Aliyowasilisha Mh.Tundu Lissu juu ya Muungano ndiyo haya.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyowasilisha Mh.Tundu Lissu juu ya Muungano ndiyo haya....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Planner, Jul 9, 2012.

 1. Planner

  Planner JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2012
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 296
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Wadau,nimeona si vibaya tunapoendelea kutafakari juu ya Muungano wetu (kuuboresha ama vinginevyo...tujikumbushe haya....

  MAONI YA MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO), MHESHIMIWA TUNDUA.M. LISSU (MB.)

  MAONI YAMSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS(MUUNGANO),
  MHESHIMIWA TUNDU A.M. LISSU (MB.)
  KUHUSU MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA YA OFISI YA MAKAMU WA RAIS(MUUNGANO) KWA MWAKA 2012/2013
  (Kanuni ya 99(7) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2007)
  UTANGULIZI

  Mheshimiwa Spika,

  Mwaka huuJamhuri ya Muungano wa Tanzania imetimiza miaka arobaini na nane tangu kuzaliwakwake baada ya Rais wa Jamhuri ya Tanganyika Mwalimu Nyerere kutia sainiMakubaliano ya Muungano na Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar Sheikh AbediAmani Karume tarehe 22 Aprili, 1964.
  Wakatianawasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2011/2012,Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) aliliambia Bungelako tukufu kwamba “… katika kipindi hicho Muungano wetu umekuwa na mafanikiokatika maeneo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa…. Muungano wetu ndio nguzo kuu yaumoja na amani.”
  Hata hivyo,Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri aliliambia Bunge lako tukufu kwamba, lichaya mafanikio hayo, “… zipo changamoto katika kumaliza vikwazo vinavyokwamishashughuli za Muungano.” Mheshimiwa Waziri hakuzitaja changamoto hizo.

  ‘MAPITO’ YAMUUNGANO
  MheshimiwaSpika,
  KatikaUtangulizi wake kwa Chapisho la Pili la Mhadhara wa Kiprofesa (ProfessorialInaugural Lecture) uliotolewa Januari 1990 na Profesa Issa G. Shivji na kupewakichwa cha Tanzania: The Legal Foundations of the Union, Profesa Yash Ghai –aliyekuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wa kwanzakutoka Afrika Mashariki – anasema kwamba kwa kuzingatia mazingira ya kuanzishwakwa Muungano na historia yake, “… kitu cha ajabu sio kwamba umekuwa namatatizo, bali ni kwamba umedumu (licha ya matatizo hayo) – na kwenda kinyumena mwelekeo katika Afrika.”
  Muunganoulidumu misuguano ya miaka ya mwanzo kati ya Mwalimu Nyerere na Sheikh Karumeiliyohusu kuongezwa kwa masuala ya fedha na sarafu katika orodha ya Mambo yaMuungano. Aidha, Muungano ulidumu mauaji ya viongozi waandamizi na wajumbe waBaraza la Mapinduzi la kwanza la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kama Makamu waRais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar Abdallah Kassim Hanga, Waziri wa FedhaAbdul Aziz Twala, Othman Sharrif, Mdungi Ussi, Saleh Saadalla na wengine wengi.
  Vile vile,Muungano ulidumu mauaji ya Sheikh Karume mwenyewe mwaka 1972; ‘kuchafuka kwahali ya hewa ya kisiasa’ Zanzibar iliyopelekea kung’olewa madarakani kwa RaisAboud Jumbe mwaka 1984; alichokiita Mwalimu Nyerere ‘udhaifu’ wa Rais Mwinyi;na kifo cha Mwalimu Nyerere mwaka 1999.
  Kwa bahatimbaya, Mheshimiwa Spika, ‘mapito’ haya ya Muungano yamekuwa yanafichwa fichwa,licha ya kauli za mara kwa mara za ‘kuelimisha umma juu ya Muungano.’ Kwasababu hiyo, zaidi ya tendo la kuchanganya udongo na matukio mengineyaliyofanyika hadharani, historia halisi ya Muungano wetu haifahamiki kwawananchi walio wengi. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwambawakati umefika sasa kwa Serikali kuweka wazi nyaraka mbali mbali zinazohusuhistoria ya Muungano wetu na ‘mapito’ yake ili Watanzania waelewe masuala yoteyaliyotokea yanayouhusu.
  Hii ni muhimuzaidi kwa kuzingatia ukweli kwamba mataifa ya magharibi kama vile Marekani na Uingerezayalikwishatoa hadharani nyaraka za mashirika yao ya kijasusi pamoja na balozizao za Tanzania zinazoonyesha jinsi ambavyo serikali za mataifa hayo zilihusikakatika kuzaliwa kwa Muungano.

  MheshimiwaSpika,
  Kuanikwa kwanyaraka zilizoko katika mamlaka mbali mbali za Serikali kutasaidia kuthibitishaau kukanusha taarifa ambazo chanzo chake ni nyaraka za kidiplomasia na kijasusiza nchi hizo kwamba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulitokana na njama zakibeberu za kudhibiti ushawishi wa siasa za kimapinduzi za Chama cha Umma naviongozi wake ndani ya Baraza la Mapinduzi Zanzibar la wakati huo.
  Aidha, nyarakahizo zitatoa mwanga juu ya kilichowasibu viongozi waandamizi wa chama hichoambao bila uwepo wao kutambuliwa rasmi, historia ya Mapinduzi ya Zanzibar na yaMuungano inabaki pungufu. Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, miakakaribu hamsini ya Muungano ni
  umri wa kutosha kwa taifa la Tanzania kuambiwaukweli wote juu ya kuzaliwa kwake na mapito ambayo limepitia katika kipindihicho.


  UKIUKWAJIMAKUBALIANO/SHERIA YA MUUNGANO
  Mheshimiwa Spika,

  Makubaliano yaMuungano ya tarehe 22 Aprili 1964 yalikuwa ni mkataba wa kimataifa kati ya nchimbili huru zilizokubaliana kuunda ‘nchi moja huru’, kwa mujibu wa ibara ya (i)ya Hati ya Muungano. Ili kutekeleza Makubaliano ya Muungano, Bunge la Jamhuriya Tanganyika lilitunga Sheria ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, 1964,Sura ya 557 ya Sheria za Tanzania. Kifungu cha 4 cha Sheria hiyo kilitangazakuunganishwa kwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na kuwa‘Jamhuri moja huru itakayoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.’
  Kwa upande waZanzibar, Baraza la Mapinduzi – ambalo ndio lilikuwa ‘Bunge’ la Zanzibar wakatihuo – halikutunga sheria ya kuridhia Makubaliano ya Muungano. Jambo hililimekuwa chanzo cha mjadala mkali katika duru za kitaaluma na kisheria juu yauhalali wa Muungano wenyewe. Kwa vyovyote vile, matokeo ya kusainiwaMakubaliano ya Muungano ni kwamba Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu waZanzibar zilikufa na nchi moja – iliyokuja baadae kuitwa Jamhuri ya Muungano waTanzania – kuzaliwa.

  MheshimiwaSpika,
  Kwa mujibu waaya ya (iv) ya Makubaliano ya Muungano na kifungu cha 5(1) cha Sheria yaMuungano, Mambo ya Muungano yaliyokubaliwa kwenye Makubaliano ya Muunganoyalikuwa kumi na moja. Haya ni mambo yaliyoko katika vipengele vya 1 hadi 11vya Nyongeza ya Kwanza ya Katiba ya Muungano. Hata hivyo, kati ya mwaka 1964and 1973 mambo mengine sita – yanayoonekana katika vipengele 12 hadi 16 vyaNyongeza ya Kwanza – yaliongezwa katika orodha ya Mambo ya Muungano.
  Hivyo basi,mwaka 1965 masuala ya fedha, sarafu na benki yaliongezwa; mwaka 1967 leseni yaviwanda na takwimu, elimu ya juu na mambo yaliyokuwa katika Nyongeza ya X yaMkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliongezwa; mwaka 1968 yaliongezwamambo ya maliasili ya mafuta, petroli na gesi asilia; na mwaka 1973 mamboyanayohusu Baraza la Mitihani la Taifa yaliongezwa.
  Aidha,Mheshimiwa Spika, Mabadiliko ya Tano ya Katiba ya mwaka 1984 yaligawa kipengelecha Nyongeza ya X ya Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kutengenezavipengele vinne vinavyojitegemea katika orodha ya Mambo ya Muungano, yaaniusafiri na usafirishaji wa anga, utafiti, utabiri wa hali ya hewa na takwimu.
  Vile vile,Mabadiliko hayo yaliongeza kitu kipya katika orodha ya Mambo ya Muungano:Mahakama ya Rufani ya Tanzania. Aidha, kipengele cha 3, yaani ulinzi,kilifanyiwa marekebisho na kuwa ‘ulinzi na usalama.’ Na mwaka 1992‘uandikishwaji wa vyama vya siasa’ nao uliongezwa katika orodha ya Mambo yaMuungano.

  MheshimiwaSpika,
  Mambo yoteyaliyoongezwa katika orodha ya Mambo ya Muungano baada ya mwaka 1964 yalikuwanje ya Makubaliano ya Muungano na nje ya Sheria ya Muungano na kwa hiyoyalikuwa batili. Hii ni kwa sababu Sheria ya Muungano – na sio Katiba za Mudaza 1964 au 1965 au ya sasa – ndio Sheria Mama iliyozaa Muungano na kuwekamgawanyo wa madaraka kati ya mamlaka za Jamhuri ya Muungano na mamlaka zaZanzibar. Sheria ya Muungano ilitungwa na Bunge la Katiba tofauti na sheria zakawaida.
  Aidha, Katibaya Muda, 1965 iliyotawala Tanzania hadi 1977 iliiweka Sheria hiyo kama Nyongezaya Pili katika Katiba na kuweka masharti kwamba Sheria hiyo haiwezikurekebishwa bila marekebisho hayo kuungwa mkono na theluthi mbili ya Wabungewote wa Tanganyika na wale wa Zanzibar. Vile vile, Katiba ya Muunganoinataja,katika Orodha ya Kwanza ya Nyongeza ya Pili, kwamba moja ya Sheria ambazomabadiliko yake yahitaji kuungwa mkono na theluthi mbili ya Wabunge wote ni“Sura ya 557 (Toleo la 1965), Sheria ya Kuthibitisha Mapatano ya Muungano waTanganyika na Zanzibar ya mwaka 1964.”
  Mambo yotehaya, Mheshimiwa Spika, yanaifanya Sheria ya Muungano kuwa na haiba ya Katiba.Kama alivyosema Profesa Issa Shivji katika The Legal Foundations of the Union:“Kila mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa sheria amefundishwa kwamba Katiba yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania inapatikana katika waraka unaoitwa Katiba yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977. Lakini, nachelea kusema, kila mwanafunziamefundishwa visivyo.
  Katiba yaTanzania inapatikana sio katika waraka mmoja, bali katika nyaraka mbili. Sheriaya Muungano, Sura ya 557 ya Sheria za Tanzania na Sheria ya Katiba ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania…. Vivyo hivyo, Katiba ya Zanzibar inapatikana katika(1) Sheria ya Muungano na (2) Katiba ya Zanzibar, 1984.” Katika masualayanayohusu Muungano, kwa mujibu wa Profesa Shivji, waraka unaotawala ni Sheriaya Muungano.
  Hii ndio kusemakwamba panapotokea mgongano kati ya Katiba au Katiba ya Zanzibar na Sheria yaMuungano, ni Sheria ya Muungano ndio inayokuwa na Katiba au Katiba ya Zanzibarinakuwa batili kwa kiasi cha ukiukaji wake wa Sheria ya Muungano.

  MheshimiwaSpika,
  Kifungu cha 5cha Sheria ya Muungano, ambacho ndicho chenye misingi mikuu ya Muunganohakijawahi kurekebishwa tangu Sheria yenyewe ilipotungwa mwaka 1964. Badalayake, Bunge limekuwa na tabia ya kukwepa kuigusa kabisa Sheria ya Muungano nabadala yake limekuwa likifanya marekebisho ya orodha ya Mambo ya Muunganoiliyowekwa kwa mara ya kwanza katika Katiba za Muda za mwaka 1964 na 1965 kwakuongeza vipengele katika orodha hiyo. Lengo la marekebisho haya, MheshimiwaSpika, limekuwa mara zote ni kuinyang’anya Zanzibar mamlaka yake chini yaSheria ya Muungano.
  Ndio maanakatika Mapendekezo ya Halmashauri Kuu ya CCM Kuhusu Marekebisho ya Katiba yaJamhuri ya Muungano na Katiba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yaliyotolewatarehe 27 Januari, 1983, CCM ilitamka kwamba “… msingi wa kuwa na orodha yamambo ya muungano katika Katiba ni kuonyesha mamlaka ya Serikali ya Zanzibarambayo yalikabidhiwa kwa Serikali ya Muungano; na msingi wa kuongeza mambozaidi katika orodha ya mambo ya muungano, kama ambavyo imefanyika mara kwamara, ni kuhamisha mamlaka zaidi ya Serikali ya Zanzibar kwenda kwa Serikali yaMuungano.”

  MheshimiwaSpika,
  Profesa Shivjianasema – katika The Legal Foundations of the Union – kwamba Bunge la Jamhuriya Muungano halikupewa mamlaka ya kuongeza Mambo ya Muungano bali lilipewamamlaka ya kutunga sheria zinazohusu Mambo ya Muungano kama yalivyofafanuliwakatika Sheria ya Muungano. Kwa maana hiyo, nyongeza zote zilizofanyika katikaorodha ya Mambo ya Muungano tangu mwaka 1964 zilikiuka Makubaliano ya Muunganona Sheria ya Muungano na ni batili. Ndio maana, kwa muda mrefu, Wazanzibariwamelalamikia masuala haya, hasa hasa masuala ya fedha, sarafu na mafuta nagesi asilia.

  MheshimiwaSpika,
  Vitendo vyakupuuza Makubaliano ya Muungano na Sheria ya Muungano iliyoridhia Makubalianovilifikia kilele chake tarehe 21 Novemba, 2000 pale Mahakama ya Rufani yaTanzania ilipotamka – katika kesi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar dhidi yaMachano Khamis Ali na Wenzake 17 – kwamba Zanzibar sio nchi na wala sio dola.Bali, kwa mujibu wa Mahakama ya Rufani, ‘hakuna ubishi wa aina yoyote kwambaJamhuri ya Muungano ni nchi moja na dola moja.’
  Kamatulivyokwisha kuonyesha, suala la Mahakama ya Rufani ya Tanzania yenyewe kuwasuala la Muungano liliingizwa kwenye orodha ya Mambo ya Muungano kinyemela nakinyume na Makubaliano ya Muungano na Sheria ya Muungano. Jibu la Wazanzibarijuu ya ukiukwaji wa muda mrefu wa Makubaliano ya Muungano na Sheria ya Muunganoiliyoridhia Makubaliano hayo lilikuwa ni kupitisha Sheria ya Mabadiliko ya Kumiya Katiba ya Zanzibar mwaka 2010.

  KATIBA YAMUAFAKA AU KATIBA YA UHURU?
  Mheshimiwa Spika,

  Misukosukoambayo imeukumba Muungano wetu tangu mwaka 1964 hailingani na hatari kubwainayoukabili hivi sasa. Kama tulivyomweleza Rais Kikwete katika waraka wetu watarehe 27 Novemba, 2011, “Muungano wetu upo katika hatari kubwa ya kuvunjikakwa sababu ya mabadiliko makubwa ya kikatiba ambayo yamefanyika katika Katibaya Zanzibar, 1984 na kutokana na Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
  Hii ni kwasababu Sheria ya Mabadiliko ya Kumi ya Katiba, 2010, inaashiria tafsiri mpya yaMakubaliano ya Muungano na ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayoinahoji misingi ya Jamhuri ya Muungano kama nchi moja, mamlaka ya Rais waJamhuri ya Muungano, na mambo muhimu ya Muungano….” Ili kufahamu jambo hilivizuri, ni muhimu kuelewa kwa undani yaliyomo katika Sheria hiyo ya Mabadilikoya Kumi ya Katiba Zanzibar.

  Mheshimiwa Spika,

  Tarehe 13Agosti, 2010, wakati Bunge la Jamhuri ya Muungano likiwa limevunjwa kwa ajiliya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2010, Baraza la Wawakilishi la Zanzibarlilipitisha Sheria ya Mabadiliko ya Kumi ya Katiba ya Zanzibar, 1984.Mabadiliko haya yaliweka msingi wa kikatiba wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa yaZanzibar inayoshirikisha CCM na Chama cha Wananchi (CUF). Kwa sababu hiyo,Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imepigiwa upatu kama Katiba ya Muafaka na, kwakiasi fulani, hii ni kweli.
  Hata hivyo,Mheshimiwa Spika, Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imekwenda mbali zaidi. Sheriahii sio tu imehoji uhalali wa orodha ya Mambo ya Muungano ya tangu mwaka 1964na nyongeza zake zilizofuata, bali pia imehoji pia misingi muhimu ya Sheria yaMuungano iliyoridhia Makubaliano ya Muungano. Kwa mtazamo huu, Katiba ya sasaya Zanzibar inaelekea kuwa ni tangazo la uhuru wa Zanzibar zaidi kuliko warakawa muafaka kati ya vyama viwili vilivyokuwa mahasimu.

  MheshimiwaSpika,
  Aya ya (i) ya Makubaliano ya Muungano na kifungu cha 4 cha Sheria ya Muunganovilitangaza muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar nakuundwa kwa ‘Jamhuri moja huru itakayoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika naZanzibar.’

  Huu ndio msingiwa maneno ya ibara ya 1 ya Katiba ya Muungano kwamba ‘Tanzania ni nchi moja nani Jamhuri ya Muungano.’ Na huu ndio ulikuwa msingi wa maneno ya ibara ya 1 yaKatiba ya Zanzibar ya kabla ya Mabadiliko ya 2010 kwamba ‘Zanzibar ni sehemu yaJamhuri ya Muungano.’ Sasa msingi huu wa Muungano umehojiwa na maneno ya ibaraya 2 ya Katiba mpya ya Zanzibar yanayotamka kwamba ‘Zanzibar ni miongoni mwanchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.’

  MheshimiwaSpika,
  Ibara ya 2(2)ya Katiba ya Muungano inampa Rais wa Jamhuri ya Muungano – kwa kushaurianakwanza na Rais wa Zanzibar – mamlaka ya kuigawa Tanzania Zanzibar katika mikoa,wilaya au maeneo mengineyo. Vile vile, ibara ya 61(3) ya Katiba ya Muunganoinampa Rais wa Zanzibar mamlaka ya kuteua Wakuu wa Mikoa katika TanzaniaZanzibar ‘baada ya kushauriana na Rais.’ Masuala ya mgawanyo wa nchi katikamikoa na mamlaka za mikoa hiyo sio, na hayajawahi kuwa, Mambo ya Muungano kwamujibu wa Sheria ya Muungano.
  Vile vilehayapo katika orodha ya Mambo ya Muungano. Ni wazi kwa hiyo, kwamba ibara za2(2) na 61(3) za Katiba ya Muungano zilikuwa zinakiuka matakwa ya Sheria yaMuungano na kwa hiyo ni batili. Sasa wazanzibari ‘wamejitangazia uhuru’ kwakutangaza – katika ibara ya 2A ya Katiba mpya ya Zanzibar – kwamba “… Rais (waZanzibar) aweza kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo kwakufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.”Aidha, kwa ibara ya 61(1), Rais wa Zanzibar hawajibiki tena kushauriana na Raiswa Muungano pale anapofanya uteuzi wa wakuu wa mikoa ya Zanzibar.

  MheshimiwaSpika,
  Wakati ambapoSheria ya Muungano ilikuwa imetambua na kuhifadhi mamlaka ya Rais wa Zanzibarkama mkuu wa dola ya Zanzibar, Mahakama ya Rufani ya Tanzania – katika Kesi yaMachano Khamis Ali na Wenzake – ilitishia moja kwa moja msingi huo kwa kutamkakwamba Zanzibar sio nchi na wala sio dola na kwa hiyo haiwezi kutishiwa na kosala uhaini.
  Sasa ibara ya26(1) ya Katiba mpya Zanzibar ‘imerudisha’ dola ya Zanzibar kwa kutamka kwamba“kutakuwa na Rais wa Zanzibar ambaye atakuwa Mkuu wa Nchi ya Zanzibar, KiongoziMkuu wa Serikali ya Mapinduzi na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.” Aidha, kwakutambua kwamba ‘Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano’ sio moja ya Mamboya Muungano kwa mujibu wa Sheria ya Muungano, Katiba ya sasa ya Zanzibarimetamka kwamba katika kesi zinazohusu ‘kinga za haki za lazima, wajibu nauhuru wa mtu binafsi’, uamuzi wa majaji watatu wa Mahakama Kuu ya Zanzibar “…utakuwa ni wa mwisho na hautokatiwa rufaa kwenye Mahakama ya Rufaa yaTanzania.”

  MheshimiwaSpika,
  Kifungu cha5(1)(a)(iii) na (iv) cha Sheria ya Muungano kinataja ‘ulinzi’ na ‘polisi’ kamasehemu ya mambo kumi na moja ya Muungano. Na hivyo ndivyo inavyosema aya ya(iv)(c) na (d) ya Makubaliano ya Muungano. Ijapokuwa ‘ulinzi’ ulichakachuliwabaadae kwa kuongezwa maneno ‘na usalama’, bado ni sahihi kusema kwamba masualaya ulinzi na polisi ni masuala halali ambayo Sheria ya Muungano iliyakasimu kwaSerikali ya Muungano.
  Na kwa sababuhiyo, ni sahihi kwa Katiba ya Muungano kutamka – kama inavyofanya katika ibaraya 33(2) – kwamba ‘Rais (wa Jamhuri ya Muungano) atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongoziwa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.’
  Hata hivyo,Mheshimiwa Spika, katika kile kinachoonekana kama hojaji kubwa ya msingi huu waMakubaliano ya Muungano na Sheria ya Muungano, ibara ya 121 ya Katiba ya sasaya Zanzibar imeunda majeshi ya Zanzibar inayoyaita ‘Idara Maalum.’
  Majeshi haya,kwa mujibu wa ibara ya 121(2) ni Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU); Kikosi Maalumcha Kuzuia Magendo (KMKM); Chuo cha Mafunzo (cha wahalifu), na Idara Maalumnyingine yoyote ambayo Rais wa Zanzibar anaweza kuianzisha ‘ikiwa ataonainafaa….’ Kuthibitisha kwamba Idara Maalum ni majeshi, ibara ya 121(4)inakataza watumishi wa Idara Maalum ‘… kujishughulisha na mambo ya siasa….’Makatazo haya hayatofautiani na makatazo ya wanajeshi kujiunga na vyama vyasiasa yaliyoko katika ibara ya 147(3) ya Katiba ya Muungano.

  MheshimiwaSpika,
  Sio tu kwambaKatiba mpya ya Zanzibar inaanzisha majeshi bali pia inamfanya Rais wa Zanzibarkuwa Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi hayo. Kwa mujibu wa ibara ya 123(1) ya Katibahiyo, “Rais atakuwa Kamanda Mkuu wa Idara Maalum na atakuwa na uwezo wa kufanyachochote kile anachohisi, kwa maslahi ya Taifa (la Zanzibar), kinafaa.” Aidha,kwa mujibu wa ibara ya 123(2), mamlaka ya Rais wa Zanzibar chini ya ibara ndogoya (1) yanaingiza “… uwezo wa kutoa amri ya kufanya shughuli yoyoteinayohusiana na Idara hiyo kwa manufaa ya Taifa.”
  Kwa maoni yaKambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, haya ni mamlaka ya kutangaza au kuendesha vitaambayo, kwa mujibu wa ibara ya 44(1) ya Katiba ya Muungano, ni mamlaka pekee yaRais wa Jamhuri ya Muungano. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikaliitoe kauli rasmi mbele ya Bunge hili tukufu kama tafsiri hii ya ibara ya 123 yaKatiba mpya ya Zanzibar ni sahihi.
  Na kama nisahihi, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali itoe tamko Bungeni ni kwanini imeiruhusu Zanzibar kujinyakulia mamlaka juu ya mambo ya ulinzi na usalamaambayo kwa historia yote ya Muungano yamekuwa ni mamlaka pekee ya Serikali yaMuungano.

  MheshimiwaSpika,
  Kifungu cha5(1)(b) cha Sheria ya Muungano kilitamka kwamba muundo wa Serikali ya Zanzibarutakuwa kama utakavyoamuliwa na sheria za Zanzibar pekee. Na hivyo ndivyoilivyokubaliwa katika aya ya (iii)(a) ya Makubaliano ya Muungano. Hata hivyo,licha ya muundo wa Serikali ya Zanzibar kutokuwepo katika orodha ya Mambo yaMuungano, Katiba ya Muungano imetenga Sura ya Nne nzima kuzungumzia ‘Serikaliya Mapinduzi ya Zanzibar, Baraza la Mapinduzi la Zanzibar na Baraza laWawakilishi la Zanzibar.’
  Kwa mujibu waProfesa Shivji katika The Legal Foundations of the Union, Sura ya Nne ya Katibaya Muungano “… haina ulazima wowote na ni kuingilia, bila kualikwa, kwenyemambo ambayo yako ndani ya mamlaka pekee ya Zanzibar.” Ndio maana Katiba mpyaya Zanzibar – kwa usahihi kabisa – imefanya mabadiliko katika muundo waSerikali ya Mapinduzi Zanzibar bila ya kuzingatia matakwa ya Sura ya Nne yaKatiba ya Muungano.

  MheshimiwaSpika,
  Katiba mpya yaZanzibar sio tu kwamba ‘imetangaza uhuru’ wa Zanzibar kwa kuhoji misingi muhimuya Makubaliano ya Muungano, Sheria ya Muungano na Katiba ya Muungano, bali piaimehakikisha kwamba uhuru huo utalindwa dhidi ya tishio lolote la Serikali yaMuungano. Hii imefanywa kwa kuweka utaratibu wa kuwepo kura ya maoni yawananchi wa Zanzibar kuhusu mabadiliko ya vifungu kadhaa vya Katiba yaZanzibar. Kwa mujibu wa ibara ya 80A(1) ya Katiba hiyo, “… Baraza laWawakilishi halitaweza kufanya mabadiliko ya Katiba kuhusiana na sharti lolotelililomo katika kifungu chochote kilichoainishwa katika kijifungu cha (2) chakifungu hiki, mpaka kwanza mabadiliko hayo yakubaliwe na wananchi kwa kura yamaoni.”
  Vifunguvinavyohitaji kura ya maoni ni vifungu vyote vya Sehemu ya Kwanza ya Sura yaKwanza inayohusu Zanzibar kama nchi na/au dola; kifungu cha 9 kinachohusuSerikali na watu wa Zanzibar; vifungu vyote vya Sura ya Tatu inayohusu kinga yahaki za lazima, wajibu na uhuru wa mtu binafsi; na kifungu cha 26 kinachohusuRais wa Zanzibar na mamlaka yake.
  Vifungu vingineni pamoja na kifungu cha 28 kinachohusu muda wa urais; Sehemu ya Pili na yaTatu ya Sura ya Nne zinazohusu Makamu wawili wa Rais, Baraza la Mawaziri naBaraza la Mapinduzi; kifungu cha 80A kinachohifadhi haki ya kura ya maoni; navifungu vya 121 na 123 vinavyohusu Idara Maalum na mambo yanayohusiana nayo.

  MheshimiwaSpika,
  Kuweka mashartiya kura ya maoni kuhusu mabadiliko ya vifungu tajwa vya Katiba mpya ya Zanzibarkuna athari ya moja kwa moja kwa uhai wa Muungano wetu. Hii ni kwa sababu hatavifungu ambavyo tumeonyesha kwamba vinakiuka misingi mikuu ya Makubaliano yaMuungano na Sheria ya Muungano haviwezi kubadilishwa bila kura ya maoni yaWazanzibari.
  Kwa manenomengine, kwa mujibu wa Katiba ya sasa ya Zanzibar, masuala ya kama Tanzania ninchi moja au la, majeshi ya ulinzi, polisi, n.k. ambayo yamekuwa Mambo yaMuungano kwa mujibu wa Makubaliano ya Muungano na Sheria ya Muungano sio Mamboya Muungano tena hadi hapo wananchi wa Zanzibar watakapoamua – kwa kura yamaoni – kuyarudisha kwa mamlaka ya Muungano. Huku, Mheshimiwa Spika, nikutangaza uhuru wa Zanzibar bila kutaja neno uhuru! Huku ni kuua Muungano bilakukiri hadharani!

