All about Edward Hosea, Mwanyika

Jamani wanajf humu ndani inaonesha kuna wanasheria wengi sana tena waliobobea ikibidi zaidi ya mwakyembe na Hosea,ndio maana hii mijadala labda haiishi,lakini pamoja na hayo siasa na misukumo binafsi nayo imetuelemea mno kiasi saa nyingine tunashindwa kutoa hoja na badala yake tunang'ang'ania misimamo yetu. Aliyemwanazuoni atakubaliana nami kuwa lazima akubali kupingwa na katika kufanya hivyo hoja yoyote anayoitoa anaitoa akiwa na open mind huku akielewa kuwa wapo watakaompinga wapo watakaomkubali na pia wapo watakaotaka kuelimishwa zaidi.Lakini katu hatowachukia wanaompinga kwani nao wanahoja zao shindani.

Baada ya kusema hayo,sasa narudi kwa HOSEA.Mhe. HOSEA wakati anachunguza sakata la Richmond alikuwa akitumia sheria namba 16 ya mwaka 1971 kadiri ilivyofanyiwa marekebisho kwa vipindi toauti.Vilevile wakati HOSEA nachunguza kuhusu sakata la balozi Mahalu vilevile alikuwa akitumia sheria hii hii. Makosa yote haya mawili yalihusisha viongozi wa serikali kwa upande mmoja na watu binafsi au makampuni yaliyoko nje ya nchi. Na katika makosa yote hayo mawili yaliyoiingoza hasara nchi yetu hakuna aliyewahi kushikwa red handed akiomba,au kupokea rushwa. Yote yanahusisha ushahidi wa kimazingira tu. Makosa yote mawili pia hayahusishi rushwa tu bali pia uhujumu uchumi.

Hivi karibuni Hosea amesikika kwenye vyombo vya habari akisema,yeye kazi yake ni rushwa na kwamba alifanya kazi kwa mujibu wa sheria ya rushwa ya mwaka 1971 ilivyokuwa,hivyo kazi yake si miktaba wala uhujumu uchumi. Jibu hili linafanana sana na alilolitoa mwanyika wakati anahojiwa na kamati ya mwakyembe. Swali hapa je,uhujumu uchumi na mikataba ni kazi ya nani? si makusudi yangu kujibu swali hili leo hapa,bali kuangalia uhalali wa kauli za HOSEA kuhusu wajibu wake kwa masuala yote hayo mawili hapo juu.
TAKURU ya zamani iliundwa kwa mujibu wa kifungu cha tatu cha sheria ya rushwa mwaka 1971 ikiwa na majukumbu yafuatayo,hapa nitanukuu
1.TO take necessary measures for the prevention of corruption in the public,parastatals and private sector.
2.To investigate and prosecute offences under the Act and other offences involving corrupt transactions.
3.Advise the governement and other parastatals organization on the ways and means to prevent corruption.
Sheria pia inaendelea kusema kuwa wakati wakitekeleza majukumu yao,watakuwa na mamlaka ya kipolisi sawa na askari mwenye cheo cha ASP.Hivyo kwa ufupi hizo ndizo kazi zao. Ukiangalia kwa haraka haraka tu utakuta kwa kauli za hosea,haguswi na richmondi kwani labda alishafanya kila jinsi kuzuia rushwa,pili alishachunguza akakuta hakuna rushwa ya moja kwa moja na tatu aliishauri serikali kwamba iendelee tu na richmond kwani hakua rushwa na haipati hasara yoyote.
Hivi kusema serikali inapata hasara au haipati ilikuwa ni kazi yake? hiyo kazi inafall wapi kati ya hizo kazi tatu kuu hapo juu? naam labda alisema kwakuwa hizo zilikuwa hadidu za rejea za uchunguzi wake. Lakini mimi naenda mbali zaidi.

Ukisoma kifungu cha 6 cha sheria hiyo ya zamani kinasema kwamba
mtu yeyote ambaye kwa kujua atampa wakala, au wakala yeyote kwa kujua atatumia kwa lengo la kumdanganya mkuu wake, risiti,akaunti au hati au nyaraka yoyote inayohusiana na mambo au shughuli yoyote ya mkuu wake wa kazi na ambayo ina taarifa feki,za kughushi au zilizopotoshwa na kwa jinsi yoyote ile zina lengo la kumdanganya mkuu,atakuwa ametenda kosa.mwisho wa kunukuu.

