Aliyesoma Elimu ya Masafa(ya Mtandao) kama Open University akikutana na waliosoma UDSM, SAUT na Mzumbe anatakiwa Kuchangia lolote?

Kuna mwanangu mmoja alipiga masters ya OUT fresh tu na gamba juu, ila cha ajabu baadaye yeye mwenyewe anakwambia haiamini hiyo masters yake na ilimbidi afanye tena admission ya MBA SAUT the guy is serious na hivi ndo anaingia final year. Nimeshangaa sana, huwa najiuliza inakuwa vipi hii!
hilo ni popoma kama mleta mada
 
GENTMYCINE leo umeandika UTOPOLO sana unajishushia heshima yako na unaonekana hujaelimika na kustaarabika.
Nenda kafanye utafiti pitia site moja inaitwa Edx hii ni elimu masafa katika mambo ya teknolijia.
Jinsi hiyo site ilivyo interactive katika kufundisha hakuna chuo bongo kina teknolijia kama za Edx.
Hii ilianzishwa na MIT na imeuzwa mabilioni ya pesa na inataka kufanywa Chuo kikubwa cha kisasa cha mtandaoni.
It is very modrrn way of teaching ambapo hata sisi ingebidi tu adapt hio teknolojia badala yake wnajitokeza watu wenye fikra za kizamani sana.
Lecture method is a very primitive way of t/ l tangu enzi za kina Plato na Sokreti kabla ya kuzaliwa kristo, ni njia ya kizamani sana, imepitwa na wakati.
Change your mind.
 
Kwanini unapenda kuanzisha threads za kukashifu wenzako? Utashambuliwa na watu wa OUT kwa vile unawakashifu
Tanzania Vyuo Vikuu ni UDSM, SAUT Mwanza, Mzumbe na Tumaini labda na kidogo sana UDOM, ila vilivyobaki hamna Kitu. Huu ni mtazamo wangu na Uheshimiwe ila ukikukwaza tafuta Sumu ya Panya Koroga unywe Ufe.
 
Ngoja nikapige pale huku nikisaka hela mambo ya fingerprint kama Mzumbe nani anataka yaani unanitaka nikae darasani wakati na akili Acha maisha yaendelee tukutane kwenye pepa na ada,mambo ya kuchungana ya nini,Mimi nataka cheti tu niongeze CV wakati wa mazishi.
Mkuu umenikumbusha kina jamaa mmoja askari alisoma uhasibu yeye alikuwa anachukua time table pale chuoni , mambo mengine hayamuhusu mtaonana siku ya paper na test, assigment anajua mwenyewe alivyofanya.
Baba zoma ikakae darasani wakati unamajukumu ya familia.
 
Anaongea vizuri sana, tena anawatoa njeee!! Ukitaka kujua ubora wa elimu ya masafa ya OUT
1. Mitaala ya OUT inasimamiwa na TCU, kuhakikisha ubora unadhingatiwa! Mbona hakifutwi kama ni dhaifu?

2. Wakigraduate mfano LLB wanakwenda Law school na kukimbizana ipasavyo na hao wa conventional!

3. Wahasibu wanaomaliza mafunzo OUT wanapita bodi za uhasibu na kupata CPA na taaluma zinginezo.

4. Interview za serikali au binafsi mnachanganywa wote humo!! Mara nyingi walomaliza OUT hupata kushinda!! Hapo vipi??

5. Unajua kuna wanataaluma nguli wa hivyo vyuo ulivyotaja ambao ni zao la OUT?? Tena wanawafundisha nyie. Au niwataje??

6. OUT ni chuo bora kabisa kwa sasa ni namba moja barani Africa kwa vyuo vinavyotoa elimu masafa miongo mwa mlolongo wa vyuo kutoka mataifa bora kabisa kielimu. Hadi UNISA walikwenda OUT kujifunza??

7. OUT ndiyo taasisi namba moja kwa mwaka 2021 Tanzania kwa matumizi bora ya TEHAMA inayotolewa na tume ya TEHAMA nchini. Hapo UD tupa kule, SUA kanyaga, Mzumbe sogeza vile, tuzo alitoa Mh. Majaliwa huko Arusha.

8. Imepata Recognition certificate kutoka ATU, unawajua hao?? 🤣🤣🤣

Kwa vigezo hivyo, nakuhakikishia kabisa kuwa wanaume wanaomaliza OUT wanapaswa kuheshimiwa. Akisimama mnapaswa mkae chini kwa heshima!! Wenzenu wanapiga nondo kwa malengo na si michezo yenu ya kufuata wanafunzi wakike vyumbani mwao muwakulena kuwapa alama (refer mhadhiri wa UDOM).
Kuna Mtu Mmoja wa TCU aliniambia kuwa Mwanafunzi Mmoja wa SAUT Mwanza ( Chuo Kiku bora cha GENTAMYCINE Tanzania ) ni sawa na Wanafunzi 15 wa OUT ( Chuo Kikuu Huria ) cha Biafra je, unakubali au unakataa?

Leo Wanafunzi wa OUT mtanikoma JF.
 
Kwani SAUT na OUT mna tofauti?.
SAUT Mwanza ndiyo Chuo Kikuu pekee Tanzania nzima ambacho kinafundisha Wanafunzi 'Brainy' kabisa na Kinazalisha 'Think Tanks' na 'Intellectuals' wa Ukweli.

Kama hujasoma SAUT Mwanza jinyonge.
 
Elimu ya online ni ya kisasa zaidi, kuliko sisi tulioenda kushinda chuoni siku nzima. Huenda Genta unaona sifa zile kashikashi za face to face, na sio content. Kadiri nyakati zinavyozidi kusogea, elimu ya online itatumiwa na wengi, kuliko hiyo ya kwenda kuvuta uzee kwenye campus za vyuo.
Mkuu nisingechokoza kwa Kuwatia Ndimu ( Kuwapandisha Hasira ) waliosoma na wanaosoma OUT ambao Wengi wao ndiyo nawaona Wanachangia huu Uzi wangu haya Madini yao ningeyajuaje / tungeyajuaje?

Napenda tu Kuchokoza ili nijue mengi.
 
Sasa popoma ni lini ulisoma chuo lakini?

Mbuzi kuchunga umemuachia nani huko bunda?
Wewe Pimbi una bahati sana ni Mtani wangu kutoka moja ya haya Makabila ya Watani zangu ya Wahaya, Waha, Wanyiramba, Wanyaturu, Warangi, Wanyamwezi na Wakara, ila usingetokea huko ungenitambua hapa JamiiForums na kujua kwanini Wimbo wa Taifa hauna Kolabo na kwanini pia Nyoka hana Ugoko.
 
Mleta mada ametumia mbinu ya uchochezi ili kuibua mjadala na kufanya watu washushe nondo zao. Educative thread!
 
We genta nawe swali gani hilo.
Sasa kuku wa kisasa na kuku wa kienyeji nani ana akili zaidi.
Utalinganisha mtu aliyejitafutia mwenyewe materials hadi akafaulu na mtu aliyesubiria kuletewa material na lecture?
Hivi ni Lecturer au ni Lecture kama ulivyoandika hapa mwishoni? Nikisema mliosoma / mnaosoma OUT hamna Kitu 'Vichwani' muwe mnanielewa tafadhali sawa?
 
SAUT Mwanza ndiyo Chuo Kikuu pekee Tanzania nzima ambacho kinafundisha Wanafunzi 'Brainy' kabisa na Kinazalisha 'Think Tanks' na 'Intellectuals' wa Ukweli.

Kama hujasoma SAUT Mwanza jinyonge.
Nilicho shangaa ni kuona SAUT katikati ya UDSM na MZUMBE...unakosa heshima sana Genta, SAUT mwenzake DSJ.
 
Wewe Pimbi una bahati sana ni Mtani wangu kutoka moja ya haya Makabila ya Watani zangu ya Wahaya, Waha, Wanyiramba, Wanyaturu, Warangi, Wanyamwezi na Wakara, ila usingetokea huko ungenitambua hapa JamiiForums na kujua kwanini Wimbo wa Taifa hauna Kolabo na kwanini pia Nyoka hana Ugoko.
Mkuu unanipiga mabiti hata Mimi😀😀😀
 
Mleta mada ametumia mbinu ya uchochezi ili kuibua mjadala na kufanya watu washushe nondo zao. Educative thread!
Huwa nafurahi sana kukutana na Watu 'Genius' kama Wewe hapa JamiiForums na ambao huwa mnanielewa upesi GENTAMYCINE na aina yangu ya Mada hapa pamoja na uibuaji wangu wa Masuala ( Issues ) ambazo huwa zinahitaji Mjadala mpana wa Wana Taaluma na Great Thinkers Kuujadili.

Watu wengi wanadhani nakashifu OUT.
 
Tupo katika mazoea ya kishamba sana, ukweli ni kwamba the age if information imerahisisha kila kitu.
Ukiwa Nyumbani unawasha computer yako unahudhuria lecture ya Yale university unasikiliza kwa makini vile profesa anamwaga madini yake kuliko profesa wangu wa UDSM SUA,SAUT ,MUM nk.
Nilipokuwa chuo nuli enjoy sana lecture za profesa lewis wa MIT, that guy is the GURU of teaching physics wf!
Yani mtu wa OUT akizama akasikiliza lecture za Yale,MIT, Birmingham, Oxford ku@@ma&&maae!! wewe ulieshinda vingweta vya chuo humkuti kabisa.
Nakumbuka niliweza kumaster quantum physics( particle in a box) kwa kufuatlia kwa adabu lecture moja ya Mjapani/mmarekani acha kabisa, darasani nilikuwa naona kama napoteza muda(levture alitushsuri tukariri baadhi ya vipengere, ujinga kabisa).
Kati ya kitu ambacho wanafunzi wa kisasa wana enjoy ni internet kuna kila lecture kila mada huna haja ya kukomaa na darasani tu.
Nakumbuka nimewaahi otea notes na maswali mtandaoni kumbe lecture kakopi na kupest 100% mtandaoni.
Nakwambia muandika mada, ma lecture wa kibongo wana copy paste kila kitu mtandaoni.
Nimefanya utafiti na ukibisha ntakutajua code za kozi za vyuo vyetu na wapi wamekopi note.
Muandika mada inawezejana umesoma chuo miaka ya 2000 kurudi nyuma internet haijawa na nguvu hivyo unamawazo ya kizamani.
Lecturers wetu kweli wanakopi notes na maswali online hasa zile sites za kulipia. Mara kadhaa nikiwa nasoma online huwa nakumbana na maswali ninayoulizwa kwenye test au UE. Alafu wanapenda kurudia maswali kutoka mwaka mmoja kwenda mwingine
 
Back
Top Bottom