M-TZ1
Member
- Jun 3, 2020
- 79
- 132
ALIYETUHUMIWA KWA UBAKAJI WATOTO 24 ARUSHA SIYO USTADHI.
Tahariri.
Hivi karibuni Jamii ya Maustadhi ilijikuta imeingizwa kwenye mashaka makubwa kisaikolojia baada ya vichwa vya habari kuonyesha Kuwepo tuhuma kwa Ustadhi mkoani Arusha za ubakaji watoto 24 wa Shule ya Mkonoo kata ya Terati wilaya ya Arusha Jiji. Hata hivyo sasa imebainika mtuhumiwa siyo ustadhi wa madrasa.
Madrasa iliyolengwa ambayo ilifungwa kufuatia tukio la tuhuma hizo iko ndani ya Masjid Rosana Hamad ulio chini ya taasisi ya Islamic Foundation yenye Makao makuu Msamvu, Morogoro
Kwa Mujibu wa Sheikh wa wilaya ya Arusha Jiji Alhaj Ijunje Mtuhumiwa aliyetajwa Mbele ya mkuu wa wilaya siyo mwalimu wa Madrasa iliyofungwa na wala hajawahi kuwa mwalimu wa Madrasa yoyote na wanafunzi waliotajwa kuathiriwa hawajawahi kuwa wanafunzi wa Madrasa hiyo ambayo mpaka sasa imefungwa.
Naye katibu wa Islamic Foundation mkoani Arusha Bwana Mfinanga amesema Imamu na Mwalimu wa Madrasa hiyo ni Ustadh Shwaibu Suleiman Kifogo Na kwamba mtuhumiwa aliyetajwa siyo kiongozi wa msikiti au madrasa hiyo kwa namna yoyote. .Bwana Mfinanga anasema hajafahamu sababu hasa ya kuhusishwa mojakwamoja na kufungwa Madrasa hiyo.
Sheikh wa wilaya ya Arusha amesema Awali msikiti huo ulifungwa kwa Amri ya mkuu wa Wilaya. Baadaye waumini wakaruhusiwa kuswali lakini mpaka sasa Madrasa haijaruhusiwa kuendelea na mafunzo. Aidha Amesema imebainika wanafunzi wengi wanaodaiwa kufanyiwa vitendo hivyo siyo waislamu.
Mkuu wa wilaya naye hivi karibuni amesikika akisema kuwa mtuhumiwa siyo Ustadhi wa Madrasa. Na kwamba ni wanahabari tu waliongeza chumvi. Wala yeye hajamtuhumu mwalimu wa Madasa.
Kwa ujumla kosa kubwa lililofanyika ni kumtaja mtuhumiwa kuwa ni Ustadhi huku ikijulikana kwamba kufanya hivyo ni kuwadhalilisha maustadhi wote ambao siku ile waliathirika sana kisaikolojia.
Wala haijafahamika sababu ya BAKWATA kutoshirikishwa kwenye hatua za awali. Naamini uongozi wa BAKWATA mkoa, Wilaya au kata ungeshirikishwa mtuhumiwa asingehusishwa na ualimu wa Madrasa.
Je sekta nyingine ingepata shambulio kubwa la kisaikolojia kama hili kwa makusudi kungekalika?
Kwa mfano mtuhumiwa aitwe Polisi, Mkuu wa Wilaya, Diwani Mwalimu wa shule ilhali hana uhusiano na cheo au wadhifa huo waathirika wangekaa kimya? Au Mwalimu wa Madrasa anaendelea kuwa mnyonge mnyongeni na haki yake mnyimeni.
....
Dr. Harith Nkussa
Mwandishi Maalum wa Mufti
Ijumaa 27.5.2022
Dar es salaam