuaji wa Reli iliyokufa chini ya utawala wao huohuo wa CCM, ni mfano wa mwizi kukurudishia kitu alichokuibia kisha akalazimisha umsifu.

Hii ni kama muda huu ambapo serikali ya awamu hii imesitisha nyongeza ya mishahara kwa wafanyakazi wa serikalini alafu baadaye serikali hiyo hiyo iongeze mishahara ambayo yenyewe ilisitisha nyongeza alafu ilazimishe kusifiwa.

Ni sawa na mtu anayekupiga kofi kisha anakubembeleza kisha anajisifu kwa kukubembeleza.

Au ni sawa na mtoto umchape kisha umpe pipi ya kumrubuni ili anyamaze.

Au ni sawa na Mwizi kakuibia Gari Kisha anakurudishia akiwa kalipaka rangi muda huo umechapika. Alafu anajisifu nimelipaka rangi, hasemi yeye ni mwizi wala haombi samahani kwa kukuibia hamna yeye anajisifu kakurudishia gari lako.

Ally Bananga apewe Dakika 10 hadi 15 kuongea, anaweza kuwafikisha CHADEMA Somewhere. Jamaa anajua kuongea, anajua kuhamasisha.

Nashukuru CHADEMA kwa kuweza kufuata baadhi ya ushauri wangu wa namna ya kuwasilisha hoja zenu Jukwaani. Kule Segerea Mlifanya vizuri kwa 80%.

Tafuteni kama kina BANANGA 3

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Apr 21, 2020
46
125
Mkuu hii ni awamu nyingine Mkuu wangu. Msitumie title ya 'mwizi' mambo yamebadilika sana...
Awamu hii ni tofauti na zilizopita, mnaposema amerudisha mmenifurahisha.

Mnaamini katika mabadiliko, mabadiliko ndio haya sasa. Wananchi wameyapata mabadiliko humohumo ndani ya CCM... Mkuu kuna mabadiliko makubwa sana unless unatumia miwani ya kiitikadi.

Mkuu mambo sahivi yanapendeza, kunanoga Mkuu.

La mwisho jiulize, kama huyu unayemuita 'MWIZI' maweza kurudisha kilichoibiwa kwa miaka 50+ ndani ya awamu moja yenye miaka 5 tuu je akimalizia na mitano mingine huoni tutapiga hatua za miaka 50+ mbele?

Haya je tukiamua kufuata na ushauri wa mzee Mwinyi je... (nisitoke nje ya mada).

JPM

Sent from my SM-J105F using JamiiForums mobile app
 
Hakuna aliyeitwa Mwizi Mkuu

imetumika Tashbiha
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
57,680
2,000
Kuna haja gani ya kuongoza chama kisichokubalika na wananchi?
Chama ambacho hakishindi bila kuiba kura.
Chama ambacho viongozi wake wanakiri hadharani kuwa ushindi wait unatokana na kuwatumia polisi na TISS.
Chama ambacho kinaitumia NEC kuwaengua wapinzani wake.
Hiki chama hakika Ni CHAMA CHA MASHETANI
 
Shida ya ninyi Upinzani hamjajua mbinu mujarabu ya kuiondoa CCM ikulu.

Ikulu haichukuliwi kwa mbinu mnazotumia
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
8,726
2,000
CHADEMA mfanyeni Ally Bananga kuwa Mwambata wa Kampeni wa Lissu jamaa anajua kuongea mpaka basi
Nimefurahia sana kazi yake pale Segerea jana
 
Apr 21, 2020
46
125
Embu nukuu hicho kipande ambacho CCM imeitwa Mwizi
[QUOTE="] Sasa kitendo cha Serikali ya awamu hii chini ya CCM kusema imeleta maendeleo katika ufufuaji wa Reli iliyokufa chini ya utawala wao huohuo wa CCM, ni mfano wa mwizi kukurudishia kitu alichokuibia kisha akalazimisha umsifu.[/QUOTE]

Mkuu kunukuu ni changamoto ila ndio hapo mkuu

Sent from my SM-J105F using JamiiForums mobile app
 
ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
1,722
2,000
[QUOTE="] Sasa kitendo cha Serikali ya awamu hii chini ya CCM kusema imeleta maendeleo katika ufufuaji wa Reli iliyokufa chini ya utawala wao huohuo wa CCM, ni mfano wa mwizi kukurudishia kitu alichokuibia kisha akalazimisha umsifu.

Mkuu kunukuu ni changamoto ila ndio hapo mkuu

Sent from my SM-J105F using JamiiForums mobile app
[/QUOTE]

Wapi mbona umeshindwa hata ku-bold?

Wapi nimesema CCM ni mwizi, au wezi?
 
Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
6,153
2,000
Ally achana naye ni kichwa ila urafiki wake na wanaccm wengi ni changamoto kwake
 
Lihakanga

JF-Expert Member
Dec 17, 2016
2,474
2,000
Kauli hiyo ni kumpigia kampeni magufuli. Kama mwizi karudisha alichoiba basi ametubu amekuwa raia mwema na dawa yake ni kumpa kazi ya kulinda mali alizorudisha na pia kumtuma atafute nyingine azirudishe.
 
residentura

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
3,661
2,000
Mkuu hii ni awamu nyingine Mkuu wangu. Msitumie title ya 'mwizi' mambo yamebadilika sana...
Awamu hii ni tofauti na zilizopita, mnaposema amerudisha mmenifurahisha.

Mnaamini katika mabadiliko, mabadiliko ndio haya sasa. Wananchi wameyapata mabadiliko humohumo ndani ya CCM... Mkuu kuna mabadiliko makubwa sana unless unatumia miwani ya kiitikadi.

Mkuu mambo sahivi yanapendeza, kunanoga Mkuu.

La mwisho jiulize, kama huyu unayemuita 'MWIZI' maweza kurudisha kilichoibiwa kwa miaka 50+ ndani ya awamu moja yenye miaka 5 tuu je akimalizia na mitano mingine huoni tutapiga hatua za miaka 50+ mbele?

Haya je tukiamua kufuata na ushauri wa mzee Mwinyi je... (nisitoke nje ya mada).

JPM

Sent from my SM-J105F using JamiiForums mobile app
Akili iliyotengeneza tatizo haiwezi kutatua tatizo hilo hilo,hata ipite miaka 1000.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom