Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Gabriel Kimolo ahamia CHADEMA

Du we jamaa una hoja dhaifu sijapata kuona. Kwa maneno mengine unataka kutuambia mnalipiza kisasi? Hivi unaweza kulinganisha nguvu waliyotokanayo akina Mwampamba Chadema na nguvu ya Kimolo?

Hakuna kulipa kisasi wala nini.........nilichokusudia ni kuwa kuhama vyama sio jambo la ajabu pasi kulilinganisha na matapishi.....usihitimishe tu kuwa hoja zangu ni dhaifu wakati hujawahi zisoma hata chembe......na kuthibitisha hili angalia stats zako na zangu ndio uanzishe mapambano na mimi
 
Viongozi wa chama cha democrasia na maendeleo (CHADEMA) mara zote wamekuwa wakisikika kupinga vyeo vya wakuu wa wilaya kwa kusema kuwa vyeo hivyo havina tija na watu wanaoteuliwa kwenye nafasi hizo hawana uwezo wa kufikiri na kutenda wanateuliwa kwasababu tu ni makada wa CCM na maswahiba wa Rais.

Katika hali isiyo ya kawaida tunashangaa kunawaona watu ambao wanadhaniwa kuwa wanauwezo kwenye chadema John Mnyika, Peter Msigwa, Godbless Lema, na Tundu Lisu ambao wamekuwa vinara wa kuwapinga wakuu wa wilaya kuwa hawana uwezo. Leo wako pamoja wametengeneza heading inayosema "MKUU WA WILAYA AHAMIA CHADEMA" Mtu aliyetimuliwa kwenye nafasi yake tangu 2010 wao bado wanamtambua kama mkuu wa wilaya. Kweli hawa ndio tunawategemea waunde baraza la mawaziri CDM ikikamata dola?

Huu ni uvivu wa kufikiri na inaonesha namna gani hawa jamaa wamefilisika sera kichwani. Ndugu Gabbriel Kimolo ambaye wao wanamuita mkuu wa wilaya ni mtu ambaye alitimuliwa kwenye nafasi yake na rais kikwete kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuongoza, ubadhilifu na mambo mengine mengi.

Mara Nyingi CCM wamekuwa wagumu sana wa kumfukuza mtu hata kama amekosea, ukiona CCM imemfukuza mtu basi ujue ameoza kabisa na habebeki lakini mtu kama huyo Leo wafuasi wa Mbowe wanampokea na kumwita kamanda?

Katika hali kama hii CHADEMA isitegemee kufika popote na ndio maana hata nguvu ya UMMA imewageukia na kuanza Oparesheni Timua Mbowe na Slaa ambayo imeshaanza kutekelezwa kwa vitendo huko Kigoma.

CHADEMA inaendelea kufukuza hazina ya vijana na wasomi, wenye uwezo na fikra mpya za kukipeleka chama mbele kwasababu ya maslahi binafsi ya Mbowe na Slaa badala yake inafurahia kula makombo ya CCM ikiamini kuwa makombo hayo hayatahiji chochote kitakachogusa maslahi ya Mbowe na Slaa.

SIAMINI KAMA MAKOMBO YA CCM YANAWEZA KUTUMIWA NA CHADEMA KUIKABILI CCM. HATUWEZI KUENDELEA KWA KUONDOA NURU NA KUKARIBISHA GIZA.

View attachment 125870
 
Tatizo la SPIN DOCTORS hawa wa CCM walioajiliwa na Nape HAWAFUNDISHIKI!

Ndiyo maana kwao kujenga hoja ni JANGA LA TAIFA?!

Hebu tujiulize CDM wanapinga uwepo wa ma-DC na ma-RC, that is fine. Sasa huyo Gabriel Kimolo umeambiwa anahamia CDM ili apewa U-DC?

Unasema Gabriel Kimolo alifukuzwa u-DC kwasababu ya ubadhilifu wa fedha! Je, ni kwanini hadi leo Serikali ya CCM haijamfikisha kwenye vyombo vya dola ili sheria ichukue mkondo wake?

Lakini kitu KIMOJA UMENIFURAHISHA ni pale ulipokiri kwamba CCM ni nambari ONE kwa kulea VIONGOZI Wabovu na wabadhilifu. Kwa hilo nakupa KUDOS!

Kwa hiyo Watanzania tujiandae kuikataa shetani CCM na mambo yake yote 2015, kwani itatuletea VIONGOZI WABOVU NA WABADHILIFU.
 
Tatizo la SPIN DOCTORS hawa wa CCM walioajiliwa na Nape HAWAFUNDISHIKI!

Ndiyo maana kwao kujenga hoja ni JANGA LA TAIFA?!

Hebu tujiulize CDM wanapinga uwepo wa ma-DC na ma-RC, that is fine. Sasa huyo Gabriel Kimolo umeambiwa anahamia CDM ili apewa U-DC?

Unasema Gabriel Kimolo alifukuzwa u-DC kwasababu ya ubadhilifu wa fedha! Je, ni kwanini hadi leo Serikali ya CCM haijamfikisha kwenye vyombo vya dola ili sheria ichukue mkondo wake?

Lakini kitu KIMOJA UMENIFURAHISHA ni pale ulipokiri kwamba CCM ni nambari ONE kwa kulea VIONGOZI Wabovu na wabadhilifu. Kwa hilo nakupa KUDOS!

Kwa hiyo Watanzania tujiandae kuikataa shetani CCM na mambo yake yote 2015, kwani itatuletea VIONGOZI WABOVU NA WABADHILIFU.

Samahani mkuu sikujua kuwa watu waliochaguliwa kiswahiba na watu ambao hawana uwezo wa u DC wakiwa CCM ndio wanakuwa dhaifu ila Wakiwa Chadema wana kuwa MAKAMANDA. Ahsante kwa taarifa.
 
1. Hakutimuliwa. alijiuzuru.
2. Si alikuwa mkuu wa wilaya? sasa ulitaka wamuiteje?
 
He is strategist....alitimiza wajibu wake kama wakuu wa wilaya nyingine ktk ukada wa ccm, intelijensia yake ikamwambia anapigwa chini u-dc ktk sababu ambazo hakuzielewa...bilashaka tiss walishatonya mkuu wa kaya maono yake ya baadae...

Kila la kheri.....kumbuka cdm ni mchukuzi wa mahamuzi magumu...usaliti havumiliki.

Kabla ya kugombea nafasi yoyote utachunguzwa vikali. Hatutaki hakina nani yule...wa usukumani.

"Shibh'umbu Jinyammapanda"
 
Mtei naskia ana laana ya nyerere

Kwa mujibu wa mabango ya kigoma ya jana yanayopinga ziara ya slaa

318039_470409646356368_212601826_n.jpg


CC Ritz
 
Last edited by a moderator:
Huwezi kuresign kwenye hamna, alishapewa barua kwamba hataendelea kuwa mkuu wa wilaya yeye akakimbilia kwa wanahabari kusema kuwa amerisgn. Sasa unadhani kwanini hakuhamia chadema tangu alipofukuzwa ukuu wa wilaya, huoni kuwa mbowe ameenda kumuomba aje cdm kusimamia saccoss?
Uyasemayo sio kweli.. alipewa barua baada ya yeye kutokeza public ndipo mkuu wa mkoa anasema tayari kuna barua yake na alishapewa taarifa juu ya kutyoendelea na kazi, huo ni usanii tu wa serikali yetu.. hata wewe unayeitetea huwa unaathiriwa na utendaji wa kisanii lakini basi kwakuwa una maslahi au mapenzi yasiyo macho basi lolote litakalosemwa vibaya (Ukweli) kuhusu serikali utaupinga tu..
 
Back
Top Bottom