Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Penny

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
575
48
1593269011352.png

Naomba msaada wa hivi vinyama vilivyoniota pembezoni mwa shimo la haja kubwa vinaitwa piles kwa kimombo, kiswahili sijui. Hivi vidude huwa vinauma na kuacha, naweza kukaa miezi 8 hadi mwaka sivisikii ila vikianza kuuma nashindwa kukaa au hata kutembea. Naomba msaada wa dakatari yoyote anayevijua aniambia chanzo na matibabu yake. asanteni

BAADHI YA WADAU WANAOELEZA KUATHIRIKA NA TATIZO HILI


UNDANI WA TATIZO LA BAWASILI

Bawasiri yaweza kuwa moja ya topic ngumu sana kuzungumziwa kiuwazi na watu, hii ni kutokana na wagonjwa wengi kuona aibu pengine ni kwasababu tatizo husika hutokea mahala pa haja kubwa. Wengine huona aibu hata kueleza tatzo hili kwa Dactari ama muhudum wa afya, bawasili ni tatizo kuwa linawatokea wanaume kwa wanawake. Naweza kusema uwepo wa tatizo hili si ajabu ukianagalia wengi wetu wanakula vyakula zaidi vilivyosindikwa, hawafanyi mazoezi na wana msongo wa mawazo uliokithiri.

Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na nje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe. Ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu tunauita HEMORRHOIDS na kwa lugha ya kingereza unafahamika kama piles.

Tatizo la bawasili huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50% ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 40 mpaka 50.

Kuna Aina kuu mbili za bawasiri

(A) Bawasili ya ndani
Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili,.Aina hii hutokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa

Aina hii imegawanyika katika madaraja manne

(1)DARAJA LA KWANZA
Hii ni bawasiri ambayo haitoki mahali pale panapohusika

(2)DARAJA LA PILI
Hii hutokea wakati wa haja na kurudi yenyewe ndani baada ya kujisaidia

(3)DARAJA LA TATU
Hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenywe

(4)DARAJA LA NNE
Hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi.

(B)Bawasili ya nje
Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu Hilo pia husababisha mishipa ya damu (vena) kupasuka na damu kuganda na kasababisha Aina ya bawasiri iitwayo THROMBOSED HEMORRHOIDS

Bawasili kwa kiasi kikubwa huletekezwa na kuongezeka kwa mganadamizi ama presha mara nyingi ni pale unapojikaza ili kutoa haja kubwa. Hivo bawasili huwatokea zaidi watu wenye matatizo ya mfumo wa umen’gemnyaji mfano unapata choo kigumu, tumbo kujaa gesi, kukosa choo kwa siku kadhaa.

Wamama wenye ujauzito pia huwa kwenye hatari kubwa ya kupata bawasili kutokana na mtoto aliye tumboni kugandamiza tumbo la chakula na hivo kuathiri utoaji wa haja kubwa, kwa bahati nzuri bawasili inayosababishwa na ujauzito huanza kuisha pale tu mama anapojifungua. Watu wenye kitambi na uzito mkubwa pia wapo kwenye hatari kubwa ya kupata bawasili kutokana na mwili kushindwa kutengeneza nishati ya kutosha kusukuma uchafu kwenye utumbo.

Wakati mwingine inatokea unaweza kuwa na bawasili lakini usipate dalili na baada ya mfupi ugonjwa huweza kupotea wenyewe. Dalili moja kubwa ambayo wagonjwa wetu wengi huipata kwa wenye bawasili ya ndani ni kuvuja kwa damu inatyoweza kuonekana kwenye toilet paper ama kinyesi, unapoona dalili kama hizi hakikisha unachukua hatua za haraka maana tayari umepata bawasiri.

Kama una bawasiri ya nje basi unaweza kupata viashiria kama uwepo wa nundu nyekundu iliyojaa damu pembeni mwa mahala pa haja kubwa, kitaalamu huitwa thrombosed hemorrhids na huambatana na maumivu makali sana wakati wa kutoa haja, kama utoaji wako wa haja ni wa kujikamua na kwenda haraka haraka, na kujisafisha kupita kiasi basi unaweza kuongeza tatizo, ianashauriwa kutotumia nguvu kubwa kujisaidia.

Si kila Unapoona kuna damu inavuja ni Bawasili
Unapoona kuna damu inavuja mahala pa haja kubwa ama unapotoa haja, basi nashauri nenda haraka hospital kuonana na Dactari na kufanya vipimo, hasa kama tatizo ni limekutokea kwa mara ya kwanza. Kuvuja kwa damu kwenye sehemu ya haja kubwa inaweza kuwa ni dalili za Saratani ya utumbo mpana . kitu kimoja cha kuvutia sana ni kwamba uwepo wa Vitamn D ya kutosha mwili hupunguza hatari ya kupata Bawasili kwa karibu 80%, kwahiyo kama tatizo linajirudia mara kwa mara basi fanya checkup kujua kama una Vitamn D ya kutosha.pia unaweza kutembelea stoo yetu ya virutubisho kwa kubonyeza hapa kupata kirutubisho chenye Vitamin zote.
  1. Kufanya mapenzi kinyume na maumbile
  2. Kuharisha kwa muda mrefu
  3. Kukaa kitako kwa muda mrefu
  4. Matumizi ya vyoo vya kukaa kwa muda mrefu
Dalili zingine za zitakazokusaidia kugundua kama una tatizo la bawasili ni;
  • Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
  • kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia
  • Kutokea uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Kujitokeza kwa kinyama katika eneo la tundu Hilo
  • Kinyesi kuwa na damu na kunuka harufu mbaya sana
HATUA NNE ZA KUZUIA KUTOKEA KWA BAWASIRI
Hapo juu tumeona kwamba chanzo kikubwa cha tatizo hili ni matatizo ya mfumo wa umen’genyaji kama kukosa choo kwa mda mrefu, kupata choo kigumu, kuharisha mara kwa mara na tumbo kujaa gesi, hivo kwa kuzuia matatizo haya basi utakuwa umejikinga na bawasili. Hivo hakikisha unafanya yafuatayo;
  1. Kula mbogamboga za majani, na nafaka zisizokobolewa, matumizi ya vyakula vya nyuzinyuzi kwa wingi husaidia kuongeza ukubwa wa kinyesi na hivo kurahisha utolewaji wake, kama mwanzo hukutumia vyakula vya nyuzinyuzi basi anza kuongeza taratibu kwenye mlo wako mpaka pale tumbo litakapozoea.
  2. Tumia machungwa kwa wingi, machungwa yana kiungo kinachoitwa flavonoids, kiungo hiki ni muhimu katika ustawi wa mishipa ya damu ya Veins, mishipa hii ndio huathirika na kuletekeza bawasiri.
  3. Kunywa maji ya kutosha kila siku, tumia kiu na rangi ya mkojo kama kiashiria cha kiasi gani cha maji unatakiwa kunywa, kama mkojo ni wa rangi ya njano inayokolea basi ni kiashiria kwamba mwili hauna maji ya kutosha na unatakiwa kunywa. Nyuzinyuzi na maji ya kutosha husaidia kulainisha choo chako na hivo kurahisisha utolewaji wake bila kujikamua.
  4. Hakikisha unapata virutubisho kwa ajili ya kusawazisha Bacteria wazuri ndani ya mfumo wa chakula, vyenye ubora wa hali ya juu usimeze kila kirutubisho.
ZINGATIA HAYA UNAPOKUWA CHOONI
1. Ruhusu mwili wako kufanya kazi kwa jinsi ulivoumbiwa, yaani pale unapojiskia haja basi hakikisha unaenda mara moja kujisaidia pasipo kujizuia, kujichelewesha kunaweza kusababisha Constipation.

2. Usikae mda mrefu chooni ukijisaidia, hii inaongeza mgandamizo katika eneo la chini kwenye mishipa ya damu na hivo kukuongeza hatari ya kupata bawasili. Tumia dakika 3 mpaka 5, ama subiri mpaka unapokuwa na haja, kama unajiskia kutoa uchafu lakni ukienda chooni kinyesi hakitoki basi tembea tembea ama fanya zoezi la Squats.

3. Usitumie nguvu kubwa kujikamua kutoa haja, tumia misuli ya tumbo kutoa haja taratibu.

4. Unapotoa haja basi hakikisha unachuchumaa kama miili yetu ilivoumbwa, watu wanaotumia njia hii mara chache sana huugua bawasili, lakini matumizi ya vyoo vya kukaa ni moja ya kihatarishi cha kupata bawasili kutokana na kwamba inahitajika utumie nguvu kubwa sana kujikamua.

TUMIA NJIA NZURI NA SALAMA KUJISAFISHA
  • Usitumie nguvu kubwa kujifuta kwa toilet paper ama wipes zingine baada ya kwenda haja, hii hufanya ngozi kulanika na kuvimba
  • Kama inawezekana jisafishe taratibu kwa kutumia maji bila sabuni, na kujifuta kwa taulo laini.
  • Kwa maeneo ambapo huwezi kutumia maji mfano kwenye vyoo vya umma, basi tumia wipes laini zenye unyevunyevu kwa umakini.
KUPUNGUZA ATHARI YA BAWASILI KAMA TAYARI UMEUGUA
Ushauri huu siyo kwamba hutakiwi kufika hospitali kupata huduma, ama kuonana na dactari wako, ni ushauri ambao tunawapa wagonjwa wetu wote kabla hawajafika Ofsini kwetu kupata huduma ya Dawa na Virutubisho.
  • Jaribu Sitz Bath, hii inajumuisha mgonjwa wa bawasili kuvua nguo na kukaa kwenye maji yenye uvuguvungu kwenye beseni kwa mda wa dak 15 mpaka 30, unaweza kukaa mara nyingi uwezavyo, hakiksha maji siyo ya moto ni ya vuguvugu, itakusaidia kupunguza maumivu.
  • Chukua kipande cha barafu kilichoganda na kukiweka mahala pa haja kubwa kwa dak 10 mpaka 15 kwa siku.
  • Chukua mmea wa Aloe-vera ukate kisha loweka kwenye maji, baada ya hapo chukua kitambaa laini loweka kwenye maji yenye aloe vera na upakae taratibu mahali pa haja kubwa.
MUHIMU: Ushauri huu ni kwa ajili ya kupata nafuu ya haraka, hivo hakikisha unafika hospitali kupata matibabu

Madhara Ya Tatizo La Bawasiri
1. Kupata upungufu wa damu (anemia)
2. Kupata tatizo la kutokuweza kuhimili choo
3. Upungufu wa nguvu za kiumekwa wanaume na Kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake
4. Kuathirika kisaikolojia
5. Kukosa moral ya kufanya Kazi na maumivu makali

Matibabu ya bawasiri yamegawanyika katika sehemu mbili na hutegemea na aina ya bawasiri
1. Tiba iliyozoeleka ni kukatwa kinyama ambayo hutoelewa hospital na kuendelea na lishe ya chakula. Hata hivyo tiba hii si nzuri kwasababu huwa haitibu chanzo cha tatizo hivyo huwa rahisi kujirudia, ndiomana katika kituo chetu tunashauri kutibu chanzo cha tatizo.

2. Tiba ya tatizo hili kwa kutumia vidonge vilivyotengenezwa kwa mimea.

Credit: LIndaafya.com
 
Naomba msaada wa hivi vinyama vilivyoniota pembezoni mwa shimo la haja kubwa vinaitwa piles kwa kimombo, kiswahili sijui.

Nadhani yanaitwa mafutuni kwa Kiswahili.
I would double check that,ni miaka mingi tangu nipitie ''Mahali Pasipo na Daktari''.
 
Main Ingredient: Hydrocortisone

Anusol-HC is a topical corticosteroid given to treat the rash, itching, inflammation, and other forms of skin disorders including eczema and psoriasis. Drugs like Anusol-HC do not cure the cause of these problems but they can quickly relieve the symptoms by interfering with the production of various substances in the body that cause these skin disorders. That is why it is imperative that corticosteroids like Anusol-HC should not be used without prior consultation of your physician, as these conditions could be a symptom of a larger problem.

Anusol-HC is for external use only.

ANUSOL-HC CAUTION
Avoid using large amounts of Anusol-HC over large areas of your body as this could lead to needless side effects somewhere else in the body.

Topical corticosteroids like Anusol-HC should not be used as the exclusive treatment for serious skin diseases like herpes, fungus, or skin tuberculosis.

Do not use Anusol-HC if you ever had an allergic reaction from using it in the past.
Prolonged use of topical corticosteroids like Anusol-HC near the eyes may cause cataracts or glaucoma.

Children are more at risk of serious side effects from Anusol-HC. Anusol-HC should not be given to infants under one year of age or for children older than 1 year more than 3 weeks.

ANUSOL-HC SIDE EFFECTS
Common side effects of using Anusol-HC may include allergic reaction, rash, irritation, acne, itching, and discoloration of skin. The side effects are more likely when the treated area is covered with waterproof bandage.

Use of large quantities of topical corticosteroids like Anusol-HC over large parts of your body should be avoided as large quantities may be absorbed into the blood stream, which could lead to serious side effects.

ANUSOL-HC INTERACTIONS
Check with your physician before combining Anusol-HC with other steroids.


ANUSOL-HC AND PREGNANCY
Topical corticosteroids like Anusol-HC may cause birth defects especially when applied in large amounts. If you are or think you may be pregnant, do not use Anusol-HC without first checking with your doctor.

Nursing mothers should switch to bottle feed while using Anusol-HC.

ANUSOL-HC DOSES
Consult with you doctor or pharmacist as the doses vary with each condition.

ANUSOL-HC OVERDOSE
There are no known symptoms of Anusol-HC overdose. However, if you suspect Anusol-HC overdose, seek medical help right away.
 
Penny. hakikisha choo chako ni kilaini, msukumo wowote tumboni kuelekea sehemu ya haja kubwa kama vile uvimbe, kuinua vitu vizito pia husababisha tatizo hili.

Kula mboga mboga na matunda kuzuia choo kigumu. If symptoms persist onana na daktari aziondoe.
 
Penny. hakikisha choo chako ni kilaini, msukumo wowote tumboni kuelekea sehemu ya haja kubwa kama vile uvimbe, kuinua vitu vizito pia husababisha tatizo hili. Kula mboga mboga na matunda kuzuia choo kigumu. If symptoms persist onana na daktari aziondoe.
Hizo Piles chanzo chake ni nini?
 
Pole sana, ndugu!

Piles ni "Bawasili" kwa Kiswahili. Inapofikia hatua kubwa, mara nyingi wanafanya upasuaji -- ambao si mkubwa.

Bawasili huweza kusababishwa na mtu kutumia nguvu nyingi wkt wa kujisaidia haja kubwa, kujifungua (kwa wanawake), kupata haja kubwa laini ambayo inatoka kwa nguvu (purging) kiasi cha kushindwa kujizuia kabisa, n.k.

Km walivyotangulia kusema wengine, epuka vyakula vikavu, na kula kwa wingi matunda, sharubati (juice) -- hasa ya ukwaju, na mboga za majani.

Kuna dawa moja ya asili ambayo sijathibitisha ufanyaji kazi wake. Ni tumba (mbegu) za ukwaju; unazisafisha kwa maji safi (vizuri ya moto), unazisaga (kwa mfano ktk jiwe lenye rough surface), kisha unapaka ktk sehemu yenye bawasili. Fanya hivyo mara 2 au 3 kwa siku. Huenda ikakusaidia.

Kila la Kheri, na Ugua Pole!
 
Ndugu wapendwa kwa pamoja, nawashukuruni sana wote mlioweza kutumia mda wenu kunisaidia katika hili tatizo. Nawaombeeni kwa Mungu awazidishie afaya na nguvu muendelee na miyoyo hiyo hiyo.
 
nimesikia hata majani ya mbono yanaweza kusaidia pia ni dawa nzuri

Umenikumbusha! Asante!

Hata mizizi ya M'bono inasaidia sana! Inaoshwa, kisha inachemshwa, na kuhifadhiwa ktk chombo (kwa mfano, chupa). Mgonjwa anakunywa nusu kikombe mara 2 au 3 kwa siku. Mizizi iliyobaki, inaweza kuchemshwa tena kwa nusu ya maji yaliyotumiwa awali.

Mizizi ya mti huu inatumika pia kutibu kikohozi kikavu. Kwa matatizo haya, ni vema kuiosha mizizi kwa maji sana (vizuri ya moto), na kuitafuna mizizi na kumeza majimaji yake tu. Ni dawa nzuri, inatibu kifaduro pia.
 
(Hemorrhoids) BAWASIRI

Definition



How To Treat Piles.jpg


Hemorrhoids

Hemorrhoids, also called piles, are swollen and inflamed veins in your anus and lower rectum. Hemorrhoids may result from straining during a bowel movement or from the increased pressure on these veins during pregnancy, among other causes.

A sometimes embarrassing topic of discussion, hemorrhoids are one of the most common ailments. By age 50, about half of adults have had to deal with the itching, discomfort and bleeding that can signal the presence of hemorrhoids.
Fortunately, many effective options are available to treat hemorrhoids. Most people can get relief from symptoms using home treatments and lifestyle changes.

Na Pia Zipo DawaZa Kienyeji Za kutibu huo Ugonjwa Wa Bawasiri au kwa jina La kitaalamu Hemorrhoids Au Piles Ukizihitaji Waweza kunitafuta

Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na+905552016614
 
Umenikumbusha! Asante!

Hata mizizi ya M'bono inasaidia sana! Inaoshwa, kisha inachemshwa, na kuhifadhiwa ktk chombo (kwa mfano, chupa). Mgonjwa anakunywa nusu...
Asante ndugu, ila huo mzizi sijawahi kuusikia kwa kweli pengine kwa msaada mzuri ni wapi ninapoweza kupata. Kama wachangiaji wengine walisome naweza kwenda kwa wamasaii.
 
Hemorrhoids Home Remedy Using Milk And Radish


Conditions Treated: Nutrition and Metabolism

Specific Conditions Treated: Hemorrhoids

Ingredients Used: Milk, Radish

Description: Piles or hemorrhoids is one of the most common ailments today. It is a varicose and often inflamed condition of the veins, inside or just outside the rectum. In external piles, there is a lot of pain but not much bleeding. In the case of internal piles, there is discharge of dark blood. In some cases the veins burst and this results in what is known as bleeding piles.

Pain at passing stools, slight bleeding in the case of internal trouble, and feeling of soreness and irritation after passing a stool are the usual symptoms of piles. The patient cannot sit comfortably due to itching, discomfort, and pain in the rectal region.

The primary cause of piles is chronic constipation and other bowel disorders. The straining in order to evacuate the constipated bowels, and the pressure thus caused on the surrounding veins leads to piles. Piles are more common during pregnancy and in conditions affecting the liver and upper bowel. Other causes are prolonged periods of standing or sitting, strenuous work, obesity, general weakness of the tissues of the body, mental tension, and heredity.
Directions For Use: Grate a radish and extract its juice. Then mix a little milk into this juice. Apply this mixture on the affected parts
Expected Results Within: 1 week
 
Hemorrhoids Home Remedy Using Goat milk


Conditions Treated: Nutrition and Metabolism

Specific Conditions Treated: Hemorrhoids

Ingredients Used: Goat milk

Description: Piles or hemorrhoids is one of the most common ailments today. It is a varicose and often inflamed condition of the veins, inside or just outside the rectum. In external piles, there is a lot of pain but not much bleeding. In the case of internal piles, there is discharge of dark blood. In some cases the veins burst and this results in what is known as bleeding piles.

Pain at passing stools, slight bleeding in the case of internal trouble, and feeling of soreness and irritation after passing a stool are the usual symptoms of piles. The patient cannot sit comfortably due to itching, discomfort, and pain in the rectal region.

The primary cause of piles is chronic constipation and other bowel disorders. The straining in order to evacuate the constipated bowels, and the pressure thus caused on the surrounding veins leads to piles. Piles are more common during pregnancy and in conditions affecting the liver and upper bowel. Other causes are prolonged periods of standing or sitting, strenuous work, obesity, general weakness of the tissues of the body, mental tension, and heredity.

Directions For Use: Take a quarter liter of goat's milk. Keep it for curdling overnight. In the morning, add an equal quantity of carrot juice to it. Blend them together and drink it. You can also have freshly prepared goat's milk yogurt with some freshly chopped carrots.
Expected Results Within: 3 days
 
Mara ya kwanza kuregister na nimeanza kimatatizo.

Mwana JF mwenzenu kwa kipindi cha miezi kama miwili hivi, nimekuwa nikipata maumivu makali wakati wa kujisaidia haja kubwa. Maumivu haya yanakuja nikiwa na choo kigumu au chepesi.

Huwa ni maumivu kama kuna kitu kinakwanguliwa au kuna kidonda hivi. Lakini pindi nikimaliza haja kubwa sisikii tena na wala sihisi kama kuna maumivu!

Hivi karibuni nilipata vurugu tumboni baada ya food poisoning, ile combination ya maumivu kwa kweli hailezeki. sehemu inayouma ni kwenye outlet (anus) pale pale na si kwingine.

Maana ningekuwa nayasikia hata kwente rectum ningeweza sema, ila ni juu kabisa wakati wa defacation.

Nilikwenda mwona Doctor, yeye aliniandikia flagyls ambazo nilizinywa wala sijapata nafuu. Alihisi kuna infection au inflammation. Sasa niko njia panda, nifanyeje? Sijui hata huko hospital nielezeje hasa hali yangu?!

Naomba mawazo pa kuanzia. Asanteni.

========= Majibu========

BAWASIRI (HEMORRHOIDS)


695px-M_44_anus_22.jpg



Bawasiri ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi. Bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.

Kuna aina mbili za Bawasiri
Nje: Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.


Ndani: Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.
Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:
Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.

Je bawasiri husababishwa na nini?
Bawasiri husababishwa na;


  • Tatizo sugu la kuharisha
  • Kupata kinyesi kigumu na kinyesi wakati mwengine kutokwa damu kisha ndio kupata kinyesi
  • Ujauzito
  • Uzito kupita kiasi (obesity)
  • Kupenda kufanya ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)
  • Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.
  • Umri mkubwa

Dalili za bawasiri



  • Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
  • Maumivu au usumbufu
  • Kinyesi kuvuja
  • Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Kujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa

Matatizo yanayoweza kutokana na Bawasiri



  • Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
  • Strangulated hemorrhoids


786813_f260.jpg


Vipimo na uchunguzi



  • Digital rectal examination
  • Kipimo cha njia ya haja kubwa (Proctoscope)
  • Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)

Matibabu
Matibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri



  • Rubber band ligation - Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.
  • Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano
  • Coagulation (infrared, laser and bipolar)
  • Upasuaji;
    • Hemorrhoidectomy
    • Stapled hemorrhoidopexy

Njia za kuzuia Bawasiri



  • High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
  • Kunywa maji ya Uvuguvugu mengi kwa siku (glasi sita hadi nane kwa siku)
  • Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa.


Kutibu kwa kutumia njia Mbadala Maradhi ya BAWASIRI:

Kila Tiba kati ya zifuatazo ni yenye kujitegemea.Chagua iliyo rahisi kwako.Isipokufaa ndipo uchague nyengine

TIBA 1: MAKAL-ARZAK

Chukua 100grm kwa kila lita moja na robo ya maji (1250ml).

Chemsha mpaka ibakie lita moja kamili.
Kunywa ujazo wa kikombe kimoja cha kahawa (50ml) kutwa mara tatu (1×3) mpaka dawa imalizike.

MWIKO : Mgonjwa asitumie nyama nyekundu aina yoyote,asile pili pili na wala asitumie vitu vikali.Badala yake atumie kwa wingi mboga za majani,matunda,maziwa na samaki.

TIBA 2:
Changanya unga wa Habat soda na Asali safi ya nyuki vipimo vya sawa kwa sawa.Halafu kunywa kijiko kimoja kimoja mara kwa mara.Fuatilishia na kumywa maji glasi moja (250ml) kila umalizapo kunywa hiyo dawa.

TIBA 3:
Jipake mafuta ya Mbarika kwenye utupu wa nyuma ambapo ndipo bawasiri hutokea.Fanya hivyo mara kwa mara, kwa sababu huirudisha hiyo bawasiri ndani.
Mbarika hujulikana vile vile kwa majina ya mbono,nyonyo au castor oil. Mkuu.@gedoTumia kisha unipe Feedback.
 
Ugonjwa uliotapakaa sana kwa wanaume wengi ktk nchi zetu za kitropiki,hali ya hewa,joto jingi,kutokunywa maji kwa wingi,choo kigumu nakujikamua sana, mwisho bawasiri, kuna sababu nyingine,kurithi ugonjwa etc, stages tofauti, inaweza kutibika ama kwa vidonge au ikiwa kubwa opersheni ni lazima.
 
Nataka kujua hivi ni nini kinachosababisha bawasir au haemorhoids kwenye njia ya haja kubwa?

Kwanza "Hemorrhoids" ama "Piles" husababishwa zaidi na mtu anapotumia nguvu kupata haja kubwa (naomba mnisamehe kama lugha si nzuri), ina maana kama unapata choo kigumu, msukumo huwa mkubwa na kutokea mkwaruzo na kusababisha veins kuvimba. Kukosa choo (constipation), mimba na umri mkubwa pia husababisha hii kitu, hasa kuanzia miaka 50. Pia kuingiliwa kinyume na maumbile husababisha. Pia leo ndio nimejua hii kitu kiswahili inaitwa Bawasir.

Ziko aina ngapi ya bawasir?.

Kwa kungalia uvimbe uliko, ziko za aina mbili, zinazotokea nje ama chini ya ngozi ya sehemu ya haja kubwa, na kuna zinazotokea ndani ya sehemu ya haja kubwa.

Je inatibika bila ya operation?

Yaweza kutibika bila kufanyiwa upasuaji, muhimu ni kula vyakula vyenye kiasi kikubwa cha nyuzinyuzi (fiber). Pia kunywa maji mengi. Hii inasaidia kukifanya choo kiwe laini na hivyo kupunguza msuguano na pia kupunguza msukumo wakati wa kutoa haja kubwa. Pia inatakiwa unapojisikia tu haja kubwa ukajisaidie, sio kuahirisha nayo ina madhara makubwa. Kuna dawa unaweza pewa, siwezi kukutajia hapa, zinasaidia na kumaliza kabisa wakati fulani.

Wanawake nao huwa wanaupata ugonjwa huu?

Ni ugonjwa unaotokea kwa jinsia zote.

Kwa nini baada ya kumaliza haja kubwa huanza kuwasha na kuwa kero?

Sana sana ukiona inawasha, huwa ni zile vimbe za nje, vimbe za ndani huwa hazina matatizo sana, kama muwasho. Lakini kwanini huwasha baada ya haja?, ni kwamba baada ya haja ile sehemu huwa imesuguliwa ama wakati unasukuma unachokoza zile vimbe katika veins.

Na kwa nini wakati mwingine huwa haitokei? Has it to do with type of foods/drinks?

Hii kitu inaweza kutokea, ikapotea kwa siku, wiki, miezi, mwaka, miaka na kurudi tena. Hivyo ni vizuri kubadili aina za vyakula na kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kwa wingi, muhimu zaidi ni kunywa maji mengi iwezekanavyo.

Pia kupunguza vyakula vyenye pilipili na binzari (hot and spicy foods) inaweza kusaidia.

Muhimu: Ni vizuri kwenda hospitali ili upate kuchunguzwa zaidi.
 
Asante mtoa mada na zaidi asante bra Mfumwa kwa elimu uliyotoa,
 
Dear, JF Doctor+ wadau.

Tafadhali ninaomba ushauri wenu (samahani kama lugha itakuwa kali kidogo). Nina kinyama kidogo kimeota sehemu ya matakoni pembeni mwa njia ya haja kubwa kuanzia nikiwa form three. Nilijaribu kuuliza siku za nyuma nikaambiwa inasababishwa na choo kuwa kikavu (kutokunywa maji) hivyo nikaanza kunywa maji kwa wingi.

Sasa naomba kujua kama kuna namna yeyote au dawa ya kukiondoa maana kinanikosesha raha sana.
Asanteni.
 
Dear, JF Doctor+ wadau.
Tafadhali ninaomba ushauri wenu (samahani kama lugha itakuwa kali kidogo). Nina kinyama kidogo kimeota sehemu ya matakoni pembeni mwa njia ya haja kubwa kuanzia nikiwa form three. Nilijaribu kuuliza siku za nyuma nikaambiwa inasababishwa na choo kuwa kikavu (kutokunywa maji) hivyo nikaanza kunywa maji kwa wingi.

Sasa naomba kujua kama kuna namna yeyote au dawa ya kukiondoa maana kinanikosesha raha sana.
Asanteni.

Surgical operation! ni suluhisho
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom