Aliyewahi kuutesa moyo wangu ananitaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyewahi kuutesa moyo wangu ananitaka

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ambassador, Jul 30, 2010.

 1. Ambassador

  Ambassador JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2010
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 932
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kuna dada mmoja nilitokea kumzimia sana miaka ya nyuma lakini pamoja na kumuimbisha nyimbo zote zikiwemo maarufu kama "akanana" hakuelewa somo. Aliamini kwamba alikuwepo mwingine ambaye yeye alimpenda kwa dhati bila kuwa muwazi kama kweli alikuwepo au ilikuwa imani yake tu. Nilimsumbua sana. Kwa kweli aliupeleka puta moyo wangu mpaka nikakosa raha ya maisha kabisaaa! Ililnichukua muda kumfuta kabisa akilini mwangu alipoondoka kwenda nje na wazazi wake.

  Huyo dada karejea nchini na jana kanipigia simu tukutane kwenye mgahawa mmoja jijini. Nilipomuuliza namba yangu kaipataje alisema cha muhimu ni kwamba namba yangu anayo, suala la ameipataje halina umuhimu wowote kwa sasa.

  Niliamua kuitika wito. Kwa kweli dada huyo kapendeza sana kuliko hata alivyokuwa wakati ule namlilia. Tulikaa nae takriban masaa matatu na kwa kweli tuliongea mambo mengi sana. Kwa ufupi alinieleza kwamba ametambua kwamba nilikuwa na mapenzi ya kweli kwake na sasa yuko tayari kuwa na mimi. Isingekuwa nimeshaoa ningemkubalia mara moja! Pamoja na kumueleza kuwa sasa nina familia alisisitiza kwamba awe hata girl friend wangu.

  Huyu dada ana nia gani na mimi kama si kunivunjia ndoa? Ni kweli nilimpenda sana lakini kwa sasa ninae wangu mwandani.
   
 2. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...hehehehe,...duuhh.
  achana nae bana. Mawasiliano yenyewe mmeyafufua jana tu!
   
 3. bht

  bht JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  achana nae si ulimpata wako wa moyo? alichezea nafasi yake
   
 4. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Wewe una msimamo gani? na huyu mke ulioko naye ulimwoa kwa vile huyo mmbeba box alikuacha au na yeye ulimpenda kama ulivyompenda ze europa woman?
   
 5. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Ashakhum si matusi...mwepuke,kuwa tayari kuwekwa vikao kusuluhisha matatzo utakayoyasababisha au... kubali mkeo amegwe siku akikujua unakifanya na huyo haramia!!
   
 6. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  usijaribu, usijaribu.....amekosa kote huk anataka kujishikisha kwako, baadhi ya wanawake wanapenda kujipotezea muda kweli, mie nilivyo na wivu nikae na mtu nusu saa aniambie namuwahi mke wangu cjui kama ningeweza huo ulimwengu, ucmkubali...yaani sasa hivi ndio anakuona wa maana japo umeoa?
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  usijitumbukize huko mzee. kazurura huko na hatimaye kakuona tena? ila cha msingi mwisho wa siku ni nyie wawili mnaojuana vyema. hata mi nina mazingira kama hayo. binti huwa tunaonana hasa kwenye matukio kama sherehe. mambo yake si mabaya hata kidogo, ila huyu humtumia mdogo wangu kiaina kurekebisha mambo. ila cha msingi ndugu ni kusonga mbele maana wanawake wana siri zao
   
 8. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  mtu akipoteza kitu ndio anajua dhamani yake..last week nilikuwa nawapeleka watoto moshi, tukacmama changbay kupata supu, nikakutana na lile langu lililoniachaga, akaangalia mazingira akajua nipo mwenyewe na watoto, akaanza oohh haaa eti nimpe dk 5 za maongezi...mxsiii ovyo kabisa....mtu hutakiwi kurudi nyuma mana hujui umeepushiwa nini.
   
