Zanzibar 2020 Alliance for Democratic Change (ADC) kuzindua Kampeni Kisiwani Pemba kesho Septemba 16, 2020

ADC Party

Member
Sep 14, 2020
28
29
8F334C78-E608-4684-AECD-D7D640F77EC1.jpeg


Chama Cha Alliance for Democratic Change (ADC) kupitia Mgombea wake wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Queen Cuthbert Sendiga, kinapenda kukuletea taarifa ya muendelezo wa Kampeni zake kuelekea tarehe 28/10/2020 huku akiwa mgombea mwanamke pekee kuanza kampeni zake hizi.

Kesho Jumatano, tarehe 16 Septemba atazindua kampeni zake Mjini Pemba - Zanzibar katika viwanja vya Shame Mmata, Soko la Mjini Micheweni.

Mgombea wetu ameshaanza kampeni na huu utakuwa ni mkutano wake wa tatu. Miwili aliifanya visiwa vya Unguja.

Mkutano wa kwanza ulizinduliwa pamoja na Ilani ya uchaguzi 2020-2025 siku ya tarehe 11/09/2020 katika viwanja vya Mnazi Mmoja huko Unguja. Mkutano wa Pili ulifanyika siku ya tarehe 13/09/2020 huko Unguja kusini, Makunduchi.

Tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa support kubwa mnayompa mgombea wetu

Imetolewa na
Devilsi Method
Meneja wa Kampeni

ADC DIRA YA MABADILIKO
 
"Maisha bora kwa watanzania wote" tukianzia na wewe Kinyungu .
Aisee mko vizuri. Mimi maisha yangu yamevurugwa sana katika miaka 5 iliyopita. Bora mje mrekebishe wananchi tuwe na maisha bora tena maana hali ni mbaya sana
 
Hahaha eti wanzindua, muda wa kampeni unaisha wao wanazinuka leo?!

Hawa ndio huwa washereheshaji wa ccm, wanawahi Diamond Jubilee mapemaa kusema uchaguzi ulikuwa huru na haki.

Ili wakumbukwe kwenye mgao wa mavyeo.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom