Aliyeshindwa kura za maoni CCM Antony Msami ahamia CHADEMA achukua fomu za ubunge

inavyoonekana huyu jamaa anachotaka ni ubunge tu na si vinginevyo sidhani kama kweli kwa hiyari yake ameamua kuwa mwanacdm kuna msukumo ndani yake (ubunge) ndo maana ameamua kuwahi huko mapema na akitoswa sijui atasemaje tena,ngoja tusubiri..
hala hala asituletee rushwa huku kwetu...tunaomba dr. atuondelee yoyote anayeonekana mbabaishaji kama ilivyokuwa kwa bavicha, asituletee habari za magamba huku ataumbuka mara moja
 
Chadema ni aibu kama watamkubali huyu jamaa kirahisi hivyo
amekuwa political figure kiasi hicho mpaka wamtetemekeeee
 
CDM chama cha MAKAPI.
Mgombea wa ubunge ccm aliyeshindwa kura za maoni Bw Anthony msami amehamia na ameomba kugombea ubunge kupitia chadema. Katibu wa chadema wa Wilaya ya Meru bw Totian Ndonde amethibitisha kuwa Msami amechukua fomu na anatarijiwa kuirudisha leo.

Bwana Msami amesema ana siri nzito ya rushwa ndani ya CCM ambapo kila mgombea alileta watu wake na kwa namna moja au nyingine wote wametoa rushwa. Anthony amekuwa akishutumiwa kuwa ni mamluki ndani ya CCM aliyetumwa na chadema kwenda kugawa kura na kufanya upelelezi amekanusha habari hiyo na kusema kuwa kimsingi watu wawili ambao watakuwa wamekiharibu chama katika kipindi hiki ni James Milya ambaye kundi la rafiki ya EL linataka SIOI apitishwe. Kundi lingine ni la BM ambalo linataka mtu wao apitishwe. Hata hivyo SIOI kama hana shida ni kajina anayeonekana ana uwezo isipokuwa anabebwa na kundi baya na chafu. Makundi yote haya mawili yamemwaga hela ya kutosha.

Msami ameulelezea kukerwa na mpango wa kuwatumia washili ambao anasema ni mambo yalipangwa kipropaganda. NI aibu kwa wazee wa CCM kukubali kubebeshwa jambo zito kama hili kuwa WAMEPANGA KUMCHINJA MBUNGE LEMA halafu inaonekana kuwa ni WASHILI wa meru.

Source: Arusha.
 
Kwa hiyo kumbe hamna utaratibu wa kuwaweka wogombea pamoja na kupigiwa kura na wananchama lipatikane jina moja ndio awe mgombea wa chama.

Mnachofanya ni kupokea amri kutoka Makao Makuu mpitisheni flani. huko ni kukaba demokrasia ndani ya chama.

Kwa hiyo Chadema mmeishateu jina la mgombea siku nyingi huko Arumeru?
Wewe yanakuhusu nini? Mbona sijakusikia ukipiga kelele kulaani rushwa iliyotumika kumpitisha Sioi/Naoa kule CCM? Peleka umakalio wako kwa hao makalio wenzako mabingwa wa rushwa duniani.
 
Wewe yanakuhusu nini? Mbona sijakusikia ukipiga kelele kulaani rushwa iliyotumika kumpitisha Sioi/Naoa kule CCM? Peleka umakalio wako kwa hao makalio wenzako mabingwa wa rushwa duniani.

Huyu ni baadhi ya viongozi wa Chadema wanaotaka watanzania tuwape nchi, kauli yake tu inakufanya umjue ni mtu wa aina gani.
 
Mbona Dr Slaa alihama CCM ktk mazingira kama haya na akagombea?!

mkuu slaa aliongoza kura za maoni.. akaenguliwa na nec na nafac yake akachukua qorro.. na ndo slaa akaingia cdm na kuuchukua ubunge.. huyu kashiriki kwenye kura za maoni na kashindwa vbaya.. hakuna mazingira yanayofanana hata kidogo..
binafci ninaona huyu jamaa yuko after ubunge.. akikosa na hapo atakuwa kama dudumizi..
 
Kama ana siri si lazima agombee ubunge kwani akizisema akiwa anamsindikiza Nassari kwenye kampeni hazitasikika au lazima awe mgombe a ubunge ndo inakuwa vema kuzitoa. Asilazimishe kugombea ubunge kwa nini asiombe kugombea kwa chama cha SAU au TLP na badala yake anataka kuleta ushuzi huku CDM. Kama CDM wamemruhusu kugombea watakuwa "the biggest lossers of the year2012"
 
Huyu anaonekana ni mlevi wa madaraka na maslahi binafsi na siyo ya wananchi
 
Pia cdm wawe makini na watu kama hawa kwani ndo sumu ya kuja kuuwa nguvu za chama baadae
 
mimi kuna jambo moja linalo nikera kwenye chama chetu cha cdm, kupokea wale waliokuwa kwenye kundi la magamba wakahama kisa wameshindwa au kunyanganywa masirai flani. Yani hawakuama kwa kuwa wameona wananchi wanaangamia au hakuchukuzwa na uozo wa magamba lakini wameama kwa kuwa wamenyima uongozi au wameshindwa katika kura za maoni za magamba. Mimi nachukia wanapo pokelewa halafu wakapewa nafasi za kugombea kuptia chama chetu maana hawa hawatufai.
Big to mpendazoe yeye alijitoa magamba mapema hakungoja kura za maoni ashindwe au adhulumiwe ndipo aone ubaya wa magamba.
 
Back
Top Bottom