Aliyetuhumiwa Kumtukana Kikwete sasa Kugombea jimbo la Musoma Vijijini....... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyetuhumiwa Kumtukana Kikwete sasa Kugombea jimbo la Musoma Vijijini.......

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Dickson Ng'hily, May 7, 2011.

 1. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #1
  May 7, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Ndugu zangu Watanzania na wale wote wenye kuitakia mema Tanzania, nawasalimu,

  Nimeona ni bora kuliweka hili wazi kwa kila Mtanzania ili ajue ni kitu gani kinaendelea. Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana, yalisemwa mengi sana juu yangu kuwa nimerudi CCM n.k. Kama ilivyo kawaida yangu, nimechelewa sana kujibu hata hivyo sikuona umuhimu wa kujibu kwani wakati muafaka ulikuwa haijafika. Wahenga walisema, uwe mwepesi wa kusikia na sio kusema. Sasa wakati umefika na ninapenda kuwaambia habari hizo hakuwa na hazina ukweli wowote. Mimi bado ni mwanachama wa CDM na ninaipenda sana..

  Baada ya kusema hayo, napenda pia kuchua fulsa hii kuwashukuru wakazi wa jimbo la Musoma Vijijini kwa mapenzi yao mema kwangu na kwa familia yangu. Pia niwashukuru kwa kuamua kuniunga mkono katika harakati hizi za ukombozi wa Taifa letu. Kutoka ndani ya moyo wangu, naomba Mpokee shukrani zangu. Pia niwashukuru wale wote waliosafiri kutoka Musoma kuja kuniomba nikubali kugombea jimbo la Musoma Vijijini katika uchaguzi mkuu ujao (2015) lakini pia wale wote walionipigia simu na kunitumia msgs kunitaka nikubali ombi hilo..SASA NASEMA KUWA NIMEKUBALI OMBI HILO LA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO MUSOMA VIJIJINI IKIWA MWENYEZI MUNGU ATATUPATIA UZIMA NA AFYA NJEMA.....

  Sababu za kukubali wito huo ni kutokana na ukweli kuwa nusu ya maisha yangu nimeyaishi Musoma both vijijini na mjini hivyo ninaijua vizuri Musoma. Huku ndiko Marehemu mama yangu alizaliwa na kukulia na ndiko alikokutana na Marehemu mzee wangu Dr Ng'hily..Huku ndiko ambako walezi wangu kwa maana ya Babu na Bibi Eliasaph magafu Samanyi wamezikwa...

  Hata hivyo, kubwa kuliko yote ni maendeleo duni waliyonayo wakazi wa jimbo la Musoma Vijijini ambao wamekuwa nyuma kimaendeleo licha ya kuwa na natural resouces za kutosha...kama vile madini,uvuvi,utalii nk. Ninaamini kwa pamoja tunaweza kuibadilisha Musoma (V) na kuwa moja ya jimbo la kuigwa katika mkoa wa mara interms of maendeleo endelevu.

  Ndg zangu, HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE...Ninawahakikishia ya kuwa sitawaangusha...Ujasiri nilionao nitautumia kudai haki na uhuru wa makazi wa jimbo la Musoma (V). Na kazi hii naifanya kuanzia sasa na ninawaomba ushirikiano wenu. Mungu awabriki sana kwa yote...
   
 2. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  kila la kheri........
   
 3. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  BIG UP; tuko pamoja. Fungueni matawi kila kijiji na kusimamia wanachama na wananchi vema kutambua harakati za CDM kuanzia sasa. Shirikiana na viongozi wilaya, mkoa, na taifa katika jitihada zako.
   
 4. Elizaa

  Elizaa Senior Member

  #4
  May 7, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 160
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ushindi unao endelea kuung`ang`ania.
   
 5. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2011
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hii ni taarifa au habari mkuu......anyway nenda kaanze kujitangaza na kuwaambia utawanyia nini?
  ndio muda wenyewe mkuu miaka minne siyo mingi
   
 6. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,945
  Likes Received: 1,270
  Trophy Points: 280
  Mbona mapema. Chama na wananchi wakiteua mwingine? Acha vurugu kama za Kabwe na urais 2015
   
 7. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #7
  May 7, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Mkuu hii ni taarifa...Kaka mimi nimeombwa na wao coz wameona kazi niliyoifanya kipindi nagombea TEMEKE...Siwezi kuwaahidi nitawanfanyia nini ila nitakchofanya ni kushirikiana nao ili sote kwa pamoja (Wao na MIMI) tuiletee Musoma Vijijini maendeleo endelevu...Wadogo zetu na watoto wetu wafurahie kuzaliwa katika jimbo hili...Asante sana kwa kunitia moyo...
   
 8. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  (wewe si ndiyo inasemekana ulilambishwa chapaa na yule jamaa wa Bank M? hahaha! yule jamaa anavaaga kibaragashia chenye mkia kama mzee small!?)

  hapa ngoja niwe mwepesi wa kusikia kwanza; nisiwe mwepesi wa kusema,
   
 9. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #9
  May 7, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Ndugu yangu Nyakageni...Shunghuli za kujiletea maendeleo, hazina muda maalum wa kuanza, so sio mapema kama ufikiriavyo...Kaka,CDM nna wananchi wanaweza kuteuwa mwingine kama ulivyosema hata hvivyo hiyo hainizuii kukubali maombi ya wanajimbo wenzangu tena wengine kutoka CCM...Kama CDM itateua mtu mwingine haina shinda, nitaungana naye kuleta ukombozi na labda niseme hivi...Cna fujo ya aina yeyote hata hivyo una haki ya kuoa maoni...Ubarikiwe.
   
 10. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kumbe utaratibu wa kugombea ubunge kwa Chadema ni rahisi hivi, tunashukuru kwa kutuarifu. Yaani mimi nikiwa nataka kugombea jimbo fulani ninatangaza tu na basi tayari nimekuwa mgombea?

  Hata hivyo nina mashaka na uwezo wako wa kujenga hoja. Kama hivyo ulivyoandika hapo juu ndivyo utakavyokuwa unajenga hoja Bungeni iwapo utachaguliwa basi Chadema tumepata seti tupu. Jimbo kuwa nyuma kimaendeleo siyo sababu ya wewe kugombea wakati hakuna ushahidi kwamba wewe ndiyo maendeleo yenyewe na bila mkakati vile utakavyofanya basi kutuletea hayo maendeleo.

  Yaani ulichosema kama sapoti ya kugombea kwako ni sawa kabisa na kauli ambazo tumekuwa tukizisikia kwa wagombea wa ccm. Unaleta maendeleo gani, kwa vipi. Uwezo huo wa kuleta maendeleo wewe umeupata wapi? Kwamba umeishi huko siyo hoja, wengi wanaishi huko hadi sasa hivi. Kwamba wazazi wako walizaliwa huko siyo kigezo cha wewe kuwa mbunge wa eneo hilo, wengi wamezaliwa huko na bado hawana vigezo vya kugombea.

  Kwanza umekiri kwamba umeshindwa kujibu hoja hapa janvini, na unatumia kigezo hicho eti kututangazia kwamba utagombea. Nashauri ukae kimya kama ulivyosema kwamba ulikaa kimya watu walipokuwa wanahoji uadilifu wako.

  Ningependa wote wanaokusudia kugombea nafasi mbali mbali 2015 kujua kwamba it will not be business as usual, we want the best.
   
 11. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #11
  May 7, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Asante ndugu yangu Saaly...
   
 12. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Alaaaaa, kumbe ni wewe? Si ni wewe ndiye uliyeropoka ushuzi pale Mwembeyanga kwenye mkutano wa Dr. Slaa hadi polisi wakakuweka ndani na ikapelekea Chadema kukosa jimbo la Temeke?
   
 13. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #13
  May 7, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Nsimba...Asante sana na ninakuhakikishia kuwa nitashirikiana nao na taarifa nilishaanza kuzisambaza kunakohusika na wakati huu ninaandaa safari ya kwenda huko...Nashukuru sana na asate kwa kuniunga mkono na kuwa pamoja nami...Tuna kazi kubwa kukijenga chama huko na nina aamini kuwa kwa pamoja tunaweza.
   
 14. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #14
  May 7, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,743
  Likes Received: 6,018
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye bluu, kauli kama za wale jamaa wanaozeekea mjengoni. Wangapi wamesafiri kutoka Musoma just kuja tu kukuomba wewe ugombee ubunge 2015? Kauli mbiu hii imepitwa na wakati kaka.

  By the way, kuna michakato mingi hadi kuteuliwa na "chama chako" kuwa mgombea hivyo pia chance ya kukosa hiyo nafasi ipo na naamini utakuwa mwaminifu na utakubali matokeo endapo lolote litatokea ikiwapo kutokisaliti chama kama wengine wafanyavyo. Labda tumwombe Mungu katiba mpya iwe imepatikana na taratibu ziwe zimebadilika ikiwepo ugombea binafsi.
   
 15. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #15
  May 7, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60

  Kaka nashukuru kwa mchango wako..
   
 16. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #16
  May 7, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Nashukuru kwa mchango ndugu yangu..
   
 17. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #17
  May 7, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  badilisha heading ya taarifa yako.........
   
 18. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #18
  May 7, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60

  Ndo maana nimejibu kuwa tuombe uzima na afya, nilichofanya mimi ni kukubali ombi je kuna kosa hapo!Nihukumu kama kwa kukubali ombi nimefanya kosa...Hata hivyo nimesema na nitarudia kusema kuwa Chama kikiteua mtu mwingine, sina tatizo, nitashirikiana naye na mimi sitagombea jimbo lolote...
   
 19. Jaxx

  Jaxx Senior Member

  #19
  May 7, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Angalia sana hiyo nyekundu maana cku ukiambiwa uwataje utaweza?...Wakiulizwa wametumwa na nani kukwambia au kukutext watajibu?....Je hao waliokwambia au kukutext wao wanakubalika kwa wananchi???.......ni dhahiri kuwa hao ni ndugu zako tu ambao pia wanajua makazi yako kwa hao waliokuja na ambao walikutext wanajua number yako ya cmu?,(Jibu rahisi ni kuwa watakuwa ni ndugu zako).
  Nina nia njema sana na wewe ndiyo maana nakutahadharisha ili ukienda kule uwe na propaganda za maana, Binafsi cpendi mbunge aliyepo kule maana amekuwa cyo mbunifu wa miradi ya maendeleo bali ana technique ya kugawia viongozi (Madiwani,Watendaji Kata?Vijiji, Headteachers/schools) vijisent vyake binafsi BADALA YA KUTETEA JIMBO LAKE LIPATE MIRADI INAYOTOKANA NA KODI YA WANANCHI/SERIKALI....Hivyo kaza buti sana maana amewateka na wamebweteka sana,Ukitoa Butiama,kiabakari,Busegwe( Kwao MB) na Mgango ambazo zina umeme pia kwa Advantage ya ''Butiama Tu''...Wilaya nzima haina umeme, haina Lami hata ya kutambikia, haina Irrigation scheme yoyote,Maji taabu wakati wako karibu na ziwa, hakuna makao makuu ya Wilaya.....Unakazi kubwa sana ya KUFANYA NDUGI YANGU...hebu anzia hapo, Pia ile fununu ya wagombea wa Musoma Vijijini kununuliwa kaa chonjo pia
  Naomba kuwasilisha..........
   
 20. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #20
  May 7, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Niiwekeje ndugu yangu....Naomba msaada wako..
   
Loading...