Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Taifa wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji ajiunga na CCM

Kwa taarifa yako, uimara na kukubalika kwa cdm ilikuwa ni uwezo binafsi wa Slaa kujenga hoja. Mbowe alikuwa anatembelea nyota Slaa na ndio maana Slaa kaondoka Mbowe kaishia kuchemsha na kuomba maridhiano yasiyo na kichwa wala miguu. Huyo Mashinji alikuwa takataka kama takataka nyingine.
Hayo ni yako ila wafia chama wanaojulikana humu hawatambui huo uwezo binafsi wala mchango wake baada ya 2015!

Naheshimu maoni yako.
 
kwanini Mwenyekiti wa Chadema asijiuzulu nafasi yake ili kupisha......mwengine atakaye kiimarisha chama?

maana ni aibu kubwa kwa Mwenyekiti Mbowe chama kumuifia mikonono mwake, bore ajiuzulu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huko alikoenda wanamuona kama guta tu. Anamuiga Waitara ? Hajui kwamba Waitara anapenda beer sana.
 
Mgonjwa akiungua kwa miaka mingi,wanaomuuguza huchoka na pia humuonea huruma kwa mateso ya maumivu ayapatayo.

MWISHO wauguzaji husema,afadharia angekufa akapumzike Kuliko mateso anayopata.

Akifa watu hulia kwa desturi ya kinaadam lakini mioyoni iko afadharia akapumzike. Mashinji alishajifia baada ya kuugua kwa muda mrefu,ikawa afadharia afe akapumzike na mateso.

Leo kazikwa kwenye kaburi CCM. HAPO HAKUNA UCHUNGU WA MSIBA. MBOWE ALAUMIWE KWA LIPI?
Mimi bado nasema Mbowe ana stahili kuubeba huu mzigo wa lawama 2015 alitukosea sana Kumpa Lowassa....wale waliopigania chama kwa moyo mmoja walitengwa kwenye baadhi ya maamuzi mazito leo upinzani umelegea.


Atuombe radhi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa Chadema jinsi ilivyo wacha watu makini watimke..

Pia nawaona na walee soon wataunga juhudi...
 
Hadi kufikia 2025 CHADEMA kitakuwa kimebaki Kama shimo la choo.***** mtaisha wote.
 
Yaani hii inaonesha kwa namna gani Chadema ni dhaifu kwenye suala la intelejensia. Chama kikuu cha upinzani ila kina mambo ya kitoto sana.

Hakuna chama cha kuindoa CCM madarakani hapa nchini maana mizizi ya vyama vyote inanyonya maji kwenye kisima cha CCM.

Mbowe 2015 akawaona watanzania ni wehu sana na kupokea mtu na kumpa kijiti cha kugombea

Bado leo hii watu wanasema Chadema ni chama cha upinzani chenye mikakati ya kushika dola kweli? Labda dola pesa ila sio dola serikali.

Ccm inatumia akili ndogo sana kupumbaza CHADEMA.
 
Labda kama hujui siasa ndio unaweza kusema hivyo. Lowassa alete wabunge wengi kwa kupanda jukwaani na kuongea dakika 2 kwa kusema "Elimu, elimu, elimu? Je, angeweza kuongea nusu saa si angekuwa rais wa Afrika mashariki kabisa. Kwa taarifa yako Lowassa aliikuta CHADEMA ikiwa bora kuliko maelezo, na hata kitambulisho cha kura kiliitwa kichinjio kwani watu walijua Lowassa atapitishwa na CCM.

Ni bahati tu watu walikuwa wanaikubali sana cdm kiasi kwamba hata Mbowe alipofanya upuuzi wa kubadili gia angani bado watu wengi waliopata kura CHADEMA. Usitoke kupotosha ukweli. Kama wabunge wengi waliletwa cdm na Lowassa akiwa na miezi miwili kabla ya uchaguzi, tuonyeshe alifungua matawi mangapi ya CHADEMA baada ya uchaguzi.

Na wewe utakuwa ni mgeni wa siasa za Tanzania

Kuna Mtanzania anachagua mgombea kwa sera zake?

Watu wako chadema sio kwa sera ni kwa sababu hawapendi CCM, na watu wao CCM kwa vile hawapendi upinzani,

Mtu anasema tu me namchagua magufuli muulize CCM ina sera gani ya uchumi hajui.
 
Intelijensia ya Chadema ni kubwa,mno huyu angekiumiza chama ikiwa angepata uongozi.
Sasa kaemda,kama mchezaji huru.

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha uongo hakuna intelejensia pale, kile chama kama makanisa ya kiroho kila ajae anaonekana ni miongoni mwao hata kama ana nia tofauti na yenu.

"Mchungaji mpagani anachunga kondoo wenye kuamini katika roho"
 
Back
Top Bottom