Aliyetoroka karantini akamatwa Iringa

Siwezi kulaumu mtu anaetoroka, hivi unawezaje kumpangia mtu sehemu ya kukaa halafu alipie kwa mfuko wake? wanajuaje kama watu wanaweza mudu hizo gharama za kukaa hoteli.

Isitoshe sehemu ambazo wanatakiwa kufikia watoa huduma udhani kama wapo trained ku deal na namna ya ku limit maambukizi kwenye maeneo yao ya kazi iwapo kuna mtu analogonjwa humo (nina uhakika wahudumu watakuwa wanaingiza vyakula mpaka vyumbani, badala ya kugonga na kuacha milangoni) if anything hizo sehemu zilizotengwa zinaweza kuwa infection centres za baadae kama bado hotel zenyewe zinatoa huduma na kwa raia wengine.

Quarantine mtu anaweza kukaa ata nyumbani kwake na familia yake kuna masharti tu ya kuishi ndani ya nyumba ambayo yeye na familia lazima waheshimu.

Wewe unamwambia mtu akakae hoteli wakati ulipi bill iweje, yaani watu aisee. Ubunifu zero.
Ndiyo maana ya wajibu. Kila mtu mzima anatakiwa afahamu wajibu wake ndiyo maana huwa hatujikojolei kwenye suruali. Maana ya kuambiwa utaingia karantini kwa mfuko wako ni kuwa ulikuwa unalifahamu swala la ugonjwa kabla hujaingia chombo cha usafiri kuja.
 
Watu wa aina hii baada ya kipindi cha karantini kumalizika wanapaswa kufunguliwa mashtaka ya kutaka kusababisha mauaji ya halaiki. Hebu fikiria jamaa alipanda taxi au daladala hadi ubungo nako akachanganyika na halaiki ya watu. Baada ya hapo akapanda basi ambamo namo kulikuwa na watu wasiopungua 30 na kukaa nao ndani ya basi hilo kwa zaidi ya saa 6. Halafu akatumia usafiri mwingine hadi kwao na sehemu zote hizo akijichanganya na watu huku akijua athari za gonjwa hilo.
Huyu ni muuaji kabisa na hafai kwenye jamii.
 
Sio lazima hatol tusikariri kuiga watu wa nje linaweza kuwa hata bweni la shule ila kunakua na police na mitutu wanalinda Mana binadamu hatupo sawa kila mmoja na akili zake na Kwenye wengi lazima wakorofi watakuwepo ndio maana kunatakiwa kuwe na eneo lenye ulinzi mkali na sio kujiweka mwenyew kwa hiyari nyumbani , Ila kusema lazima hoteli si kwel ijaandikwa hivyo Kuna watu tuko wazaliwe hajawai hata kuingia hotelini Sasa leo akalale hotelini kwasababu ya majanga ya kolona c upuuz huu
Quarantine ni hotel si jengo la serikali na lenye ulinzi
Dah mamlaka na sera juu ya afya zetu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dogo nimesema wenye mamlaka wakiamua namaanisha wanaweza kupeleka muswada bungeni na kubadilisha sheria kisha ikawa kama nilivyoshauri na kuandika hapo juu.
Huwezi kusoma sentensi na ukaelewa kwa kina?
Usirudie tena kuniita Dogo you cunt pumbavu kabisa
 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amesema alipigiwa simu na mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Dniale Chongolo na akamjulisha kuhusu mtu aliyetoroka karantini.

Mtu huyo baada ya kutoroka Dar alionekana yuko Iringa, uongozi wa wilaya walishirikiana na jeshi la polishi kujua anapokaa mtu huyo na wamempeleka kantini.

Mtu huyo inasemekana alitoka Norway, na ana siku nne tangu aingie hapa Tanzania. Alikaa karantini siku tatu na kuamua kutoroka.

Nyumba aliyokaa pia iko chini ya karantini na mganga mkuu wa wilaya atawapima wote wanaoishi katika nyumba hiyo.

Kasesela amesema kuna mwingine wiki iliyopita alitoroka karantini ya Tunduma na hadi sasa hawajui yuko wapi, lakini mtu huyo alikuwa Mmalawi.


Sent using Jamii Forums mobile app
Hii habari imenifanya niitafakari sana ile kauli ya Rais wa Philipino Rodrigo Durtete aliyoitoa jana.
 
Selfish kabisa, watu wengine sijui wana matatizo gani upstairs? Halafu hao wanaokuwa karantini hawawekewi ulinzi nje kuwazuia kutoka? Sawa karantini kila mtu anaweza kukaa kwake, lakini anapenyaje mtaani asigusane na watu? Kwake ni wapi? Angalia kama huyo mama, kwake ni iringa huko, Mungu aepushie mbali, lakini kama anao na amepandikiza mbegu, wataathirika watu wangapi kutokana na u selfish wake? Kuna mambo yanatia hasira sana.
 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amesema alipigiwa simu na mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Dniale Chongolo na akamjulisha kuhusu mtu aliyetoroka karantini.

Mtu huyo baada ya kutoroka Dar alionekana yuko Iringa, uongozi wa wilaya walishirikiana na jeshi la polishi kujua anapokaa mtu huyo na wamempeleka kantini.

Mtu huyo inasemekana alitoka Norway, na ana siku nne tangu aingie hapa Tanzania. Alikaa karantini siku tatu na kuamua kutoroka.

Nyumba aliyokaa pia iko chini ya karantini na mganga mkuu wa wilaya atawapima wote wanaoishi katika nyumba hiyo.

Kasesela amesema kuna mwingine wiki iliyopita alitoroka karantini ya Tunduma na hadi sasa hawajui yuko wapi, lakini mtu huyo alikuwa Mmalawi.


Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa wanao toroka watatuletea matatizo.
 
Kilatha, Kwani alikuwa hajui kama kuna karantini ya kulipia?
Hadi anapanga safari ya kuja alitakiwa ajiandae la sivyo abaki huko huko
Hizo safari unafikiri zinapangwa siku ya safari? Si ajabu tiketi kanunua miezi 2 au 3 iliyopita, na hapo pengine anatakiwa akae wiki 2 au 3. Bila shaka majibu ya mwanzo ni hasi, na rushwa inavyoendekezwa, kaachiwa aondoke, halafu huko nyuma wamebanwa ndio wanamfuatilia tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom