Aliyetembea na Mke wa Mtu Apofuliwa Macho kwa Tindikali Uingereza

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,109
2615334.jpg

Eneo la tukio likiwa na mabaki ya tindikali na alama za adamu Friday, July 24, 2009 11:46 AM
Mwanaume mmoja nchini Uingereza yupo mahututi hospitalini baada ya kupewa kipigo cha nguvu, kupofuliwa macho yake na kisha kulazimishwa kunywa tindikali baada ya kutembea na mke wa mtu. Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 24 alimwagiwa tindikali aina ya sulphuric pamoja na kuchomwa chomwa na visu na kupigwa na matofali baada ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke ambaye alikuwa mke wa mtu.

Familia ya mwanamke huyo raia wa Uingereza mzaliwa wa Pakistan inasemekana ilifanya shambulizi hilo kwa kuamini kuwa mapenzi yao yameitia aibu familia yao.

Kipigo alichopewa mwanaume huyo na wanaume wanne waliokuwa wameficha sura zao kilimuacha akiwa amepofuka jicho lake moja, ulimi wake ukiwa na majeraha makubwa kutokana na kuunguzwa vibaya na tindikali huku koromeo lake nalo likiwa limeunguzwa na tindikali hiyo.

Mwanaume huyo pia alichomwa kisu mara mbili kwenye mgongo wake na alipigwa na tofali usoni mwake lililosababisha paji lake la uso lipate ufa.

Mwanaume huyo raia wa Denmark mwenye asili ya Asia inasemekana alifanya mapenzi na mke wa mtu ingawa mwanamke huyo aliwaambia maafisa wa polisi kuwa uhusiano wao haukuwa wa kimapenzi.

Mwanaume huyo alishambuliwa julai mbili mwaka huu karibu na nyumba yake aliyopanga na kuhamia hivi karibuni ili awe karibu na mwanamke huyo mashariki mwa jiji la London.

Shuhuda mmoja wa tukio hilo alisema kuwa mwanaume huyo baada ya shambulio hilo alinyanyuka huku akipiga kelele na kujigonga kwenye mti katika harakati za kukimbilia nyumbani huku akipiga kelele za kuomba maji.

"Alikuwa akipiga kelele za kuomba msaada lakini kwakuwa alikuwa hajui kiingereza vizuri watu walifikiria ni mlevi pombe zimemzidia" alisema shuhuda mwingine wa tukio hilo Kay Dice, 52.

Mwanamke huyo naye amepewa ulinzi wa polisi baada ya kuonekana maisha yake ya hatarini.

Kiongozi mmoja wa jumuiya ya wapakistan alisema "Mauaji au mashambulizi kama haya ya kulinda heshima ya familia hutokea sana kwenye jamii yetu ya Pakistan, tunajaribu kuwaelimisha watu waache utamaduni huu wa kufanya mauaji au mashambulizi kwa imani za kulinda heshima ya familia zao".

Polisi wamewakamata watu saba kuhusiana na shambulizi hilo, watano kati yao waliachiwa kwa dhamana wakati wawili walipandishwa kizimbani moja moja kwa tuhuma za kujaribu kuua.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=2615334&&Cat=2
 
Back
Top Bottom