Aliyoyazungumza Rais Samia baada ya kuwasili nchini akitokea New York - Marekani

Nchi yake ni Zanzibar, akagombee Urais huko kwao...!

Huku ni Tanganyika na tunataka tuongozwe na raia na Rais Mtanganyika...

Kosa lilifanyika na akaupata Urais kama kuokota dodo chini ya mti muoarobaini. Hakuwezi kufanyika kosa kama hilo tena...

Na hakuna cha sijui muungano au baba yake muungano. Hayo ni ya Nyerere na Karume...

We have to stop this stupidity of the so called "unwillingly and forcefully union of Tanganyika & Zanzibar" once and for all...!!
Kudaadeki!

Mungu fundi sana 😁😁😁😁😁😁😁
 
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Samia Suluhu Hassan amerejea nchini na kupokelewa na watanzania wakiongozwa na Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (JNIA) jijini Dar Es Salaam leo tarehe 25 Septemba 2021 akitokea jijini New York nchini Marekani alikohudhuria Mkutano wa 76 wa Baraza la Umoja wa Mataifa.

Katika hotuba aliyoitoa baada ya kupokelewa, Rais Samia amesema yafuatayo kwa ufupi.​
  • SHUKRANI KWA WATANZANIA KWA MAOMBI.
Rais Samia amewashukuru watanzania kwa kuiombea safari ya kwenda Umoja wa Mataifa, Mwenyezi Mungu amewawezesha wameenda na kurudi salama. Rais Samia amesema "Niwashukuru watanzania wote kwa sala na dua zenu wakati wote mkiwa mnaniombea. Nivishukuru zaidi vyama vya siasa ambavyo vimekuja kuunga mkono na kunipokea; huu ndiyo utanzania."
  • TUIJENGE NCHI YETU KWA MATOFALI NA NONDO MADHUBUTI.
Rais Samia ameeleza kuwa taifa limejengwa katika awamu tofauti na kwa sasa sisi sote tunatakiwa kuungana na kulijenga taifa kwa matofali na nondo imara ili Tanzania isimame. Rais Samia amesema "Kuzungumza kwenye taasisi kama ile (Umoja wa Mataifa) ni jambo jema na la pili ni utekelezaji wa yale tuliyoyazungumza. Niwaombe sana watanzania wote tuungane, tushirikiane, tufanye kazi pamoja kujenga taifa letu (Tanzania). Taifa (Tanzania) ambalo kwa miaka 60 sasa limekuwa likijengwa kwa awamu na hatua mbalimbali. Kila awamu imekuwa ikiweka matofali katika kujenga taifa letu; niwaombe kwa umoja wetu, mshikamano na upendo tujenge kwa matofali na nondo madhubuti ili tuweze kulisimamisha vyema taifa letu."
  • TUMEIFAHAMISHA DUNIA KUWA TUPO IMARA
Rais Samia amesema Tanzania tulipata fursa ya kusema na ulimwengu ikiwa imewakilishwa na Mkuu wa nchi (Rais) baada ya miaka 6 na dunia imeelezwa kuwa Tanzania imara na itafanya kazi na dunia. Rais Samia amesema "Tumekwenda kwenye safari (Umoja wa Mataifa); safari ambayo kwa miaka sita tumekuwa tukiwakilishwa na ngazi ya uwaziri na ubalozi lakini hatukwenda kama kiongozi wa nchi (Rais wa JMT). Mara hii tumeweza, tumekwenda, tumeshiriki na dunia inawasalimia."

Pia akaongeza "Safari yetu tulipokelewa kwenye Umoja wa Mataifa na kusimama kwetu kama Tanzania na kuzungumza tuliwahakikishia ulimwengu na Umoja wa Mataifa kwamba Tanzania tupo na tupo imara na tutaendelea kufanya kazi na dunia."
  • FURSA MBALIMBALI ZA KIJAMII, KISIASA NA UCHUMI.
Rais Samia ameeleza kuwa katika safari hii kuna mambo mengi yamefanyika yenye manufaa kwa nchi yetu ikiwemo diplomasia, uwekezaji, mazingira, UVIKO-19 sambamba na kukutana na viongozi mbalimbali wa nchi na taasisi za kimataifa. Rais Samia amesema "Katika mkutano ule (Umoja wa Mataifa) tulikuwa na mambo manne makubwa; masuala ya uchumi kwa ujumla, masuala ya UVIKO-19, utawala bora na mambo ya mazingira. Kwa niaba yenu niliiahidi dunia na Umoja wa Mataifa kwamba Tanzania tutayafanyia kazi yote haya ili nasi twende na dunia inavyokwenda."