 9. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2010
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Fikiria mkeo&familia yako halafu jiulize mchezo wa siku moja au kadhaa na huyo binti itakuongezea nini maishani mwako..Kama ni mdhaifu utaingia kwenye 18 zake.. Yani mie mtu aliyenitesa simpi nafasi tena nikiwa committed asahau ilhali sitaruhusu mazingira ya kumpa nafasi!

  Kumbuka "woman's heart is a deep sea of secrets" nimeona hii signature kwa mwanaJF mmoja!..mie ni mwanamke na naelewa tulivyo!!
   
 10. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Kwa kifupi huyo dada amejawa na ujinga na anaamini kukukataa wewe imekuwa mkosi kwake na kama bado anaendelea kuitwa MISS wakati kwa umri wake anatakiwa kuwa MRS atafanya juu chini na wewe umrudie hata kwa kuvunja ndoa yako. Wachanga huwa sana na imani hizo ndio maana binti kutoa jibu sikutaki si rahisi ila atakusumbua mpaka ukate tamaa
   
 11. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #11
  Jul 30, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ..hehehehe...'lile' as if lishakuwa lidubwana fulani!
  Ungempa tu dakika tano za 'kuungama'
  au unauruka kwa makusudi tu huu msitari;
  "sameheni kila mtu aliyewakosea ili Baba yenu wa mbinguni apate kuwasamehe ninyi makosa yenu"
  Namsifu mtoa mada, mheshimiwa balozi hapa ambaye alitoa masaa matatu 'ya mkewe' kumsikiliza aliyemkosea.
   
 12. bht

  bht JF-Expert Member

  #12
  Jul 30, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  afu dearest huyo wako wa zamani kuna analokutafutaga huyo........khaaa!!
   
 13. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #13
  Jul 30, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  halafu unaonekana huna mcmamo wa maisha yako, yaani upo upo tu hujitambui...haipendezi hata kidogo.
   
 14. bht

  bht JF-Expert Member

  #14
  Jul 30, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  afu dearest huyo wako wa zamani kuna analokutafutaga huyo........khaaa!!
   
 15. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #15
  Jul 30, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Huyo ni kidudumtu mvunja ndoa za watu
   
 16. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #16
  Jul 30, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  duuuh, wewe mshabiki kweli aisee...ha ha ha ahaaa!
  Mheshimiwa bado anakumbukia jamani, Nyamayao mpe nafasi bana 'ajielezee'...


  Ambassador, pamoja na kwamba 'kanona' usikutoke udenda bana, bomu la kutega hilo!
   
 17. bht

  bht JF-Expert Member

  #17
  Jul 30, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Belly mi hata kama sijawa committed simtaki kabisa......aliye damage moyo wangu to the extent that vipande vimekuwa vigumu kuunga, asidiriki hata kuniaota
   
 18. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #18
  Jul 30, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  ana jipya bac? yote yale yale ya zamani, ohh ulikuwa ni bahati yangu sema bac tu shetani alinipitia..yaani hana jipya kabisa,...nadhani umeshafika pale, binti yangu(mtoto wa mr) kaenda kununua maji counter akakutana nae huko, kamhoji mpo na dady pia?..mtoto akamjibu hapana...katoka nae nje kamshika mkono...nilichukia na supu ckuimaliza tukajiondokea....yaani imekuwa kero kabisa.
   
 19. tete'a'tete

  tete'a'tete JF-Expert Member

  #19
  Jul 30, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 474
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Achana naye! huko nje alikokua ameupiga umalaya umemshinda ndio anaona we wa kuja kula makopo! aisee hebu na wewe mrikie ili ajifunze....hana adabu huyo...Ingekuwa mimi angeipata....hata hiyo kunipigia ningesikia sauti yake ningemzimia simu....
   
 20. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #20
  Jul 30, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Kubali yaishe!
   
Loading...