Aliyoyasema Msemaji Mkuu wa Serikali kwenye Mkutano wake na Wanahabari leo

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
YALIYOJIRI WAKATI MKURUGENZI WA IDARA YA HABARI – MAELEZO NA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI, GERSON MSIGWA AKITOA TAARIFA YA WIKI KUHUSU MASUALA MBALIMBALI YA UTENDAJI WA SERIKALI LEO SEPTEMBA 12, 2021 DODOMA.

# Kuna baadhi ya maeneo yamepata changamoto ya kukatika kwa umeme, ni kwa sababu ya kazi kubwa inayoendelea ya kubadilisha nguzo zilizooza, na hivi sasa Serikali imeamua kuweka nguzo za zege kwa lengo la kutatua changamoto hiyo.

# Hali ya uzalishaji wa umeme kwenye nchi yetu ni nzuri, tunaendelea kuzalisha zaidi ya Megawati 1,600, mahitaji yetu ni Megawati 1,200 na tuna ziada ya Megawati 400.

# Kuna sehemu chache za nchi yetu ambazo bado hazijafikiwa na gridi ya Taifa, ikiwemo Mkoa wa Kigoma, wiki iliyopita wananchi wa Kigoma walipata changamoto ya mgao wa umeme, ambapo Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani alikwenda kufanyiakazi changamoto hiyo.

# Mkoa huu wa Kigoma ambao unapata umeme kwa kupitia uzalishaji wa majenereta, kuna changamoto moja ya kimsingi kwamba Kigoma inahitaji Megawati 8 ili iweze kutimiza mahitaji yake, lakini umeme unaozalishwa pale kwa kiwango cha juu ni megawati 7.9 kwa hiyo ikitokea hitilafu ya uzalishaji wa umeme ule wa Megawati 5 za umeme wa jua, basi mkoa unapata changamoto hiyo.

# Hata hivyo Serikali imeamua kupeleka mashine nyingine 2 ili kuongeza katika mashine zinazotumia mafuta kwa ajili ya uzalishaji wa umeme, na matarajio yetu ni kwamba hadi kuifikia Disemba mwaka huu mashine hizi mbili zitakuwa zimezalisha takribani Megawati 2.5 kuongezea pale kwenye Megawati 7.9 na hivyo kuanzia mwezi Disemba mwaka huu Kigoma haitakuwa na tatizo la umeme.

# Juhudi kubwa inayofanywa na Serikali ni kuunganisha na Gridi ya Taifa huu Mkoa wa Kigoma na maeneo mengine ambayo hayajafikiwa na Gridi ya Taifa, kwa kujenga “line” ya Msongo wa Kilovoti 33 yenye urefu km 42 kutoka Nyakanazi hadi Kakonko, na hii itafanya Wilaya ya Kibondo kuunganishwa na Gridi ya Taifa, kazi hii itakamilika mwezi Disemba 2021.

# Pili Serikali inakamilisha ujenzi wa line ya Msongo wa Kilovoto 33 yenye urefu wa km 22, hii inaunganisha Wilaya ya Kasulu na Kibondo na mradi huu utakamilika mwezi Desemba mwaka huu.

# Na hivyo Wilaya ya Kasulu itaunganishwa na Gridi ya Taifa kutokea Kibondo, pia kukifanya kile kituo cha Kasulu kuzalisha Megawati 3.75 na kupeleka Kigoma. Sasa Kigoma itakuwa na Megawati 12 na hivyo kumaliza kabisa tatizo la umeme.

# Serikali inakamilisha ujenzi wa Msongo wa Kilovoti 132 yenye urefu wa km 395 kutoka Tabora hadi Kigoma kupitia Nguruka, mradi huu utagharimu fedha za ndani kiasi cha shilingi bilioni 69 na utakamilika mwezi Oktoba 2022, njia hii itaunganisha Mkoa wa Kigoma na Gridi ya Taifa kupitia upande wa Tabora.

# Vilevile Serikali inakamilisha mradi wa ujenzi wa umeme katika mto Malagarasi utakaozalisha Megawati 49.5 na mradi huu ukikamilika utakua umeongeza umeme katika Gridi ya Taifa na sasa umeme utaanza kupelekwa katika maeneo mengine ya nchi na mradi huu utakaokamilika Disemba 2024 utagharimu shilingi bilioni 308.

# Baada ya mabadiliko ya Menejimenti yaliyofanywa pale MSD kuwezesha wataalamu pamoja na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali na sasa hali ya upatikanaji wa dawa imeanza kuimarika.

# Kati ya mwezi Machi na Agosti, Serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 263 ambazo zimesaidia kununua dawa kwa bei nafuu, na kati ya hizo shilingi bilioni 223 zimetumika kununua dawa na shilingi bilioni 39 zimetumika kuwalipa wazabuni.

# Hali ya upatikanaji wa dawa kwenye vituo vyetu kupitia MSD imeongezeka kutoka asilimia 21 hadi asilimia 62, matarajio ya Serikali ni kuwa upatikanaji wa dawa kuendelea kuimarika.

# MSD imefanya jitihada mbalimbali kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa dawa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha inaagiza dawa kutoka kwa wazalishaji, faida yake ni kwamba sasa bei za dawa zimepungua hadi asilimia 50, na hivyo fedha zetu zilizotengwa kwa ajili ya dawa zinatuwezesha kupata dawa nyingi kwa ajili ya watanzania.

# Jitihada nyingine iliyofanyika ni kuzungumza na hao wazabuni wa dawa moja kwa moja ili zisipite kwenye mikono mingi na hivyo dawa hizo kuuzwa kwa gharama zaidi, kazi kama hii imefanyika pia kwenye vifaa tiba ambavyo gharama zake zimepungua zaidi ya asilimia 50.

# Mpango wa Serikali kwa sasa ni kuhakikisha inafanya kazi kubwa ya kujenga vituo vya afya 500. Kuna vituo vya afya 220 mmeshajulishwa fedha zile za tozo zinakwenda kutusaidia kuongeza vituo vya afya katika ngazi ya tarafa na Serikali imepeleka milioni 250 kwenye kila eneo kwa ajili ya kuanza ujenzi.

# Lengo la Serikali ni kuhakikisha Watanzania wanapata huduma ya “dialysis” kwa gharama ya chini ya shilingi 100,000, pia gharama za vipimo mbalimbali zitapungua mfano kipimo cha mkojo kutoka shilingi 1,000 hadi kuifikia shilingi 400.

# Serikali inatambua juu ya kupanda kwa bei ya mafuta ya kula, bei hizi zimepanda kutoka katika soko la dunia na kwa sasa bei imepanda kutoka dola 500 hadi 700 kwa tani moja na kwa sasa tani moja ni zaidi ya dola 1,000 na hivyo imesababisha kupanda kwa bei ya mafuta hapa nchini.

# Nchi yetu inazalisha tani 240,000 za mafuta ya kula na mahitaji yetu ni tani 600,000 za mafuta ya kula kwa hivyo kuna upungufu kidogo, jitihada zinazofanywa na Serikali ili kutatua changamoto hiyo ni kuongeza jitihada za kusimamia uzalishaji wa mbegu za mafuta ya alizeti na pia kuhakikisha tunapata mafuta kutoka kwenye mbegu za pamba.

# Serikali imetoa shilingi bilioni 11 kwa ajili ya kuagiza mbegu za kupanda kwenye mashamba, lengo ni kuhakikisha mikoa mitatu ya uzalishaji wa mbegu za alizeti (Dodoma, Singida, na Simiyu) inaongeza uzalishaji kwa kiasi kikubwa.
# Serikali imetoa fedha za kuagiza miche ya michikichi, tunataka kuzalisha miche ya michikichi takribani milioni 1.5 ili uzalishaji wa mafuta ya mawese ufanyike, lakini pia Serikali inazungumza na wawekezaji wa viwanda vya kusafisha mawese ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa mafuta ya kula nchini.

# Shirika la Posta limezindua Huduma za Pamoja za Posta, tumeanza na kituo kimoja pale Dar es salaam na Dodoma na lengo letu ni kwamba ndani ya mwaka huu tutaenda mikoa 10 na ndani ya miaka miwili tutaenda mikoa 17, baada ya hapo tutamaliza mikoa yote. Tunataka hadi kuifikia mwaka 2025 tuwe na vituo vya Huduma za Pamoja nchi nzima katika wilaya zote, Shirika letu la Posta lina ofisi 300 nchini nzima.

# Utafiti umefanywa na kugundua kwamba Watanzania wanatumia muda mwingi kupata huduma mbalimbali, sasa Shirika letu hili la Posta limeamua kuwa wakala wa huduma mbalimbali na lengo ni kujibu matokeo ya utafiti uliofanywa kwamba Watanzania wanatumia hadi wiki nne kupata huduma. Tunataka Shirika la Posta liwasaidie Watanzania kupata huduma mbalimbali za hati ya kusafiria, bima, huduma za vizazi na vifo na huduma za TRA, huduma zote zipatikane sehemu moja.

# Tunataka Shirika la Posta liwasaidie Watanzania kupata huduma mbalimbali kama hati ya kusafiria, bima, huduma za vizazi na vifo, na huduma za TRA. Huduma zote zipatikane sehemu moja.

# Serikali imewekeza kupitia Shirika la Posta kiasi cha shilingi bilioni 49.5 kwa ajili ya kuhakikisha mpango huu unafanikiwa kwa ajili ya Watanzania kupata huduma hii.

# Serikali imefanya mageuzi makubwa katika Shirika la Posta na kuhakikisha sasa linakwenda kidigitali na kuwa na maduka ya mtandaoni ili Mtanzania mahali popote alipo aweze kuagiza na kupata bidhaa yoyoye anayohitaji. Pamoja na hayo, shirika bado linaendelea kutoa huduma zake zote ikiwemo za vifurushi.

# Shirika letu la Posta ni mwanachama katika Umoja wa Posta duniani na hivyo linaweza kuwasiliana na mashirika mengine duniani, Tanzania ni makao makuu ya Posta kwa bara la Afrika na ni Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji la Posta.

# Hivi karibuni Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imekubaliana na TANESCO kwamba itatumia shirika hilo la umeme kusambaza Mkongo wa Taifa, tunataka mtandao uwafikie Watanzania kama ambavyo umeme umewafikia Watanzania wengi mpaka wanaoishi kwenye nyumba za tembe.

# Tunataka Mtanzania akipata njia hiyo ya mawasiliano katika nyumba yake aweze kupiga simu, kupata intaneti na kutumia televisheni kupitia mtandao.





# Serikali imeendelea kutoa elimu na kuwahamasisha Watanzania kuchukua tahadhari pamoja na kupokea chanjo. Chanjo imeendelea kutolewa ambapo zaidi ya Watanzania 345,000 wameshapata chanjo. Kampeni kubwa inayofanyika sasa ni kupeleka chanjo vijijini ili Watanzania wengi waweze kuipata. Mwishoni mwa Septemba au mwanzoni mwa Oktoba 2021 tutakuwa na Wiki ya Uchanjaji ambapo viongozi wetu na wananchi kote nchini watapata chanjo.

# Rais Samia Suluhu Hassan ameidhinisha shilingi bilioni 50 ziende kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwa ajili ya kuongeza ununuzi wa mahindi. Tayari shilingi bilioni 14 zimeshatolewa.

# Uzalishaji wa mahindi umekuwa mkubwa sana kwenye nchi yetu, tumezalisha ziada ya tani 900,000 za mahindi. Fedha hizo zitasaidia kununua mahindi kwa wakulima na kuongeza tani 100,000 kwenye hifadhi ya NFRA.

# Serikali imeidhamini Bodi ya Mazao Mchanganyiko (CPB) kupatiwa mkopo wa shilingi bilioni 50 ili ikanunue mahindi kwa wakulima ambapo maindi hayo yatauzwa nje ya nchi na kwenye Shirika la Chakula Duniani (WFP).

# Serikali ina mpango wa kujenga Maeneo ya Burudani (Recreation Areas) kwa ajili ya watu kupumzika na kufanya michezo mbalimbali. Tayari tumeshaanza ujenzi hapa Dodoma na Geita lakini lengo letu ni kujenga kwenye mikoa yote kadiri hali itakavyokuwa inaruhusu.

