Aliyetaka kumuua mandela jela maisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyetaka kumuua mandela jela maisha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gumzo, Aug 1, 2012.

 1. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MHUSIKA mkuu wa mpango wa kumuua Nelson Mandela, wiki iliyopita katika Mahakama Kuu ya nchi hiyo alipatikana na hatia ya uhaini kwenye kesi moja iliyodumu kwa takriban miaka 10 na atahukumiwa jela maisha.

  Mike du Toit alikuwa mhadhiri wa chuo kikuu na kiongozi wa kundi la kibaguzi la Jeshi la Kaburu la Chama cha Boeremeg, baada ya kupatikana na hatia na mahakama kusema atahukumiwa siku zijazo kuhusiana na jaribio lililoshindwa la kumpindua Mandela mwaka 2002 nchini Afrika Kusini, wanasheria akiwemo Steve Mhokholo, wamefunguka na kusema hukumu yake itakuwa kifungo cha maisha jela.

  Mashahidi waliieleza mahakama kuwa du Toit na wenzake walipanga kumuua Mandela ambaye mwaka 1994 alikuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini pia walikusudia kuwapiga risasi weupe wenzao ambao wangepinga mtazamo wao wa kuwa taifa kamili la kibaguzi la Makaburu.

  Du Toit alitaka kukiondoa madarakani kwa nia ya mapinduzi chama tawala cha African National Congress (ANC) na mahakama kuu nchini humo imesema atahukumiwa katika tarehe itakayotangazwa baadaye.
   
Loading...