Aliyewahi kuwa Waziri (Arcado Ntagazwa) kizimbani kwa utapeli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyewahi kuwa Waziri (Arcado Ntagazwa) kizimbani kwa utapeli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 24, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Tue, Apr 24th, 2012

  [​IMG]
  Arcado Ntagazwa


  A former minister, Arcado Ntagazwa (65) and two others on Monday appeared before the Kisutu Resident Magistrate's Court in Dar es Salaam charged with obtaining 74.95m/- by false pretence.


  State Attorney Ladislaus Komanya alleged that on October 22, 2009 at Msasani Mikoroshini area in Dar es Salaam, with intent to defraud, Senator Miselya (60), Ntagazwa and Dr Webhale Ntagazwa obtained 5,000 caps and 5,000 t-shirts worth 74.95m/- belonging to Mr Noel Severe.

  It is further alleged that the accused had promised to pay the owner of the said goods within one month when they knew that they were not speaking the truth. The accused pleaded not guilty and two of them – Arcado Ntagazwa and Webhale Ntagazwa – managed to get bail after securing two sureties who signed 12m/- bond each.

  The case was adjourned to May 7 for another mention. Meanwhile, a Guinea Bissau national yesterday appeared before the same court charged with trafficking 1.7 kilogrammes of heroin worth 57.8m/-. According to the State Attorney Esther Kyalo, the accused is Alberto Mendez (49), a businessman residing in Bamako, Mali.

  The accused was not allowed to enter any plea or get bail. The case was adjourned to May 7 for another mention as police investigations are going on. According to the charge sheet, it is alleged that on April 15, this year at Julius Nyerere International Airport, Mendez was found trafficking 1.7 kilogrammes of heroin from Guinea Bissau to an unknown destination.


  By JULIUS BWAHAMA, Tanzania Daily News

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Those T-shirt, and Hats it seems they are very expensive to end up coasting up to Millions of Tshillings? (74 millions?)
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,814
  Trophy Points: 280
  Mzee Ntagazwa pole. Kumbe pamoja na Polisi kukukamata na kuahidi kulipa hilo deni hukulipa hadi umeburuzwa mahakamani?
   
 4. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2012
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  WAZIRI wa zamani wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Arcado Ntagazwa (65), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kujibu mashitaka ya kujipatia mali ya Sh milioni 74 kwa njia ya udanganyifu.

  Katika kesi hiyo iliyosomwa mahakamani hapo jana, Ntagazwa anashitakiwa pamoja na mtu anayedaiwa kuwa ni mtoto wake, Dk. Webhale Ntagazwa (29) na Seneta Julius Miselya (60).

  Baada ya kusomewa mashitaka na kuyakana, waliachiwa kwa dhamana isipokuwa Miselya ambaye hakuwa ametimiza masharti ya dhamana kwa wakati huo.

  Wakisomewa mashitaka yao jana mbele ya Hakimu Liud Chamshama, Mwendesha Mashitaka Wakili wa Serikali, Ladislaus Komanya alidai kuwa Ntagazwa na wenzake hao walijipatia mali hiyo kwa udanganyifu.

  Walidaiwa kuwa Oktoba 22, 2009 maeneo ya Mikoroshini Msasani katika Wilaya ya Kinondoni, washitakiwa kwa nia ya udanganyifu walijipatia kofia 5,000 na fulana 5,000 kutoka kwa Noel Severe zenye thamani ya Sh milioni 74.

  Ilidaiwa na Komanya kuwa washitakiwa hao walimdanganya Severe kuwa bidhaa hizo wangezilipa baada ya mwezi mmoja tangu kupewa mzigo huo, jambo ambalo hawakulitekeleza.

  Washitakiwa hao walikana mashitaka yao na wakili wa Ntagazwa, Alex Mgongolwa aliomba dhamana kwa wateja wake akidai kuwa Ntagazwa ni mtu anayeaminika, kwa kuwa alipata kuwa Waziri na Mbunge kwa muda mrefu.

  Wakili wa Serikali hakuwa na pingamizi kwa washitakiwa kupewa dhamana kwa sababu mashitaka wanayokabiliwa nayo yanadhaminika kisheria.

  Hakimu Chamshama naye hakuwa na pingamizi, hivyo kutoa dhamana kwa washitakiwa kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika, watakaosaini hati ya dhamana ya Sh milioni tano.

  Washitakiwa walitakiwa kutoa Sh milioni 12 taslimu au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo, kutotoka nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila ruhusa ya Mahakama na kukabidhi mahakamani hapo hati zao za kusafiria.

  CHANZO: Habari leo, 24 April 2012
   
 5. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Maskini Mzee Ntagazwa namheshimu sana!! Lakini mimi si mjuvi wa sheria lakini cha kujiuliza ni kwamba "wanadaiwa" au walitapeli? kwani kama walikubaliana kwamba wachukue mzigo halafu wakiuza ndiyo walipe, kama mzigo hawajafanikiwa kuuza ni Utapeli?

  Huyo mzee kwa sasa ni Mwanachama wa CHADEMA na ni mtu ninayeamini ni muumini mkubwa sana wa maadili!!
   
 6. O

  OPORO Member

  #6
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haki itendeke
   
 7. Nyamburi

  Nyamburi JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii issue nafikiri inahusisha N.G.O fulani ambayo Ntagazwa alikua kama mmoja wa watu wa bodi ya udhamini wa hiyo Ngo,sasa nafikiri walikua na shughuli yao na waliomba kutengenezewa fulana hizo kwa minajiri ya hela za wafadhili zikifika wangelipa,kwa hiyo Ntagazwa amehusika kwa kua yeye ni mmoja wa watu wa bodi ya udhamini wa hiyo Ngo,na si kua alichukua vifaa hivyo kwenda kuuza
   
 8. wagaba

  wagaba JF-Expert Member

  #8
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 829
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  ndo maana wastaafu hawadumu. sasa na umri wote huo kupelekwa mahakamani si kutaka moyo usimame bure(vifo visivyotarajiwa).
  huyo anayemdai ameamua kumfix mzee wa watu. kesi ya madai imegeuzwa ya kutapeli! pole mzee. I hope ameweka wakili makini. otherwise atapelekwa speed ya 3.75G
   
 9. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #9
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kimahesabu sio ghali sana. Kumbuka zilikuwa 10,000 pieces. Ni wastani wa Shs. 5,000 kwa kila T-Shirt na 2,400 kwa kila Cap. (Bei ya jumla shs 7,400 kila kimoja).
   
 10. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #10
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,286
  Likes Received: 597
  Trophy Points: 280
  Huyu mzee nilifikiri ni miongoni mwa watanzania wachache waadillifu. Aliwahi kukoswakoswa risasi akiwa mkuu wa ACS kanda ya kaskazini miaka ya uwaziri mkuu wa Kawawa (Baada ya hapo akatofautiana sana na Kawawa). Sijui amekuja kujihusisha vipi na tapelli Miselya.
   
 11. k

  kim jong un JF-Expert Member

  #11
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  huyu mzee ni mwadilifu sana alikuwa ni usalama wa taifa myaka fulani akatofautiana na viongozi wakubwa wakambambikia kesi kuwa si mtanzania eti ni raia wa burundi wakamsimamisha sasa baada ya kuamia chadema amekuwa anawindwa sana make ana marafiki bado ndan na alishawai kumtuhumu mkurugenzi wa usalama kuwa hafanyi kazi vizuri.............
   
 12. Oluoch

  Oluoch Senior Member

  #12
  Apr 24, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tusihukumu........tuache mahakama itende kazi yake
   
 13. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #13
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Senator Miselya ni nani kwa wale mnaomfahamu maana Gagnija ame Hint kwenye Post yake kwamba jamaa ni tapeli. Hebu tupeni mwanga jamani!!
   
 14. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #14
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,915
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 160
  Mzee nilikuomba usiende vyama vya upinzani kuna matapeli huko: sasa umekutana na seneta miselya kakuingiza pabaya na wewe pensheni umeimaliza, CDM hawawezi kukuokoa labda ungekuwa MANGI
   
 15. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #15
  Apr 24, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hapa unaweza kuta vijana wa mjini wamemwingiza mtegoni mzee bila kujua.
   
 16. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #16
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwaka 2009 wakati wa tukio Ntagazwa alikuwa bado yuko CCM. Wacha kupotosha mambo.
   
 17. k

  kabombe JF-Expert Member

  #17
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 15,566
  Likes Received: 8,509
  Trophy Points: 280
  Alichukua kwa ajili ya kampeni za ubunge 2010...ili akipata ubunge alipe kupitia posho.Ubunge kakosa matokeo yake ndio haya.
   
 18. M

  Miruko Senior Member

  #18
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 8, 2008
  Messages: 173
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Fulana na kofia zilikuwa za Ngo ya Aford,zilikuwa zimedhaminiwa na wafadhili, zikiwa na ujumbe wa kuwapinga mafisadi. Zilichapishwa kwa mtoto wa severe (mkwe wa manvi). Kabla hazijaingia mtaani, gazeti la Mtanzania likaandika kuwa fulana hizo za kisiasa za CCJ. Mfadhili aliposikia akajitoa kwa kuwa hataki kujihusisha na siasa. Ndio kisa kina Ntagazwa wakashindwa kulipa.
   
 19. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #19
  Apr 24, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Uko sahihi kabisa mkuu
   
 20. k

  kingmaker Member

  #20
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nakubaliana na wewe mia kwa mia, ila huyo mtoto wa mamvi ndio alieyeenda kusema kwa Mamvi na RA ya kuwa hizo fulana ni za kuwakashifu mafisadi na ndio wakaenda kutoa magazetini na mfadhili akajitoa. So, RA na magazeti yake yawajibike....pamoja na Mamvi.

  Kimbunga kinakuja!
   
Loading...