# Tumepeleka shilingi bilioni 1.5 kwenye Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ili kuimarisha michezo. Aidha, Serikali imeondoa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye nyasi za bandia ili kuimarisha miundombinu ya michezo. Pia, Serikali ina mpango wa kujenga Maeneo ya Michezo (Sports Arena) kwenye Mikoa ya Dar-es-Salaam na Dodoma.


# Serikali imeihamasisha sekta binafsi kujenga vituo vya michezo ambapo wapo walioanza kujenga lakini ni jambo ambalo serikalini tunaliangalia kwa karibu na wakati wowote tutawajulisha tunayotaka kufanya katika kuhakikisha tunazalisha vipaji vingi vya michezo.


# Dhamira ya kujenga Uwanja wa Mpira jijini Dodoma bado ipo, Serikali inakamilisha michoro ambapo mchakato huu ukikamilika, zabuni itatangazwa na ujenzi utaanza.


# Soko la Kariakoo litakaporudi litakuwa na hadhi ya soko la kimataifa lenye mazingira mazuri, salama na yanayovutia ambapo wafanyabiashara wataweza kufanya shughuli zao masaa mengi zaidi kama ilivyo kwenye mataifa mengine yaliyoendea.


IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO

IMG-20210912-WA0026.jpg
 
Haya mbona hukuyasema wewe BWANKU!? KULIKONI? 😳😳😳
 
Tuondolee upumbavu wako hapa. Mnamkana leo Chakubanga? Ndiyo kishaweka hadharani kila kitu. Ikulu moto unawaka, lumumba moto unawaka na ndani ya Baraza la Mawaziri moto unawaka.
Hayo peleka mtaa wa ufipa wasaidie kuyasema
 
Serikali ieleze wananchi ni lini miradi yote mikubwa ulopangwa na serikali ya awamu ya tano inakamilika au imefikia wapi.

1. Bwawa la kufulia umeme la Mwalimu Nyerere mto Rufiji.

2 Kukamilika kwa ujenzi wa madaraja ya Selander na lile la Lukongo/Busisi.

3. Ujenzi wa uwanja wa ndege wa Msalato Dodoma ambao fedha zake ni mkopo kutoka AfDB.

4. Ujenzi wa uwanja wa mpira wa Dodoma ambao fedha zake zilikwishatengwa na zinatoka Morocco kwa msaada wa mfalme Mohammed.

5. Kukamilika kwa mradi wa umeme vijijini wa REA.

6. Kwanini bado twagiza mbegu za mazao kutoka nje, tumeshiundwa kutengeneza mbegu zetu wenyewe?

7. Ni lini serikali inataka kuwepo na wazalishaji wakubwa wa mafuta ya kula badala ya kuendelea kuagiza kutoka nje?
 
Haya mbona hukuyasema wewe BWANKU!? KULIKONI? 😳😳😳

Pole pole tumekusikia. Tusaidie zaidi kuelewa hili: Kitengo cha utafiti wa madawa asili kilianzishwa Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili mwanzoni mwa miaka ya 70. Je, tangu wakati huo nini matokeo ya utafiti huo. Umekuwa kiongozi mwandamizi katika Chama, tusaidie kulielewa hili.
 
Hizo data sina shaka nazo maana wapishi wa hizo data ni walewale wa awamu ya 5 sema tuu chakula ni tofauti

Hongereni watz kwa uchumi wa kasi wenye tozo nyingi
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Hao jamaa hata wakiandika data kama zote, wewe amini tu asilimia 80 ni uongo. Hivi tunaanzaje kuwaamini hao jamaa? Sura zilezile za miezi kadhaa iliyopita.
 
Serikali iko makini sana.
Asante Msemaji wa Serikali.
Kwa suala la Umeme Kigoma very Excellent. 🙌🙌🙌
 
Amepiga porojo kibao sioni maana hicho cheo....kwa sasa amekusanya dondoo magezeti week nzima kayaweka summary ndio kasoma......bado haja convince lolote upuuzi
 
Back
Top Bottom