Sawa Hosea hakuona rushwa,je hakuona pia kipengele hiki cha sheria? je katika mkatba wa richmond hakukuwa na nyaraka feki zenye lengo la kumpotosha mkuu,je kusema kwamba richmond ina ubia na kampuni ile waliyoitaja na kuthbitisha hilo kwa business kadi hakukuwa na lengo la kumpotosha mkuu?je,ukweli kwamba richmond haikuwa mtu kisheria yaani sio kapuni halali kwa kuwa inakosa usajili tanzania na huko USA haipo na kwamba hata kama ilisajiliwa hapa nchini usajili wake haukuwa halali kwa kuwa hatuna one man company kwa mujibu wa kifungu cha tatu,moja cha sheria ya makampuni.je,waliohusika hawakuwa na lengo la kumpotosha mkuu?
Watu wote waliokuwa wakideal na richmond walikuwa wanajua nini kinachoendelea toka mwanzo hadi mwisho,na ukweli wote hapo juu walikuwa wanaujua je,hakuwa na nia ya dhati ya kumpotosha mkuu? ili aingie mkataba na mtu asiyekuwepo(yaani fictitious person?) Hosea hili hakuliona kabisa? Kama hakuliona anatofautiana vipi na sisi walei(laymen) wa taaluma ya kuchunguza rushwa? basi ameprove incomptence kwenye taasisi yake iwapo atashindwa kuthibitisha hili.Basi uchunguzi wake ulijikita kwenye nini? yaani ni vitu gani alivyoviangalia hadi akaandika ripoti?
Je,kama vigezo hivyo hapo juu havikwepo kwa maana kwamba kampuni ilitoa nyaraka feki juu ya uwepo wake kisheria na maafisa wetu wakavipokea na kumwaminisha mkuu ili anendelee kuingia mkataba je,hakukuwa na harufu ya rushwa iliyowapofusha maafisa wetu wasiweze kuchunguza zaidi juu ya uwezo wa richmond kisheria na kama je,imetimiza masharti yote ya sheria za tanzania?Mbona ukisoma mkataba wa richmodn maafisa wetu wanasaini kabisa kauli zao kwamba wameridhika richmondi ni kampuni halali kisheria na haijavunja sheria yoyote ya tanzania,wakati kwa hakika imevunja sheria ya makampuni na sheria ya mikataba ya mwaka 1961.

Sawa Hosea atasema yote haya si kazi yake na hayakuwamo Richmondi. Ok,si kazi yake ndiyo lakini jaji mmoja kwenye kesi ya Donoghue v,stevenson[1932]QB aliwahi kusema "....iwapo tutakwenda hatua moja kwanini isiwe hamsini?" HOSEA alifikiaje uamuzi wa kumshitaki balozi mahalu? alijuaje kuwa pale kuna mkono wa rushwa wakti mazingira yake yalikuwa swa na richmond? Ni kwanini HOSEA alitumia kifungu cha sita katika suala la mahalu kumtia mahalu hatiani wakti kwenye richmond hakukitumia?ilikuwaje katika mashtaka ya mahalu Hosea huyohuyo akamchaji pia balozi mahalu na uhujumu uchumi pamoja na wizi kama mtumishi wa umma kwa mujibu wa sheria ya kanuni ya adhabu(pena code cap16) na pia sheria ya rushwa 1971,wakati kwa mujibu wa sheria ya mwaka 1971 hakuwa na mamlaka ya kuestablish makosa hayo?

Mamlaka ya kuchaji mahalu kwa kutumia penal code na Economic and organised crimes control Act aliyapata wapi.Hivyo basi kama aliweza kwenye hili la mahalu tultegemea aweze pia kwenye richmond kwani kanuni za haki zinasema "justice must not only be done but must be seen to be done" na katiba yetu intambua equality before the law. Ni kutokana na mashaka haya niliyoataja hapo juu ndio maana mhe. Hosea anatuhumiwa kuhusika kwa namna moja au nyingine kwenye sakata la richmond kwa kuufumbia macho uovu wa wazi.
Na kama mwanazuoni? utafiti wowote unasehemu ya hitimisho na mapendekezo,ambayo tulitegemea hosea aseme,pamoja na kuwa kazi yangu si kuangaliwa mikataba na masuala ya uhujumu uchumi,lakini katika utafiti wangu au uchunguzi nimegundua mapungufu yafutayo kwenye mkataba wenyewe na kwenye uhalali wa kampuni ya richmond kisheria ambao napendekeza ziundwe tume maalumu zenye mamlka ya kuchunguza uhalali wa mkataba huu nk.ili kujiridhisha zaidi. Hapa angekuwa safe,lakini yeye alikana kabisa na kusema mchakato wote ulizingatia sheria na ulienda kwa kufuata vipengele vyote wala hakuna harufu ya rushwa na wala hatupati hasara.mmh HOSEA ulienda mbali mno uliposema vipengele vyote vya sheria vilifuatwa je,na kanuni za manunuzi zinazosema tenda itangazwe siku 45 na wao wakatangaza siku kumi je,huko kulikuwa ni kufuata sheria? au ripoti ya PPRA hakuiona?

Kwa mantiki hii mimi na wadau wengine ndio maana tunashawishika kukubali kuwa Mhe.HOSE anawajibika katika sakata hili la Richmond unless aje na maelezo ya kuridhisha zaidi lakini sio kujibu wadau kwa jazba.
 
Nadhani ukirejea yale mapendekezo ya nyingeza ya kamati teule ya Bunge yamemtaja mkurugenzi wa Takukuru kuhusika na sakata la Richmond kwa nia ya kuupotosha umma na kuficha uozo (Corruption).

Ninajiuliza hiki kiburi anachokionesha kimetoka wapi? na ninaanza kupata shaka kuwa ameanza kubip kupitia media kuhusu akaunti za wabadhirifu wa BOT kuwa wanaakaunti mahala mahala, ukifuatilia kwa makini makala za magazetini zinasema kuwa taarifa za uhakika kutoka vyombo vya uchunguzi vya dola vimegundua akaunti hizo, je ni kusema kuwa anataka kutumia rungu hilo la kutaka kuwaumbua vigogo ili aogopwe?? I believe he must go and wapo watu safi ambao wanaweza kuiongoza taasisi ya takukuru bila yeye. Ninaamini kuwa anakesi ya kujibu huju mheshimiwa. Kummbukeni adhabu ya malika aliyeasi ni laana milele yote hivyo doa alilojiwekea litamsumbua maisha yote.

mimi sio nguli wa sheria ila ninashawishika kuwa sheria ilikiukwa na aliyeikiuka bebe msalaba wake.
 
