Aliyeuchoma Moto Uume wa Mumewe Kujibu Mashtaka ya Mauaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyeuchoma Moto Uume wa Mumewe Kujibu Mashtaka ya Mauaji

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Dec 5, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 5, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Aliyeuchoma Moto Uume wa Mumewe Kujibu Mashtaka ya Mauaji
  [​IMG]
  Friday, December 04, 2009 6:05 PM
  Mwanamke wa nchini Australia aliyeuchoma moto uume wa mumewe aliyetembea nje ya ndoa na kupelekea kifo chake, atapandishwa tena kizimbani mwezi januari mwakani kujitetea kuhusiana na mauaji ya mumewe. Mwanamke mwenye wivu wa nchini Australia, Rajini Narayan mwenye umri wa miaka 44 amepandishwa kizimbani leo ijumaa akikabiliwa na mashtaka ya mauaji, kusababisha moto na kuhatarisha maisha ya watu.

  Rajini ambaye ni mama wa watoto watatu, alizichoma moto sehemu nyeti za mumewe Satish Narayan, mwezi disemba mwaka jana baada ya kumvizia akiwa amelala aliporudi toka kwenye ulevi.

  Satish alipata majeraha makubwa sana katika sehemu zake za siri na alifariki wiki chache baada ya tukio hilo.

  Moto ulioziteketeza sehemu za siri za mumewe uliiteketeza pia nyumba ya familia yao na kusababisha hasara ya dola milioni moja.

  Katika vikao vilivyopita vya mahakama, majirani wa Rajini waliiambia mahakama kuwa Rajini aliwaambia "Mimi ni mke mwenye wivu sana, uume wake ni mali yangu na niliamua kuuchoma moto ili mtu mwingine yoyote asiupate".

  Rajini aliwaambia pia majirani zake kuwa hakutarajia nyumba yao ingeteketea kwa moto huo.

  Katika kikao cha leo cha mahakama, wakili wa utetezi aliiomba mahakama impe muda zaidi Rajini wa kuanda utetezi wake.

  Mahakama imekubali maombi hayo na kuiahirisha kesi hiyo hadi tarehe 22 mwezi januari mwakani.

  Narayan yuko nje kwa dhamana.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3677662&&Cat=7
   
 2. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  That girl is wicked!
   
Loading...