Aliyotabiri Shibuda yaanza kutimia: CCM inaanza kufia mikononi mwa Kikwete

CDM weupe!bla bla nyingi!raia wameanza kustukia taratibu!

Nakupa test moja (wewe na magamba wenzenu): Nendeni mahali popote mkutane na na wafanyakazi/wafanyabiashara ambao pato lao ni chini ya laki tano kwa mwezi (na ndio majority hapa nchini) waombeni wawachangie MUONE MOTO UTAKAWAZUKIA!

Mchana huu nimeshuhudia kwa macho yangu mwenyewe watu wanaolipwa shilingi elfu 80 tu kwa mwezi wakimchangia Nassari! Huu ni ushahidi kuwa raia wameanza kukushtukieni nyinyi MAGAMBA!
 
CDM weupe!bla bla nyingi!raia wameanza kustukia taratibu!

njaa mbaya sana, malima bunduki ya nn?na utasikia kila wazir ana jeshi lake hapo ndipo patakuwa na kilio cha kusaga meno. sababu mawazir wote mafisad kwa hiyo lazima uwe na jeshi la kukulinda,rahis jk anaye analake la kulinda ufisadi wake pinda nae ndo hivyo tena.hawasafishik hao hata jik bado wana madoa endelea kujipendekeza
 
Kwa hiyo tuendelee na haya majizi yenu yanayotewmbea na masilaha, mapesa, na pasipoti mbili mbili kwa sababu tu hayatakuja mabadiliko ikiingia CDM?

Na hiyo hoja ya mtoa mada ya kwa nini siku siku hizi CCM inahangaika sana kufanya kampeni kulibakiza jimbo hujaijibu? Huamini iwapo hicho ni kielelezo tosha kwqamba imekabwa sana siku hizi kuliko nyuma. Kielelezo kingine ni kuanguka kwa kura za CCM -- za urais na za wabunge mwaka 2010 ukilinganisha na 2005.

Bado una makengeza makali kuliona hilo? Ni watu wa ajabu kweli kweli nyie CCM!

OK ccm ilipata ushindi wa 60% 2010, badala ya >80% 2005, je ikishinda kwa 51% 2015 utaikubali?? Ujue kuwa kura za uchaguzi ziko chini ya usalama wa taifa na wanauwezo mkubwa sana wa kumfanya mtu wao ashinde. Hii ndiyo sababu nikasema Usalama wa Taifa UWT ni kama KGB ya russia, bado ina uwezo wa kuamua nani awe raisi wa Russia na siyo kura za warussia kama unabisha nenda umuulize Putin aliyekuwa raisi akamaliza muda wake wa vipindi viwili akawekewa mtu wa kumshikia na hivi sasa amerudi tena. je wewe unafikiri warussia hilo wanalipenda? Hata kama ccm itakufa bila ya kuisambaratisha UWT hii taasisi bado itaendelea kutuchagulia viongozi wa kitaifa. Lakini UWT ndo nani? hawa ni watanzania wenzetu kwenye level zote za maisha ambao wamekuwa recruited kulinda na kuendeleza mtandao wa viongozi wa JMT ili waendelee kujinufaisha na raslimali zetu wote. wako mitaani, ni walimu, ni madaktari, ni wabunge, ni maafisa wa majeshi, ni wahasibu, ni wafanyabiashara, ni mameneja, madirector, katibu wakuu, mawaziri nk nk genge kubwa linaloperate kama mafia/KGB. Wana uwezo wa kumuua mtu, kumpamba na kufanya lolote na kusitokee chochote.
 
Back
Top Bottom