Aliyetimuliwa kanisani kisa vazi asema alionewa na kiatu chake cha "uingereza" kiriharibiwa!!!!

Yaani unampa mwenzako ili wewe ubaki uchi au wazi, maana ulilazimshwa tu kufunika ukapata upenyo, angekupiga kabisa sio kukusukuma tu
 
Sisi waislam swala la mavazi msikini ni non negotiable liko wazi, ukitaka kuvaa uchi nenda huko kwa wanaotunga sheria na kuzipitia time to time,, quran haipitiwi ni kusoma na kuelewa kama hutaki basi sio mwislam ,, very clear, ni ajabu na kweli mnampenda mama yetu mariam mama wa Yesu ila mavazi yake ya hijab hamyataki
 
Ohh! to tell you the truth, mnatia huruma mno because you dont have even a single idea with what you are worshiping,

Romans have deceived and ambush you for such a long time not only the two of you but 1 billion people around the globe,

but its my prayer to God, day and night to show you the right path!

Amen!

Tell us, where do you worship?
 
Ushauri; jitahidini sana kusoma NENO la Mungu kuliko kupigana ngwara huku jf au kushinda kama kijiweni ambapo high percent hapajengi sana kiroho, kwani ipo mizaha mingi. wapo watu wanaopambana day and night humu kutafuta likes, rep power na wingi wa threads au replies.
Zaburi 1 : 1-6

1.1 Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
1.2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
1.3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.
Sawa mkuu mimi nilidhani nawewe upo jf , kumbe I was wrong . Hata hivyo nashangaa umetuonaje vijiweni kama nawewe haupo. Nadhani wewe ni bingwa wa mistari hivyo ni ngumu kushindana na wewe. Asante sana kwa mchango wako.
 
nakumbuka hata Yesu alishawai kupiga sarakasi alipokuta watu wanauza njiwa ndani ya hekalu na kuadilisha fedha, nadhani katekista ilibidi aende zaidi kama vijana wa kariakoo, angerarua vivazi vyote ili uyo mtembea uchi aende uchi kabisa> Dini zetu zimeingiliwa....si wakiristo tu hata waislam unakuta mtoto kavaa mpaka nicab ila uku anatembea anachezesha makalio kwenye hijab aliyoimodify ili ibane mwili. Dini zote tukemee ujinga wa hawa dadazetu. Wala mtu asikebehi juhudi za uyo katekista...Jaman kama makalio au mabega si tutaoneshana chumbani??ya nini katika nyumba za ibada???


Mkuu umenena vyema alimvumilia sana ilitakiwa afanyiwe kitu ambacho kingekuwa mfano kwa waumini na watembea uchi wengine,kanisa kama kanisa ni sem yakuabudu nakufanya toba sio naingia Kanisani kumuomba Mungu then mtu anakuja na mavazi ya makwazo anakaa mbele yako na bahati mbaya binadam tulivyoumbwa labda ulikuwa ktk tafakari,umenyanyua uso ukimuangalia aliye mbele yako ghafla unajikuta umeanguka tena ktk dhambi.ifike wakati dada zetu watambue,kwa dhati kabisa kwamba Kanisni ni sehem Takatifu na'si sehemu yakuonyeshana mabega au misuli ya miguu.wanatangaziwa nakutangaziwa lakini wapi!!!!nakumbuka kuna kipindi nasali Parokia ya Magomeni palikuwaga na utaratibu,mtu akija ameva min skirt/suruali anakabidhiwa kitenge na akija mabega wazi anakabidhiwa sijui ilikuwa taulo sikumbuki vizuri,baada ya mwezi Kanisani pakawa na heshma yake,me nadhan utaratibu huu ungeenezwa ktk Makanisa yote leo mambo yakuambiana sijui umenivunjia kiatu changu nilichokinunua Uk yasingekuwepo,huyo angekabidhiwa tuu taulo lake afunike mabega,hivyo ingekuwa juu yake akabadilishe nguo kwao,atoke akakae nje au ajifunike taulo akiwa ktk Ibada.
 
Yaani unampa mwenzako ili wewe ubaki uchi au wazi, maana ulilazimshwa tu kufunika ukapata upenyo, angekupiga kabisa sio kukusukuma tu

Hahahahaa!!mkuu huyo dada nahisi ana upungufu wakinga inayofanana na jina lako ktk akili yake.."FIKIRI KWANZA",akili yake inaonekana haina uwezo wakufikiria vizuri yaani ameona mwenzake ametolewa kwa kukosea kanuni anamsaidia then anataka avunje yy kanuni aliyoshaadhibiwa nayo mwenzake!!haingii akilini labda mtu ujitoe ufaham kwanza ndo ufanye hivyo,ajabu sana haya mambo
 
Uyo ndio yale madhehebu ya Magari,kazi yao ni kutangatanga tu hawajui kwa nini wanaishi,hana lolote analojua khs RC wala bible..

Absolutely, amepigiliwa ujinga na vijidhehebu waganga njaa anakuja kutapika hapa bila kujuwa anachoandika. Wewe unapopretend kuokoka or whatever haalafu ukasema uongo ulio dhahiri bila shaka unadhihirisha kuwa unaongozwa na pepo mchafu wala roho mtakatifu hayupo ndani yako. Unaponiambia mimi Mkatoliki naabudu sanamu wakati sijawahi kufanya hivyo, ama hujui maana ya kuabudu na ulokole wako feki, au pepo linalokuongoza limekudanganya hivyo.
 
Wakati mwanamke wa kivazi kilichositisha ndoa kanisani kwa dakika kadhaa akidai hakuwa na tatizo kuvaa vile, Katekista wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Peter, Yohane Maboko, amesisitiza kuwa alikiuka maadili ya Kanisa.
Mwanamke huyo ambaye ameendelea kukataa kutaja jina lake, huku njia zingine zikimtaja kwa jina la Restituta Kalemera, alidai juzi kuwa kivazi hicho cha mabega wazi hakikuwa tatizo kanisani, bali ni unyanyasaji tu wa Katekista huyo.

Akizungumza juzi, alidai kuwa Katekista Maboko alimsukuma na kumwangusha katika ngazi ndefu za Kanisa hilo lililoko Oysterbay, Dar es Salaam.

"Wakati Katekista akinitaka nitoke nje, ghafla alinisukuma nikaanguka kwenye ngazi na kudakwa na mtu mwingine aliyeniokoa, la sivyo ningeumia vibaya," alidai.

Alidai kilichomsikitisha ni kudaiwa kutaka kuingia kanisani akiwa amevaa nguo zilizoacha mwili wazi, jambo ambalo si la kweli, kwa kuwa alikwenda kanisani hapo akiwa na kitambaa kilichofunika mwili.

"Nilipofika kanisani, nilikutana na Katekista akimrudisha mtu mwingine, ghafla alitokea bibi harusi aliyevalia nguo ambazo hazikuruhusiwa kanisani, akaniomba skafu niliyokuwa nayo, nikampa nami kubaki wazi mabegani,"
alidai.

Baada ya kuvua kitambaa hicho, alidai alitaka kuingia kanisani ili kuchukua funguo za gari, lakini alikutana na Katekista kwenye ngazi, ambaye alimwamuru atoke nje naye akaendelea kumsihi kuwa anakwenda kuchukua funguo za gari ndani, hata hivyo hawakukubaliana.

Aliendelea kudai, kuwa Katekista alipomsukuma na kuanguka, baada ya kudakwa alichanganyikiwa akidhani kanisani ni sehemu ya malumbano, akakimbilia ndani kutafakari, huku kiatu chake alichonunua nje ya nchi (Uingereza) kikiwa kimeharibika.

Alidai kuwa akiwa kanisani, Katekista alimfuata tena na kumsihi atoke nje, jambo lililosababisha ndugu zake wamzingire kiongozi huyo wa Kanisa na kumhoji kwa jazba, sababu ya kumsukuma ndugu yao na kuhatarisha maisha yake.

Baada ya malumbano huyo, alitoka nje ya Kanisa na kuacha utaratibu mwingine ukiendelea, huku akilalamika kwamba Kanisa ni sehemu takatifu hivyo hapatakiwi kuwa uwanja wa mapigano na kwamba limeacha kazi ya kufundisha na kuomba ielezwe wazi watu wavae nini.

Akijibu tuhuma hizo, Katekista Maboko alimpongeza mwandishi kwa kushuhudia tukio hilo na kutoa habari yake na kuongeza kuwa utaratibu wa jinsi ya kuingia kanisani kwa maharusi, umekuwa ukifundishwa tangu kuandikishwa kwa ndoa hadi mafundisho ya ndoa.

Alisema dada huyo alipofika kanisani hapo, alikuwa na wanawe wawili waliokuwa na mavazi yaliyoacha sehemu za miili yao wazi, na aliwaelewesha lakini yeye akabisha.

"Niliwashika mikono na kuwapeleka uliko ubao ili wasome maelekezo ya kinachotakiwa kuvaliwa, lakini yeye alilazimisha kuingia huku akisema Mungu haangalii mavazi, bali roho," alisema Katekista Maboko na kuongeza kuwa wakati akieleza hayo, ndipo wanandugu walipofika na kumhoji.

Kuhusu miwani yake kuvunjwa, alisema wakati akiwa amezungukwa na watu kama 30 kwa lengo la kumchanganya, aliendelea kujenga hoja kuwa kanisani zipo taratibu zinazotakiwa kuzingatiwa, lakini mmoja wao alitumia nguvu na kuvunja miwani hiyo.

Hata hivyo, alisema mtu huyo aliomba samahani na kulipa kiasi cha fedha, ambapo walipeana mikono kama ishara ya kusameheana.

Katekista Maboko alisema kwa ufupi kilichotokea, ni kukosekana kwa busara kwa waumini hao, kwani vipo vibao vinavyotoa maelekezo juu ya utaratibu unaotakiwa na unaopaswa kufuatwa!!!!


I have come to conquer not to bow!
 
Hao wanaume wanaotamani mabega nao ni wazima?
At least sasa ngoma droo. Sio misikiti peke yake inayowabana wanawake kujisitiri maumbo yao..:rolleyez:
 
Hao wanaume wanaotamani mabega nao ni wazima?
At least sasa ngoma droo. Sio misikiti peke yake inayowabana wanawake kujisitiri maumbo yao..:rolleyez:

Mie nadhani nikujibu tu kwa kifupi kuwa ni wazima, tena sana.
 
wakatoliki wanashangaza sana local radio zao baada ya kusalisha rozari wanapiga mugongomugongo na alaji,

kanisani kwao wamejaza masanamu na kuyaabudu jambo ambalo ni chukizo kwa Mungu.

Wanamuabudu mungu mke wanamuita mama kanisa [yezebeli] ila wao wamemtungia jina wanamuita 'mama bikira maria'

Angalia ghafla na sherehe zao ni mtindo wa lager kwa kwenda kia mpaka askofu tena wanaziombea kabisa,

Wamebadili amri kumi za Mungu ukisoma kitabu cha KUTOKA zile amri ni tofauti na walizojiundia wao,

Hawatumii Biblia na hata waumini wakienda nazo ni bure wanatumia kitabu chao kinaitwa misali ya waomini ambayo masomo waliopanga vatican ndo hayo tu watakayosoma ambayo ni 2% tu ya Biblia nzima.

Hakuna kumpelekea maombi Mungu lazima umpelekee mama kanisa kwanza walifukua mifupa yake na kujidanganya eti amepaa mbinguni,

Wanaabudu wafu na kufanya ibada za kuwaomba mizimu wao wanawaita watakatifu jambo ambalo ni kinyume kabisa cha NENO.
Wanaenda kuwanyenyekea na kuwaomba toba wanadamu tena wa dhambi wa kawaida kabisa eti wawaondolee dhambi.

nikija kwenye hili sakata siungi mkono watu kuvaa nguo zisizo na heshima ila Yesu alikuja kwa waliopotea alijichanganya na makahaba, majambazi na mafisadi hakuwahi kuwahukumu bali aliwapa NENO ambalo lilibadilisha maisha yao,

sehemu kama kanisa sio kwaajili ya waliohaki bali waliopote pale ndo mahala pa kuwakusanya waasherati, machangudoa walevi, wezi, waongo na wenye dhambi wote ili wapewe NENO la uzima hivyo wangetumia mwanya huo kuwahubiria namna ya kuvaa kwa staa na sio kuwafukuza,

kwani Yesu alikuja kutafuta kilichopotea tena akasema utaijua kweli nayo kweli itakuweka huru,

wakatoliki badilikeni na wewe mkatoliki unaefikiri unamwabudu Mungu wa kweli katika Roho na Kweli jitafakari usijekuwa unaabudu kinachoabudiwa vatican ambacho ni chikizo mbele za Mungu.

Pokea like.. ..
 
Hao wanaume wanaotamani mabega nao ni wazima?
At least sasa ngoma droo. Sio misikiti peke yake inayowabana wanawake kujisitiri maumbo yao..:rolleyez:

Msikitini gani unawabana wanawake actually kwetu sisi waislam mwanamke anaruhusiwa ku pray msikitini but inakuwa vizuri zaidi na malipo wake yanakuwa makubwa zaidi atakapo sali nyumbani kwake..
 
duh!!!,kwa hiyo kama hatukuwa tunavaa nguo unavyoona wewe ni vema kuendelea kukaa uchi?,your arguments are too low bro,u better piga ki100 tu kama huna cha kuchangia.

The point hapa is that we should not misquote the past to mistreat women. since we only copied how to dress we should not be so excessive on limiting the copying. The disgusting issue here is that it only applies to women so that men can feel less horny? or whats the logic? If the matter is so important let it go into the constitution so that women know that they are breaking the law when they show there knees or whatever it is that you don't want women to show.
 
Wewe na kizazi chako ndio mliokuwa mnakaa uchi,

Weka hapa kabila lako nikupostie picha mlivyo kuwa mnavaa kabla ya mkoloni na mwarabu kuja kuwasitiri. Hata adamu na eva baada ya ku do walicho ki do wali realize kwamba wako uchi lakini unfortunately miafrika haikujua kuwa iko uchi. sasa hivi wamekuwa eti ndio mods wa kuvaa
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom