Aliyetangazwa Amekufa, Ahudhuria Mazishi Yake Mwenyewe!!! Hii ni kweli jamani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyetangazwa Amekufa, Ahudhuria Mazishi Yake Mwenyewe!!! Hii ni kweli jamani?

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, Oct 30, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [TABLE="width: 491"]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD]
  [​IMG]
  Gilberto Araujo[/TD]
  [TD]
  Mwanaume aliyehudhuria mazishi yake alisababisha kizaa zaa nchini Brazili na kupelekea baadhi ya ndugu zake kuzimia na wengine kumkimbia kwa hofu.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Muosha magari katika mji wa Alagoinhas nchini Brazili, Gilberto Araujo mwenye umri wa miaka 41, alisababisha mtafaruku mkubwa pale alipohudhuria mazishi ambayo yalikuwa kwaajili yake.

  Mtafaruku huo ulitokea pale kaka yake Gilberto, Jose Marcos, alipotakiwa na polisi aende hospitali kuutambua mwili wa ndugu yake ambaye alitajwa kuwa ameuliwa kwa kupigwa risasi.

  Jose aliutambua mwili huo na kusema ni kweli wa mdogo wake Gilberto na kuruhusiwa kuuchukua mwili huo kwaajili ya taratibu za mazishi.

  Wakati taratibu za mazishi zikielekea ukingoni, Gilberto aliwahi nyumbani kwao baada ya kukutana na mtu aliyempa taarifa kuwa nyumbani kwao wanajua amefariki dunia na hivyo mazishi yanafanyika.

  Baadhi ya watu kwenye mazishi walizimia na wengine walikimbia baada ya kumshuhudia aliyetajwa kuwa ni marehemu ametokea mbele yao akiwafuata.

  Shemeji yake Gilberto akilielezea tukio hilo alisema kuwa mtafaruku ulianza pale habari zilipoanza kusambaa mtaani kuwa muosha magari ameuliwa kwa kupigwa risasi.

  "Polisi walimuita mume wangu na kumuambia kuwa kaka yake ameuliwa kwa kupigwa risasi na mwili wake uko monchwari hivyo alitakiwa aende kuutambua", alisema mke huyo wa kaka yake.

  Iligundulika baadae kuwa mtu halisi aliyeuliwa katika tukio hilo alikuwa ni Genivaldo Santos Gama.

  "Kwa jinsi walivyokuwa wakifanana na wote walikuwa waosha magari ndio maana watu walidhani ni Gilberto ameuliwa", alisema mama yake Gilberto.

  "Nina furaha sana, kitu gani ambacho mama anaweza kusema baada ya kuambiwa kuwa mtoto wake amefariki halafu baadae anamuona yuko hai", alisema mama yake Gilberto, bi Marina Santana.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. snochet

  snochet JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 1,271
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  hivi Balali naye si alihudhuriaga ya kwake?....ila hamna aliyezimia.
   
 3. B

  BatteryLow JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  inawezekana alizimia mwenyewe baada ya kuona watu wanavyomlilia kumbe si kweli, nilivyo na roho nyepesi ningejitokeza pale mbele na kusema ukweli
   
 4. Endangered

  Endangered JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 929
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  watu walikuwa wanamlilia, walipoumona ghafla wakamkimbia. kasheshe hii.
   
 5. w

  wakunyata Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 14, 2012
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ingekuwa ndo mimi ningejificha hadi wazike alafu naibuka usiku wakiwa wanajiandaa kugonga msosi. sipati pichaaaa!!!..
   
Loading...