Alizaliwa Mweusi Lakini Amebadilika Rangi na Kuwa Mzungu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alizaliwa Mweusi Lakini Amebadilika Rangi na Kuwa Mzungu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Babuji, Jul 27, 2009.

 1. B

  Babuji Senior Member

  #1
  Jul 27, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  'Tafadhali Mungu, ibadilishe ngozi yangu niwe kama mzungu' nilikuwa nikiomba dua kila siku kabla ya kulala. Kwa kawaida mtu ungeona ni ndoto lakini kwangu imekuwa kweli kwani hivi sasa nimekuwa mweupe na naonekana kama mzungu' Hayo ni maneno ya Luke Davis ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 44 ambaye alizaliwa akiwa mweusi 'tii' kutokana na baba mwafrika toka Nigeria na mama mzungu kutoka Ireland.

  [​IMG]
  [​IMG]

  "Nikiwa na umri wa miaka mitano nilikuwa nikisali kila siku nikimuomba mungu abadilishe rangi ya ngozi yangu niwe mzungu. Nilikuwa nikikaa kwenye nyumba ya kulelea yatima nikiwa na watoto wengi wa kizungu ambao mara kwa mara walikuwa wakininyasasa kwa rangi ya ngozi yangu" hayo ni maneno ya Luke Davis ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 44 ambaye alizaliwa akiwa mweusi 'tii' kutokana na baba mwafrika toka Nigeria na mama mzungu kutoka Ireland.

  Nikiwa na umri huo wa miaka mitano nilishafahamu kuwa katika dunia hii kuna vitu ambavyo mtu huwezi kuvipata au kupewa kama rangi ya ngozi yako ni nyeusi.

  "Tafadhali Mungu, ibadilishe ngozi yangu niwe mzungu kama wenzangu" nilikuwa nikinong'ona nikiomba dua kila siku kabla ya kulala. Kwa kawaida mtu ungeona ni ndoto lakini kwangu imekuwa kweli.

  Leo hii nikiwa na umri wa miaka 44, kutokana na ugonjwa wa rangi ya ngozi wa vitiligo nimekuwa kama mzungu.

  Ukiniona mtaani hutafikiria hata kidogo kuwa zamani nilikuwa ni mtu mweusi.

  Alama pekee ya rangi yangu ya asili ni ni kijialama kidogo mgongoni cha rangi nyeusi ambacho hakizidi unene wa sentimeta moja.

  Ingawa ubaguzi wa rangi umeendelea kuisumbua jamii, siku hizi nina maisha bora nikiwa kama mzungu.

  Ingawa watu wengi wataendelea kupinga kuwepo kwa ubaguzi wa rangi hapa Uingereza naweza kukwambia kuwa ubaguzi huo bado upo.

  Naamini mtu yoyote mweusi anayeishi nchi hii anajua hilo na lazima atakuwa ameishakumbana na matatizo hayo.

  Kwa mfano niliwahi kutakiwa kufanya kazi kwenye bucha ingawa nilikuwa sijui chochote kinachoendelea kwenye kazi hiyo na nisingepewa kazi hiyo kama ningekuwa mweusi.

  Baada ya kupewa kazi hiyo mmiliki wa bucha hiyo aliniambia wazi kuwa kazi hizo hazikuwa kazi ambazo watu weusi walikuwa wakiruhusiwa kuzifanya.

  Nilinyong'onyea kusikia hivyo. Niliamua kuikataa kazi hiyo kwakuwa nilifikiria nitakuwa kama vile nimeidharau asili yangu.

  Nikiwa kama mtu mweupe sasa hivi sihofii tena kutukanwa au kushambuliwa barabarani vitu ambavyo nilivizoea sana nilipokuwa mweusi. Najua marafiki zangu weusi wanaendelea kusumbuliwa hivyo hadi leo.

  Wakati tulipokutana wanafunzi wa zamani wa shule yetu, nilishuhudia rafiki yangu wa zamani ambaye alikuwa ni mweusi akipachikwa majina ya kibaguzi na wazungu waliokuwa wamelewa.

  Nilikasirika sana lakini nashukuru ngozi yangu ni nyeupe na siku hizi sipati matatizo kama hayo tena.

  Hakuna kitu nilichofurahia kama watoto wangu wawili wa kike ambao hivi sasa wana umri wa miaka 22 na 20 walipozaliwa wakiwa weupe kama wazungu wakiwa hawana hata doa moja la damu yangu ya Kinigeria.

  Tangia walipozaliwa nimemshukuru mungu kuwa wamezaliwa weupe kwahiyo hawatapuuzwa kutokana na rangi ya ngozi zao.

  Story kamili gonga hapa
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2639434&&Cat=7
   
Loading...