Aliyesoma umeme VETA anaweza kuajiriwa ndani ya meli?

Political stability

JF-Expert Member
Apr 7, 2021
906
1,396
Wakuu, nina swali fupi tu hapa

Hivi kwa mtu aliyesoma umeme au plumbing and fitting chuo cha VETA, je anaweza kuajiriwa au kupata kazi ndani ya meli... ?
 
Sidhani aiseee labla kwa wale waliosoma chuo cha bandari ndio wana course tofauti tofauti za meli, boat, Panton n.k
 
Kwa vyeti vya VETA tu hauwezi kuajiriwa melini ni lazima usome kozi fupi za ubaharia(Mandatory Course) ambazo ni 1.Elementary First Aid
2.Ship Security Awareness
3.Fire Fighting Technique
4.Personal Survival Technique
5.Personal Safety and Social Responsibility

Kwa kusoma kozi hizo fupi inakuwa ni kigezo Cha mtu yoyote kupanda meli yoyote. Baada ya kuwa na hizo certificate za awali unaweza ukaomba kazi melini kama fitter au plumber.

Kwenye meli Kuna kazi nyingi kutokana na aina ya meli na mizigo wanayobeba. Kwenye meli nyingine watahitaji fundi Bomba/nurse/welder/bar maid/waitress/galley boy/fitter/winch man.

Galley boy haitaji fani yoyote huyu kazi yake ni kuosha vyombo, kukata mboga na nyanya pia kusafisha mess za melini.

Kwenye meli kila mtu mwenye fani tofauti anatakiwa ila hizo kozi ni lazima usome ili uelewe mazingira ya meli na namna ya kupambana na changamoto za moto, kuzama na hatari zozote zinazoweza kutokea.
 
Ni lazima usome hizo zote tano, au kozi moja wapo kati ya hizo
 
Je Bro, kwa mtu mwenye degree ya electrical engineering akisoma mandatory course anaweza kupata kazi Dubai?
 
Back
Top Bottom