Augustoons,

Tunashukuru kwa maelezo yako!!! Nadhani mwenzetu amelewa sheria, unajua ninyi wanasheria siku zote munatafsiri sheria kulingana na jinsi zinavyo favour upande wenu!!!

Nadhani kaka yetu mpendwa Dr. Hosea, kila akiziangalia sheria anaona hana kosa...

Lakini anajisahau kwamba sisi wananchi (yaani Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) ndio tunaosema uwepo wake kwenye ile taasisi utasababisha hiyo vita ikose tija!

Hatuhitaji yeye atumie sheria, sisi waajiri wake ndio tunataka aondoke!
 

Hosea usisubiri kufukuzwa, ng'atuka
Tanzania Daima

MKURUGENZI wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Edward Hosea, ni miongoni mwa viongozi wanaotuhumiwa kuisafisha Kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond dhidi ya tuhuma za kuipata zabuni hiyo kwa njia zisizostahili.
Hosea anakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu wadhifa wake huo, baada ya ripoti ya Kamati Teule ya Bunge, iliyoundwa kuchunguza uhalali wa upatikanaji wa zabuni hiyo, inayoligharimu taifa hasara ya mamilioni ya shilingi kila siku, kupendeza hatua hiyo dhidi yake.

Sababu zilizotajwa na kamati hiyo za kumtaka Hosea kuachia ngazi, ni kutoa ripoti ya uongo kwa umma wa Watanzania, ikieleza kutokuwapo kwa aina yoyote ya rushwa au ufisadi katika mchakato wa upatikaji wa zabuni hiyo kwa Kampuni ya Richmond.

Mbali ya Hosea, viongozi wengine waliotajwa kuhusika katika kashfa hiyo ambao wamekwishaachia nyadhifa zao, ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

Wengine walioachia ngazi sambamba na Lowassa, ni aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Ibrahim Msabaha.

Kuachia madaraka kwa viongozi hao kulionyesha dhana ya uwajibikaji ilivyoanza kushika kasi hapa nchini baada ya kipindi kirefu cha viongozi kugoma kuwajibika, hata wanapobainika kufanya makosa ya wazi katika utendaji kazi wao.

Kwa hao waliokwishaachia madaraka, sisi tunasema wamefanya jambo jema kwa sababu wametimiza wajibu wao na wamefungua milango kwa wengine kufuata nyayo zao, wakibainika kuwa katika mazingira kama hayo yaliyowakuta mawaziri hawa watatu.

Kinachotushangaza, ni kitendo cha Hosea ambaye tunaamini kuwa licha ya kutajwa katika kashfa hii, ni mtu mwenye hekima na anayeheshimu misingi ya uongozi bora, kukataa kuachia ngazi.

Tunapenda kueleza msimamo wetu wazi kuhusu suala hili kuwa, Hosea anapaswa kujiuzulu haraka kutokana na kashfa zilizoelekezwa kwake na Kamati ya Bunge, ambazo ushahidi wa mazingira unaonyesha kuwa zina kila chembechembe ya ukweli.

Tunajua kwamba Hosea hakutarajia kukutana na hali hii, lakini tunamtaka azingatie kauli ya Rais Jakaya Kikwete wakati akieleza mazingira yaliyolazimisha kung'atuka kwa Lowassa kuwa, kilichotokea kwake ni ‘ajali ya kisiasa'.

Tunamtaka Hosea atambue kuwa, asipokubaliana na ukweli huo na kuamua kuachia ngazi mwenyewe, anaweza kupambana na dhahama ya kulazimishwa kujiuzulu au hasira za wananchi zitakazomlazimisha kuikimbia ofisi yake, jambo ambalo litazidi kuharibu sifa yake katika jamii.

Tunapenda kumshauri Hosea awe msomaji mzuri wa nyakati, asibaki akiamini kuwa nyakati hazibadiliki, asifikiri kuwa Kamati ya Bunge ilikosea kuwataka mawaziri wawajibike na wakawajibika, asifikiri Rais Kikwete alikosea kuamua kulivunja Baraza la Mawaziri. Atambue kuwa rais alilazimika kuchukua uamuzi huo kutokana na uzito wa suala lenyewe.

Hivyo kwa uzito huo huo, tunamtaka Hosea apime uzito wa tuhuma zinazomuandama, yeye na taasisi anayoiongoza, kisha achukue uamuzi wa kuachia ngazi hata kama katika kujipima ataona hahusiki. Atambue kuwa kama si yeye, basi wasaidizi wake walihusika na yeye kama kiongozi wao, anapaswa kuwajibika.

Kwa sababu bado tunampenda na kumuheshimu Hosea, tumeamua kumueleza msimamo wetu ambao ndio msimamo wa wengi, vinginevyo, kama hatatusikiliza, basi tutamtaka Rais Kikwete amfukuze.
 
Waziri Simba amruka Hosea

na Kulwa Karedia
Tanzania daima

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala (Bora), Sofia Simba, amesema hatima ya Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Edward Hosea, kujiuzulu iko mikononi mwake mwenyewe.
Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu juzi jioni, Simba alisema ofisi yake haihusiki na uamuzi huo kwa vile si iliyomteua kushika wadhifa huo.

