Aliyoyazungumza Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mh. Simon Ezekiel Odunga katika vipindi vya power breakfast na alasiri lounge

ALWATAN KIZIGO

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
539
642
Wilaya ya Chemba ina ardhi kubwa ya kutosha yenye rutuba sana inayofaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali kama vile dengu, ulezi na mengineyo mengi. Karibuni sana Vijana kufanya kilimo katika wilaya ya Chemba.

Wilaya yangu inahakikisha asilimia 5 za Vijana na kina mama zinatoka na kuwafikia walengwa kupitia vikundi.

Bomba la mafuta kutoka Hoima mpaka
Tanga litapita pia na Chemba.Hivyo Chemba pia itanufaika na mradi huo kwa kiasi kikubwa.

Tunaupanga mji wa Chemba kuwa mji wa kisasa kwa kupima ardhi.

Tutatenga eneo maalumu kwa ajili ya Kazi za sanaa kama vile ilivyo Hollywood .

Chemba ni fursa adhimu kwa sababu makao makuu ya nchi yanahamia Dodoma
, hivyo kuna fursa kubwa za uwekezaji,biashara na viwanda kwa sababu umbali kutoka Dodoma mjini mpaka Chema ni Kilometa 137 tu.

Barabara ya Lami kutoka Dodoma mpaka Arusha inapita Chemba.Hivyo ni fursa nzuri kwa ajili ya wafanyabiashara wa maduka na nyumba za kulala wageni.

Tumechimba miundombimu ya kuvuna maji ya mvua katika mashule , miundombinu ambayo inaweza kuhifadhi maji kwa kipindi cha nusu mwaka.

Huku Chemba tumejiwekea sharti la kuchimbiwa visima vya maji katika kila mradi utaokuja kufanya Kazi na Wilaya yetu.Yani kama mkandarasi akipewa tenda basi ni lazima kwanza achimbe kisima cha maji kwa ajili ya wananchi.

Chemba kuna mifugo mingi karibuni wawekezaji wa viwanda vya ngozi na nyama .
Tunajenga machinjio ya kisasa Chemba.
Hakuna haja ya kuuza juice na vikaranga Dar Es Salaam wakati unaweza kuja Chemba ukfanya kilimo na ukapata hela nyingi kuliko hapa Dar.
Vijana njooni Chemba

Ofisi yangu iko wazi masaa yote kumpokea mwekezaji yeyote kwa mikono miwili anayetaka kuja kuwekeza Chemba ma tutampa ushirikiano wa kutosha.
 
Back
Top Bottom