Alizwa Pesa na Hawara, Arudi Kwa Mkewe Kuomba Radhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alizwa Pesa na Hawara, Arudi Kwa Mkewe Kuomba Radhi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Jul 28, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,158
  Likes Received: 5,589
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Alizwa Pesa na Hawara, Arudi Kwa Mkewe Kuomba Radhi[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #e1e1e1"]
  [TD]

  [/TD]
  [TD]Tuesday, July 26, 2011 6:09 PM
  HASSAN ABDUL [39] mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam, amemuangukia mke wake kwa kutembea kwa kutumia magoti kwa lengo la kuomba radhi baada ya kufilisiwa na kuibiwa fedha na aliyekuwa hawara yake[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Hatua hiyo ya kuomba radhi imekuja baada ya mwanaume huyo kugundua kuwa alikuwa ameibiwa fedha kiasi cha shilingi milioni ishirini na tano na mwanamke aliyekuwa na uhusiano nae wa kimapenzi aliyemtaja kwa jina la Husna [27] kwa kuiba kadi ya ATM na kwenda kuiba fedha hizo na kutimkia kusikokujulikana.

  Mwanamke huyo aliiba kadi ya kutolea fedha bila mwanaume huyo kutambua kwa kuwa siku aliyoiba alizidiwa na kinywaji na kufanikiwa kwenda kutoa fedha hizo na kutimka nazo kusikojulikana.

  Abduli alidai kuwa, mwanamke huyo alifanikiwa kuiba fedha hizo kwa kuwa alikuwa anafahamu namba yake ya siri na mara kwa mara huitumia kwa kuwa walikuwa wakiaminiana na kudai hata namba ya siri ya kadi ya mwanamke huyo alikuwa anaifahamu.

  Mara baada ya mwanamke huyo kutoa fedha hizo alirudisha kadi hiyo nyumbani kwake ili mwanaume huyo akija aikute na kuchukua vitu muhimu ambavyo aliona vingemsaidia na kuacha kila kitu kama kilivyo ndani ya chumba hicho na kutokomea mitaani.

  Hatua hiyo ya kuomba radhi imekuja baada ya baadhi ya marafiki wa karibu na Abduli kumpa hongera mke wa Abduli kwakuwa Abduli alinunua shamba na kiwanja kwa wakati pamoja na pia walimtaka mke huyo wa Abduli awe makini na mkopo aliyochukua Abduli.

  Ndipo mke huyo Khadija [29] aliyebahatika kuzaa nae watoto wapatao wawili alipofahamu mambo hayo na kumbana mume wake kuhusu manunuzi ya viwanja hivyo ikiwemo na mikakati ya kutumia mkopo huo.

  Ndipo Abduli hakuwa na cha kuongea kuhusiana na fedha hizo kwa kuwa hawara yake alishamuibia ikiwemo na hati ya manunuzi ya shamba ambalo alikuwa amemnunulia.

  Abduli aliitisha kikao cha wazee na kumuomba radhi mke wake na kufafanua jinsi alivyoibiwa fedha hizo na kufafanua hati ya kiwanja ameihifadhi na kubainisha shamba alikuwa amemnunulia mwanamke huyo ambaye amemuibia kwa kuwa alikuwa na ujauzito wake.

  Hata hivyo mke wa Abduli alilia kwa uchungu kusikia maneno hayo na ghafla alianguka chini na kupoteza fahamu kwa dakika kadhaa na kupelekea awahishwe zahanati kwa matibabu.

  Haijajulikana kama mke wa Abduli amekubali kumsamhehe mumewe kwa aliyoyafanya au la.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. L

  Laura Mkaju Senior Member

  #2
  Jul 28, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 194
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mhh!! wala hahitaji kupewa msamaha, bali amevuna alichopanda.
   
 3. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Hadithi hii haina ukweli kwa sababu zifuatazo:
  1. Aliwezaje kuchukua Sh. 27millioni kwenye ATM kwa siku moja? maana ATM ina ukomo wa kuchukua pesa kwa mara moja na katika saa 24, na katika ATM zote huwezi kuchukua pesa zaidi ya milioni moja kwa siku moja.

  2. Pesa hizo yawezekana ziliwekwa na huyo mwanaume kwenye account ya hawara, na hawara akapotea kusikojulikana, so mwanume akatunga hadithi ya kuibiwa pesa kwenye account yake wakati ukweli ni kuwa ni yeye mwenyewe aliziweka au alimpa huyo hawara taslimu.
  3. Kama hati za ununuzi wa shamba alikuwa nazo hawara, huwezekano kwamba na pesa alipewa hawara na siyo kwamba aliibiwa ni 99%.
   
 4. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Hapa ndio kwa wale wanaosave na waume zao pesa zao na kujihudumia kwa kila kitu kwa kigezo cha woman power, mwenzio anatumia tu na mwanamke bila huruma, sababu anajua wewe unapenda majukumu naa unaweza kujihudumia.kuweni makini mtalizwa mchana kweupe?????
   
 5. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #5
  Jul 28, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,401
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  malipo ni hapa hapa duniani
   
 6. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  Mmmmh......! Hilo nalo neno kwakweli!
   
 7. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ee Mungu turehemu, tuepushe na majanga kama haya, tupe akili ya kukimbia. Lakini usitutie majaribuni..... Amen
   
 8. B

  BeNoir Member

  #8
  Jul 28, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na ukimwi huu bado tu watu wako busy!!!!!!!!
   
 9. NYENJENKURU

  NYENJENKURU JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  .Huyo jamaa anatunga tu.Uwezi kuchua zaidi ya 1MIL kwa ATM za Tanzania.Labda kama pesa alikuwa nazo huyo mama.
   
 10. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #10
  Jul 28, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Huyu hawara:
  1. Amemuambukiza jamaa UKIMWI.
  2. Amemuibia jamaa mihela!
  3. Amevuruga ndoa ya jamaa
  4. Amemuachia jamaa deni kubwa alipokopa hizo hela.
  5. Amempandishia mke wa jamaa presha.
  6. Amemshushia jamaa hadhi mbele jamii inayomzunguka!
  Tabu tupu!
   
 11. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #11
  Jul 28, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Nilikuwa naisoma hii habari naona huyu jamaa katunga uongo ambao unashikwa kijinga kabisa
   
 12. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #12
  Jul 28, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Ngereja, nakubaliana na wewe 100%. Jamaa kampa kwa hiari yake mwenyewe, sasa ddem kapotea ndo anatunga uongo. tungemuelewa kama dem katoroka na atm.
   
 13. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Duh kuna dogo mmoja mitaa flani hivi kaachana na mkewe baada ya ndoa ya miezi km minne tu, akajifanya mjanja akajirusha MEEDA akaopoa mtoto matata sana, tatizo dogo mgeni sijui pande hizo, demu bana akampa chuchu jamaa anyonyeee weeeeee hahahhahha jamaa akalala usingizi fofofo demu akachukua wallet ya jamaa, halafu kwenye wallet jamaa alikuwa kakusanya mafao yake ya mwezi demu akalamba kila kituuu. kesho yake jamaa anaamka aanajikuta mweupeeeeeeee anabaki kumlaumu ex wife wake eti ana gundu hahahahahaha
   
 14. Ennie

  Ennie JF-Expert Member

  #14
  Jul 28, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 7,145
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Pumbavu sana huyo jamaa,asingefilisiwa na huyo hawara yake ange confess? Eti amemnunulia shamba kwa vile ana mimba yake,mkewe aliyezaa watoto wawili amemnunulia nini? Mkopo kachukua kimya kimya,shamba kanunua kimya kimya leo amesafishwa ndio anarudi kwa wife wafunge mkanda deni lilipwe! Wanaume wakware aaarrghh!
   
 15. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #15
  Jul 28, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Wewe umewahi kumliza mtu?

  Tiba
   
Loading...