Aliyoyatamka Nape Nnauye baada ya jaribio la kuuawa Tundu Lissu

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,203
23,020
Video clip hii inawakilisha silent sympathisers wa Tundu Lissu tuliomo ndani ya CCM. Tupo wengi tu.

Kwenye clip hii Nape Nnauye anaonyesha kuguswa, kusikitishwa na kuwa na hofu kubwa sana baada ya Tundu Lissu kumiminiwa risasi kadhaa. Ni wana CCM wengi tuliguswa na tukio lile ambalo lilituachia bumbuwazi na simanzi kubwa tusijue ni nini kilikuwa kinaendelea nchini.

Miaka 3 baadaye, bado hofu ndani ya chama chetu ni kubwa - ni vile watu tupo kimya tu lakini wengi wamenyamaza kwa ajili ya kutetea vitumbua vyao tu.

Lakini kusema za ukweli, wana CCM ambao hatukuzoea kuyaona na kuyasikia haya yanayoendelea - tunatamani upendo, amani na masikilizano virudi ndani ya chama chetu.

Hivyo basi tunaamini kabisa kwamba kambi ya upinzani ikichukua dola, itatusaidia sana wana CCM kurudi kwenye mstari na kujipanga kwa upya.

Huyu wa kwenye hii clip anatuwakilisha wana CCM wengi tu...

 
Nimewaza nikagundua utekaji ulishamiri wakati madelu akiwa waziri mambo ya ndani . ukapungua na kupotea alipotolewa
 
Kesi za jinai hazikomi hata Kama muhanga alishasamehe!
Kweli, upo sahihi mkuu!

Na ikipindishwa pindishwa basi vigilantes tutachukua hatua kwa kuwaadhibu wakosaji kadiri ya uzito wa kosa lao!

Mheshimiwa Lissu ameshawasamehe, wapenda haki bado tunataka haki itendeke, huwezi kumpiga mtanzania risasi mchana kweupe tukakuacha hivi hivi ukiendelea kutamba, unastahili kutangulia ukaonane na Mungu akupe adhabu yako mapema
 
Back
Top Bottom