Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Gabriel Kimolo ahamia CHADEMA

wale wa mabango na maandamano ya kuchumia tumbo wamuandalie na huyo mkuu wa wilaya kwa maamuzi aliyochukua maana hawa jamaa sijui ni wa jinsi gani.
moto moto motooooooo.......unguza ccm
 
Alikuwa mkuu wa wilaya ya Mbozi kabla ya dr.M.Kadeghe, ana msimamo sana aliwekewa zengwe, juu ya kununua kahawa mbichi
 
Gabriel Kimolo ni Mrangi, sasa Lumumba waje waseme warangi ni watu wa kaskazini
 
Jaman kimolo namkubali sana kutokana na msimamo wake hata hivyo ni msimamo wake kuhusu kahawa kuuzwa mbichi au kavu ndo ilifanya asipewe tena nafasi baada ya kuwa na mvutano na Maghembe kama waziri wa chakula na waziri mkuu. Naendelea kufarijika kuona watu makini wanaunga mkono CHADEMA karibu sana kiongozi
 
hii nayo kali, alikuwa bado anafanya kazi kama mkuu wa wilaya?
ha ha ha mkuu jamaa aliitwa na kandoro na kuambiwa hayupo miongoni mwa wateule wapya akakimbilia kujiuzulu leo anakimbilia chadema kweli wamezoea kuokota makapi
 
Kandoro/Serikali yasema kujiuzulu kwa Kimolo ni kujikosha

05/05/2012

Serikali mkoani Mbeya, imeshangazwa na kitendo cha Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Bw. Gabriel Kimolo kutangaza hadharani juu ya kujiuzulu kwake ilhali alikuwa akijua wazi kuwa hayumo katika orodha ya wakuu wa wilaya wapya watakaoteuliwa na Rais.

541845678.JPG



Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo alasiri, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro amesema kitendo cha Mkuu huyo kutumia vyombo vya habari kutangaza kujiuzulu ni kujikosha kwa jamii kwani anajua wazi kuwa hayumo ndani ya orodha ya Wakuu wa Wilaya wapya.

Bw. Kandoro alisema kuwa Mkuu huyo wa Wilaya alimfuata ofisini kwake Machi 24 mwaka huu na kumueleza kuwa amepata taarifa za kutokuwemo katika orodha ya Wakuu wa Wilaya wapya.

Akasema, Mkuu huyo alifika ofisini kwake na kumueleza kuwa alipata taarifa hizo Machi 23 kutoka katika idara inayohusika kwamba jina lake halimo. Bw. Kandoro alisema kuwa katika maelezo yake, Mkuu huyo alikuwa akilalamika kwanini ameachwa wakati yeye ni mtendaji mzuri kwa Wilaya na Taifa.

Kwa hivyo, Kandoro anashangazwa na kauli ya Kimolo kwa kuwa anaamini hakupaswa kujiweka hadharani na kulaumu makampuni. Alisema kuwa alichokifanya ni kujikosha kwa jamii ili isishangae wakati uteuzi mpya wa Wakuu wa Wilaya utakapotangazwa na kwamba Bw. Kimolo anapaswa kukubali matokeo ili aweze kuondoka kwa amani.

Hali kadhalika, alimtaka kuacha kuyapaka mayope baadhi ya makampuni kwamba yamehusika kwa namna moja ama nyingine juu ya kudorora kwake kuhusu utendaji wake kudorora.
--

Source: Kandoro/Serikali yasema kujiuzulu kwa Kimolo ni kujikosha - wavuti.com
 
Mgemuuliza kwanza yeye anajiunga na CDM ipi? CDM ya Zitto au Slaa? CDM family au asili?. Yawezekana hajui hata akifanyacho.
 
Jaman kimolo namkubali sana kutokana na msimamo wake hata hivyo ni msimamo wake kuhusu kahawa kuuzwa mbichi au kavu ndo ilifanya asipewe tena nafasi baada ya kuwa na mvutano na Maghembe kama waziri wa chakula na waziri mkuu. Naendelea kufarijika kuona watu makini wanaunga mkono CHADEMA karibu sana kiongozi
hana lolote huyo ni mvivu na mzembe kupindukia
 
Katika hali ya kuonyesha CCM hapako shwari leo mkuu wa Wilaya Gabriel Kimolo amevua gamba na kuvaa Gwanda hii leo ni kwenye Kongamano linaloendelea muda huu katika hotel ya Land mark ambapo wangeni rasmi ni Tundu Lisu, Mnyika, Lema, Msigwa, Heche na Kilewo.

Akiongea na watanzania waliojana kwenye kongamano hilo Kimolo amesema CCM inakufa na kuna kila ishara za CCM kufa mfano kuuwa waandishi wa habari, kutesa wana harakati, kutumia nguvu nyingi kuzoofisha upinza hasa CHADEMA pia amewaomba watanzania kujiunga na chadema kwani kwasasa ni tumaini la watanzania na kuna kila ishara kuwa inaenda kuongoza nchi...


Nawasilisha

============
Gabriel Kimolo, alijiuzulu mwezi Mei 2012 (Ref https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/262111-mkuu-wa-wilaya-ya-mbozi-atangaza-kujiuzulu.html ) kufuatia madai kuwa alikuwa akikejeliwa na wafanyabiashara wakimwita Mbwa!

amehamia CDM baada yakumwagwa-mambo yote ZZK alivyowakalia koooni mpaka raha
 
Nakumbuka mwaka juzi alimwaga manyanga alipokataa maagizo kutoka kwa wakubwa akiwa DC,aliwachana live kuwa yeye hapangiwi afanye nini na asifanye nini na kamwe hawezi kuendeshwa na kuingiliwa kwenye mipango yake ya kuwatumikia wananchi kwa ajiri ya kukidhi mahitaji ya wakubwa fulani

Wenye kukumbuka vyema mtakuwa mnakumbuka,karibu sana kwenye ukombozi kamanda.
 
Mods, kama mnaweza kufuta michango inayochochea ubaguzi, udini na ukabila nitashukuru sana. Haiingii akilini kuona watu wanaendeleza chuki na uchochezi dhidi ya uchaga na makabila mengine. Hii ni hatari. Si dhani kama cdm wanamalengo hayo na isiwape nafasi watu wachache walichukulie hilo kama mtaji wao wa kisiasa.

Tabia hii ikiendelea jf, kwa njia moja ama nyingine ikitokea vita ya ukabila mtakuwa mmechangia. Naipenda jf na nisingependa ikumbwe na kashifa hiyo.
 
dah.huyu kimolo namfaham toka akiwa mkuu wa wilaya ya makete miaka ya tisin ,mkewe ni polisi trafk,cjui kama ,bado yupo kazin,ni mwenyeji wa wa mkoa wa manyara,wilaya ya babati,,mwaka jana alijiuzulu ukuu wa wilaya akiwa mbozi,kwa kifupi ninavyo mfaham
 
Back
Top Bottom