“Uamuzi wa kujiuzulu uko mikononi mwake mwenyewe…hadi sasa mimi sijapata taarifa ya kujiuzulu kwake…ndiyo nasikia kutoka kwako mwandishi, hata hivyo, nalifuatia suala hili,” alisema.

Alisema suala la Hosea kuachia ngazi liko mikononi mwa Rais Jakaya Kikwete, kwa kuwa ndiye aliyemteua kushika wadhifa huo, hivyo yeye (Simba) hana uwezo huo.

“Unajua anayestahili kukubali au kukataa ombi hilo ni yule aliyemteua kushika wadhifa huo…naye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akikubali sawa, akikataa sawa,” alisema Waziri Simba.

Alisema licha ya ukweli kwamba, TAKUKURU iko chini ya ofisi yake, Waziri Simba hakutaka kuingia ndani licha ya kuzagaa kwa habari kwamba Hosea anajiandaa kujiuzulu wakati wowote kuanzia sasa.

Alipoulizwa yeye atapokeaje hatua ya kujiuzulu kwa kiongozi huyo, Waziri Simba alisema hana kinyongo kwa vile huo ni uamuzi wake atakao kuwa ameamua.

Kwa upande wake, Hosea alisema hivi sasa hana mpango wa kuachia ngazi kwa kuwa kazi alizofanya zilizingatia sheria na utaratibu uliowekwa.

“Mimi nilishughulikia suala hili kwa mujibu wa taratibu zote zilizowekwa, sasa nashangaa kuona kila siku watu wanasema nijiuzulu, suala hili naliacha mikononi mwa vyombo vya sheria,” alisema.

Alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na kituo cha televisheni ya Taifa (TvT) kutoka kisiwani Zanzibar anakohudhuria kikao cha wakuu wa taasisi za kuzuia na kupambana na rushwa kwa nchi za Afrika Mashariki.

Alisema alishughulikia suala hilo kwa mujibu wa sheria ya kuzuia rushwa ya mwaka 1971, sasa anashangaa watu wote wanamtaka ajiuzulu juu ya kashfa ya Richmond.

Hosea amekuwa katika mtihani mkubwa baada ya Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa kuchunguza Kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond kumhusisha kwenye sakata la kashfa ya ufisadi yeye baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali.

Hatua hiyo ilitokana na Hosea kupitia taasisi yake kutoa taarifa za awali kwamba Richmond pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, hawakuhusika katika mchakato mzima wa sakata la Richmond.

Lakini baada ya Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk. Harrison Mwakyembe kuwasilisha ripoti hiyo bungeni wiki iliyopita, alimtaka Hosea kujiuzulu wadhifa huo baada ya kubainika kuwa alitumika kumsafisha Lowassa na kampuni hiyo.

Hadi sasa mawaziri watatu akiwemo, aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Ibrahim Msabaha waliamua kuachia ngazi.
 
TAKUKURU wawajibishwe

2008-02-16 08:59:29 Na Gaudensia Mngumi, Dodoma

Bunge la Tanzania limepitisha mapendekezo 23 ya kamati yake teule iliyokuwa ikichunguza mkataba tata dhidi ya Serikali na kampuni ya Richmond,


1. moja ya mapendekezo hayo ikiwa ni kuitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ipanguliwe na wakuu wake kuwajibishwa.

2. Halikadhalika, bunge limeitaka serikali kuyafanyia kazi mapendekezo hayo ndani ya miezi mitatu ijayo na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji Bungeni.

3. Serikali imeahidi kuyafanyia kazi mapendekezo hayo mara moja na kwa hatua ya kwanza imeunda timu ya wataalam ya kuchambua mapendekezo ya taarifa hiyo.

4. Mbali na kuipingua TAKUKURU na kuwawajibisha wakurugenzi wake wakuu (akiwemo Bw. Hosea), Bunge linapendekeza serikali kuchunguza ili kupata taarifa halisi ya uchunguzi Taasisi hiyo juu ya kampuni ya Richmond kwani ile waliowasilisha, ikiwa hata haina, tarehe utakuwa si yenyewe.

5. Mapema akichangia hoja bungeni, Mbunge wa Nzega, Bw. Lucas Selelii (CCM), ambaye pia alikuwa mjumbe wa kamati ya kuchunguza Richmond alisema taarifa zilizowafikia zinaonyesha kufichwa kwa ripoti halisi ya taasisi hiyo.

6. ``TAKUKURU ilichunguza kwa miezi sita lakini taarifa waliyotoa haikuwa hata na tarehe, hii inaonyesha dhahiri kuwa taarifa halisi ilifichwa na umma ulipewa taarifa ya kupanga,``

7. alisema na kuongeza kuwa ``serikali ichunguze na ibaini faili lililokuwa na majina ya wamiliki wa Richmond linalosemekana kuvurugwa na kutuletea taarifa hizo katika mkutano wa 11 mwezi Aprili, mwaka huu``.


8. Katika mapendekezo mengine, serikali imeombwa iondokane na utaratibu wa kutumia mawakala katika ununuzi wa mitambo ya kuzalisha umeme na kuhakikisha kuwa wizara husika ina taarifa za bei halisi ya mitambo kila wakati.

9. Serikali pia imetakiwa kufanya marekebisho ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995.

10. Mengine ni kumtaka Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT) pamoja na Bodi ya Wakurugenzi wachunguze uhalali wa malipo ya dola za Marekani milioni 35,561,598 badala ya dola za Marekani milioni 30,696,598 zilizopaswa kulipwa kwa kampuni ya Dowans, kuiongezea meno Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2004 ili iweze kuchukua hatua pale kanuni za manunuzi zinapovunjwa.
 
Akisoma hotuba ya kuahirisha Bunge jana hadi Aprili 8 mwaka huu, Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda alisema serikali imekubali mapendekezo yote yaliyotolewa na Kamati Teule ya Bunge.

1. Kufuatia hatua hiyo serikali imeunda timu ya wataalamu ya kuchambua mapendekezo ya taarifa hiyo.

2. Alisema wajumbe wa timu hiyo ni Ikulu - Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tume ya Mipango, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Bodi ya Wasajili ya Wakandarasi.

3. Alisema wengine ni Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi (PPRA), Ofisi ya Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Tume ya Maadili.

4. Alisema timu hiyo itachunguza kwa kina taarifa ya Kamati Teule ya Bunge na pia taarifa za majadiliano zilizomo katika kumbukumbu za Bunge (Hansard).

`5. `Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge imetoa mapendekezo mbalimbali yanayotakiwa kufanyiwa kazi. Nalihakikishia Bunge kuwa tutayapa uzito unaostahili mapendekezo hayo kwa kuzingatia katiba, sheria, kanuni na taratibu mbalimbali za nchi yetu na kuwasilisha ushauri wake serikalini.``

6. Aliipongeza kamati hiyo kwa kazi nzuri. Alisema ni lazima serikali iwajibike ipasavyo na isizembee hadi kufikia hatua ya kuundiwa kamati na Bunge.

``Kwa nini serikali ifikishwe katika hatua ya kuundiwa kamati teule wakati inao uwezo mkubwa wenye utaalamu wa kutosha. Katika hili serikali haikuwajibika ipasavyo,`` alikiri Waziri Mkuu.

7. ``Kwa hiyo jibu sahihi kwa serikali ni kufanya kazi kwa umakini na uadilifu mkubwa. Ahadi yangu kwa Bunge hili ni kuhakikisha timu hii mpya ya mawaziri inatimiza wajibu wake ipasavyo,`` alisisitiza

8. serikali wamejifunza mengi na kuongeza kuwa utaratibu wa kuunda kamati teule upo kwa lengo la kuwezesha tu kuwepo kwa `checks and balances`.

9. Alikumbusha kuwa utaratibu wa kuunda kamati utumike inapobainika kuwa sheria, taratibu na kanuni mbalimbali zimepuuzwa na serikali katika utendaji wake.

10.Kwa hiyo, dawa ya kweli kwa serikali kuepuka kuundiwa kamati teule za bunge ni Serikali kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa na kutanguliza mbele uzalendo na maslahi ya taifa letu. Vinginevyo kamati hizi zitaendelea kuundwa,``alisema na kuahidi serikali kujipanga upya.
 
Quote: Hosea:-

``Nataka jamii ielewe kwamba kazi zangu nazifanya kwa mujibu wa miongozo ya kifungu 1971 cha sheria ya kupambana na rushwa. Kazi yetu haikuwa kusema kwamba mkataba huo ulikuwa mbaya au mzuri. Sheria hiyo inataka taasisi kuchunguza iwapo kuna rushwa au hakuna, na sisi hatukuona kuwepo kwa rushwa,`` alisema.
``Rushwa inahusisha watu wakubwa, wenye uwezo mkubwa kiuchumi, baadhi yao wanamiliki magazeti� Hivyo, kupambana na rushwa sio jambo rahisi, wengine wanadhana kwamba kupambana na rushwa ni kuingilia maslahi yao,`` alisema.

Quote: Kamati Ya Mwakyembe:-

4. Mbali na kuipingua TAKUKURU na kuwawajibisha wakurugenzi wake wakuu (akiwemo Bw. Hosea), Bunge linapendekeza serikali kuchunguza ili kupata taarifa halisi ya uchunguzi Taasisi hiyo juu ya kampuni ya Richmond kwani ile waliowasilisha, ikiwa hata haina, tarehe utakuwa si yenyewe.

5. Mapema akichangia hoja bungeni, Mbunge wa Nzega, Bw. Lucas Selelii (CCM), ambaye pia alikuwa mjumbe wa kamati ya kuchunguza Richmond alisema taarifa zilizowafikia zinaonyesha kufichwa kwa ripoti halisi ya taasisi hiyo.

6. ``TAKUKURU ilichunguza kwa miezi sita lakini taarifa waliyotoa haikuwa hata na tarehe, hii inaonyesha dhahiri kuwa taarifa halisi ilifichwa na umma ulipewa taarifa ya kupanga,``

7. alisema na kuongeza kuwa ``serikali ichunguze na ibaini faili lililokuwa na majina ya wamiliki wa Richmond linalosemekana kuvurugwa na kutuletea taarifa hizo katika mkutano wa 11 mwezi Aprili, mwaka huu``.


Hosea, aachie ngazi tu maana haya yliyosemwa na kamati ni aibu kwake na taasisi nzima, kama sio taifa letu zima.
 
Wana Jf Mesoma Ya Aougust????????subirini Maajabu Ya Dunia Wanakuja Wengi Tu.....
 
Nadhani tukirudi nyuma katika msukosuko wa BOT tutaona kwamba Bilali pia alikuwa na kiburi kama huyu Hosea. Bilali pia aliwaambia watu wa magazeti kwamba hatajiuzulu na mara tu akatoweka kwenda USA na hapo akaandika barua ya kujiuzulu.
Sasa huyu Hosea siku zake zimekwisha fika na ni zile dakika za mwisho tu ndizo zilizobakia. Kama hataki kujiuzulu basi atafukuzwa na rais J.Kikwete.

Lakini kama kiburi chake kitaendelea hivi basi tutamuomba rais J.Kikwete ampe fundisho la kutosha. ATASTAAFISHWA KWA MANUFAA YA UMMA. Akipewa uamuzi huu kutoka kwa rais J.Kikwete basi hapatia kazi tena katika serikali ya Tanzania na mashirika yote ya serikali.
Atabkia naye kuuza ASALI kama wale wengine.Huwezi kuupotoza umma na halafu ukabakia kwenye cheo chako na kuzidi kusema uwongo.
 
Naanza kupata wasiwasi na PhD ya huyu ndugu Hosea. Hivi anataka kutuambia nini tuamini anachosema? Inakuaje siku 45 watu wameona kuna kasoro na kasoro hizo chanzo ni rushwa. Hata majivu hakuyaona. Taarifa toka kwa wafanyakazi wa PCCB ni kwamba taarifa ya uchunguzi iliyotelwa na Hosea kuhusu richmond ilifanyiwa editting baada ya kuonekana majina ya watu wazito kuhusika moja kwa moja. Waliochunguza sakata hilo waote wamehamishwa toka ofisi za PCCB makao makuu. Kama wanabisha waseme tuwaweke ubaoni
 
Kwa mantiki hii mimi na wadau wengine ndio maana tunashawishika kukubali kuwa Mhe.HOSEA anawajibika katika sakata hili la Richmond unless aje na maelezo ya kuridhisha zaidi lakini sio kujibu wadau kwa jazba.[/QUOTE]

wana JF, nimepitia hoja hii nzito kuhusu HOSEA, lakini TAARIFA ya MWAKYEMBE imetuacha SOLEMBA. Kwa sababu haijawataja watuhumiwa ili tuwajue na ushahidi wa kuwa na hisa katika RICHIMOND.

Inaonekana Mwakyembe anamuogopa LOWASSA ndiyo maana kamsafisha mwishoni, SIASA NI MCHEZO MCHAFU. Kwa nini nasema hivyo?, kwa sababu:-
1. Hosea anaweza kutuzidi maarifa akituomba tumpe kifungu cha Sheria Na. 16 ya kuzuia rushwa kinachohusu HARUFU YA RUSHWA, MAZINGIRA YA RUSHWA na Mkataba mbovu.
2.Mwakyembe amekanusha kumtaja ROSTAM AZIZ, sasa nani atamsaidia Hosea kutaja watuhumiwa,
3.Ukurasa wa 18 wa taarifa ya Mwakyembe umeelezea vipengele vitano katika taarifa ya HOSEA kama ifuatavyo:-
-Mchakato wa kumpta Mzabuni ulikuwa wa wazi na ushindani:

Kamati ya Mwakyembe ingejua kuwa Wizara ya madini ina uwezo
kisheria kusimamia mchakato wa manunuzi kwa niaba ya TANESCO
kwa kuwa ni wizara moja, hata Wizara nyingine ingefanya kazi
hiyo kama haja ipo ya kufanya hivyo.

-Hakuna ushahidi uliopatikana kuthibitisha vitendo vya
Rushwa,.... Pia hakuna ushahidi uliopatikana wa afisa yeyote
serikalini kumiliki hisa au madaraka katika Richmond....

Tume ya Mwakyembe imetuletea majungu ambayo hayawezi
kutusaidia kuwapeleka watuhumiwa mahakamani. Tume ina jukumu
la kumsaidia Hosea kupambana na rushwa kwa kuwa ni janga la
kitaifa, ushahidi wa kisheria unapokosekana, uwajibishaji wa
kisiasa, kiutawala unaweza kutumika kupunguza kasi ya rushwa.

Labda TUME ingependekeza HOSEA awekewe kipengele cha sheria
itamruhusu kushughulikia kuwawajibisha watuhumiwa kwa HARUFU
ZA RUSHWA AU MAZINGIRA YA RUSHWA!

Kwa kasi ya Hosea akipewa nafasi ataua watu kwa pressure!

-Kamati maalumu iliyoundwa haikupata muda wa kutosha kuifanyia
uchambuzi kampuni ya RICHMOND...

Huo ni udhaifu mkubwa ambao TAKUKURU waligundua na kwa
udhaifu huu matokeo mabaya yalianzia hapa.

Kwa hiyo atafutwe aliyepaswa kurekebisha kasoro zinazotokana
na kamati iliyoundwa na LOWASSA, MSABAHA AU KARAMAGI!

-Utafiti wa kina haukufanywa kutambua uwezo wa
kampuni .....Richmond ....!

TAKUKURU walitimiza wajibu wao wa kuishauri serikali katika
hili, wasingeweza kuanzisha kesi mahakamani bila kuwa na
ushahidi na watuhumiwa.

TUME itupe majina halisi ya watuhumiwa wa RUSHWA na siyo
SIASA!

-Mapungufu machache yaliyokuwepo lakini ni ya 'kawaida
kiutendaji' na hayakuhusisha rushwa au .....

Tume ya MWAKYEMBE iliegemea kipengele hiki, ikumbukwe kauli
hii inayotolewa kwenye vyombo vya habari ni UFUPISHO wa
maelezo marefu na mengi mno ukimpa nafasi mhusika kujieleza!

HATA hivyo sisi wataalam wa habari tunajua kuwa HOSEA ana maadui wengi nje(hata baadhi ya wabunge) na ndani ya TAKUKURU tukianzia na msaidizi mkuu wa Hosea (Lilian Mashaka) hutuuzia habari nyeti, lakini wakati wa TUME hii kulikuwa na mawasiliano ya karibu sana Dr. Mwakyembe, wakati sisi wataalam tunaijua picha yote!

Mwakyembe, Lilian Mashaka, awadhi Mohamed na wengine tumewahifadhi tupeni majina ya watu gani wapelekwe mahakamani?

Pia TUME itoe kila kifungu cha sheria iliyokiukwa na kila mtuhumiwa kwa kuwa ina wataalam wa sheria waliobobea, mtaani tumeikosa sheria inayotokana na maoni yao.

NAIPONGEZA TUME KAMA HARUFU ZA RUSHWA UWAJIBISHAJI WAKE UWE NI WA KIUTAWALA NA KISIASA kila tunapokosa ushahidi wa kina. Pia kukosa ushahidi wa moja kwa moja iwe ni mwanzo wa tume kama hii kusaidia kupiga vita rushwa!

SANDE
 
Nadhani tukirudi nyuma katika msukosuko wa BOT tutaona kwamba Bilali pia alikuwa na kiburi kama huyu Hosea. Bilali pia aliwaambia watu wa magazeti kwamba hatajiuzulu na mara tu akatoweka kwenda USA na hapo akaandika barua ya kujiuzulu.
Sasa huyu Hosea siku zake zimekwisha fika na ni zile dakika za mwisho tu ndizo zilizobakia. Kama hataki kujiuzulu basi atafukuzwa na rais J.Kikwete.

Lakini kama kiburi chake kitaendelea hivi basi tutamuomba rais J.Kikwete ampe fundisho la kutosha. ATASTAAFISHWA KWA MANUFAA YA UMMA. Akipewa uamuzi huu kutoka kwa rais J.Kikwete basi hapatia kazi tena katika serikali ya Tanzania na mashirika yote ya serikali.
Atabkia naye kuuza ASALI kama wale wengine.Huwezi kuupotoza umma na halafu ukabakia kwenye cheo chako na kuzidi kusema uwongo.


WanaJF, tuachane na siasa, soma taarifa ya MWAKYEMBE, linganisha na majibu ya Hosea zanzibar.

Kila mmoja wetu atupe majina ya wala rushwa waliotajwa na kama na katika kurasa zipi.

MWAKYEMBE aishauri serikali kubadili sheria ya rushwa ili iwe sheria ya harufu na mazingira ya rushwa tuone kama watasalimika watu hapa.

Naifagilia Tume ya mwakyembe, itupe majina ya watuhumiwa kama kweli imewagundua.
 
SANDE SIJAKUELEWA HATA MOJA INGAWA NIMERUDIA SANA KUSOMA POST YAKO.
unaweza kutufafanulia zaidi?? au nawe uliisoma ripoti ya mwakyembe juu juu?
 
SANDE SIJAKUELEWA HATA MOJA INGAWA NIMERUDIA SANA KUSOMA POST YAKO.
unaweza kutufafanulia zaidi?? au nawe uliisoma ripoti ya mwakyembe juu juu?

Msanii, Sande anataka apewe majina ya wala rushwa kwa ushahidi wa tume ya Dr. Mwakembe.

Mimi nafikiri tumtafutie majibu badala ya kulumbana wana-JF, mimi bado sijapata majibu lakini nayatafuta nitamjibu.

Shabani.
 
SANDE SIJAKUELEWA HATA MOJA INGAWA NIMERUDIA SANA KUSOMA POST YAKO.
unaweza kutufafanulia zaidi?? au nawe uliisoma ripoti ya mwakyembe juu juu?

mkuu sande nimekupata baada ya mrisho kufafanua
naomba kufuta kauli yangu ya awali niliyoiquote hapo juu
 
Msanii, Sande anataka apewe majina ya wala rushwa kwa ushahidi wa tume ya Dr. Mwakembe.

Mimi nafikiri tumtafutie majibu badala ya kulumbana wana-JF, mimi bado sijapata majibu lakini nayatafuta nitamjibu.

Shabani.

Hoja ya sande kama ni ya kweli, MWAKYEMBE na kamati yake wanastahili kushtakiwa kama hakuna ushahidi wa rushwa na siyo HARUFU YA RUSHWA AU MAZINGIRA. La, itungwe itungwe sheria mpya ya kuzuia rushwa itakayotamka HARUFU ZA RUSHWA NA MZINGIRA YA RUSHWA!