  MheshimiwaSpika,
  Kwa mtazamo waKatiba ya sasa ya Zanzibar, hatuna tena nchi moja inayozungumzwa katika Katibaya Muungano bali tuna nchi mbili. Kwa mtazamo huo huo, masuala ya ulinzi nausalama, polisi, n.k. sio tena Mambo ya Muungano kwa sababu sasa kila nchi inamajeshi yake na kila moja ina Amiri Jeshi Mkuu wake. Aidha, tuna marais wawili,wakuu wa nchi wawili viongozi wa serikali wawili. Haya yote yanakiuka moja kwamoja Makubaliano ya Muungano, Sheria ya Muungano na Katiba ya Muungano.
  Kwa upandemwingine, kwa mtazamo wa Katiba ya sasa ya Zanzibar, Rais wa Muungano hana tenamamlaka ya kugawa mikoa na wilaya kwa upande wa Zanzibar, na wala hawezikumshauri tena Rais wa Zanzibar anapoteua Wakuu wa Mikoa wa Tanzania Zanzibar.Aidha, Mahakama ya Rufani ya Tanzania – licha ya kuwa moja ya Mambo ya Muunganokwa mujibu wa Katiba ya Muungano – haina tena mamlaka ya kusikiliza na kuamuarufaa zinazohusu haki za msingi na uhuru wa mtu binafsi zinazotoka Zanzibar.Yote haya hayapo katika Makubaliano ya Muungano na Sheria ya Muungano lakiniyapo katika Katiba ya Muungano.
  KURUDISHWA KWASERIKALI YA TANGANYIKA

  MheshimiwaSpika,
  Katika maoniyetu kuhusu Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni ilionyesha jinsi ambavyo “tafsiri hii mpya ya Makubaliano ya Muunganona Katiba ya Jamhuri ya Muungano imetiliwa nguvu kubwa na Muswada wa Sheria yaMabadiliko ya Katiba ambayo imeipa Zanzibar nafasi na ushawishi mkubwa katikautungaji wa Katiba Mpya.”
  Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni ilionyesha kwamba, kwa mujibu wa Sheria hiyo, “Rais waZanzibar sio tu kwamba ana mamlaka karibu sawa na Rais wa Jamhuri ya Muunganobali pia ana kura ya turufu katika mchakato mzima wa Katiba Mpya.” Aidha,tulithibitisha jinsi ambavyo “… ushawishi mkubwa wa Zanzibar hauishii katikakura ya turufu aliyo nayo Rais wa Zanzibar pekee yake (bali) Zanzibar inaushawishi mkubwa vile vile kutokana na nafasi kubwa iliyo nayo katika vyombovingine vinavyoundwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba….”

  MheshimiwaSpika,
  Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni inarudia tena tahadhari iliyoitoa wakati huo kwamba: “Mashartihaya ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba yana athari kubwa kwa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania kwa sababu yanakiuka Makubaliano ya Muungano ya mwaka1964, Katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano na hata Katiba ya sasa yaZanzibar….” Na kama tulivyosema wakati huo, “… tafsiri hii mpya ya Makubalianoya Muungano na ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inarudisha mezani mjadala juuya muundo wa Muungano wetu na nafasi ya iliyokuwa Tanganyika katika Muunganohuo.”

  MheshimiwaSpika,
  Kama ilivyo kwaChama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinaamini kwamba katika mazingira ambayo upande mmoja wa Muungano umejitangaziauhuru kama ambavyo tumeonyesha hapa, huu ni wakati muafaka kuanzishwa tena kwaSerikali ya Tanganyika.
  Katikamazingira ambayo upande mmoja wa Muungano sio tu una Serikali kamili, Bungekamili, Mahakama kamili, wimbo wa taifa, bendera ya taifa, na sasa una nchikamili yenye mipaka na eneo la bahari linalojulikana, una majeshi yake na AmiriJeshi Mkuu wake, huu ni muda mzuri kwa Serikali ya Tanganyika kuzaliwa upya.Katika mazingira kama haya, Mheshimiwa Spika, upande wa pili wa Muunganounatakiwa kuwa na vitu vyote hivyo pia ili uweze kujadiliana na upande wakwanza katika hali ya usawa.
  Huu ni wakatiwa kurudishwa tena kwa Serikali ya Tanganyika kama ilivyopendekezwa na Tume yaRais ya Chama Kimoja au Vyama vingi mwaka 1991 na Tume ya Kissanga mwaka 1998,na kama ilivyopendekezwa na Kundi la Wabunge 55 wa Bunge hili tukufu na kuungwamkono na Serikali ya Rais Ali Hassan Mwinyi kabla ya hoja hiyo kutunguliwa naBaba wa Taifa mwaka 1993!
  KURA YA MAONIJUU YA MUUNGANO

  Mheshimiwa Spika,

  Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni inatambua kwamba Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inaielekezaTume ya Katiba kuongozwa na misingi mikuu ya kitaifa ya kuhifadhi na kudumisha‘kuwepo kwa Jamhuri ya Muungano.’ Hata hivyo, baada ya kujitokeza kwa wananchiwanaopinga kuendelea kuwepo kwa Jamhuri ya Muungano, Mwenyekiti wa Tume yaMabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba amesema kwamba wale wanaopingaMuungano nao wajitokeze kutoa maoni yao kwa Tume.
  Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni inataka Serikali itoe kauli mbele ya Bunge hili tukufu ninamna gani maoni ya wale wanaotaka kiini macho hiki cha Muungano kiisheyatashughulikiwa na Tume ambayo imepewa jukumu kisheria la kukihifadhi nakukidumisha kiini macho hicho? Ni kipi kitakachoizuia Tume ya Warioba kupuuzamaoni ya watu hao kwa hoja kwamba Sheria inaielekeza Tume kuratibu na kukusanyamaoni na kutoa mapendekezo ya kuhifadhi na kudumisha Muungano?

  Mheshimiwa Spika,

  Katika miezi yakaribuni kumejitokeza makundi ya wananchi, hasa kwa upande wa Zanzibar, ambayoyamedai kwamba iitishwe kura ya maoni ya wananchi ili kuamua kama bado kunahaja ya kuendelea na Muungano. Makundi haya, yakiongozwa na kundi la Uamsho,yameshambuliwa sana hadharani kwa kudaiwa kwamba yanataka kuvunja Muungano. Nawatu ambao wameongoza mashambulizi dhidi ya wana-Uamsho ni viongozi waandamiziwa CCM, wakiwemo viongozi wakuu wastaafu wa chama hicho.

  MheshimiwaSpika,
  Katika maoni yaKambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Muswada wa Sheria ya Mabadiliko yaKatiba tulisema kwamba “… hofu … ya kuwaudhi ‘Wazanzibari’ ndio imepelekeakimya kikuu – ndani ya CCM na ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano – juu yaukiukwaji mkubwa wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano uliofanywa na Sheria yaMabadiliko ya Kumi ya Katiba ya Zanzibar, 2010.” Naomba nikiri kwamba tulikoseakusema hivyo.
  Tulichotakiwakusema wakati ule, na tunachokisema sasa, ni kwamba kimya kikuu ndani ya CCM nandani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya ukiukwaji mkubwa wa Makubalianoya Muungano na Sheria ya Muungano pamoja na Katiba kinatokana sio tu na ‘hofu’ya kuwaudhi Wazanzibari bali pia kinatokana na ukweli kwamba viongoziwaandamizi wa CCM pamoja na wa Serikali yake walishiriki katika ukiukwaji huo!
  Wao ndiowanaoongoza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ndio waliondaa Muswada waSheria ya Mabadiliko ya Kumi ya Katiba ya Zanzibar. Na wao ndio wanaoongozaSerikali ya Jamhuri ya Muungano waliokula kiapo cha kuihifadhi, kuilinda nakuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Na kwa hiyo wao ndio walioiruhusuZanzibar kutangaza uhuru kwa Mabadiliko haya ya Katiba yake.

  MheshimiwaSpika,
  Kwa viongozihawa na chama chao kuibuka sasa na kuwatuhumu wana-Uamsho na makundi menginekwamba wanataka kuvunja Muungano kwa kudai kura ya maoni ya wananchi wakati waowenyewe wamekaa na kupitisha marekebisho ya Katiba ambayo tayari yamevunjaMakubaliano ya Muungano, Sheria ya Muungano na Katiba ya Muungano ni kilele chajuu cha unafiki wa kisiasa. Mashabiki hawa wa Muungano waeleze walikuwa wapiwakati Zanzibar inatangaza uhuru wake kwa kuchanachana Makubaliano ya Muungano,Sheria ya Muungano na Katiba ya Muungano.

  MheshimiwaSpika,
  Kwa walewanaodai kwamba wana-Uamsho wanataka kuvunja Muungano kwa sababu tu ya kudaikura ya maoni, tunaomba tuwakumbushe yafuatayo. Kwanza, kwa mujibu wa Baba waTaifa katika kitabu chake Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania: “Huko nyumabaadhi ya viongozi wa Zanzibar wapinzani wa Muungano wamewahi kudai tufanyereferendum kwa Zanzibar kuhusu Muungano. Tukakataa kwa sababu safi kabisa.”
  Hapa Mwalimualikuwa anamzungumzia aliyekuwa Rais wa Zanzibar Alhaj Aboud Jumbe, WaziriKiongozi Ramadhani Haji Faki na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Bashir EbassuahKwaw Swanzy waliong’olewa madarakani mwaka 1984 baada ya ‘kuchafuka kwa hali yahewa ya kisiasa.’
  Aidha,Mheshimiwa Spika, katika kitabu hicho hicho Mwalimu Nyerere anasema yafuatayojuu ya kilichotokea kwenye Bunge hili hili wakati wa Bunge la bajeti la mwaka1993: “Tarehe 30 Julai, 1993 wakati wa mkutano wa bunge la bajeti ukiendelea,zaidi ya wabunge 50 kwa pamoja walitoa taarifa ya kusudio la kuwasilisha hojaBungeni ambayo inadai (kwamba) kuendelea na mfumo huu wa Muunganousiowaridhisha wananchi wengi wa upande mmoja ni kuhatarisha kuendelea kudumukwa Muungano….
  Hivyo basiwabunge hawa wanaliomba Bunge … liazimie kwamba Serikali … ilete MuswadaBungeni kabla ya Februari 1994, kurekebisha katiba ya Jamhuri ya Muungano ilikuwezesha uundaji wa ‘Serikali ya Tanganyika’ ndani ya Muungano…. Tarehe 20Agosti, 1993 wabunge wahusika waliwasilisha taarifa nyingine … iliyokuwainalitaka Bunge … liazimie kwamba Serikali … iandae kura ya maoni ambayoitafanyika kabla ya 31 Desemba, 1994 ili kupata maoni ya wananchi wa Tanzaniajuu ya kuundwa kwa “Serikali ya Tanganyika” ndani ya Muundo wa Muungano….”
  Pili,Mheshimiwa Spika, Katiba ya sasa ya Zanzibar ambayo mashabiki wa Muunganowameileta kwa kupitia Sheria ya Mabadiliko ya Kumi ya Katiba tayari imewapawananchi wa Zanzibar haki ya kuamua, kwa kura ya maoni, mambo mbali mbaliyanayoihusu nchi hiyo na namna itakavyoongozwa. Mashabiki hawa wa Muunganowakubali kuvuna walichopanda, wasibeze wale wote wanaotaka kutumia haki ya kuraya maoni kuamua hatma ya Muungano na nafasi ya Zanzibar ndani au nje yake.

  MheshimiwaSpika,
  Ni wazi, kwakuzingatia ushahidi huu, kwamba madai ya kuwa na kura ya maoni ya wananchi ilikuamua masuala makubwa yanayohusu Muungano wetu ni ya siku nyingi na yametolewana watu na taasisi mbali mbali. Madai haya hayajaanzishwa na wana-Uamsho walaCHADEMA. Ni wazi vile vile kwamba kura ya maoni inaruhusiwa kwa mujibu waKatiba ya sasa ya Zanzibar.
  Kwa sababuhizi, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaungana na wale wote ambao wamedai, nawanaendelea kudai kuitishwa kura ya maoni ya wananchi ili waweze kuamuamustakbala wa nchi yetu. Kuendelea na kiini macho cha Muungano wakati Serikalizote mbili na chama tawala cha CCM wanauvunja kivitendo kutaipelekea nchi yetukwenye njia ya Ethiopia na Eritrea, au Sudan na Sudan Kusini au Yugoslavia yazamani.
  Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni inataka Watanzania waamue, kwa kura ya maoni, kama badowanataka kuendelea na Muungano na kama jibu lao ni ndio, ni muundo gani waMuungano wanautaka. Kama, kwa busara zao, wataamua kwamba nusu karne yaMuungano inatosha basi itakuwa afadhali kwenda njia ya Czechoslovakia ya zamanikuliko kwenda njia ya Yugoslavia ya zamani, au Ethiopia na Eritrea au Sudan naSudan Kusini.
  Mwisho,Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali iwaelezeWatanzania juu ya hatua, kama zipo, ilizozichukua kuzuia ukiukwaji huu waMakubaliano ya Muungano, Sheria ya Muungano na Katiba. Na mwisho, Serikali itoekauli mbele ya Bunge hili tukufu kama – kwa ukiukwaji huu wa Makubaliano yaMuungano, Sheria ya Muungano na Katiba ya Muungano – Bunge hili tukufu litakuwandani ya mamlaka yake kuchukua hatua za kumshtaki Rais kwa mujibu wa ibara ya46A ya Katiba kwa kushindwa kuihifadhi, kuilinda na kuitetea Katiba ya Muunganokama kiapo cha kazi yake kinavyomtaka.

  HITIMISHO
  Mheshimiwa Spika,
  Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wajumbe wote wa Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni chini ya uongozi wa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani BungeniMheshimiwa Freeman A. Mbowe kwa ushauri na ushirikiano uliowezesha maandaliziya maoni haya. Aidha, niwashukuru familia yangu – mke wangu mpenzi AliciaBosensera na mapacha wetu Agostino Lissu na Edward Bulali – kwa kuendeleakuvumilia upweke unaotokana na ‘Daddy’ kuwa mbali muda mwingi kwa sababu yamajukumu mazito ya kibunge.

  Aidha,niwashukuru wapiga kura wangu wa Jimbo la Singida Mashariki kwa imani na nguvuwanayonipa kila siku kwa kuendeleza msimamo wetu thabiti wa kukataakunyanyaswa, kunyonywa na kupuuzwa na ‘Ndaa ya Njou’! Mwisho naomba nichukuefursa hii kuwashukuru viongozi, wanachama na wapenzi Chama cha Demokrasia naMaendeleo (CHADEMA) na wananchi wote wa Tanzania ambao wameendelea kutuungamkono na kututia nguvu katika kipindi hiki muhimu katika historia ya nchi yetu.Ninawaomba waendelee kutuunga mkono na kututia nguvu katika siku ngumu na zamajaribu makubwa zinazokuja!

  MheshimiwaSpika,
  Baada yamaelezo haya marefu, naomba kukushukuru na wewe binafsi na naomba kuwasilisha.
  —————————————————————
  Tundu Antiphas Mughwai Lissu
  MSEMAJI & WAZIRI KIVULI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO)
  KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI


  Nawasilisha!
   
 2. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
 3. m

  mazakwela Member

  #3
  Jul 9, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi nafikiri kuendelea kuukumbatia muungano ni sawa na kukumbatia mzinga wa nyuki. Hapa majuzi nilikuwa naongea na wazanzibar wawili, kwanza walitubeza sana wabara kuwa hatujui siasa ndo maana tunashadadia muungano, na walinipa mlolongo wa mambo kibao, ambao wao wanaamini serikali ya muungano inawabana. na kwa kuzingatia hotuba ya jembe (Lissu) bungeni, wananchi waamue tu, japo tayari inafahamika kuwa wenzetu hawautaki.
   
 4. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #4
  Jul 9, 2012
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Kabla ya Muungano, je, RAIA wa Tanganyika na Zanzibar waliulizwa kama WANAUTAKA? Inaonekana dhahiri kwamba Muungano uliwekwa kwa maslahi ya wachache, ndio kisa cha kuhojiwa leo, miaka 48 baadaye. Tukishafika miaka 50, nadhani hautakuwapo tena. Kama wenyewe wanaitaka nchi yao, basi WAACHIENI!
   
 5. s

  sokolaboro JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 312
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hakuna haja ya kuwa na muungano. tunataka Tanganyika yetu. Unaunganaje na watu wachache milioni moja kwa milioni arobaini halafu tuwe na haki sawa za kimaamuzi katika muungano wakati wao wana chao nasi hatuwaamulii katika chao. wao wanashiriki kutuamulia chetu
   
 6. m

  mkataba Senior Member

  #6
  Jul 9, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 147
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nishaanza kampeni ya uhuru hapa mtaani na kutoa machapisho ya Tanganyika yetu (sarafu, bendera, logo, etc) kabla ya muungano.
   
 7. BWANYEENYE

  BWANYEENYE Member

  #7
  Jul 9, 2012
  Joined: Jun 2, 2010
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  patamuuuuuuuuuuuuuu hapooooooooooooo
   
 8. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mmmm Jisomee mwenyewe, hapa unaweza kuandika kitabu kizuri tu cha elimu ya uraia.
   
 9. mangikule

  mangikule JF-Expert Member

  #9
  Jul 11, 2012
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 3,171
  Likes Received: 1,256
  Trophy Points: 280
  Hivi kweli CCMABWEPANDE hawayaoni au kuyajua haya!! Ni mshangao wa karne!! Kila siku tunaimbishwa kama mazuzu tu muungano ni suala "NYETI" hakuna kujadili. Hata mwenyekiti wa msitu wa MABWEPANDE alikuwa amekataa kwenye katiba mpya hakuna mjadala wa MUUNGANO usiwepo au usiwepo!!
  Mwenzio anataka talaka weye wamng'angania wani? Na ameandika talaka nzuri ya kisheria kama katiba ya ZNZ 2012. Mwache mwache jamani eboo!!
  Ahsante Jembe la nguvu lima, fukua, uozo utokeze ili upate mwanga na kupona!!
   
Loading...