Aliyotabiri Shibuda yaanza kutimia: CCM inaanza kufia mikononi mwa Kikwete

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Yatimia aliyosema john Shibuda Mbunge wa Maswa alipompa JK vidonge vyake- kwamba CCM itamfia mikononi mwake. Tunayaona pole pole tangu Igunga na kata nyingi za udiwani -- ambayo CCM mwaka mmoja tu na nusu hivi hivi waliyachukuwa kwa ulaini, sasa hivi wanatumnia nguvu kubwa kweli kweli pamoja na ahadi lukuki za uongo (JK mwenyewe alitoa maelfu ya ahadi 2010 hajatimiza hata moja).

Hali kadhalika CCM wameongeza utumiaji nguvu kupitia vyombo vyao vya dola kama vile mapolisi wao, NEC isyokuwa na haki na ambayo imeafiki kuwanyima fursa maelfu ya vijana ya kupiga kura kwa kutowaandikisha makusudi kwani inajua wengi wa hao vijana ni CDM.

CCM inazidi kuzororota kila kukicha na mtu anayezorota mara nyingi hupenda kutumia maguvu ya mwisho kama vile matke ya farasi anayekaribia kukata roho.

Yote haya CCM wanafanya kwa kuona siku zao za kutokomea zinakaribia.
 
Heeh! Kwani hujaliona hilo? sasa hivi mawaziri wa JK wameanza kusafiri na mapesa cash waliyoibia wananchi, silaha na pasipoti mbili mbili ili kuwa tayari saa zoite kukimbia nchi kupitia exit point yoyote ile kwa muda mchache. Kufa kwa CCM kunaashiria balaa kubwa kwa Watz walionyonyeka na mafisadi hayo.
 
shibuda anapewa promo za kijinga sana

he is a political *****
 
Kikwete atakumbukwa na CCM kama Mikhail Gorbachev aliyeisambaratisha USSR
 
USSR ilisambaratika lakini KGB ilibaki matatizo ya Warussia yako vilevile, bila kuisambaratisha tiss hata kama ccm wataondoka hapatakuwa na mabadiliko ya kweli
 
Kwa hiyo tuendelee na haya majizi yenu yanayotewmbea na masilaha, mapesa, na pasipoti mbili mbili kwa sababu tu hayatakuja mabadiliko ikiingia CDM?

Na hiyo hoja ya mtoa mada ya kwa nini siku siku hizi CCM inahangaika sana kufanya kampeni kulibakiza jimbo hujaijibu? Huamini iwapo hicho ni kielelezo tosha kwqamba imekabwa sana siku hizi kuliko nyuma. Kielelezo kingine ni kuanguka kwa kura za CCM -- za urais na za wabunge mwaka 2010 ukilinganisha na 2005.

Bado una makengeza makali kuliona hilo? Ni watu wa ajabu kweli kweli nyie CCM!
 
Vipo viashiria vingi tu vya kuonyesha CCM is on its way out. Minyukano ya wenyewe kwa wenyewe ambayo ingawa wanajidai haipo -- ipo dhahiri sana, mfano ni uteuzi wa huy0 huyo mgombea wao Siyoi.

Pili kwa kuwa hali inazidi kuwaelemea huko Arumeru, bila haya wametoa maagizo kwa chombo cha walipa kodi -- TBC kutoa habari za upande wa CCM tu!

nawaambia hizi rafu ni kutokana na kushikwa pabaya, wameshikwa kwenye ma*****!
 
Mie nimekuwa najiuliza -- kwa nini walimtumia fisadi Mkapa kuwafanyia kampeni ya ufunguzi? peke yake hili limekumbusha mengi sana kuhusu yeye huku mengine hayakuwapo awali -- na hakika imesababisha CCM kuchukiwa zaidi in a few percentage points down!

Wanatapatapa sana!
 
nina kadi nyingi hapa za mwaliko kutoka kwa wananchi wa rombo kwenda kuchangia shughuli za maendeleo,bila posho kuongezwa mi ntazitoa wapi????????joseph selasini mbunge wa rombo - chadema
 
Kwa hiyo tuendelee na haya majizi yenu yanayotewmbea na masilaha, mapesa, na pasipoti mbili mbili kwa sababu tu hayatakuja mabadiliko ikiingia CDM?

Na hiyo hoja ya mtoa mada ya kwa nini siku siku hizi CCM inahangaika sana kufanya kampeni kulibakiza jimbo hujaijibu? Huamini iwapo hicho ni kielelezo tosha kwqamba imekabwa sana siku hizi kuliko nyuma. Kielelezo kingine ni kuanguka kwa kura za CCM -- za urais na za wabunge mwaka 2010 ukilinganisha na 2005.

Bado una makengeza makali kuliona hilo?
Ni watu wa ajabu kweli kweli nyie CCM!

Kwenye red: Siyo makengeza, bali ni upofu tu. Na hili ndilo linalitatiza taifa kutokwenda mbele kiuchumi -- wenzetu hawa CCM daima huona maovu nsdiyo mema, na atakuapia kwa miungu yao yote kwamba giza ni mchana!

Wameanza kukwepa mada na kuleta mambo ya posho! Rudini kwenye mada, CCM inaterereka haiterereki? CDM haipandi inapanda? Viashiria si vipo?

Upofu mkubwa huu!
 
Kuhusu viashiria vya kuporomoka kwa CCM ni baada ya uchaguzi wa 2005 na JK mwenyewe alikiri -- kutoka kura mil 8 hadi kura mil 5! Akina Makongoro Nyerere walimpa laivu sababu yake ya kudorora.
 
Yatimia aliyosema john Shibuda Mbunge wa Maswa alipompa JK vidonge vyake- kwamba CCM itamfia mikononi mwake. Tunayaona pole pole tangu Igunga na kata nyingi za udiwani -- ambayo CCM mwaka mmoja tu na nusu hivi hivi waliyachukuwa kwa ulaini, sasa hivi wanatumnia nguvu kubwa kweli kweli pamoja na ahadi lukuki za uongo (JK mwenyewe alitoa maelfu ya ahadi 2010 hajatimiza hata moja).

Hali kadhalika CCM wameongeza utumiaji nguvu kupitia vyombo vyao vya dola kama vile mapolisi wao, NEC isyokuwa na haki na ambayo imeafiki kuwanyima fursa maelfu ya vijana ya kupiga kura kwa kutowaandikisha makusudi kwani inajua wengi wa hao vijana ni CDM.

CCM inazidi kuzororota kila kukicha na mtu anayezorota mara nyingi hupenda kutumia maguvu ya mwisho kama vile matke ya farasi anayekaribia kukata roho.

Yote haya CCM wanafanya kwa kuona siku zao za kutokomea zinakaribia.
CCM kama chama kinaishi kwa umaarufu wa historia yake tu kwa sasa, na si vinginevyo.
Living on its lost glory!

Kisiasa CCM kwa leo haina itikadi wala dira inayowaunganisha wanachama-no unifying ideology.
Na inavyoelekea chama kinazidi kutekwa na mafisadi ambao si tu wana pesa zao za kufanya wayatakayo, mbaya zaidi ni chama kukosa uwezo wa kuwadhibiti watu hawa.
Kwa lugha nyepesi chama kimekuwa club ya wafanya biashara wenye uwezo wao huku wakisundikizwa na wafuasi wao walionunuliwa.
Katika mazingira haya chama hakina itikadi, sera wala muelekeo wa jumla ila personal interests za watu wenye nyadhifa nzito.
Si jambo la kushangaza kuwa kadri siku zinavyoenda chama kinazidi kuelemea kwenye serikali ili kipate uhalali wa kupumua kisiasa.Na ndio tunaona polisi na vyombo vingine vikitumika kuua upinzani dhidi yake.
Siyo siri mimi ni mwanachama wa CCM lakini kwa itikadi inayotawala leo , maswala yote ni mimi kwanza, watu baadaye.

Ni pale tu ambapo matatizo yangu nikishindwa kuyatatua , na yakiwa sawa na ya wengine ndio nitakiunga chama kwa nguvu zote, lakini leo ni survival of the fittest.
 
Yatimia aliyosema john Shibuda Mbunge wa Maswa alipompa JK vidonge vyake- kwamba CCM itamfia mikononi mwake. Tunayaona pole pole tangu Igunga na kata nyingi za udiwani -- ambayo CCM mwaka mmoja tu na nusu hivi hivi waliyachukuwa kwa ulaini, sasa hivi wanatumnia nguvu kubwa kweli kweli pamoja na ahadi lukuki za uongo (JK mwenyewe alitoa maelfu ya ahadi 2010 hajatimiza hata moja).

Hali kadhalika CCM wameongeza utumiaji nguvu kupitia vyombo vyao vya dola kama vile mapolisi wao, NEC isyokuwa na haki na ambayo imeafiki kuwanyima fursa maelfu ya vijana ya kupiga kura kwa kutowaandikisha makusudi kwani inajua wengi wa hao vijana ni CDM.

CCM inazidi kuzororota kila kukicha na mtu anayezorota mara nyingi hupenda kutumia maguvu ya mwisho kama vile matke ya farasi anayekaribia kukata roho.

Yote haya CCM wanafanya kwa kuona siku zao za kutokomea zinakaribia.

The last kicks of a dying horse!
 
Kwa mara ya kwanza CHEERS TO SHIBUDA from pro-CDM!!Kumbe CDM mnamkubali kamanda/mpiganaji Shibuda eenh?
 
Back
Top Bottom