Naifagilia tume ya mwakyembe.
 
unajua nashsngaa sisi waTz mbona kikwete hahusishwi katika richmond???
nani mwenyekiti wa baraza la mawaziri? yapi yaliyopindishwa katika kikao cha baraza la mawaziri? kikwete alichukua hatua gani muda wote huo? kwanini kikwete alimuondoa yule mama mwakilishi wa IMF kurudi kwao ?
kwanini hakumfukuza msabaha baada ya huyo mama kumwambia hilo, badala yake akafanya mabadiliko ya mawaziri akaingia karamagi?

ni kitu gani alimwambia msabaha kamgeuka kule msibani kwao bagamoyo?
kwanini file la usajili brela limepotea?
kwanini ridhwani kikwete aliuza share zake kwa ama lowassa ama rostam?

kama tunataka kumaliza tatizo sio hawa watoto wa ufisadi kikwete aondoke mwenyewe kwanza.
jiulize hili:
unajua kikwete alimwambia lowasa asiwatimue richmond kama city wotbaada ya lowasa kuona hawa jamaa hawaeleweki. na unajua kuwa kikwete aliandika kimemo ili lowasa asiwatimue hao jamaa?

tumwombe lowassa aseme ukweli hamwezi kuamini hilo, unajua ni kwanini kamati kuu ya chama ilitumika kummaliza lowassa?
tutazame mbali tusifarijike na utumbo huu wa kikwete hana lolote na kama atamaliza miaka yote 5 ni bahati kila kashfa yumo waombe bungeni IPTL uone kikwete ataugua kabisa!!!!!!

hebu jadilini kikwete na nafasi yake katika richmond na document zote alipewa kopi azisome je alijibu nini kama sio NDIYOOOOOOOOOOO?????
 
Asante sana kwa uchangiaji wenu,unaoruhusu hoja pinzani nazo kujikita mahala,mie nauita ni "open minded thinking".
Kwenye ile taarifa ya kamati kuna mambo mengi sana na ndio maana waziri mkuu hata kaunda kamati nyingine kupitia yale mapendekezo na kuona ni jinsi gani yanatekelezeka bila kuathiri haki za watu au kuwaonea wengine. Kikubwa kilichobainika na kamati ya mwakyembe ni ukiukwaji wa wazi wa taratibu za tendering uliofanywa na wizara,maafisa wake na kitu kinachoonekana kama shinikizo la waziri mkuu. Ukiukwaji wa taratibu huo kwa wenyewe sio rushwa tena kisheria unafall katika administrative law,bali umebeba pia mambo mengine kibao yanayoibua masuala mengine ya kisheria. Point kubwa hapa ni ukiukwaji wa sheria ya tendering na kutofanya due diligence ambayo inategemewa kwa reasonable man wa calibre ya AG,na maafisa wa wizara.
Ukiukwaji kama huu kwa kawaida adhabu zake zipo administratively sio judiciary.Adhabu zao ni kama kushushwa vyeo,kuhamishwa vitengo kwani vile walivyopo sio competent n.k.Sasa HOSE yeye anakuja wapi? Kila mtu katika ile ripoti anasehemu yake aliyochangia kama ni nengligence tunasema contributory negligence.
Kama walivyo wengine HOSEA sehemu inayomgusa ni hii:
Ukisoma kifungu cha 6 cha sheria hiyo ya zamani kinasema kwamba
mtu yeyote ambaye kwa kujua atampa wakala, au wakala yeyote kwa kujua atatumia kwa lengo la kumdanganya mkuu wake, risiti,akaunti au hati au nyaraka yoyote inayohusiana na mambo au shughuli yoyote ya mkuu wake wa kazi na ambayo ina taarifa feki,za kughushi au zilizopotoshwa na kwa jinsi yoyote ile zina lengo la kumdanganya mkuu,atakuwa ametenda kosa.mwisho wa kunukuu.

Sawa Hosea hakuona rushwa,je hakuona pia kipengele hiki cha sheria? je katika mkatba wa richmond hakukuwa na nyaraka feki zenye lengo la kumpotosha mkuu,je kusema kwamba richmond ina ubia na kampuni ile waliyoitaja na kuthbitisha hilo kwa business kadi hakukuwa na lengo la kumpotosha mkuu?je,ukweli kwamba richmond haikuwa mtu kisheria yaani sio kapuni halali kwa kuwa inakosa usajili tanzania na huko USA haipo na kwamba hata kama ilisajiliwa hapa nchini usajili wake haukuwa halali kwa kuwa hatuna one man company kwa mujibu wa kifungu cha tatu,moja cha sheria ya makampuni.je,waliohusika hawakuwa na lengo la kumpotosha mkuu?


Hapa tu,akiclear hapa anapeta,mi ningekuwa wakili wake ningejikita kutafuta defense mahali hapa zaidi,kwani sehemu nyingine zote za sheria namba 16 yupo clean.Hatuna sheria ya harufu wala moshi wa rushwa.Neno harufu au moshi wa rushwa linatokana na sheria ya ushahidi ya ya mwaka 1967 nadhani THE LAW OF EVIDENCE ACT,kifungu cha 3 hadi 15 kinachozungumzia circumstancial evidence, Circumstancial evidence ndio inayounda mazingira au harufu ya tukio la rushwa. Ndio maana nikasema hata katika kesi ya balozi mahalu inayoendelea hakukuwa na rushwa ya moja kwa moja kesi imeenda mahakamani on circumstantial evidence.Na kesi za namna hii huwa ngumu sana kuliko zile za kumshika mtu papo kwa hapo.
Hayo yote ya kamati kuwataja watuhumiwa au la sioni kama ni msingi sana kwa mhe.Hosea ambaye namheshimu sana kama mwalimu wangu somewhere.Ila ni wazi wenzie hata kama wana hila mbaya naye wanataka kumkamatia hapa.Ningeomba mtu mwenye ripoti ya HOSEA atumwagie hapa ile tuweze kujadili vizuri zaidi kwa kuilinganisha na findings za mwakyembe.
 
Back
Top Bottom