Pia ameeleza "Tulipata fursa ya kuonana na watu mbalimbali; nilionana na Rais wa Benki ya Dunia, Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Biashara Duniani, wafanyabiashara wa Marekani waliowekeza na wanaotaka kuja Tanzania, Marais kadhaa lakini orodha ilikuwa ndefu wengine nilimwachia Waziri wa Mambo ya Nje anisaidie kuwaona. Kwa ujumla Tanzania tuliombwa kuonana na watu wengi sana ambao wote wangependa kufanya kazi na sisi."

Kazi Iendelee

View attachment 1952410

View attachment 1952416View attachment 1952417
Hili taifa sijui watu wake wataacha lini ushamba wa kipuuzi. Sasa kulikuwa na haja gani ya kwenda kujazana pale airport wakati wangewe kwenda kukutana huko kwenye jumba lao la kupiga madeal
 
Nchi yake ni Zanzibar, akagombee Urais huko kwao...!

Huku ni Tanganyika na tunataka tuongozwe na raia na Rais Mtanganyika...

Kosa lilifanyika na akaupata Urais kama kuokota dodo chini ya mti muoarobaini. Hakuwezi kufanyika kosa kama hilo tena...

Na hakuna cha sijui muungano au baba yake muungano. Hayo ni ya Nyerere na Karume...

We have to stop this stupidity of the so called "unwillingly and forcefully union of Tanganyika & Zanzibar" once and for all...!!
Ndoto ni sehemu ya mawazo pia
 
... Rais Samia amesema "Tumekwenda kwenye safari (Umoja wa Mataifa); safari ambayo kwa miaka sita tumekuwa tukiwakilishwa na ngazi ya uwaziri na ubalozi lakini hatukwenda kama kiongozi wa nchi (Rais wa JMT). Mara hii tumeweza, tumekwenda, tumeshiriki na dunia inawasalimia."

Kwanini kiongozi wa nchi hakwenda kwa muda wote huo? Kwanini na yeye asiwakilishwe na mawaziri na mabalozi? Kilichofanya kiongozi wa nchi asiende wakati huo leo kimeisha?
Majukumu ya kitaifa yalikuwa mengi sana na Hayati Magufuli aliomba ayatekeleze na sasa Rais Samia ameona ni vyema aende. Yote ni mambo mema kwa manufaa ya taifa letu pendwa la Tanzania.
 
hahahaha alienda kuipasha dunia sio?
Rais anatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM.

Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020/2025 Sura ya Saba (7), Kipengele cha 132, ukurasa wa 184 inaelekeza:
"Kuimarisha sauti ya Tanzania na taswira yake katika medani ya uhusiano wa kikanda na kimataifa.”
 
Rais anatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM.

Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020/2025 Sura ya Saba (7), Kipengele cha 132, ukurasa wa 184 inaelekeza:
"Kuimarisha sauti ya Tanzania na taswira yake katika medani ya uhusiano wa kikanda na kimataifa.”
Hivi kuna Rais au mjumbe kutoka Taifa lolote lile ambaye katiba hotuba yake amesema anakubaliana au aumependezwa na hoja au msimamo wa Tanzania kama ulivyowasilishwa na huyo mama kwenye hiyo hotuba yake.

Kama yupo ningependa kujua.

Kama hayupo maana yake huyo mama aliongea utopolo tu.

Yaani mimi hiyo safari yake pamoja na hotuba yake, vyote viwili navifafananisha na safari ya mama Maria Nyerere kwenda kwenye mkutano wa kampeni wa Magufuri, pamoja na yale maneno yake kwamba wao wengine wamekwenda pale ili ionekane uwanja umejaa.


hicho ndio alikwenda Samia kufanya kwenye mkutano wa UN, Kujaza ukumbi, na kuonekana kwamba amekwenda.

hamna kitu kingine.

zaidi ametumia tozo vibaya, basi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom