Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Gabriel Kimolo ahamia CHADEMA

Sina shaka Ex DC Kimolo amefanya utafiki wa kina kwani amekuwa ktk serikali ya CCM tangu amalize digrii yake masters ktk demography na kwenda NBS na ndipo Sumaye kumteu kwenda kuwa DC na sasa naami kabisa CCM ina madudu ambayo big shot kama Sumaye is aware of the party kuwa kinataka kupasuka na ndio maana Mh. Kimolo anaogopa bomu kumpasukia.
 
Viongozi wa chama cha democrasia na maendeleo (CHADEMA) mara zote wamekuwa wakisikika kupinga vyeo vya wakuu wa wilaya kwa kusema kuwa vyeo hivyo havina tija na watu wanaoteuliwa kwenye nafasi hizo hawana uwezo wa kufikiri na kutenda wanateuliwa kwasababu tu ni makada wa CCM na maswahiba wa Rais.

Katika hali isiyo ya kawaida tunashangaa kunawaona watu ambao wanadhaniwa kuwa wanauwezo kwenye chadema John Mnyika, Peter Msigwa, Godbless Lema, na Tundu Lisu ambao wamekuwa vinara wa kuwapinga wakuu wa wilaya kuwa hawana uwezo. Leo wako pamoja wametengeneza heading inayosema "MKUU WA WILAYA AHAMIA CHADEMA" Mtu aliyetimuliwa kwenye nafasi yake tangu 2010 wao bado wanamtambua kama mkuu wa wilaya. Kweli hawa ndio tunawategemea waunde baraza la mawaziri CDM ikikamata dola?

Huu ni uvivu wa kufikiri na inaonesha namna gani hawa jamaa wamefilisika sera kichwani. Ndugu Gabbriel Kimolo ambaye wao wanamuita mkuu wa wilaya ni mtu ambaye alitimuliwa kwenye nafasi yake na rais kikwete kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuongoza, ubadhilifu na mambo mengine mengi.

Mara Nyingi CCM wamekuwa wagumu sana wa kumfukuza mtu hata kama amekosea, ukiona CCM imemfukuza mtu basi ujue ameoza kabisa na habebeki lakini mtu kama huyo Leo wafuasi wa Mbowe wanampokea na kumwita kamanda?

Katika hali kama hii CHADEMA isitegemee kufika popote na ndio maana hata nguvu ya UMMA imewageukia na kuanza Oparesheni Timua Mbowe na Slaa ambayo imeshaanza kutekelezwa kwa vitendo huko Kigoma.

CHADEMA inaendelea kufukuza hazina ya vijana na wasomi, wenye uwezo na fikra mpya za kukipeleka chama mbele kwasababu ya maslahi binafsi ya Mbowe na Slaa badala yake inafurahia kula makombo ya CCM ikiamini kuwa makombo hayo hayatahoji chochote kitakachogusa maslahi ya Mbowe na Slaa.

SIAMINI KAMA MAKOMBO YA CCM YANAWEZA KUTUMIWA NA CHADEMA KUIKABILI CCM. HATUWEZI KUENDELEA KWA KUONDOA NURU NA KUKARIBISHA GIZA.

zz.jpg
 
Si bure,tuna miaka mingi sana kupata uhuru...sio wa bendera...wa mawazo! Kungali na watu mnaishi zama za ukoloni bado...
 
Umeandika pasipo kujua nini unachokiandika, kwanza kabisa ungetakiwa uchanganue na kujiuliza maswali yafuatayo
1. Wanaohamia CHADEMA je ni wanachama walioachwa au kufukuzwa kutoka CCM?
2. Wanaohamia CCM je ni wanaCHADEMA walioachwa au kufukuzwa CHADEMA?

Ungejibu maswali haya kabla ya kupost hiki ulichokipost.
1. Tambua kuwa hakuna MwanaCCM aliyehamia CHADEMA baada ya kuachwa au kufukuzwa CCM wote wanahamia wakiwa bado wanachama hai na wanajiunga CHADEMA kwa mapenzi yao pasipo kufuata fedha wala vyeo.

2. Tumeshuhudia wote wanaojiunga na CCM kutokea CHADEMA ni wale waliofukuzwa na wengine kuvuliwa vyeo kwa makosa mbalimbali, na kwa andiko lako hili ni CCM ndio inayochukua MIZOGA kutoka CHADEMA mfano, J.Shonza, M.Mwampamba, Chriss Lukos na wengineo ambao tumeshuhudia ni jinsi gani walivyoingia huko CCM na matamshi yao yalikuwa yanalenga nini na je Wameimarisha CCM au wameibomoa?
3. Tulinganishe hao waliojiunga CCM kutokea CDM ni wa upande upi waliokisaidia chama kujenga heshima yake naomba tulinganishe hawa wafuatao

- Alphonse Mawazo - Kutoka CCM kwenda CHADEMA
- Juliana Shonza, Mtela Mwampamba na Chriss Lukos - Kutoka CHADEMA kwenda CCM
Linganisha mafanikio ya watu hawa utakuja na jibu ya nini ulichokiandika na kujua mawazo yako ulikuwa unayapeleka wapi.
 
Swala si uhai wala ufu wa mhamiaji, bali uwezo na haiba ya mtu husika. Huwezi kula makombo yaliyoharibika wakati chakula kizuri kipo. Huu si wakati wa Chadema kushangilia upokeaji wa wanaccm dhaifu kama mtaji wa kisiasa.
 
Wanaokula makombo ni MACCM wanachukua wananchi walioachwa na Chadema ,Kinana alikuwa anafanya nini na akina BRyson huko chunya,Kikwete kafanya nini na akina Shonza na Mtela ,
 
chadema siyo chama cha maana hata kidogo hata viongozi wake wote wapo kilaghai siyo vinginevyo.
 
CDM kufa haifi,
Mtakosa Usingizi mpaka mpate wehu.
Mjaribu kila mbinu mmechemsha,Ukanda,Vita,Udini,Ukabila,Ugaidi ndiyo kwaaanza Chadema inazidi kupendwa.
Sisi tunasonga mbele.
Mtajitahidi kutunga Mashairi yanawafurahisha ninyi tu, katu vijana wa leo hawayafurahii.
Watakula pesa zenu, lakini kura wala hampati.
:peace:peoplesssss Pawaaaaaaaaaaaaaaa
 
Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Mbozi ndg Gabriel Kimolo alijiuzulu nafasi hyo 2012 acha kupotosha eti alifukuzwa 2010. Mchana mwema mkuu
 
Swala si uhai wala ufu wa mhamiaji, bali uwezo na haiba ya mtu husika. Huwezi kula makombo yaliyoharibika wakati chakula kizuri kipo. Huu si wakati wa Chadema kushangilia upokeaji wa wanaccm dhaifu kama mtaji wa kisiasa.
Kimolo hakufukuzwa ali-resign mwenyewe, kwakuwa serikali haikutaka kuaibika ikadai tayari kulikuwa na barua ya kumfukuza! ccm haijawahi kumfukuza mtu kwa utashi wake pasipo msukumo toka nje (upinzani) kama una kumbumbu lianzishe hapa tukupe data. Kimolo aliita press conference akaeleza sababu za kujiuzulu, waliokombolewa kifkra walimuelewa ila wale wanaotawaliwa kifikra kama wewe hawakumuelewa walibaki na ujinga wao.
 
Huwezi kuresign kwenye hamna, alishapewa barua kwamba hataendelea kuwa mkuu wa wilaya yeye akakimbilia kwa wanahabari kusema kuwa amerisgn. Sasa unadhani kwanini hakuhamia chadema tangu alipofukuzwa ukuu wa wilaya, huoni kuwa mbowe ameenda kumuomba aje cdm kusimamia saccoss?
 
Back
Top Bottom