Aliyevujisha barua ya walimu kutakiwa kuvunja makundi yao ya whatsapp asakwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,482
9,242
Picha

WAKATI Waratibu Elimu Msingi wakiagizwa kuvunja kwa makundi sogozi (WhatsApp group), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Dk Semistatus Mashimba, ametangaza kumsaka aliyevujisha barua inayoagiza kuvunjwa kwa makundi hayo.

Barua hiyo tangu Agosti 19, mwaka huu, imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha kuwaelekeza waratibu kata wote kuvunja makundi yote ya sogozi yanayojihusisha na mawasiliano kwa walimu.

Agizo la kuvunjwa kwa makundi sogozi kwa walimu linakuja ikiwa Chemba inakumbukumbu mbaya ya kufutiwa matokeo ya darasa la saba kwa shule zote wilayani humo.

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), lilifikia uamuzi huo baada ya kubainika undaganyifu uliofanywa na maofisa elimu ambapo nyezo iliyotumika katika udanganyifu huo ulikuwa ni makundi sogozi.

Chemba ina shule za msingi 103 ambapo wanafunzi 5,362 walijiandikisha kufanya mtihani wa darasa la saba mwaka jana wakati wanafunzi 5,171 ndio waliofanya mtihani uliofutwa na NECTA.

Dk Mashimba alisema hatua hiyo ilichukuliwa kuepuka yaliyojitokeza mwaka jana ambapo shule za wilaya zote zilifutiwa matokeo ya mitihani ya darasa la saba. Alisisitiza kuwa sasa wanamsaka aliyevujisha barua hiyo.

“Mwaka jana makundi ya ‘WhatsApp’ yalibainika kutumika kuwasiliana na kuvujisha mitihani, jambo ambalo si kweli.

Hata hivyo, hiyo ilisababisha shule zetu zote 103 zifutiwe matokeo. Kutokana na hayo, tumeamua kuvunja makundi sogozi yote ya Waratibu Elimu na si ya watumishi wengine.” Alieleza. Alisema kwa sasa ofisi yake inafuatilia nani aliyepiga picha na kurusha barua hiyo kwenye mitandao.

“Waratibu Elimu Kata Chemba wapo 26 hivyo tunafuatilia kujua nani aliyefanya hivyo kwakuwa wapo wachache. Akibainika hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake,”alisema.

Barua hiyo iliyosainiwa na Josephat Ambilikile kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chemba, inaelekeza kuvunjwa kwa makundi hayo ya ‘Whatsapp’ yanayojihusisha na kutoa au kupokea taarifa zozote zinazohusu utendaji wa taaluma na utaalamu, zinazomgusa mwalimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba katika utendaji wake wa kila siku hadi hapo watakapojulishwa vinginevyo.

Katika barua hiyo ambayo nakala yake ilipelekwa kwa Walimu Wakuu,Waratibu Elimu Kata wote walitakiwa kuvunja makundi hayo hususani yanayotumika kutoa au kupokea taarifa zozote zinahusu utendaji kitaaluma.

“ Pia ofisi imebaini kuwepo kwa mkundi ya whatsapp katika halmashauri yetu yanayotoa na kupokea taarifa mbalimbali za kielimu na kijamii,” alisema.

Barua hiyo imetaja makundi hayo kuwa ni ya Walimu Wakuu waliovuliwa madaraka na Walimu Wakuu wapya, Walimu Wakuu waliopo madarakani, maofisa elimu kata na Walimu Wakuu ngazi ya kata na wilaya na mengineyo yanayofanana na hayo.
 
Wa Tz kwa kujipa mizigo isiyo ya lazima! Sasa WhatsApp haikuhusika na uvujaji/udanganyifu wa mitihani, wanajisumbua nini kuyafuta makundi? Hilo limevuja, sasa anatafutwa aliyevujisha. Juhudi, nguvu na muda unaopotezwa kwa haya mambo yataongeza ufaulu wa watoto?
me naona kama udanganyifu ulianza kitambo tu kabla hizi whatsap hazijaingia..
 
Huyo DED naye hana kazi nyingine za kufanya au? Sasa kama hilo agizo amekiri mwenyewe kulitoa, nongwa iko wapi? Si alitoa agizo hilo kwa nia njema? Au hiyo barua ilikua ni ya siri kiasi kwamba ingehatarisha usalama wa nchi kwa kusambazwa kwake kwenye hiyo mitandao ya kijamii!
 
Wa Tz kwa kujipa mizigo isiyo ya lazima! Sasa WhatsApp haikuhusika na uvujaji/udanganyifu wa mitihani, wanajisumbua nini kuyafuta makundi? Hilo limevuja, sasa anatafutwa aliyevujisha. Juhudi, nguvu na muda unaopotezwa kwa haya mambo yataongeza ufaulu wa watoto?

Nashindwa kuoanisha elimu, akiili na busara za hao maofisa wanaoomba walimu wafute makundi hayo ya whatsapp, hivi wanashindwa kutafuta suluhisho jingine muafaka na sio kugombana na technologia inayokua kila siku?
 
Picha

WAKATI Waratibu Elimu Msingi wakiagizwa kuvunja kwa makundi sogozi (WhatsApp group), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Dk Semistatus Mashimba, ametangaza kumsaka aliyevujisha barua inayoagiza kuvunjwa kwa makundi hayo.

Barua hiyo tangu Agosti 19, mwaka huu, imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha kuwaelekeza waratibu kata wote kuvunja makundi yote ya sogozi yanayojihusisha na mawasiliano kwa walimu.

Agizo la kuvunjwa kwa makundi sogozi kwa walimu linakuja ikiwa Chemba inakumbukumbu mbaya ya kufutiwa matokeo ya darasa la saba kwa shule zote wilayani humo.

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), lilifikia uamuzi huo baada ya kubainika undaganyifu uliofanywa na maofisa elimu ambapo nyezo iliyotumika katika udanganyifu huo ulikuwa ni makundi sogozi.

Chemba ina shule za msingi 103 ambapo wanafunzi 5,362 walijiandikisha kufanya mtihani wa darasa la saba mwaka jana wakati wanafunzi 5,171 ndio waliofanya mtihani uliofutwa na NECTA.

Dk Mashimba alisema hatua hiyo ilichukuliwa kuepuka yaliyojitokeza mwaka jana ambapo shule za wilaya zote zilifutiwa matokeo ya mitihani ya darasa la saba. Alisisitiza kuwa sasa wanamsaka aliyevujisha barua hiyo.

“Mwaka jana makundi ya ‘WhatsApp’ yalibainika kutumika kuwasiliana na kuvujisha mitihani, jambo ambalo si kweli.

Hata hivyo, hiyo ilisababisha shule zetu zote 103 zifutiwe matokeo. Kutokana na hayo, tumeamua kuvunja makundi sogozi yote ya Waratibu Elimu na si ya watumishi wengine.” Alieleza. Alisema kwa sasa ofisi yake inafuatilia nani aliyepiga picha na kurusha barua hiyo kwenye mitandao.

“Waratibu Elimu Kata Chemba wapo 26 hivyo tunafuatilia kujua nani aliyefanya hivyo kwakuwa wapo wachache. Akibainika hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake,”alisema.

Barua hiyo iliyosainiwa na Josephat Ambilikile kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chemba, inaelekeza kuvunjwa kwa makundi hayo ya ‘Whatsapp’ yanayojihusisha na kutoa au kupokea taarifa zozote zinazohusu utendaji wa taaluma na utaalamu, zinazomgusa mwalimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba katika utendaji wake wa kila siku hadi hapo watakapojulishwa vinginevyo.

Katika barua hiyo ambayo nakala yake ilipelekwa kwa Walimu Wakuu,Waratibu Elimu Kata wote walitakiwa kuvunja makundi hayo hususani yanayotumika kutoa au kupokea taarifa zozote zinahusu utendaji kitaaluma.

“ Pia ofisi imebaini kuwepo kwa mkundi ya whatsapp katika halmashauri yetu yanayotoa na kupokea taarifa mbalimbali za kielimu na kijamii,” alisema.

Barua hiyo imetaja makundi hayo kuwa ni ya Walimu Wakuu waliovuliwa madaraka na Walimu Wakuu wapya, Walimu Wakuu waliopo madarakani, maofisa elimu kata na Walimu Wakuu ngazi ya kata na wilaya na mengineyo yanayofanana na hayo.
Siri za ikulu zinavuja wasitafutwe waliovujisha, hawa wanyonge ndo wanaotafutwa? Ni kuwaonea tu.
 
Huyo DED naye hana kazi nyingine za kufanya au? Sasa kama hilo agizo amekiri mwenyewe kulitoa, nongwa iko wapi? Si alitoa agizo hilo kwa nia njema? Au hiyo barua ilikua ni ya siri kiasi kwamba ingehatarisha usalama wa nchi kwa kusambazwa kwake kwenye hiyo mitandao ya kijamii!
Zinavuja za ikulu itakuwa za walimu ? Asitafute umaarufu naye huyu, alitakiwa amsake snayevujisha mitihani
 
Huyo DED naye hana kazi nyingine za kufanya au? Sasa kama hilo agizo amekiri mwenyewe kulitoa, nongwa iko wapi? Si alitoa agizo hilo kwa nia njema? Au hiyo barua ilikua ni ya siri kiasi kwamba ingehatarisha usalama wa nchi kwa kusambazwa kwake kwenye hiyo mitandao ya kijamii!

PhD yake ni questionable, badala ya kumtafuta aliyevujisha mitihani wanamtafuta mtu mwingine kabisa, huyo akili zake akapimwe mkojo
 
Kwani hiyo barua ni ya siri au ya wazi kwa watendaji wote??
Pia kwani kuna ubaya gani barua ikisambaa mitandaoni kama njia ya kifikishiana ujumbe?
Au DED wa Nchemba bado anaishi dunia ya enzi za mwalimu???

Ujinga ni adui mkuu wa binadamu
 
Jinga sana umeshindwa kukamata akiye vujisha mitihani anataka kutafuta aliye vujisha libarua la kazi gani

Hii ni aina ya watendaji tulio nao heti group za watsap lina vujisha angekuwa na akili angechukua simu zote
 
Huyu DED inaonekana kuwa hana kazi ya maana ya kufanya, yeye hajui kwamba hata nyaraka za siri kabisa za Mamlaka za Kijasusi kama vile CIA ambazo ziko classified kama "TOP SECRET" nimekuwa zikivujishwa???? Sembuse hiyo barua yake???!! Hizi ni zama za utandawazi
 
Wa Tz kwa kujipa mizigo isiyo ya lazima! Sasa WhatsApp haikuhusika na uvujaji/udanganyifu wa mitihani, wanajisumbua nini kuyafuta makundi? Hilo limevuja, sasa anatafutwa aliyevujisha. Juhudi, nguvu na muda unaopotezwa kwa haya mambo yataongeza ufaulu wa watoto?
Ma DED wengine bado wanausingizi sana
 
Anazingua uyo DED nae wapi alipoiandika iyo barua kuwa ni SIRI aache wasumbua Walimu awape stahiki zao
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom