Aliyeshtakiwa kwa kosa la kutoa lugha ya matusi dhidi ya polisi, Kashinda kesi Mtwara

Mwee

JF-Expert Member
Feb 17, 2018
240
602
Mtuhumiwa Adolph Msafiri aliyekuwa akishtakiwa kwa kosa la kutoa lugha ya kuudhi dhidi ya Jeshi la Polisi ameachiwa huru na mahakama ya Mwanzo huko mkoani Mtwara baada ya kuonekana hana kesi ya kujibu. Mtuhumiwa huyo alikamatwa kwa kuweka ktk ukurasa wake wa Facebook, picha ya Askari Polisi wakishambulia raia kwa risasi siku ya maandamano ya Chadema na kuandika "KUNA TOFAUTI KATI YA POLISI NA TAKATAKA".

Hakimu Lawrence Nyoni aliyesililiza kesi hiyo amesema upande wa mashtaka umeshindwa kuonesha kosa katika maneno ya Adolph. "Mtuhumiwa alisema kuna tofauti kati ya polisi na takataka, na kweli tofauti ipo, nyie ni polisi na hamfanani hata kidogo na takataka. Sioni kosa la kumshtaki kwahiyo namuachia huru"

Awali Mtuhumiwa alipokua akijitetea alimhoji askari wa upelelezi aliyekuwa mahakamani hapo kuwa "wewe ni polisi?" Akajibu "ndio" akamuiliza tena "unafanana na takataka?" Akajibu "hapana", mtuhumiwa akasema "kwahiyo unakubaliana na mimi kwamba kuna tofauti kati ya polisi na takataka sio?". Askari huyo hakujibu.

Adolph ni mwanafunzi wa sheria, Chuo Kikuu Huria kampasi ya Dar es Salaam.!

My take
Polis ebu angalieni na makosa ya kushtaki mnajidhalilisha.
 
Kitu nilijifunza baada ya siku moja baadhi yao wakijidanganya kunipeleka kituoni wengi wao wanafikiri mahakama ni chombo cha kukamilisha matakwa yao!.. baadhi yao hawajui ata tips za kisheria wanajidhalilisha, wanapaswa kuwa smart kuitunza heshima yao! na ya kazi waliyopewa na jamuhuri..afande mmoja smart(educated) alipata shida sana kuwatoa kwenye mori isiyo na mantiki!
 
Back
Top Bottom