Aliyoyasema Rais Kikwete Kabla hajagombea Urais... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyoyasema Rais Kikwete Kabla hajagombea Urais...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by zubedayo_mchuzi, Apr 18, 2012.

 1. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,922
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Ilikuwa februari 27.2005 alikuwa CCM MKOA WA PWANI.
  Rais wa jamhuri wa Muunagano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete Kabla hajajiingiya katika mpambano wa nafasi ya URAIS mwaka 2005 alitoa hutuba nzito katika Ofisi ya CCM MKOAN PWAN FEB 27 2005 Na kufafanua kilicho msukuma kugombea wadhifa

  Katika makala haya nitaeleza baadhi ya maneno aliyotamka Rais Kikwete ambayo yamo katika hotuba yake aliyoitoa kwa Waandishi wa habari waliokuwa wamehudhuria mkutano huo.

  Ni vizuri kurejea aliyo yatamka Rais Kikwete kabla hajagombea.Ili kama ni hukumu na lawama zimwendee kihalali pasipo kumwonea kisiasa.

  Hotuba ilianza kwa kusema "Ndugu waandishi wa habari,Nimekuwa natakiwa kutamka kama ninayo nia ya kugombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi wa mwaka huu 2005 au hapana
  Nimewaiten hapa leo kutamka rasmi kuwa nimeamua kufanya hvyo na kwamba wiki ijayo nitakwenda Dodoma kuchukua fomu kwa hiyo,alisema Dk kikwete.

  Kwanini Nimeamua kugombea.
  Nimeamua kugombea nafasi hii ya juu kabisa ya Uongozi wa nchi yetu kwa sababu zifuatazo
  (1) Nimeamua kuitumia haki yangu ya msingi ya kidemokrasia kama Raia wa Tanzania kwa mujibu wa katiba ya nchi yetu.Naamini ninazo sifa zinazotakiwa na katiba kwa mtu anayefaa kugombea nafasi hyo.

  (2) kufuatia mashauriano na Watu mbalimbali kama vile wazee,Vijana ,kinamama,wasomi,wakulima,wafanyakazi na wana CCM,Wamenipa Moyo wa kujitokeza na kunihakikishia kuwa wataniunga mkono.

  3. Hata hvyo natambua kwamba sababu hizo pekee hazitoshi.Nina hakika swali la msingi ambalo kila mtu atakuwa anajiuliza ni; HIVI huyu ndugu Anataka kuwa RAIS ila Afanye nini? Ni swali halali ambalo sina budi kulitolea maelezo na ufafanuzi.

  Nimeamua kujitokeza kuomba nafasi hii kwa nia ya kupata fursa ya kupendekeza SERA na Program za utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM NA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI.Kadhalika nipate fursa ya kuchukua hatua muafaka kwa masuala muhimu ya kitaifa na kimataifa ambayo ama hayakugusiwa kwenye ILAN au Mazingira ya Wakati huo yataelekeza yaangaliwe kwa Namna tofauti.

  Katika miaka kumi ya uongozi wa Awamu ya TATU YA MH.BENJAMIN .W.MKAPA.Nchi yetu imepata mafanikio Makubwa karibu ktk maeneo yote pamoja na uchumi,huduma za jamii,Miund mbinu,utawala bora na kidemokrasia

  Amani na utulivu vimeendelea kustawi na maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanaonekana.Hivi sasa Tanzania inasifika na kuheshimika Duniani KOTE.Mafanikio haya yanastahili kudumishwa na kuendelezwa kwa NGUVU MPYA.ARI MPYA NA KASI MPYA na Serikali ya Awamu ya NNE

  Kuimarishwa kwa Demokrasia na utawa

  Uhusiano wa kimataifa.

  Je katika vipindi vyote hvyo yametekelezwa.
  Mungu bariki Tanganyika Mungu Ibariki Tanzani.
   
Loading...