All bark no bite?

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,832
2,790
Nimekaa na kuanza kutafakari hali na mabadiliko ya mwenendo wa hawa wanasiasa wetu nikilinganisha na enzi hizo za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere , Alhaj Ally Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa na sasa Jakaya Mrisho Kikwete

1. Mwalimu J. K. Nyerere
Alifanya kazi katika maadili halisi, mihimili ya Serikali ilifanya kazi zake ipasavyo. Katika uongozi wake nakumbuka aliwahi kumtimua waziri mmoja Joseph James Mungai kwa scandal ya sukari, ni muasisi wa Azimio la Arusha lililokuwa na kila aina ya mazuri kwa maslahi ya taifa. Uongozi wake ulikubalika na wananchi.


2.Alhaj Ally Hassan Mwinyi "Mzee Ruksa", alifanya kazi kwa kujiamini kiasi chake akaweza kupambana na hali mbalimbali ya mbinu za rushwa, alianzisha harakati mbalimbali kama vile "Mfagio wa Chuma" ikiwa ni ishara ya kupambana na rushwa. Ndiye aliye lipindua Azimio la Arusha, kuingiza soko huria na mfumo wa vyama vingi. ALIAHIDI SANA KUPAMBANA NA RUSHWA.

3. Benjamin William Mkapa, Aliingia madarakani kwa nguvu ya Mwalimu ambaye alimuamini sana kwani ni mwanafunzi wake wakati Mwalimu akifundisha Pugu Secondary, Benjamina alikuwa na akili sana. Katika kipindi chake cha uongozi kama rais nitamkumbuka kama DALALI, Benjamin ameuza sana mashirika ya umma, migodi, na pia nitakumbuka kwamba alikuwa ni mtetezi mzuri sana wa mawaziri wake pale wananchi walipowanyoshea vidole kwa tuhuma mbali mbali, mzee huyu alibaki kutaka ushahidi uletwe kwake. Pia nitamkumbuka kwamba aliingia pale Jengo takatifu akaanzisha meza ya kuuza "nyanya" Aliitumia kauli mbiu "UWAZI NA UKWELI" kana kwamba yeye ni muwazi na mkweli "Mr Clean" tukabaki kumwamini kumbe kioo tulichodhani ni TRANSPARENT kilikuwa ni TINTED hatukuona alichokuwa akikifanya nyuma ya pazia. Huyu ni rais wa kwanza kutuhumiwa kumiliki mgodi. Hakuwahi kumuwajibisha waziri hata mmoja na sikumbuki kama aliwahi kulivunja baraza la mawaziri kwa kulisuka upya ingawa lilivurunda sana. Imani ya wananchi kwa CCM ilianza kufifia

4. Jakaya Mrisho Kikwete, huyu amekuja na kauli mbiu ya kuunganisha jamii akaweza kupata kura nyingi sana za urais. Hakika wananchi tumekuwa na matumaini naye hadi sasa tuna matumaini naye. Ndani ya miaka miwili tu JK ameweza kukumbana na misukosuko ya kisiasa hadi ikabidi kupangua baraza la mawaziri na baadaye alilazimika kulivunja baraza hilo, cha kushangaza amekuwa akiwarudisha watu wale wale kwa asilimia kubwa. Alikuwa na Kauli mbiu isemayo ARI MPYA, KASI MPYA na NGUVU MPYA, nasema alikuwa nikiwa na maana sasa hana. Ndani ya kauli mbiu hii kulikuwa na KIBWAGIZI "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA" Yeye huyu ndiye wa kwanza kuweza kulazimika kuvunja baraza la mawaziri kutokana na KASHFA zinazohusu UFISADI (FRAUD. Tofauti na rais aliye mtangulia huyu anasikiliza kelele za wanachi.
SASA tunamuomba atege zaidi masikio kwa wananchi kwani wanayo maoni mazuri sana kuweza kumsaidia, kelele hizi za wananchi ni kupitia VYOMBO vya HABARI ikiwamo JF.
Ahadizote za kupambana na mafisadi kwa ari kasi na nguvu mpya ziko wapi?? Tunayo imani bado.


TAKUKURU HAITUFAI KARABATI
IMARISHA USALAMA WA TAIFA
MIKATABA FEKI VUNJA
MFUMUKO WA BEI SHUSHA
 
Back
Top Bottom