Aliyetapeli kwa kujiita Afisa Usalama wa Taifa akamatwa Iringa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,117
Gabriel Kaserikali Mkazi wa Mbezi Mwisho, Dar es salaam anatuhumiwa kumtapeli Mohamed Nassoro mfanyabiashara wa magari wa Magomeni Dar es salaam kwa kujitambulisha ni mtumishi kutoka Idara hiyo

Akiwa Iringa alijitambulisha kwa baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Iringa kuwa yeye ni Afisa kutoka Makao Makuu Dodoma, hivyo wamchague Leonard Mgina kuwa Mwenyekiti wa CCM na kwamba hayo ni maelekezo kutoka mamlaka ya juu ya Serikali

Kamanda wa Polisi ACP Allan Bukumbi amethibitisha kumshikilia mtuhumiwa huyo na tayari amefikishwa Mahakamani.

======================

Jeshi la Polisi mkoani Iringa linamshikilia Gabriel Kaserikali (34) Mkazi wa Mbezi mwisho Jijini Dar es salaam kwa tuhuma za kujifanya mtumishi wa Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari, leo Alhamisi Oktoba 13, 2022 Kamanda wa Jeshi la mkoani humo, ACP Allan Bukumbi amesema tukio hilo limetokea Oktoba Mosi, 2022 katika shule ya Sekondari ya Wasichana ya Iringa iliyopo kata ya kihesa Manispaa ya Iringa mkoani humo.

Aidha ACP Bukumbi amedai mtuhumiwa alijitambulisha kwa baadhi ya wajumbe wa mkutano Mkuu wa CCM, Wilayani Iringa kwamba yeye ni Afisa usalama wa Taifa kutoka Makao Makuu Dodoma huku akiwaeleza wajumbe hao wamchague ndugu yake aitwaye Leonard Mgina kwenye nafasi ya uenyekiti Wilaya kwamba ni maelekezo kutoka mamlaka ya juu za Serikali.

Kamanda huyo amesema kuwa baada ya Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi na kubaini kuwa mtuhumiwa huyo siyo mtumishi wa idara ya usalama wa Taifa lakini pia alifanikiwa kumtapeli mfanyabiashara wa magari wa Magomeni jijini Dar es Salaam.

"Tumefanya uchunguzi na kubaini kuwa mtuhumiwa huyo siyo mtumishi wa idara ya usalama wa Taifa kwa sababu amemtapeli Mohamed Nassoro mfanyabiashara wa magari wa magomeni jijini Dar es salaam baada ya kujitambulisha kuwa ni mtumishi kutoka Idara hiyo" amesema ACP Bukumbi

kamanda huyo amedai kuwa baada ya mtuhumiwa huyo kujitambulisha kuwa mtumishi wa idara hiyo ndipo walifanya makubaliano ya malipo ya awamu ya kiasi cha Sh18.5 milioni lakini hakuweza kulipa kiasi chochote na kisha kutoweka na gari hilo.

Hata hivyo, Mtuhumiwa amefikishwa Mahakamani kujibu tuhuma hizo.

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom